Iaa_tz

Iaa_tz Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Iaa_tz, College & University, Arusha.

Institute of Accountancy Arusha is a Public Owned Institute offering courses in Accountancy, Finance, Banking, Computing, Procurement and Other business courses in levels from Certificate, Diploma, Bachelor and Masters Degree

Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Tanga wakipata elimu walipotembelea Banda la chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA) Katika Maad...
16/08/2026

Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Tanga wakipata elimu walipotembelea Banda la chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA) Katika Maadhimisho ya Wiki ya Elimu,Ujuzi na Ubunifu Kitaifa Tanga.

Aidha tunawakaribisha watu wote waendelee kutembelea Banda letu ili kupata taarifa mbalimbali kuhusu IAA.

Dirisha la Maombi kwa ngazi ya Cheti (Certificate), Stashahada (Diploma) na Shahada ya Uzamili (Master’s Degree)liko wazi.

Karibu tukuhudumie.

Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) tunashiriki maadhimisho ya Wiki ya Elimu,Ujuzi na Ubunifu Kitaifa Tanga ambayo  yameanza t...
15/08/2026

Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) tunashiriki maadhimisho ya Wiki ya Elimu,Ujuzi na Ubunifu Kitaifa Tanga ambayo yameanza tarehe 15 Agosti 2026, katika viwanja vya shule ya sekondari Usagara Tanga.

Tunawakaribisha Wanafunzi,Wazazi na wadau mbalimbali wa Elimu kuendelea kutembelea Banda letu ili kupata taarifa zaidi kuhusu programu zetu za masomo, na fursa mbalimbali zitolewazo na chuo.

Dirisha la Maombi kwa Ngazi ya Cheti (Certificate), Stashahada (Diploma) na Shahada ya Uzamili (Master’s Degree) liko wazi.

Karibu Tukuhudumie
Iaa Nextlevo

DC MAGOTI ATEMBELEA BANDA LA IAA KIZIMKAZI FESTIVALMkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Mhe. Petro Magoti ametembelea...
13/08/2026

DC MAGOTI ATEMBELEA BANDA LA IAA KIZIMKAZI FESTIVAL

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Mhe. Petro Magoti ametembelea banda la Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA) katikaTamasha la Kizimkazi (Kizimkazi Festival) visiwani Zanzibar.

Mhe. Magoti amepongeza kazi kubwa inayofanywa na chuo katika kuandaa wataalam wenye maarifa na ujuzi wa kisasa, akisisitiza kuwa mchango wa IAA ni wa thamani kubwa katika kujenga taifa imara kiuchumi na kielimu.

Aidha, Mhe. Magoti amesema anathamini nafasi ya IAA katika kuimarisha rasilimali watu na kuendeleza elimu bora nchini Tanzania.

Tunawakaribisha wanafunzi, wazazi, walezi, wadau wa elimu na wananchi kwa ujumla kuendelea kutembelea banda lake ili uweze kupata taarifa zaidi kuhusu programu zetu za masomo, fursa za kujiunga na huduma mbalimbali zitolewazo na chuo.

Dirisha la Maombi kwa ngazi ya Cheti (Certificate), Stashahada (Diploma) na Shahada ya Uzamili (Master's Degree) liko wazi.

KARIBU IAA TUKUHUDUMIE.

KARIBU BANDA LA IAA  KIZIMKAZI FESTIVAL 2026Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) tunashiriki katika Kizimkazi Festival inayofan...
13/08/2026

KARIBU BANDA LA IAA KIZIMKAZI FESTIVAL 2026

Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) tunashiriki katika Kizimkazi Festival inayofanyika Kizimkazi, Zanzibar. Tunakukaribisha kutembelea banda letu ili uweze kupata taarifa zaidi kuhusu programu zetu za masomo, fursa za kujiunga, na huduma mbalimbali zinazotolewa na Chuo.

Dirisha la maombi kwa ngazi za Cheti (Certificate), Stashahada,(Diploma) na Shahada za Uzamili, (Master's Degree) liko wazi.

KARIBU TUKUHUDUMIE

11/08/2026

KUELEKEA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UTALII 2026

Katika kuadhimisha Siku ya Utalii Duniani Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kimeandaa Kongamano la nne la Kimataifa la Utalii litakalofanyika tarehe 25 Septemba 2026 katika Hoteli ya Gren Melia jijini Arusha.

