15/12/2021
Chimbuko la Kiswahili.
Ni kufafanua namna Kiswahili kilivyoanza. Asili ya Kiswahili.
Taja nadharia tatu zinazoeleza chimbuko la kiswahili.
i. Kuwa Kiswahili ni lugha ya mseto.
Kiswahili ni tukio la maingiliano ya kibiashara, kijamii na hata kindoa baina ya wenyeji wa
Pwani na Waarabu.
Ø Haja ya Waarabu kuwasiliana na watumwa wao wa Kibantu ilisababisha kuchanganya
kwa maneno ya lugha za Kibantu na yale ya Kiarabu ili waweze kuelewana na hivyo
lugha lugha iliyochipuka ikawa ya Kiswahili(mchanganyiko wa Kibantu na Kiarabu.
Ø Shughuli za kibiashara-Waarabu walipofika kwa shughuli hizi hawakufika na wake zao
hivyo kulikuwa na uhaba wa wanawake wa Kiarabu hivyo wakaanza kufunga ndoa na
wanawake Waafrika na kupata watoto waliojifunza Kiarabu na Kibantu na lugha
iliyozungumzwa ikawa Kiswahili(lugha chotara-mchanganyiko wa Kiswahili na
Kibantu).
ii. Kuwa Kiswahili ni lahaja ya Kiarabu.
Ø Kuna idadi kubwa ya msamiati wa kiarabu katika kiswahili.
§ Ghadhabu – hasira.
§ Nadra -chache.
§ Tisa - kenda.
§ daima – milele.
Ø Lugha ya kiswahili imefungama sana na mafunzo ya dini ya Kislamu (ambayo ililetwa na
Waarabu toka Uarabuni). Vile vile miongoni mwa wale wanaojiita Waswahili ni wafuasi
wa dini ya Kislamu. Wao hutumia majina ya Kislamu k**a vile Mohammed, Rehema,
Ramadhan n.k.
Ø Nyimbo za taarab hapo awali zilikuwa zikiimbwa kwa mashairi ya kiarabu na baadaye
zikaanza kuimbwa kwa mashairi ya Kiswahili.
iii. Kuwa Kiswahili ni lugha ya Kiafrika yenye asili ya kibantu.
Mtazamo hushikiliwa na wengi. Unashikilia kwamba Kiswahili ni Kibantuk**a vile
Kikamba, Kizulu, Kiganda n,k.
Tetea kauli kwamba Kiswahili ni kibantu.
Ø Maumbo ya maneno kwa Kiswahili na lugha za kibantu yana viambishi.
k.m mu-ndu.
m-tu
Ø Kuna mfanano wa kimsamiati katika lugha ya Kiswahili na lugha za Kibantu.
k.m kuhoa, korora, kooa.
Ulimi.lulimi
Ø Lugha ya Kiswahili mara nyingi huwa na muundo wa silabi wazi/huru. Mfumo huu vile
vile hudhihirika katika lugha nyingi za Kibantu.
Kikombe/shikombe.
Kitabu/sh*tapu.
Ø No