29/09/2026
Meneja wa ICT wa Kundi la Habari la Alshifaa Ameshambuliwa na Kulazwa Hospitalini Baada ya Kuvamiwa na Watu Wanaosukiwa Kuwa Majambazi eneo la Kisauni.
Benedict Rading, alishambuliwa leo mwendo wa saa kumi na moja na nusu asubuhi (5:30 asubuhi) akiwa njiani kuelekea kazini na kundi la vijana takriban wanane waliokuwa wamejihami kwa panga katika eneo la Kisimani, kaunti ndogo ya Kisauni.
Rading amepata majeraha mabaya na hivi sasa anapigania maisha yake katika Hospitali Kuu ya Pwani (Coast General Hospital).
Vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na simu za mkononi, kompyuta mpakato/sanjari ya ofisini (tablet), na kitambulisho chake cha kitaifa vilichukuliwa na wavamizi hao.