Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo Huu ni Ukurasa Rasmi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) formerly Bagamoyo College of Arts.

The main aim is to develop and promote Tanzanian arts and culture and impact knowledge of the same to existing and future generations from anywhere in the world. Its roles and functions are as follows
• Provision of high quality training programs
• Provision of consultancy services
• Conduct research
• Production of arts and culture products through audio, visual, performing and multimedia in orde

r to promote an appreciation of customs and traditions of the people of Tanzania

Vision Statement
To be a dynamic Arts and Culture Training Centre of Excellence in Africa

Products and Services of TaSUBa
Training programs and services
TaSUBa offers varieties of training programs in dance, drama, music, acrobatics, music production, fine arts, media design etc. The programs are categorised as follows;
A. Short Courses Programs for 2, 4 and up to 6 months
B. Long Course Programs
i. Two years Certificate program
ii. One year Certificate program
iii. Two years Diploma program
C. Consultancy services and Research in arts and culture

Bagamoyo International Festival of Arts and Culture
Bagamoyo international festival of arts and culture, this is an annual event normally conducted in the last week of September. The festival promotes the institute and its products as well as gives positive reputation among the community. Centre of Excellence
TaSUBa is an EAC Centre of Excellence for visual and performing arts training with an overall objective of aiming at addressing Partner States’ requirements for the preservation, promotion and development of the visual and performing arts within the East African Community. Its specific objectives include conducting training programmes in visual and performing arts, theatre in development, Stage Technology and Arts and Culture Management for practitioners within the region; promoting arts and culture research activities; providing arts and culture consultancy services advising partner states’ governments on matters related to the preservation, promotion and development of visual and performing arts and coordinating and managing the ex*****on of the East African Arts and Culture festival in liaise with the East African Community secretariat.

08/06/2026

Muda Africa Wawavutia Watazamaji kwa "Frozen Dance"

Kikundi cha dance kinachofahamika kwa jina la Muda Africa kimeonyesha uwezo mkubwa wa kisanaa kwa kuonesha uchezaji wa dansi unaojulikana k**a "Frozen Dance" uliowavutia na kuwaacha watazamaji vinywa wazi!

Wanakikundi hao walionesha ubunifu, umakini na ushirikiano wa hali ya juu kwa kufanya miondoko iliyokuwa ikisimama ghafla k**a sanamu na kisha kuendelea kwa ustadi mkubwa. Umahiri huo uliwafanya watazamaji kufurahia burudani hiyo huku wakitoa makofi na shangwe za pongezi.

Maonesho haya yameendelea kuthibitisha kuwa sanaa ya dansi ni jukwaa muhimu la kuonesha vipaji, ubunifu na uwezo wa wasanii wa Tanzania katika kutoa burudani yenye mvuto kwa jamii.

🇹🇿

07/06/2026

TaSUBa Yaibuka Kidedea Katika Mashindano ya Kirafiki Dhidi ya MARUCO

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imeibuka kidedea katika mashindano ya kirafiki dhidi ya Marian University College (MARUCO) yaliyofanyika kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, urafiki na kukuza vipaji vya michezo miongoni mwa wanafunzi wa taasisi hizo.

Katika mchezo wa mpira wa miguu, TaSUBa ilionyesha kiwango cha juu na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya MARUCO.

Aidha, katika mchezo wa mpira wa wavu (volleyball), TaSUBa ilitawala mchezo huo na kushinda seti zote tatu mfululizo.

Kwa upande wa netiboli (netball), TaSUBa iliendelea kung'ara baada ya kuibuka na ushindi mkubwa wa magoli 36-11 dhidi ya MARUCO, matokeo yaliyoonyesha uimara na maandalizi mazuri ya timu hiyo.

Mashindano hayo yamekuwa fursa muhimu ya kuimarisha mahusiano kati ya TaSUBa na MARUCO huku yakitoa nafasi kwa wanafunzi kuonesha vipaji vyao vya michezo sambamba na shughuli zao za kitaaluma.

Washiriki kutoka pande zote mbili walionesha nidhamu, ushirikiano na ushindani wa kirafiki uliolenga kujenga umoja na kuendeleza michezo katika taasisi za elimu ya juu.

07/06/2026

TaSUBa vs Marian University College (MARUCO)

05/06/2026

Umuhimu wa Wazo katika Utengenezaji wa Makala

Mkufunzi wa TaSUBa, Mwalimu Cyprian Frank, ameeleza kuwa utengenezaji wa makala unahitaji maandalizi mazuri ili kufikisha ujumbe kwa usahihi kwa wasomaji.

Amesema makala zinaweza kuwa za aina mbili, ambazo ni makala fupi au makala ndefu, kulingana na madhumuni na maudhui yanayokusudiwa.

