01/03/2024
BILA USU ADUI MBUSU
Makau na Mutua waliwasili jijini Mwambao kwa kishindo kikubwa. Ni siku ambayo kwao , hawangeweza kuitia kapuni kuche kusiche. Waliisubiri kwa hamu na hamumu k**a vile Waislamu hungojeavyo mwezi Kongo wa Ramadhani. Hapo awali , walikuwa wameyasikia mengi kuhusu Jiji hilo la kitalii. Si fukwe za bahari, Ngome ya Yesu almaarufu Fort Jesus, Kivuko cha Feri, Daraja la Kuelea baharini, Hoteli za kifahari na mengi mengineyo. Hayo pamoja na mengi , yaliwapa ari na ghera ya kutaka kulizuru jiji hilo. Leo wamelifika, Wana raha k**a Paka aliyeachiwa kitoweo kukilinda. Vicheko vya aiskirimu vinayeyusha vidu mashavuni. Makau alikuwa tayari ashaijua lafudhi ya pwani.
Walivuka Feri Kisha wakaabiri matwana kuelekea Lunga Lunga, huko wangekuwa mwenyeji wa rafiki yao wa dhati Kasolo. Kasolo aliwakaribisha kwa upwamu na kwa vyakula vya kipwani k**a vitumbua , kaimati , bajia , kashata , biriani na kadhalika. Mutua alisikika akiapa kutorudi tena Ukambani kutokana na mlo huo mtamu ushindao wa uki wa mfalme nyuki.Makau alipomwona Mwanakombo akipita ,alistaajabu k**a mja aliyemwona Osama mwenye uhasama usiokoma hadi siku ya kiama.Mwanakombo alikuwa bintiye Omari Sharif.Mtoto wa wenyewe aliumbwa akaumbika ,alihulukwa akahulukika,ungedhani ni malaika aliyetoroka mbinguni. Akimwaga hamsini barabarani na kumwacha Makau Kinywa achama kiasi cha nsi kupenya na kupamba makao koromeoni.
Ni bayana kuwa mabinti wengi mtaa huo walikuwa wa kuwatoa waume uderere. Mutua na Makau walishindwa wachague yupi na wamwache yupi. Lakini walipokuwa wakipigwa mandarin kujionea mandhari ya Lunga Lunga, waliokuja kujionea mbuzi waliokuwa wakilala barazani nje ya maduka kila kulipokuchwa. Asubuhi, wangeraukia marikiti na kula chochote walichokipata. Mutua na Makau walishangaa sana jinsi watu wa pale Lunga Lunga walivyokuwa zuzu kwani kwao mbuzi hao walikuwa kitegauchumi. Hawakujua kuwa , jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza kinene.....
Kiswahili kivume,
Kwa hisani ya mwalimu George