Fanikiwa Journalism School - FJS

Fanikiwa Journalism School - FJS

Comments

INAKUAJE,WASHKAJI
###xvidokm
Nyimbo ya mwanafunzi wa fanikiwa jounalist
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na Utangazaji Fanikiwa wakifuatilia hotuba ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli wakati wa kufunga Bunge la Tanzania
Natumia nafasi hii kuwapongeza darasa la Mikumi(Mikumi Class)kwa kumaliza muda wao wa masomo katika chuo bora cha Uandishi wa habari na utangazaji Fanikiwa.Mnaingia kwenye 'soko' la ajira na kujiajiri(Ujasiriamali),enendeni mkafanye kazi kwa bidii ili mkitangaze vyema chuo chenu cha Fanikiwa.
Rais-Serikali ya wanafunzi(FJS).
mebio
UJUWE KTK MAISHA YATAKIWA KUPAMBANA JUU YA MAISHA UTAFTAJI UKULIMA UFANYA BIASHALA UBUNIFU NDO MAISHA YA KUPAMBANA VIJANA WENZANGU TUPAMBANE TUCHAPE KAZI VIJIWENI SIO PAZULI PANAPOTOSHA
naitwa ayoub napenda xan utangazaji na wandxh wa habar ila kwa xax nip tabora naxomea mamb ya ICT INFORMATION COMMINICATION AND TECHNOLOGY xax nataka kujua nikija nitapata nafax 0746363241
oya mambo vip?
Ni kwa neema tu mungu ni mwema
Belnda
JulasPerogadsn

Fanikiwa Journalism School is a private educational institution located at Arusha kwa Mrombo.

Operating as usual

25/01/2021
21/01/2021

Karibu Fanikiwa Journalism School

Karibu Fanikiwa Journalism School

16/01/2021

Asante sana Michael Lukindo kwa ku-'share' uzoefu wako na wanafunzi wa Fanikiwa Journalism School. Karibu tena.
"What you do to yourself will die with you, but what you do to others is immortal"

Asante sana Michael Lukindo kwa ku-'share' uzoefu wako na wanafunzi wa Fanikiwa Journalism School. Karibu tena.
"What you do to yourself will die with you, but what you do to others is immortal"

12/01/2021
09/01/2021

0756508071
www.fjs.ac.tz

0756508071
www.fjs.ac.tz

20/08/2020

Karibu Fanikiwa Journalism School

Karibu Fanikiwa Journalism School

07/08/2020
31/07/2020

Fanikiwa Journalism School
0756508071

24/07/2020
13/06/2020
29/05/2020
16/05/2020

BUNI BIASHARA YAKO WIKI HII
Kuna msemo wa kingereza unaosema “No body has a money problem, but it is always an idea problem”. Yaani, “Hakuna mtu mwenye tatizo la ukosefu wa fedha, bali tatizo ni ukosefu wa wazo(la kibiashara) linaloweza kumwezesha kupata fedha.”

Fedha ziko kwenye mawazo yako. Usikubali kupoteza hali ya kutafuta mawazo mapya au kuboresha mawazo yako ya zamani, au kujifunza namna mpya ili upate kipato au ili utoke mahali ulipo kiuchumi, au ili ukabiliane na mikwamo mbalimbali ya kiuchumi. Usikubali kuingiza baridi katika mawazo yako, bali chochea moto zaidi akilini mwako kila siku mpaka upate upenyo wa namna ya kujitawala kiuchumi! Mgagaa na upya, hali wali mkavu, ukikata tamaa utakwenda na maji!

Ukipoteza hali ya kutafuta mawazo kwasababu yeyote ile, akili yako italala, na utakuja kukurupukia kufanya biashara hasa zile ambazo ni za kuingizwa mjini na matapeli. Zoezi la kutafuta mawazo ni zoezi la kudumu, zoezi endelevu hadi kichwa chako kiwe k**a dish la kunasa mawimbi ya jinsi ya kufanikiwa duniani.

