03/03/2026
🌙 Makosa ya Wazazi Ramadhani ⚠️
🌱 Epuka kunafanya makosa haya kwa watoto wako ndani ya mwezi mtukufu wa Ramdhani ✨
Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni fursa ya malezi bora kwa watoto. Hata hivyo, wazazi wengi wanakosa hatua muhimu:
1️⃣ Kutojumuisha Kiimani
Watoto wanakula sahur(daku) na iftar bila kuelewa dua na shukrani.
💡 Dondoo: Somesha dua fupi kabla ya kula. Fanya pamoja!
2️⃣ Kutozingatia Ratiba na Nidhamu
Hakuna schedule ya ibada, kusoma Qur’an, au muda wa kujifunza.
💡 Dondoo: Weka ratiba rahisi, rahisisha mtoto kufuata.
3️⃣ Kuzingatia Chakula Zaidi ya Malezi
Chakula kizuri, lakini mtoto haelewi maadili ya Ramadhani.
💡 Dondoo: Shirikisha mtoto kuandaa chakula, soma dua pamoja, fundisha shukrani.
4️⃣ Kutochukua Muda wa Familia
Iftar bila familia, hakuna hadithi za Kiislamu, hakuna mazungumzo ya malezi.
💡 Dondoo: Fanya iftar na familia, soma hadithi, uliza maoni ya mtoto.
5️⃣ Kudumisha Tabia Mbaya
Wazazi wanavumilia tabia mbaya bila kufundisha jinsi ya kurekebisha.
💡 Dondoo: Pongezi tabia njema, elezea adhabu kwa upendo, si hasira.
✨ Ramadhani si tu kufunga, bali kujenga tabia, kiimani na maadili