02/12/2023
KAZALIWA MOINA
Ukimwita nyangorii, moina tamwita mimi
Kimwita hata wikii, tabaki na moina mi
Kijaribu moinani, moina tabaki nami
Kazaliwa moinaa, mbili kumi na mbilii
Kajiita profesaa, jina hilo la utani
Kati mwengine pasta, kiwa hata mzahani
Hayo yote akiitwa, tampa raha moyoni
Kazaliwa moinaa, mbili kumi na mbilii
Yote hayo nayaacha, na kulenga kwenye mada
Ya heri ya kuzaliwa, siku yako profesaa
Uanzapo huu mwaka, wa baraka na faraja
Kazaliwa moinaa, mbili kumi na mbilii
Mema yakutendekee, kwa wema ulionao
Heri afya ya pekee, ni la kwangu ombi kwako
Ndoto zote zitimie, kihimili shida zako
Kazaliwa moinaa, mbili kumi na mbilii
Nahisi bahati kubwa, kuwa nawe moinani
K**a rafiki mkubwa, kote kwangu maishani
Siku hi ya kuzaliwa, ikupe nachotamani
Kazaliwamoinaa, mbili kumi na mbilii
Niruhusu niuweke, awinoo wino wangu
Jamvi na likunjike, siku hii maalumu
Ngiapo kwenye uzee,na awe nawe munguu
Kazaliwa moinaa,mbili kumi na mbilii
πππππππππππππππππππ
Jibambe boyπ»
Send a message to learn more