Imeandikwa “Naye atakuwa k**a mti uliopandwa kando kando ya vijito vya maji, uzaao matunda yake kwa majira yake, wala jani lake halinyauki, na kila alitendalo litafanikiwa (Zaburi 1:3)” Inawezekana hajafikia kiwango hiki cha kufanikiwa kibiashara, lakini endelea kukomaa tu, mpaka utoboe! Kwasababu “Mwenye haki huanguka mara saba na kuinuka tena”.

WAZO ZURI LA BIASHARA LINA SIFA GANI?
Kuna mtu wa Nairobi mwenye mawazo makubwa kuliko facebook, lakini hayajawahi kumsaidia! Na kuna mtu wa Morogoro mwenye mawazo madogo(ya kawaida) ya kuuza ubuyu kwa jumla na reja reja kwa mia mia, na ametajirika! Usidanganyike, kufanikiwa kibiashara hakutegemei ugunduzi wa hali ya juu tu au kuwa na mtaji mkubwa(fedha) peke yake! Kuna watu wana mitaji mikubwa lakini hawajui kitu cha kufanya! Anza na hali uliyonayo! Anza na hali uliyonayo wiki ijayo.

HESABU HIZI ULIJIFUNZA DARASA LA NGAPI?
1. UNGA WA MUHOGO + MAJI YA MOTO = UGALI
2. WAZO + MAARIFA 15 = BISHARA
3. LIMAU +TANGAWIZI+PILIPILI KICHAA+KITUNGUU SWAUMU+MAJI MOTO+ KITUNGUU MAJI =DAWA YA KOLONA
4. WAZO + USHAURI WA AINA 4= BIASHARA
5. WAZO + FEDHA ZAKO AU ZA WENGINE = BIASHARA
6. WAZO +WAZO =O
7. FEDHA + FEDHA =O
8. MUDA +KITABU = WAZO
9. MWANAUME +MWANAUME= O
10. MWANAUME +MWANAMKE=MTOTO
11. WAZO +MAARIFA +MUDA=BIASHARA
12. MUDA +MUDA = O

K**a unapenda kujifunza zaidi kuhusu somo hili, Mimi Joseph Mayagila(Mkurugenzi wa Fanikiwa Journalism School Arusha), Nimeandika kitabu chenye kurasa 50, chenye kichwa KUBUNI BIASHARA IKUPASAYO. Nitakuuzia kitabu hiki kwa mkopo wa siku 30, kwa bei ya shilingi elfu tano(5000/=). Kitabu hicho nitakutumia kwa whatsap au kwa email yako katika mfumo laini(soft copy). K**a unahitaji kitabu hicho tuma neno “KITABU KWA MKOPO” kwa whatsap kwenda namba 0715 76 96 15, kisha utapata kitabu hicho baada ya dakika kumi tu ukisha kamilisha kujaza fomu maalum ya mkopo nitakayokutumia kwa whatsap.

Pia k**a unataka kupata kitabu hiki kwa kulipa taslim(cash). Tuma neno “KITABU KWA CASH” kwa whatsap kwenda namba 0715 76 96 15. Kisha nitakutumia kitabu hicho baada ya dakika 10. Kisha baada ya kukipokea kitabu hicho, ndipo utafanya malipo. UKILIPA KWA CASH NITAKUTUMIA ZAWADI YA FUNZO LA ZIADA.
KARIBU TUNOE VICHWA KATIKA, KIPINDI HIKI CHA KORONA(0715769615)

11/05/2020

LEO NAOMBA NIKUFUNDISHE BIASHARA KIBABE!
K**a Facebook ingegunduliwa na Mtanzania wa pale Sumbawanga, unadhani ingekuwa kampuni kubwa ya kimataifa k**a ilivyo sasa? Jibu unalo! Kufanikiwa kibiashara ni zaidi ya kugundua jambo jipya. Inategemea umegundua nini, nani yuko nyuma yako, au nani anaunga mkono huo ugunduzi, vinginevyo utakesha! Ndiyo maana jambo la kuhusiana na wadau, au kuhusiana na watu maalum(key people) ni muhimu kwako k**a unataka kufanya biashara katika mfumo wa kitajiri.