Tunawakaribisha wataalam, watafiti, wawekezaji, taasisi za umma na binafsi na wadau wote wa utalii kushiriki kongamano hili, ambalo litahusisha mijadala ya masuala muhimu yanayohusu maendeleo endelevu ya utalii, ubunifu, matumizi ya teknolojia, ushirikishwaji wa jamii, fursa za uwekezaji na maendeleo ya sekta ya Utalii nchini.

Kauli Mbiu ya Kongamano hilo ni: "Digital Agenda and Artificial Intellegence to Redesign Tourism". Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana nasi kwa namba 0784263942.

IAA YANG’ARA TUZO ZA TEHAMA 2026Mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Imani Penza ameibuka mshindi katika kipenge...
10/08/2026

IAA YANG’ARA TUZO ZA TEHAMA 2026
Mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Imani Penza ameibuka mshindi katika kipengele cha ICT Business Leader kwenye Tuzo za TEHAMA 2026 huku kampuni na miradi inayohusishwa naye ikifanya vizuri katika vipengele mbalimbali na kuipa IAA jumla ya tuzo nne katika makundi hayo.

Tuzo hizo zilizotolewa Agosti 09 2026 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angella Kairuki

Penza, ambaye ni Mwanzilishi wa Shamba Direct na CABO GROUP, ameshinda tuzo ya ICT Business Leader huku Shamba Direct ikiibuka mshindi katika kipengele cha 'Digital Entrepreneurship Initiative' .

Aidha, 'Elimu Space' imepata nafasi mbili katika tuzo hizo, ikishika nafasi ya pili katika 'Digital Entrepreneurship Initiative' na nafasi ya tatu katika 'Digital Business Innovation'

Penza ameeleza kuwa mafanikio hayo yamechangiwa na mazingira wezeshi, mwongozo na fursa zinazotolewa na 'IAA Business Startup Centre' kupitia programu na usaidizi unaolenga kuwawezesha wanafunzi kukuza bunifu, mawazo yao na kuyabadilisha kuwa miradi na biashara zenye uwezo wa kuleta matokeo chanya.

IAA inaendelea kuhamasisha wanafunzi kutumia fursa zinazotolewa kupitia IAA Business Startup Centre ili kukuza mawazo mapya, kuanzisha biashara bunifu na kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

MWANAFUNZI IAA AIBUKA KINARA TUZO ZA TEHAMA 2026 KATIKA UTAFITIMwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Rahmani Mbahe...
10/08/2026

MWANAFUNZI IAA AIBUKA KINARA TUZO ZA TEHAMA 2026 KATIKA UTAFITI

Mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Rahmani Mbahe amefanya vizuri katika Tuzo za TEHAMA 2026 baada ya kushika nafasi ya pili katika kipengele cha 'Best Innovation Research Award' akionesha uwezo katika ubunifu na utafiti unaotumia TEHAMA kutengeneza suluhisho zenye tija.

Tuzo hizo zimetolewa tarehe 9 Agosti 2026 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angella Kairuki, ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuhamasisha ubunifu, utafiti na matumizi ya teknolojia katika maendeleo ya jamii na uchumi.

Mafanikio ya Mbahe ni sehemu ya matokeo ya juhudi za IAA Business Startup Centre, ambayo imekuwa ikitoa mazingira wezeshi, mwongozo na fursa kwa wanafunzi wa IAA kukuza mawazo yao ya ubunifu, utafiti na ujasiriamali na kuyabadilisha kuwa miradi yenye uwezo wa kutatua changamoto za jamii.

Kupitia IAA Business Startup Centre, wanafunzi wamekuwa wakipata fursa za kuendeleza mawazo yao, kupata ushauri na kuandaliwa kushiriki katika majukwaa mbalimbali yanayotambua ubunifu na matumizi ya TEHAMA.

IAA inaendelea kuwataka wanafunzi kutumia fursa zinazopatikana kupitia IAA Business Startup Centre; ili kuendeleza ubunifu, utafiti na mawazo ya kibiashara na kuyafikisha katika hatua ya utekelezaji.

