18/01/2022
Habarin wazazi na walezi, watoto huwa katika wakati mgumu sana baada ya matokeo kutoka... Ukiwa k**a mzazi, pesa uliyotoa miaka 4 ni kweli inauma sana na hasa ukifikiria ulivyojinyima kulipa ada..
Usichukue maamuzi ya kumpiga mtoto au kumsemea maneno mabaya. Hii hupelekea watoto wengine kutoroka nyumbani au kuchukua maamuzi ya kujiua. Hiyo ni hasara kubwa sana kwa wazazi. Nawasihi sana omba Mungu kwanza baada ya kupata majibu/matokeo mabaya ya mtihani wa mtoto wako, kisha yakubali na mshukuru Mungu..
Nimegundua kuwa watoto hupitia wakati mgumu sana wakati wa mItihani. Kuna maroho ya kipepo huzunguka kuharibu hatima za watoto wetu. Usimlaumu mtoto hujui alikutana na nini katika chumba cha mtihani. Wengine hupata hofu ya ajabu hata kupoteza ujasiri wa kujibu mitihani, mwingine anasahau, na majibu anayajua na mwingine anaugua ghafla katikati ya mtihani.
Nawashauri wazazi.
1. Mtie moyo mtoto wako kumwondolea maumivu ya kufeli. Usionyeshe ukali, hasira, lawama au kejeli kwani inaweza kumsababisha kujiua, kuingia kwenye madawa ya kulevya, bangi na tabia mbaya akidhani anapoza machungu kumbe ndo anaharibu na kupotea zaidi..
2. Mwambie maneno ya matumaini kuwa anaweza kufanya vizuri tena. Kwa kipindi hiki usimruhusu kwenda kijijini au kwa ndugu wengine kwa ajili ya kupoteza mawazo.. No kaa naye mpaka hapo baadaye. Wengine huwapeleka kwa bibi. Hapana usijaribu kufanya hilo kosa..
3. Mwambie unampenda sana na muonyeshe kuwa imetokea haikuwa malengo yake.. Muonyeshe kuwa anaweza tena..
4. MUonyeshe uko tayari kumsaidia ili asonge mbele hata k**a kwa wakati huo unaona huna pesa Kabisa...
Usionyeshe kumkatia tamaa au haupo tayari kuendelea kupoteza pesa zako tena..
5. Muombee na umkumbatie baada ya maombi. Endelea kumwombea tena na tena.
6. Kwa siku kadhaa muonyeshe upendo mkubwa sana ikiwezekana mletee hata zawadi.. Usikubali kumpoteza mtoto wako sababu ya matokeo maana matokeo anaweza kuyatafuta tena, ila mtoto akipotea kwa kujiua hutampata tena.
Happylife iko tarayari kushirikiana na wewe kumpa muelekeo mtoto wako tupigie. #0768043682