04/09/2020
TABIA ZA VIZIWI
Tabia ni matendo au mwenendo unaojirudia na kujenga mazoea ya kutendeka.
Tabia hupimwa au kuchunguzika kwa kutumia misingi ya kisayansi,kiimani au kijamii.
Tabia inaweza kuwa nzuri au mbaya kutegemeana na misingi hiyo.
Zifuatazo ni baadhi ya tabia za viziwi
1️⃣ Viziwi huongea kwa kukosa msawazo wa sauti. Anaweza kuongea kwa kutoa sauti kubwa sana au ndogo sana isioeleweka au kusikika vizuri.
2️⃣ Hukwazika haraka sana wasipotimiziwa mahitaji yao ndani ya wakati
3️⃣ Viziwi wengi hutembea kwa kuburuza au kusugua viatu chini. Kwa kuwa hawasikii sauti itokayo miguuni mwao, huona kawaida.
4️⃣ Hujiamulia mambo yao wenyewe. Mara nyingi huwa hawataki kuongozwa na mtu anayesikia katika mambo yanayowahusu.
5️⃣ Huwa na tabia ya kutomaliza maongezi wanapoyaanza,hivyo hufanya maongezi kuwa marefu.
6️⃣ Asilimia 90% ya viziwi ni wapole kitabia. Ukali na hasira wanazokuwa nazo ni matokeo ya kutotimiziwa mahitaji yao kwa sababu ya ugumu wa mawasiliano, kudharauliwa,kudhihakiwa, kunyanyapuliwa na kuchokozwa.
7️⃣ Viziwi wengi wana vipawa na ni watendaji wazuri wanaojali muda. Wakati wengine wanaosikia wanapozungumza wao hujikita kwenye shuguli zao.
8️⃣ Uziwi ukubwani huwaletea viziwi hali ya kutojiamini au kujitenga. Hii hutokana na wao kuogopa kudharauliwa au kudhihakiwa na wanaosikia.
9️⃣ Huchelewa kujitambua katika umri sahihi kutokana na ugumu wa mawasiliano wakati wa ukuaji, hususana viziwi wa kuzaliwa.
🔟 Baadhi ya viziwi hasa wa ukubwani hawapendi kutumia lugha ya alama badala yake hupendelea kutumia lugha ya mazungumzo kwa kusoma midomo.
Mwenye swali, boresho, nyongeza
Mbarikiwe sana
🙏🏿🙏🏿🙏🏿