10/08/2021
DALILI ZA CYBERATTACKS KATIKA MAGARI YANAYOTUMIA UMEME.
K**a nilivyosema katika post iliyopita kuwa ni kweli magari yanayotumia umeme yanaweza kudukuliwa na kusababisha madhara makubwa.Miaka ijayo yatakuwa ni sehemu ya maisha yetu ila changamoto kubwa tutakayokabiliana nayo ni cyberattackers.
Mpaka sasa kuna taarifa nyingi tu zinazoelezea matukio ya udukuzi wa magari ya umeme unaoendelea katika mataifa makubwa mfano nchini Marekani moja ya magari yanayotengenezwa na kampuni ya TESLA yanayofahamika k**a Tesla model x yalidukuliwa na si mara moja kwa magari hayo kudukuliwa. Lakini pia nchini Israel katika chuo cha ben, walifanya uchunguzi wa magari hayo kwa kubadilisha tu mfumo wa picha na alama za barabarani na mwisho wa siku gari walilolifanyia jaribio hilo lilipoteza mwelekeo.
Wataalamu wa teknolojia ya magari haya wamekuwa wakitoa tahadhari kubwa kwa watumiaji kuhusu uhalifu huu ambao unaweza kupelekea maisha yao kuwa hatarini.Bwana Jin Ye ambaye ni mtaalamu wa magari na teknolojia aliwahi kutoa viashiria viwili vikuu vitakavyomfanya mtu kutambua kuwa gari lake limeingiliwa na cyberattackers (wadukuzi/ hackers).
Kwanza kabisa charge ya gari huwa inaisha kwa muda mfupi sana.Cyberattackets wanauwezo wa kupunguza uwezo wa charge ya gari kwa 50% kwa kutumia mbinu za kisasa hivyo basi unapohisi charge ya gari lako inapungua kwa haraka basi anza kufanya uchunguzi.
Pili speed ya gari hupungua na kuwa ndogo sana pale unapokuwa barabarani.
Hivi ni viashiria viwili vikuu vitakavyokufanya uhisi kuwa mfumo wa ulinzi wa gari yako wajanja wameuingilia.
Lakini pia hata katika vituo vya hadhara vya kuchaji navyo pia vipo hatarini kuingiliwa na wajanja hawa.
๐Like
๐Follow