Kuna mtu maskini mwenye mawazo makubwa kuliko facebook, lakini hayajawahi kumsaidia! Na kuna mtu tajiri mwenye mawazo madogo(ya kawaida) ya kuuza ubuyu jumla na reja reja kwa shilingi mia mia, na ametajirika! Usidanganyike, kufanikiwa kibiashara hakutegemei ugunduzi wa hali ya juu tu au mtaji mkubwa(fedha) peke yake! Kuna watu wana mitaji mikubwa lakini hawajui kitu cha kufanya! Lakini jambo ambalo nina uhakika nalo ni kwamba usipojifunza kuweka fedha zako au za watu wengine hatarini ili ziongezeke, hutakuwa salama! Yaani, usipojifunza kujihatarisha utaingia hatarini zaidi.

Miaka kadhaa iliyopita niliwahi kuweka pesa zangu katika usafirishaji wa abiria na pesa nyingine nikaziweka katika kuanzisha taasisi ya mafunzo kwa waandishi wa habari. Lakini rafiki yangu mmoja, yeye wakati huo aliamua kuweka fedha zake benki ili ziwe salama. Mtu mmoja akawa anasema, “Tajiri hajawa tajiri bado, na maskini hajawa maskini bado, mpaka ipite miaka 25.” Je alitumia vigezo gani kutoa kauli hiyo wakati sisi wote, wakati huo, mimi na rafiki yangu, tulikuwa tumeajiriwa sehemu moja na tukilipwa mishahara inayolingana? Jibu unalo!

Mtu mmoja aliwahi kujitangazia umaarufu kuwa atakuwa tajiri sana ulimwenguni kwa kuwa alikuwa amegundua kutengeneza kinywaji kitamu kuliko cocacola!
Ukweli ni kwamba hata k**a ukigundua kinywaji ambacho ni kitamu mara nne zaidi kuliko cocacola leo, haitamaanisha moja kwa moja kwamba utafanikiwa kibiashara kuliko kampuni ya coca cola, k**a huna mifumo ya kibiashara ambayo inazidi mifumo ya kampuni ya coca cola, ili uitumie mifumo hiyo kuuza kinywaji chako kipya.

Je unayo mifumo ya kutangaza kinywaji chako kuliko cocacola inavyotangazwa kwenye televisheni, magazeti na mitandao ya kijamii? Je wewe una “madepoti” k**a waliyonayo nchi nzima na duniani kote?
Je umejenga mifumo ya usambazaji au kutoa leseni kwa wafanyabiashara wengine(franchising) ili kinywaji chako kiwepo kila mahali ili wateja wasipate shida kukipata? Je unaona hayo magari ya usambazaji mchana na usiku kwa ajili ya kusambaza kinywaji kwa wateja nchi nzima? Je hao wafanyakazi maelfu wa cocacola unawaona?

Hizo friji wanazogawa bure kwa kila muuza soda nchi nzima, na hivo viti vyenye chapa za coca cola unaviona? Je unao mkakati wa kujitangaza sokoni, kiasi kwamba kila mahali penye sherehe kinywaji chako kisikosekane? Watu walionyuma(back office) ya hiyo biashara ya coca cola wewe unawajua?
K**a huna mifumo katika biashara yako, hata k**a ungegundua kichwaji kitamu kuliko ile divai aliyoitengeneza YESU kwenye harusi ya Kana Galilaya, bado tu biashara yako itakuwa ni ya kukupatia ugari tu, na si ya kukupatia utajiri!

Je kwenye biashara yako unayo mifumo, au wewe ndiye mifumo? Umeme hauwezi kufika mahali ambapo haujajengewa miundo mbinu. Hali kadhalika biashara yako haiwezi kufika mahali ambapo haujaijenga mifumo ili ifike hapo. Kuna mifumo mingine huwezi kuijenga wewe mwenyewe, ila inaweza kujengwa na wadau, au wawekezaji katika wazo lako la kibiashara, ama serikali kupitia sera zake mbalimbali ili kujenga mazingira bora ya kibiashara kwa ujumla katika nchi au katika eneo lako la kibiashara.

