23/05/2024
Maelezo mseto kuhusu mbinu ya Taswira.
Taswira ni picha inayojengeka akilini mwa msomaji au msikilizaji wa kazi anuai za fasihi.
Kuna aina tofauti tofauti za taswira. Ni K**a vile:
1.Taswira oni –inajitokeza unapopewa picha ya mahali, mtu, kitu au hali na dhana tofauti .
Mathalan:
Halima amejikunyata kwenye kochi.
Picha nzuri zimetundikwa ukutani.
Moto mkubwa uliteketeza makao yao.
2.Taswira sikivu-hapa unawahi picha akilini kwa kigezo cha kusikia kwa masikio .
Mathalan:
Malenga mteule akikariri shairi kwenye Msiba wa Kujitakia.
Mangwasha anasikia sauti za wakimbizi wengine nje ya kanisa.
3.Taswira mwonjo-aghalabu huhusishwa na picha dhanaifu ya kima fulani k**a ulaji wa milo au viambata au chochote cha ladha fulani kwa kutumia ulimi.
Mathalan.
Jasho lake lilikuwa sawa na chumvi nilipompa pambaja.
Chakula hichi ni asali.
4.Taswira mnuso – ni picha inayokuzwa kwa uwezo wa pua zinapobainisha harufu za namna fulani.
Mathalan:
Mitungi ya gesi ya plastiki ilichomeka na harufu kutapakaa kila mahali.
Tulihisi mapishi yenyu ya mahamri tukiwa bustanini.
5.Taswira hisi – huegemea hisia za wastani za binadamu k**a vile huruma, hasira, furaha,huzuni, jazba na kadhalika.
Mathalan:
Njaa ilimkeketa matumbo na kumdhoofisha kabla ya kuzirai.
Mgonjwa alighuna kwa uchungu mkubwa.
Kumbuka: Taswira zaidi ya moja zinaweza kuwa kwa kauli moja.
6.Taswira Mguso – msomaji huwahi hisia za kuguswa kwa viganja vya mkono au mikono au vitu visio hai ilivyo kawaida tu kwa hali tofauti.
Mathalan:
Halima alimpapasa Ali na kumlaza kitandani taratibu.
7. Taswira mwendo- aghalabu huhusisha kubadili makao kwa mtu, kiumbe mwingine au kitu.
Aghalabu hujenga Taswira oni moja kwa moja.
Mathalani:
Halima alisimama na kuelekea pembezoni mwa bahari k**a malaika.
Tawi lilininginia kwa madaha kisha kuyumbishwa ghafla kabla ya kuangoka na kuanguka chini.
Ubainifu wa Taswira katika ushairi na kazi zingine huweza kuchimuzwa kwa mbinu hizi za lugha:
Takriri au urudiaji ainati-neno au muundo(usambamba)
Kwa mfano:
Walisima k**a kigingi cha umeme kwa hofu. Hofu ya kutojua kesho. Hofu ya kutojua mgeni wao usiku huo alileta zawadi gani. Hofu ya kutojua nina wao yu wapi.
Tashbihi.
Kwa mfano:
Yerimina amesimama wima sawa na jenerali.
Istiara.
Kwa mfano :
Maisha ni bembea.
Jazanda.
Kwa mfano:
Ndoa ni bembea.
Dunia ni mtihani mkuu. Hamna aliyefuzu stashahada hii mia fi mia.
Naomba mnoe maelezo haya na myajaze zaidi yawe mkufu wa kuvishwa wanagenzi na wakufunzi ili sote tufanikishe jahazi la elimu. Shukran.