15/09/2026
❤️ WAULIZE WAZAZI
Ukipata nafasi, muulize mama, baba, mjomba,ndugu, “Unaendeleaje?” Usisubiri mpaka wakuambie wamechoka. Kuna mambo hawasemi, kuna changamoto wanabeba kimya kimya, na kuna wakati wanatamani ungejua ili uwafae.
Wazazi wengi hutumia maisha yao kutujali sisi, hata wanapopitia mambo mazito. Usichukulie ukimya wao k**a kwamba wako sawa. Wapigie simu, wakae nao, wasikilize na uwape moyo. Wakati mwingine, swali dogo la “Ninaweza kukusaidia na nini?” linaweza kuwafanya wajisikie hawako peke yao.
🙏 Leo, usiwaze tu. Waulize wanaendelea vipi...
❤️ SirLoochu