Je unafuatilia huu ugunduzi wa dawa ya kolona duniani? Ukifuatilia aliyegundua dawa husika, mahali alipo, na watu waliyesimama nyuma yake, utaweza kujua k**a atakuwa na biashara ya kuuza dawa ulimwengu mzima au k**a atawauzia wanakijiji wenzake tu na ndugu zake k**a mmachinga wa barabarani. Inabidi tuamke na tuanze kujifunza jinsi ya kufanya biashara na dunia, na kwa viwango vya dunia, na kwa kasi ya dunia! Tanzania bado hatujawa na makampuni makubwa ya kutoa fedha rundo kwa watu wenye mawazo mazuri ya kibiashara ya kubadilisha ulimwengu(global company). Kujenga mazingira hayo wezeshi na mifumo yake ni jukumu letu sisi sote. Hata kwa kusoma ujumbe huu ni mwanzo wa kujenga mazingira hayo. Kwa mfano leo ghafla bin vu, umegundua dawa ya kolona, lakini mpaka ujikusanye kusanye na kuweka dawa hizo katika viwango vya kisasa ili ziweze kufikia watu wengi, wa mbali na wa karibu, na kulinda haki zako miliki, pengine itakuchukua muda mrefu sana ambapo hata kolona yenyewe itakuwa imeshakwisha duniani. Ila kwa uwezo wako utaweza kuhudumia majirani zako na watu wa wilaya yako k**a alivyofanya babu wa Loliondo, lakini itakuwa ngumu kutengeneza kampuni ya kimataifa inayokusanya fedha dunia nzima k**a anavyofanya face book. Unajua ni watu wangapi walikufa kwenye foleni wakati wakisubiri kupata huduma ya babu wa Loliondo?

Imeandikwa “Ondoka uangaze kwa kuwa nuru yako imekuja, maana tazama giza litaifunika dunia, bali BWANA atakuzukia wewe…kwa kuwa wingi wa bahari utageuzwa kukujia, Utajiri wa mataifa utakuwasilia… Nitalegeza viuno vya wafalme ili kufungua milango mbele yako…Nami nitakupa hazina za gizani na mali zilizofichwa mahali pa siri…”(Isaya 60,45)
K**a unapenda kujifunza zaidi kuhusu somo hili, Mimi Joseph Mayagila(Mkurugenzi wa Fanikiwa journalism School Arusha), Nimeandika kitabu chenye kurasa 50, chenye kichwa KUBUNI BIASHARA IKUPASAYO. Nitakuuzia kitabu hiki kwa mkopo wa siku 30, kwa bei ya shilingi elfu tano(5000/=). Kitabu hicho nitakutumia kwa whatsap au kwa email yako katika mfumo laini(soft copy). K**a unahitaji kitabu hicho tuma neno KITABU KWA MKOPO kwa whatsap kwenda namba 0715 76 96 15, kisha utapata kitabu hicho baada ya dakika kumi tu ukisha kamilisha kujaza fomu maalum ya mkopo nitakayokutumia kwa whatsap.
Pia k**a unataka kupata kitabu hiki kwa kulipa taslim(cash). Tuma neno KITABU KWA CASH kwa whatsap kwenda namba 0715 76 96 15. Kisha nitakutumia kitabu hicho baada ya dakika 10. Kisha baada ya kukipokea kitabu hicho, ndipo utafanya malipo.
KARIBUNI TUNOE VICHWA KATIKA KIPINDI HIKI CHA KORONA ILI TUBUNI BIASHARA ZAIDI!

