16/07/2026
CHETI HALALI CHA NIKAHA KATI YA SHEIKH WALID NA BELLA CHAONEKANA !
🇹🇿 Dar es Salam, Tanzania // Cheti cha ndoa ya halali kati ya Sheikh Walid na mtalikiwa wake dada Bella kimepatikana .
Cheti Hicho kinamrejeshea hishma Sheikh Walid na kumwondolea lawama zilizoibuka mitandaoni kuhusu hishma ya Sheikh.....lawama zilizopelekea yeye kuvuliwa cheo chake cha Shekhe Mkuu wa mkoa wa Dar es Salam
Kwa mjibu wa cheti hicho, Sheikh Walid alimuoa mwanamke huyo kisheria na katika taratibu za Kiislamu tarehe 16-10-2024, ila alimtaliki baada ya miezi 3
Utata upo kwenye uhalisia wa mtoto...ambapo mwanamke huyo anadai ni damu ya Sheikh.....lakini Sheikh anapinga hilo na kusema mtoto huyo hatokani na yeye.
Sheikh amesisitiza lazima vipimo vya DNA/ vifanywe kubaini k**a kweli mtoto huyo ni damu yake, ila mwanamke huyo amekataa jambo hilo
Waraka huu wa nikaha utawaaibisha watu wanaotumia mitandao ya kijamii hasa tiktok, facebook na YouTube kumpaka tope Sheikh kuwa alienda kinyume na maadili
Cheti hiki aidha kimeiletea fedheha kuu Bakwata.
Waislamu wote nchini Tanzania wanaamini kuwa ugomvi wa mwanamke huyu na Sheikh ndio uliopekekea Bakwata kumvua cheo cha Sheikh Mkuu wa mkoa, Shekhe Walid.
Sasa ni wazi kuwa Sheikh hakufanya uchafu na mwanamke huyo....alikua mkewe wa halali
Hivyo wanaotumia mitandao ya kijamii kumtia doa Sheikh Walid... tafadhali, komeni, Sheikh ni msafi k**a pamba
La zaidi mumuombe msamaha na maghfirah Mola wenu kwa kumchafulia jina na kumtuhumu vibaya na kumtia aibu Sheikh huyo.
Bella pia ni dada yetu mwislamu - anazo haki zake - lakini- amekosea kupeleka ugomvi huo mitandaoni.
Madhara yake yamekua makubwa kuliko faida yake
Angeendelea tu kutafuta haki kupitia vyombo vya sheria ila sio kuileta kadhia hii mitandaoni
Mimi binafsi nimeiona video yake akikana kuwa hakua ameolewa na Sheikh kisheria....walikua washikaji tu
Huu ni uongo !!
kausema tu ili amzalilishe Sheikh na kumtia aibu machoni mwa watanzania..
Ukweli ni kwamba huyu mwanamke ana hasira moyoni...
anayafanya haya makusudi k**a njia muwafaka kwake yeye kumpiga vita Sheikh, na kulipiza kisasi cha kutalikiwa.
Sababu ni kuwa...Sheikh alipomtaliki huyu dada hakuwa tayari kutalikiwa, alikua hataki atalikiwe...!!
Amesikika wazi wazi akisema bado anampenda Sheikh, ila Sheikh aliharakisha kumtaliki.....
Lakini yote tisa, kumi ndugu zangu watanzania....tuchungeni hishma ya Sheikh na dada huyo....kwani wote wawili Wana hasira hivi sasa
Sheikh amejizuia mno kuzungumzia kadhia hii na pia kumjibu dada huyo, ila eleweni dada huyo si msomi....anaweza kusema lolote au kuzua lolote muradi tu Sheikh apate aibu mbele ya watu
Hapa tunatazama haki mbili
1 - Haki ya Sheikh pamoja na kuilinda na kuchunga hishma yake, na huo ni wajibu wetu wa lazima katika kidini
2 - Kuichunga haki na hishma ya dada huyo hasa kwa kuzingatiwa ni mwislamu mwenzetu , tena amesilimu tu kutoka dini ya ukristo kwa ajili ya kuupenda uislamu
Dada huyo ana haki alindwe na kuhifadhiwa na waislamu wala si kuzomwa
Kwa hilo, hii ni kadhia ya mme na mke iliovuja na kuingia mitandaoni tu
Tusichukue mirengo mikali juu ya kadhia hii
Wallahi tumebanwa katikati ya haki mbili kuu mbele ya Mwenyeezi Mungu SWT
Mimi hapa naogopa tayari, hii kadhia nzito
Tumieni hikma sana tusijeni kutumbukizwa motoni kwa ajili ya kadhia hii, epukane sana jambo hili.
Tusitumieni mitandao ya kijamii kueneza habari za uongo kuwahusu, au kuwadhalilisha
Kwa sasa, wote wawili wanahitaji huruma na msaada wetu.
Tuwasitirini tu. 🙏🙏
Jamani waislamu, comment neno " Astaghfirullah ....! " ni Bora zaidi..... Afwan 🙏