Kulingana na Maandiko

Kulingana na Maandiko Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Kulingana na Maandiko, Dar es Salaam.

01/06/2025

MAMBO 10 AMBAYO MWANADAMU WA ASILI HAWEZI KUYAFANYA .

"MWANADAMU WA ASILI" ni mtu ambaye hajazaliwa upya au hajazaliwa kwa Roho Mtakatifu. Mtu huyu yuko katika hali ya kifo cha kiroho na ni mtumwa wa dhambi.

MWANADAMU WA ASILI HAWEZI;

1. HAWEZI KUELEWA UKWELI WA KIROHO

Rejea: 1 Wakorintho 2:14

Mwanadamu wa asili hawezi kuelewa mambo ya Roho kwa kuwa ni mambo ya kiroho.

2. HAWEZI KUMTAFUTA MUNGU

Rejea: Warumi 3:11

Hakuna mtu anayetafuta Mungu; mwanadamu wa asili hujiepusha na Mungu.

3. HAWEZI KUMPENDEZA MUNGU

Rejea: Warumi 8:8

Wale walio katika mwili hawawezi kumpendeza Mungu.

4. HAWEZI KUITII SHERIA YA MUNGU

Rejea: Warumi 8:7

Akili ya kimwili ni uadui kwa Mungu na haitii sheria yake.

5. HAWEZI KUFANYA MEMA YA KWELI (MEMA MBELE ZA MUNGU)

Rejea: Isaya 64:6, Warumi 14:23

Matendo mema bila imani hayakubaliki kwa Mungu; ni k**a matambara machafu.

6. HANA UHIARI WALA UTASHI WA KUMJIA KRISTO

Rejea: Yohana 6:44

“Hakuna awezaye kuja kwangu isipokuwa Baba aliyenituma amvute.”

7. HAWEZI KUWA NA IMANI IOKOAYO

Rejea: Waefeso 2:8–9

Imani ni zawadi kutoka kwa Mungu; haitokani na uwezo wa mtu wa asili.

8. HAWEZI KUTUBU DHAMBI/HANA TOBA YA KWELI

Rejea: 2 Timotheo 2:25

Ni Mungu anayempa mtu toba ya kweli; mwanadamu wa asili hawezi kutubu peke yake.

9. HAWEZI KUMPENDA MUNGU

Rejea: Warumi 1:30; Yohana 3:19–20

Mwanadamu wa asili ni adui wa Mungu na hupendelea giza kuliko nuru.

10. HAWEZI KUIPOKEA INJILI KWA FURAHA NA UNYENYEKEVU

Rejea: 1 Wakorintho 1:18

Ujumbe wa msalaba ni upuuzi kwa wale wanaopotea.

01/05/2025

Kristo anawagiza watu wajikane wenyewe, wauchukue msalaba wao,
na kumfuata
(Mathayo 16:24)

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kulingana na Maandiko posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share