Meatu Yetu

Meatu Yetu Duka

26/08/2022

🙌🎩 Karim Benzema is the winner of the UEFA Player of the Year Award!
🏆 ¡Benzema, premio al Jugador del Año de la UEFA!
👏 Félicitations, Karim !
|

Bando letu
12/09/2021

Bando letu

31/08/2021
19/08/2021

ISHU YA AZAM FC KUBADILI LOGO ..
IPO HIVI
Author Agosti, 2021

KLABU ya Azam FC imezindua nembo mpya ya timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021-22 na michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat' alisema kuwa lengo kuu la kuzindua nembo hiyo ni kutaka kuitangaza timu hiyo kisasa wakati huu wakielekea kwenye michuano ya kimataifa huku akiweka wazi kuwa malengo yao makubwa k**a klabu ni kufika kwenye hatua ya makundi katika Kombe la Shirikisho Afrika (CC).

"Maandalizi hayaanzii tu kwa wachezaji ni mfumo ambao unaanzia kwenye kila idara na ndio maana tumeamua kuzindua logo yetu mpya ambayo itaitangaza timu yetu kwenye michuano ya kimatifa lakini pia sisi k**a viongozi tumejiwekea malengo ya kuhakikisha tunafika mbali zaidi ingawa hatua ya makundi ndio kipaumbele chetu cha kwanza," alisema.

Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa, ambaye ameipongeza timu hiyo kwa hatua iliyofikia tangu ilipoanza rasmi kujulikana na kuwaahidi kushirikiana na uongozi katika kutengeneza ajira nchini.

"Uwekezaji kwenye Azam FC umetoa fursa kubwa sana ya ajira kwa vijana, wachezaji na madaktari na k**a Azam walivyosema wametoa ajira ya zaidi ya watu 120 hivyo ni jambo la kupongezwa na sisi k**a Serikali tunaahidi kutoa ushirikiano ili kuongeza fursa zaidi za ajira kwa vijana nchini," alisema.

Katika hatua nyingine Bashungwa alisema kuwa anaipongeza Azam media kwa uwekezaji wake katika soka la Tanzania kwani limeongeza nguvu kwa klabu kwa miaka 10 ijayo huku pia akiipongeza Shirika la habari Tanzania (TBC) kwa kuingia mkataba na TFF kwenye thamani ya Sh3 bilioni, kwa miaka 10 kwa ajili ya utangazaji wa mechi kwa njia ya sauti.

"Mabiliano yaliyowekwa na Azam media na TBC yataleta tija kwa klabu zetu kwenye uendeshaji tofauti na miaka ya nyuma ambapo klabu zilikuwa ombaomba," alisema.

Akizungumza kwa niaba ya Rais wa TFF katibu mkuu wa (TFF) Wilfred Kidau alisema kuwa anaipongeza Azam FC kutokana na mchango wao mkubwa kwenye soka la Tanzania na kuahidi kuendelea kushirikiana kwenye fursa mbalimbali kwa mafunaa ya Mpira wa Miguu.

"Azam wamekuwa wadau wetu kwenye maendeleo ya soka nchini na hivyo sisi k**a shirikisho tutaendelea kushirikiana ili kuona Mpira wetu unafikia mbali zaidi," alisema.

Katika uzinduzi huo wageni mbalimbali walihudhuria wakiwemo Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia na Katibu wake Mkuu Wilfred Kidau.

Wengine waliohudhuria ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Hamisi Taletale maarufu k**a Babu Tale.

(Bongo sports)

16/08/2021

Tu nakuja Kivingine kabisa!!!!
Stay connected,
Tulia hapohapo Ulipo!!!!!!

06/05/2020

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia Mbunge wa Kishapu, CCM, Suleiman Masoud Suleiman kwa tuhuma za kukutwa na Silaha 16, Risasi 536 pamoja na Nyara za Serikali.

Address

Mwanhuzi
Bariadi

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00

Telephone

+255625554711

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Meatu Yetu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category