10/02/2020

Photos from Fanikiwa Journalism School - FJS's post

29/01/2020
25/01/2020

www.fjs.ac.tz 0756508071

10/01/2020

Karibu Fanikiwa Journalism School, maombi ya kujiunga na chuo kwa muhula wa March 2020 yanapokelewa January mpaka February 20, 2020
Pakua application form kupitia www.fjs.ac.tz
0756508071

25/12/2019
29/11/2019

Mkulugenzi wa Shirika la Marekani la On Eagle Wings Inc, Juliana Kitenge akitoa mada kuhusu kuandika habari za Kansa kwa wanafunzi hapa Fanikiwa Journalism School. Leo ni siku ya maveterani (waliosoma hapa chuoni miaka iliyopita).
Asante sana On Eagle Wings Inc. kwa udhamini wenu

29/11/2019

Karibu Fanikiwa Journalism School Arusha, muhula mpya unaanza March 15, 2020.
Pakua (download application form) form ya maombi kupitia www.fjs.ac.tz
0757508071

22/11/2019

Mahafali ya 12 ya Fanikiwa Journalism School leo November 22, 2019.
Karibu nawe utimize ndoto yako, muhula mpya ni March 15, 2020
www.fjs.ac.tz
0756508071

22/11/2019
21/11/2019

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na aliyewahi kuwa mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na mwandishi wa gazeti la Daily News, Ndugu Assah Mwambene, akitoa mada katika mhadhara kuhusu sheria za habari na jinsi ya kufanikiwa katika fani ya uandishi wa habari hapa chuoni Fanikiwa Journalism School

13/11/2019
04/11/2019

Karibu chuo bora cha uandishi wa habari, utangazaji na uaandaji wa vipindi vya radio na TV.
Uasjili unafanyika November 01 - 10, 2019, pakua (download) application form kupitia www.fjs.ac.tz
0756508071

30/10/2019

Karibu Fanikiwa Journalism School, chuo bora cha uandishi wa habiri, utangazaji na uandaaji wa vipindi vya Radio na TV. Muhula mpya unaanza March 15, 2020. Tunaanza kupokea maombi January 2020

www.fjs.ac.tz
0756508071

28/05/2019

Leo tumetembelewa na Mh Job Ndugai speaker wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Karibu bandani kwetu ujionee tunavyotoa mafunzo kwa vitendo...
www.fjs.ac.tz
0756508071

28/05/2019

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Professor Joyce Ndalichako katika banda la Fanikiwa Journalism School kwenye maoneso ya vyuo vya kati na vikuu Jamhuri Stadium Jijini Dodoma.

www.fjs.ac.tz
0756508071

27/05/2019

Karibu ushuhudie tunavyo toa mafunzo kwa vitendo, tupo banda #17 Jamhuri Stadium Dodoma May 27 - 31, 2019 Faninkiwa Journalism School

www.fjs.act.tz
0756508071

26/05/2019

Karibu banda namba 17 Fanikiwa Journalism School kwenye maonesho ya vyuo vya kati na vyuo vikuu uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma (May 27 - 31, 2019).
#0756508071 www.fjs.ac.tz

06/04/2019

Karibu Fanikiwa Journalism School kwa mafunzo bora ya uandishi wa habari, utangazaji na uandaaji wa vipindi vya Radio na TV

Dowload application form kupitia www.fjs.ac.tz

31/01/2019

Karibu Fanikiwa Journalism School kwa mafunzo bora ya uandishi wa habari na utangazaji wa Radio na TV. Muhula mpya was masomo inaanza March 05, 2018

16/01/2019

Fanikiwa Journalism School - FJS

14/08/2017

Arusha Journalism Training College chuo bora cha uansidhi wa habari na utangazaji.. Tunakukaribisha kwa mwaka wa masomo 2017/2018 unaoanza September 2017.. Tembelea website yetu www.ajtc.ac.tz au 0756508071 au 0789508071

31/07/2017

ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLLEGE (AJTC)
KILICHOPO ARUSHA KWAMROMBOO
REG./PWF/045

Mkuu wa chuo cha AJTC - anatangaza nafasi za masomo katika ngazi ya Astashahada (Certificate) na Stashahada (Diploma) kwa muhula utakaoanza tarehe 20/09/2017

Kozi zinazotolewa:-
1. Cheti cha awali cha uandishi wa habari (Basic Technician Certificate in Journalism NTA Level 4),
2. Cheti cha Uandishi wa Habari na Utangazaji wa Redio na TV (Technician Certificate in Journalism, NTA Level 5)
3. Diploma ya Uandishi wa Habari na Utangazaji wa Redio na TV (Ordinary Diploma in Journalism, NTA level 6)


SIFA ZA MWOMBAJI
(A) ASTASHAHADA (CERTIFICATES)
Mwombaji awe amehitimu kidato cha nne na kufaulu angalau masomo manne (4) kwa alama D.

