04/10/2025
🏃🏼♀️🏃🏼♀️🏃🏼♀️🏃🏼♀️🏃🏼♀️
These are KISWAHILI lesson notes for form 1 - 4 - KENYAN CURRICULUM. ORDER BOOKS VIA WHATSAPP
04/10/2025
🏃🏼♀️🏃🏼♀️🏃🏼♀️🏃🏼♀️🏃🏼♀️
14/04/2024
KANZI YA KISWAHILI
Vidato 1-4
===================
BETHANY BOOKSHOP
INQUARIES: 0714 494451
Till no 800281
28/02/2024
https://vm.tiktok.com/ZMM8wmV8x/
TikTok · ziontv23 Check out ziontv23's video.
28/02/2024
KANZI YA KISWAHILI
TikTok · ziontv23 Check out ziontv23's post.
28/02/2024
TikTok · ziontv23 Check out ziontv23's post.
14/10/2023
KISWAHILI
102/2 -LUGHA
U(JI)FUNZAJI NA UTAHINI
===============================================================
MFUATANO MWAFAKA WA KUJIBU MASWALI
Karatasi ya lugha 102 / 2 huwa na ufahamu, ufupisho, matumizi ya lugha na isimujamii. jumla ya alama ni 80.
Mwanafunzi aanze kujibu maswali kwa mfuatano ufuatao; matumizi ya lugha, isimujamii, ufahamu kisha ufupisho. Yaani, anza kwa swali la 3, 4, 1 kisha 2.
Mfuatano huu huanza kwa maswali yenye mchakato mwepesi wa utafsiri ( matumizi ya lugha na isimu jamii) na kumalizia yale maswali yenye mchakato tata wa utafsiri wa maswali ( ufupisho na ufahamu)
Hatari ya kutofuata mfuatano huu ni kuwa mwanafunzi huenda akashindwa kukamilisha kujibu maswali yote na kwa hivyo kupata alama za chini sana.
LUGHA 102/2
MASWALI ALAMA DAKIKA UTAFSIRI WA MASWALI
1 Ufahamu 15
2 Ufupisho 15
3 Matumizi ya lugha 40
4 Isimujamii 10
JUMLA 80 dakika 150 ( saa 2 1/2 )
Idadi ya makosa ya mwanafunzi katika mtihani huathiri alama jumla. Kwa hivyo, ni muhimu kwa mwanafunzi kuelewa aina za makosa ili ayaepuke
Aina za Makosa za Kuepukwa
1. Makosa ya sarufi
2. Makosa hijai
Makosa ya Sarufi
Matumizi mabaya ya alama za uakifishaji,
kutumia herufi kubwa au ndogo mahali pasipofaa.
Matumizi yasiyofaa ya ngeli na viambishi, viunganishi, nyakati, hali, vihusiano na kadhalika.
Mpangilio wa maneno katika sentensi.
Mnyambuliko wa vitenzi na majina.
Kuboronga sarufi.
Kuacha neno linalohitajika au kuongeza neno lisilohitajika katika sentensi.
Matumizi ya herufi kubwa
Makosa ya Hijai / Tahajia
Haya ni makosa ya maendelezo.
Kutengalisha neno kwa mfano 'aliye kuwa'.
Kuunganisha maneno kwa mfano 'kwasababu'.
Kukata silabi visivyo afikapo pahıbizoni k**a vile, İngan-o' Kuandİka herufi isiyofaa kwa mfano 'ongesa' badala ya 'ongeza'.
Kuacha herufi katika neno kwa mfano 'aliekuja' badala ya laliyekuja'
Kuongeza herufi isiyohitajika k**a Vile 'piya' badala ya 'Pia'.
Kuacha alama inayotarajiwa katika herufi k**a vilej, i
Kukosa kuandika kistari cha kuendelezea neno afikiapo pambizoni au kukiandika mahali pasipofaa. Kuacha ritifaa au kuiandika mahali pasipofaa, kwa mfano ngombe, ngom'be, ng'ombe, ngo'mbe n.k.
Kuandika maneno kwa kifupi k**a Vile k.v., k.m., v.v., n.k. na kadhalika.