IAA YAIBUKA KIDEDEA  TUZO ZA TEHAMA 2026, UHIFADHI MAZINGIRAMwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Abdulswamad Azh...
10/08/2026

IAA YAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA TEHAMA 2026, UHIFADHI MAZINGIRA

Mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Abdulswamad Azhary ameshika nafasi ya pili katika kipengele cha ICT for Environmental Conservation kwenye Tuzo za TEHAMA 2026, akitambuliwa kwa ubunifu na matumizi ya TEHAMA katika kusaidia uhifadhi wa mazingira.

Tuzo hizo zilizotolewa tarehe 9 Agosti 2026 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angella Kairuki kutambua vijana, watafiti na wabunifu wanaotumia teknolojia kutengeneza suluhisho kwa changamoto mbalimbali za kijamii na kimazingira.

Ushindi wa Azhary ni matokeo ya mazingira ya ubunifu yanayoendelezwa na 'IAA Business Startup Centre' na ushahidi wa uwezo wa wanafunzi wa IAA katika kutumia TEHAMA kwa ajili ya kulinda mazingira na kuchangia maendeleo endelevu.

IAA inaendelea kuhimiza wanafunzi, watafiti na wabunifu kutumia fursa zinazopatikana kupitia IAA Business Startup Centre kuendeleza mawazo yao, kufanya utafiti na kuanzisha ubunifu unaoweza kutatua changamoto na kuleta mabadiliko chanya katika jamii na mazingira.

BACHELOR DEGREE IN ECONOMICS AND PROJECT MANAGEMENT➡️ The bachelor degree in economics and project management is designe...
10/08/2026

BACHELOR DEGREE IN ECONOMICS AND PROJECT MANAGEMENT

➡️ The bachelor degree in economics and project management is designed with the focus of producing graduates with the necessary skills and knowledge in the fields of economics and project management.

➡️ Graduates are expected to have high expertise in handling profound aspects of economics and social development through formulating sound economic plans and policies as well as implementing them, be insightful problem solvers, and be critical thinkers.

➡️ Furthermore, he or she should be able to make dynamic judgments, empirically test, and adapt economic and project management models to complex economic and project management models.

➡️ The graduate must be able to apply the theories and practices learned to disentangle complex economic and project management challenges with the focus of advancing the industrialized economy and the well-being of the people.

Minimum Entry Qualifications:
➡️ Form Six (VI)
Two principal passes in the following subjects: Economics, Accountancy, Commerce, Physics, Chemistry, Biology, Agri culture, Geography, History or Advanced Mathematics with an aggregate of four
points obtained from the scoring: A=5, B=4, C=3, D=2,
E=1, S=0.5, F=0

➡️ NTA LEVEL 6
Diploma in Economics and Project Management, Project Planning and Management, Finance, Accountancy, Taxation, Procurement or Insurance with an average of “B’’ or a minimum GPA of 3.0. or Foundation Programme of the OUT with a minimum GPA of 3.0.

➡️ This programmes available at our Arusha Campus

➡️ Apply online now using the link on the poster above, or send your details through WhatsApp at 0742833444.

Welcome to IAA!

MAONESHO YA NANENANE 2026 YAHITIMISHWA.Chuo Cha Uhasibu Arusha-IAA chenye makao yake makuu jijini Arusha kimeshiriki kik...
08/08/2026

MAONESHO YA NANENANE 2026 YAHITIMISHWA.

Chuo Cha Uhasibu Arusha-IAA chenye makao yake makuu jijini Arusha kimeshiriki kikamilifu kwenye maonesho ya Nanenane Kanda ya Kaskazini yaliyokuwa yanafanyika katika viwanja vya Themi-Njiro na kuibuka mshindi wa tatu katika kundi la Taasisi za Elimu na Mafunzo.

IAA kuibuka mshindi wa tatu katika kundi hilo la taasisi nyingi za elimu na mafunzo, ni ishara tosha kuwa chuo kimeendelea kuonesha ubora na ubunifu katika utoaji wa elimu inayokidhi na kuendana na mahitaji ya soko la ajira.

Aidha, IAA inaendelea kuwakaribisha wanafunzi wote wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu, kujiunga na programu za astashahada, stashahada, shahada na shahada ya uzamili kwa mwaka wa masomo 2026/2027.

Maonesho ya Nanenane kwa mwaka 2026 yalikuwa na kaulimbiu "TAMBUA SOKO, ONGEZA TIJA, KUTEKELEZA DIRA 2050"

Address

Arusha

Telephone

+255742833444

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Iaa_tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share