12/02/2020
https://www.youtube.com/watch?v=tsQp0a5NcFk
Hujambo na karibu kwa mafunzo kuhusu program zote za adobe na
hii ni adobe swahili
usisahau kusbscribe.
Leo tutajifunze jinsi ya kuleta videos na kuunda mradi wa kwenye Adobe premier pro.
Mradi wa faili unaweza kujumuisha vitu kadha k**a; video, music, voice over, picha, graphics na pia animation files.
Wacha tuhamishe video clips chache ili tujifunze nazo jinsi ambavyo clips zimeunganishwa na Project file, nitakwenda kwenye Media browsing panel na nibrowse ‘4 hour media’, na kwenye media folder upande wa kushoto, utaona folda zote zilizo kwenye kompyuta yako na upande wa kulia utaona yaliyomo kwenye folda utakayochagua.
Sasa niko kwenye media files folder, na nitadouble click kwenye kipande hiki hapa ili ifunguke na kitafungua kwenye source monitor na kucheza filamu.
Ninaweza pia kuchukua hiki kifaa cha bluu kinachojulikana k**a playhead na kudrag kwa sehemu tofauti ya video, fahamu kwamba sina haja ya kubonyeza kwenye playhead ili kuisongeza, naweza tu kuibonyeza mahali ninapotaka iende.
PERSILAISYMAKENABD23
Ikiwa ninataka kuchagua clip hizi sita, nitaclick hapa, kisha niscroll chini kwa nikiwa nimeshikilia shift key na nichague clips hizo sita, kisha nitaright click kwa clip yoyote na kuchagua ‘import’, hii pia itaonekana kwenye project panel.
Uhamishaji wa clips huunda master clips katika Pro ambayo ni shortcut ya media file. Nitabonyeza project media panel na kudeselect clip hizi, unaweza kuona niko kwenye list view na nina information kuhusu clips hizi k**a vile idadi ya frames kwa sekunde ya clip na kadhalika.
Ninaweza pia kuhamia kwenye icon view kwa kubonyeza icon button kwenye kona ya kushoto,ni vizuri kufahamu icon view ni muhimu kwa sababu huonyesha picha ndogo ya clip.
PREMIERE pro inajua eneo la media files ambazo zimeunganishwa na clips, na ikiwa media file itasonga sehemu nyingine, utahitaji kuelezea Premiere pro kule ambapo hio media file iko. Ndani ya media files tunaweza kupanga video clips kwa kutumia folda maalum iitwayo Beans. Unaweza kuunda hizi Beans kwa kubonyeza button hii iliyo kwenye kona ya chini upande wa kulia mwa Project panel.
Nitaita hii 'Short' na kubonyeza kando ila jina hii ihifadhiwe, na ikiwa nitadouble click, itafunguka kwa frame yake yenyewe. Hapa utagundua kuwa, beans na project panel zina chaguzi sawa. Pia kuna shortcut ya kuhamisha clips kwa beans: Chagua clips tatu na uclick kwa clip ya kwanza, kwa kushikilia shift key, bonyeza kwenye clip ya mwisho na udrag sehemu hizi kwenye Bean button na sehemu hizo zitawekwa kwenye Bean na kuitwa 'Short 2', zimekua highlighted na ukidouble click utaziona.
Unaweza pia kuweka bean katika beans kwa kuselect hizi beans, kuhold shift key na kuzidrag kwenye bean button na kuita Bean mpya: ‘Media’, na nikidoube click utaona bean iliyo na beans ndani yake.
Nitachukua folda katika windows au Mac iOs, unabrowse kwenye media folder na nikibadilisha folda hizo majina, location za clip hizo zitabadilikia kwa sababu ya kubadilisha jina ya folda iliyo na clip hizo.
Kwa hivyo, nikirejea kwenye premiere pro, na utaona clips hizi zilipata alama za maswali na kwenda offline, na labda uliona kwamba PREMIERE pro ilipata media hizo na kuziunganisha tena. Ikiwa nitabonyeza moja ya haya, zitarejea kwenye skirini.
Nitamaliza kwa kufunga Beans hizi ili kuepuka beans hizo kuingia kwenye interface .
Nitarudi nyuma na ku-undo haya yote kwa kubonyeza crtl + z na nitapata media tena. Premiere Pro itakuuliza ni sehemu ipi umehamisha clips ikiwa ulizihamishia eneo tofauti kwa compyuta yako. Ikiwa hio itatokea, unaweza browse clips za kwanza ambazo hazipo na premiere pro itapata zingine.
Fahamu kua niki right click kwenye clip hizi, ninaweza kuzichagua na zifafanuliwe kwenye explorer, au finder k**a ningekua natumia software ya Mac iOs.
Hapa kuna clip ambayo iko highlighted na nitaiclick na kuita hii "trees" kisha kubonyeza mbali ili jina ihifadhiwe.
Nitakurudisha kwenye media na utaona kuwa filing haijabadilika, kumbuka kua clips zilizo ndani ya premiere pro ni viungo tu vya media files na sio faili za media zenyewe, kwa hivyo kubadili jina ya shortcut file haibadilishi faili za media zenyewe..
Kwa hivo hivyo ndivyo unahamisha media kwa project iliyo tayari ili uweze kuhariri katika Adobe Premiere Pro.
https://www.youtube.com/watch?v=tsQp0a5NcFk
Hujambo na karibu kwa mafunzo kuhusu program zote za adobe na hii ni adobe swahili usisahau kusbscribe. Leo tutajifunze jinsi ya kuleta videos na kuunda mrad...