(B) STASHAHADA (DIPLOMA)
Mwombaji awe amehitimu kidato cha sita na kufaulu angalau masomo mawili (2) kwa principal pass moja na subsidiary moja. (yaani nanagalau E moja na S moja)
AU
Mwombaji awe na cheti (Certificate) cha kozi anayoomba au inayofanana na hiyo anayotaka kusoma toka chuo kinachotambulika na serikali.

Maombi yatumwe moja kwa moja chuoni kabla ya tarehe 20/08/2017 (aambatanishe na index number, mwaka aliofanya mtihani, tarehe ya kuzaliwa, na tsh 20,000). Chuo kimesajiliwa na NACTE kwa jina Arusha Journalism Training College

Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba
0756508071 au 0763201585 au 0659715770 au 0755780131 Application form zinapatika chuoni na kwenye website yetu www.ajtc.ac.tz

Videos (show all)

Karibu Fanikiwa Journalism School

Location

Category

Telephone

Address


Arusha,Tanzania
Arusha
PO BOX 15689, ARUSHA TANZANIA

Opening Hours

Monday 07:00 - 18:00
Tuesday 07:00 - 18:00
Wednesday 07:00 - 18:00
Thursday 07:00 - 18:00
Friday 07:00 - 18:00
Saturday 07:00 - 18:00
Other Schools in Arusha (show all)
Upendo Friends School Upendo Friends School
Mateves-Kisongo
Arusha, +255 784 398099

Arusha Wisdom Trainning College Arusha Wisdom Trainning College
13886
Arusha, MOLLEL HOUSE,THIRD FLOOR,ROOM NO 104

Briefly Arusha Wisdom Training College is the largest trainer in the heart of Arusha city in Tanzania.

ESAMI ESAMI
Njiro Hill
Arusha

The Eastern and Southern African Management Institute (ESAMI) is an intergovernmental regional management training and development centre.

Yakini Schools Yakini Schools
PO Box 1134
Arusha

Yakini School was established in 2008. In 2013, the school as over 300 students, with classes starting from Baby Class up to Class 7.

New Vision Mereran School New Vision Mereran School
Arusha

a School based at Mireran in Sima Njiro District. A school that helps the maasai communities living in the area less fortunate/orphans/single parent HIV

Mother Oda Vocational Training Center Mother Oda Vocational Training Center
80
Arusha, 80

TAARIFA MBALIMBALI KUHUSU CHUO, CHA UFUNDI STADI MOTHER ODA

Cheka School Cheka School
Kiranyi, Sakina
Arusha

Cheka School is a free English and Swahili medium nursery and pre-primary school for the children of the Kiranyi area of Sakina. http://chekaschool.com/

Tanzania Adventist Secondary School - TASS Tanzania Adventist Secondary School - TASS
Arusha, P.O.BOX 737, USA-RIVER

Tanzania Adventist Secondary School is owned and operated by the North East Tanzania Conference of Seventh-day Adventist Church.

Islong Pre & Primary Schools Islong Pre & Primary Schools
Ngaramtoni
Arusha, P.O.BOX 2485

Islong pre & primary schools

Kilima Music Academy. Kilima Music Academy.
Njiro
Arusha, 255

An Institution that looks to encourage its learners in the Music discipline, through Music education and opportunities for International qualifications.

St Constantine's International School - Town Campus St Constantine's International School - Town Campus
Serengeti Road
Arusha

St Constantine's International School - Town Campus - is a small school that follows the Cambridge International Primary Program. We are located in the centre of Arusha Town next to Barclay's Bank.

Capricorn Institute Of Technology Capricorn Institute Of Technology
14931
Arusha, 255

Capricorn institute of technology,the college that understands you...karibu uone madanikio kwa haraka bila kujali umri.