Mwalimu Cyprian amesisitiza kuwa kabla ya kuanza kuandika makala, mwanafunzi au mwandishi anatakiwa kuwa na wazo la msingi litakalomwongoza katika uandishi wake. Wazo hilo husaidia kupanga maudhui, kubainisha lengo la makala na kuhakikisha ujumbe unaandikwa kwa mtiririko unaoeleweka.

04/06/2026

TaSUBa Yawapiga Msasa Wanachama wa Baraza la Wazee Tanzania

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imeendelea kutekeleza jukumu lake la kukuza na kuendeleza sanaa nchini kwa kuwapatia mafunzo ya uimbaji wanachama wa Baraza la Wazee Tanzania.

Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha washiriki kupata maarifa na mbinu za kisasa za uimbaji ili kuboresha uwezo wao wa kutunga, kuimba na kuwasilisha muziki kwa kiwango cha kitaalamu.

TaSUBa imeeleza kuwa itaendelea kushirikiana na makundi mbalimbali ya kijamii katika kutoa mafunzo ya sanaa ili kuhakikisha vipaji vinaendelezwa na muziki unakuwa chombo muhimu cha maendeleo ya jamii.

03/06/2026

"Vipaji huzaliwa, lakini wasanii huandaliwa. Karibu TaSUBa kwa mwaka wa masomo 2026/2027 ujifunze, ubobe na ufanikiwe katika dunia ya sanaa na utamaduni."

30/05/2026

TaSUBa na Tamasha la Kimataifa la Bagamoyo Vyatajwa Kukuza Sanaa Tanzania

Mkazi wa Bagamoyo, Bw. Shabani Ramadhani, ameeleza kuwa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imekuwa na mchango mkubwa katika kukuza, kuendeleza na kutangaza sanaa nchini Tanzania kwa miaka mingi.

Amesema uwepo wa TaSUBa umeiwezesha Bagamoyo kuwa kitovu muhimu cha sanaa na utamaduni, huku ikitoa fursa kwa vijana wengi kupata elimu ya sanaa na kuendeleza vipaji vyao katika nyanja mbalimbali za ubunifu.

Bw. Ramadhani pia amepongeza Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, akieleza kuwa tamasha hilo limekuwa jukwaa muhimu linalowakutanisha wasanii kutoka Tanzania na mataifa mbalimbali duniani kwa ajili ya kubadilishana uzoefu, kuonesha kazi zao na kuimarisha ushirikiano wa kiutamaduni.

29/05/2026

Jukwaa (Stage) Bora, Performance Bora

Mtaalamu wa stage ambaye pia ni mkufunzi katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Bw. Felix Sesoa anaeleza teknolojia ya majukwaa (Stage Technology) kuwa ni sehemu muhimu katika mafanikio ya maonesho yoyote ya sanaa, kwani huchangia kwa kiasi kikubwa ubora wa uwasilishaji wa kazi za wasanii kwa hadhira.

Anaeleza kuwa teknolojia ya majukwaa inahusisha matumizi ya vifaa na mifumo mbalimbali ya taa, sauti, mapambo ya jukwaa, pamoja na mbinu za kiufundi zinazowezesha maonesho kufanyika kwa ufanisi na kuvutia watazamaji.

"Hata k**a wasanii wana vipaji vikubwa, maonesho yao yanaweza kupungua thamani endapo hayatasaidiwa na teknolojia bora ya jukwaani," anasema Mwl. Sesoa.

28/05/2026

Ufinyanzi: Sanaa Inayoendelea Kuishi Enzi na Enzi

Mkufunzi wa sanaa ya ufinyanzi kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Bw. Sunday Kamangu, amewaasa wasanii wanaojihusisha na sanaa ya ufinyanzi kuendelea kuwa wabunifu zaidi katika kazi zao ili kukuza na kuendeleza sanaa hiyo ya asili.

Amesema ufinyanzi ni sehemu muhimu ya urithi wa sanaa na utamaduni wa Tanzania, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuuenzi na kuurithisha kwa vizazi vijavyo kupitia elimu na mafunzo kwa vijana.

Aidha, amesisitiza kuwa vijana wanapaswa kutumia vipaji vyao vizuri kwa kujifunza mbinu mbalimbali za kisasa bila kuacha misingi ya sanaa ya jadi ili kuhakikisha maarifa ya ufinyanzi yanaendelea kudumu na kuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya sanaa nchini.

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) tunawatakia Waislamu na Watanzania wote Eid Al-Adha njema yenye amani, u...
26/05/2026

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) tunawatakia Waislamu na Watanzania wote Eid Al-Adha njema yenye amani, upendo na baraka tele.

Eid Mubarak!

Address

Bagamoyo
32

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo:

Shortcuts

Share