04/01/2022
WAHUSIKA
Mzee Mago
Ni mzee anayemiliki mkahawa mshenzi. Watu huja mkahawani kunywa chai na kuzungumzia mambo muhimu yanayowahusu. Anahusika katika kutetea haki za wanyonge.
· Umuhimu: kielelezo cha watu wanaotetea haki za wanyonge katika jamii;
· Mpenda haki/mtetezi - hakupuuza ule uvumi bali alijaribu kuutafutia suluhisho.
· Mwenye bidii - shughuli ya kupigania na kuzuia mipango ya watu wakubwa sio rahisi. Ilibidi mzee Mago ajinyime, awatafute wenzake wazungumze na kulijadili jambo hili ambalo lilikuwa nyeti sana kwao.
· Mshawishi - aliwashawishi wanyonge wenzake watafute wanasheria waaminifu ili wasaidie kufafanua vipengele vigumu vya sheria k**a njia ya kuwavukisha vikwazo ili wapate suluhisho.
· Mzinduzi - aliwazindua wenzake na kuwapa nasaha kuhusu maendeleo. Aliwazindua kwamba maendeleo yanahitaji mchango wa kila mtu - wa k**e kwa wa kiume, wadogo kwa wakubwa n.k. Aidha, aliwatahadharisha kwamba wachunguze ni maendeleo gani yatakayowanufaisha.
· Mzalendo – anawanasibi wananchi wenzake wakubali maendleo yanayopiga hatua nchini mwao.
· Mwoga – anajawawa na wasiwasi anapozungumza na jitu lilokuja mkahawani (uk. 7).
Kabwe
Ni mmoja wa wenyeji wa Madongoporomoka. Tunampata mkahawani akifanya mazungumzo na kina Mago.
· Mshirika - alishirikianana wanyongewenzake katika kutafuta ufumbuzi wa kunyakuliwa kwa ardhi yao.
· Mtumainifu - anaamini kuwa sheria inaweza kuwa suluhisho la matatizo yao.
· Mpenda amani na haki - alitaka watafute suluhisho linalofaa kwa watu wa Madongoporomoka.
Bi. Suruta
· Ni hodari katikakutoahojakwenye mashauriano. Anawapiku wanaume wote.
Bi. Fambo
· Mwanamke mojawapo wa wanyonge.
· Ni mwelewa masuala ya unyanyasaji.
· Anaeleza bayana kwamba wakubwa hawajali wanyonge wakihamishwa kwenye ardhi watakwenda wapi.
Jitu la miraba minne
Ni jitu linalokuja mkahawani kula.
· Kubwa – ni dovu la mtu; lina shingo