Kiswahili kitukuzwe

Kiswahili kitukuzwe Kikiangazia Kiswahili Kwa ufasaha na utendeti wa hali ya juu iwezekanavyo.

13/12/2019

JE SAMAKI HUNYWA MAJI?

Nauliza nijibiwe,mwenzenu nione raha
Langu jibu nipatiwe,nasaka yenu nasaha
Kwa swali msikerewe,naapa sina mzaha
Nauliza nijibiwe, je samaki hunywa maji?

Nauliza nijibiwe,je samaki hunywa maji
Pia nami nitambuwe,nijivishe langu taji
La ukweli nilijuwe,niwapiku wajuaji
Nauliza nijibiwe,msafiri nije jua

Nauliza nijibiwe,msafiri nije jua
Samaki niwaelewe,nipate kuwatambua
Midomo siwapanuwe,kwa kijiko kuwapea
Nauliza nijibiwe,maji huyanywea vipi?

Nauliza nijibiwe,maji huyanywea vipi?
Moyo wangu unituwe,nijue taaza wapi
Nimewafuga mwenyewe,sijui nifanye lipi
Nauliza nijibiwe,si ujinga kuuliza

Nauliza nijibiwe,si ujinga kuuliza
Naona bora wapewe,wasitete kawabeza
Makini nish*takiwe,zao haki kapuuza
Nauliza nijibiwe,mwenye jibu alitoe

Nauliza nijibiwe,mwenye jibu alitoe
Kesho nisisingiziwe,kama kosa nikosoe
Narai haki wapewe,na maji niwapatie
Nauliza nijibiwe,Msafiri nifahamu

Nauliza nijibiwe,Msafiri nifahamu
Kwa bayana niambiwe,kujua ninayo hamu
Kinishe na kiwewe,nitulie kiwa humu
Nauliza nijibiwe, Je samaki hunywa maji?

Msafiri Makini
Mugendi Mutegi

Address

Iddmgandi370mariakani
Nakuru

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kiswahili kitukuzwe posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Kiswahili kitukuzwe:

Shortcuts

Share

Category