21/01/2024
๐๐๐๐๐๐: 021/366
๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐, ๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐๐,
Ndoa yako na lolote, katika hiyo akidi,
Usitoe kwa yeyote, huwezi jua hasidi,
Abadani usiote, tajiumiza zaidi,
Kuna ya kubaki siri, kwa watu yasitokee,
Pili hali ya kifedha, huwasumbua watu,
Ingawaje una kadha, yanatayo k**a kutu,
Matatizo ama fedha, kwao usiambe katu,
Kuna ya kubaki siri, kwa watu yasitokee,
Shida za kifamilia, pia ziwe siri yako,
Mtu aweza tumia, hilo kuleta anguko,
Kwa asilimia mia, yaweke moyoni mwako,
Kuna ya kubaki siri, kwa watu yasitokee,
Hata zile zako ndoto, na yote maazimio,
Ama yawe ya kipato, au ya mafanikio,
Kinyume chake majuto, usemapo kwa mwenzio,
Kuna ya kubaki siri, kwa watu yasitokee,
Ukitoa msaada, tena kwa zako hisani,
Usichapishe jalida, ukaona burudani,
Kwako isiwe ni mada, ijiandike usoni,
Kuna ya kubaki siri, kwa watu yasitokee,
Kuna ya kubaki siri, kwa watu yasitokee,
Siri zako binafsi, usimtolee mtu,
Usiwe tena mwepesi, huenda ni mtukutu,
Igeuke iwe kesi, wakuite paka mwitu,
Kuna ya kubaki siri, kwa watu yasitokee,
Hata kesho utendalo, usiseme ร silani,
Lilo hilo usemalo, ni silaha mkononi,
Atakumaliza nalo, kabla uwe mwanzoni,
Kuna ya kubaki siri, kwa watu yasitokee,
๐๐ก๐ข๐๐ง๐: ๐๐๐๐๐๐๐ ๐. ๐๐๐๐๐๐
๐ฟ๐๐ร ๐๐ข : ๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐
๐๐๐๐โ๐: 21 ๐๐๐ 2024
๐๐๐๐๐, ๐๐๐๐๐