Kuandika tarakimu kwa mfano 27-08-2013
MATUMIZI YA LUGHA
1. Durusu mada zote, mathalan:
MADA ZA MATUMIZI YA LUGHA – MIKAKATI YA KUDURUSU
SAUTI ZA KISWAHILI
AINA ZA MANENO
MWINGILIANO WA AINA ZA MANENO
MANENO NA VIAMBISHI MAALUM
MISINGI YA MANENO (VIAMBISHI,MIZIZ,MOFIMU,SILABI,SHINA)
UUNDAJI WA MANENO ( kuunda nonino kutokana na vitezi, n.k)
UMOJA NA WINGI
NGELI ZA NOMINO
UPATANISHO WA KISARUFI
UAKIFISHAJI
MNYAMBULIKO WA VITENZI/ KAULI ZAVITENZI
NYAKATI / NJEO NA HALI
UDOGO NA UKUBWA WA NOMINO
SENTENSI ZA KISWAHILI
SENTENSI TATA / SENTENSI ZENYE MAANA ZAIDI YA MOJA
UKANUSHAJI NA UYAKINISHAJI
MSEMO HALISI NA MSEMO WA TAARIFA
MATUMIZI YA KAMUSI
vinyume / antonimu
visawe/maneno yenye maana sawa
vitate / maneno yanayokaribiana kimatamshi
polisemia / maneno yenye maana zaidi ya moja
kutunga sentensi kwa maagizo fulani
majina ya makundi
methali, nahau, msamiati n.k
Kanuni
Afahamu silabasi na kinacholengwa katika swali.
Adurusu mada na vijimada vyote. Rejelea jedwali hapo juu.
Mfano: KCSE 2022 – sentensi tata. Tambua vigezo vinavyozua utata katika sentensi.
Mtahiniwa atambue mitego au vijisehemu katika swali aliloulizwa Kwa mfano, kanusha sentensi ifuatayo kwa udogo katika ngeli Ya Kl. VI. Hapa kuna mitego mitatu.-kukanusha,udogo na ngeli
KCSE 2014: Andika sentensi ifuatayo katika wakati ujao hali timilifu. Dobi huwapigia watu nguo pasi. Hapa pana vitahini viwili (mitego), navyo ni; (i) wakati ujao (ii) hali timilifu.
KCSE 2011: Tumia kivumishi kionyeshi kisisitizi cha karibu pamoja na nomino katika ngeli ya YA-YA kutunga sentensi. (alama 2) . Hapa pana vitahini vitatu, yaani;
kivumishi kionyeshi kisisitizi
ngeli za nomino ya YA-YA
masafa ya kionyeshi ( cha karibu)
Atoe mifano katika jibu lake hata k**a hakuulizwa. Kwa mfano, akiambiwa aeleze maana ya sauti mwambatano, aseme ni konsonanti mbili au zaidi zinazofuatana na hutamkwa k**a sauti moja, ndoa.(mfano).
Kila swali lijibiwe pahali pake. Mtahiniwa asilijibu kwingine kisha kutumia vishale kuonyesha liliko jibu, atumie maelezo.
Anaweza kupigia mstari suala aliloulizwa. Kwa mfano akiambiwa atunge sentensi kwa kutumia kitenzi kishirikishi kipungufu, jibu lake anaweza kuandika hivi; mtoto yy kitandani.
Asiache pengo, ajaribu kujibu maswali yote bila kuacha nafasi zozote wazi.Kuacha pengo kunatangaza kutojiandaa vizuri kwa mtahiniwa husika.
Atazame alama mabanoni kwenye swali ili atambue vipengele vinavyotahiniwa. Kwa mfano, akiulizwa atambue matumizi ya 'na' katika sentensi:
Juma na Ali wanapigiana mpira.( alama 3)
Anstahili atambue matumizi matatu tofauti ya na kwa sababu kuna vipengele vitatu.
Asitoe majibu mawili ya kubahatisha kwa kutumia neon ‘au’
Kwa mfano akiambiwa atoe sifa mbili za sauti /b/ asiseme ni ghuna au si8huna. Iwapo hana uhakika, basi aorodheshe (i) ghuna (ii) sighuna
Mtahiniwa akiambiwa aonyeshe aina ya maneno katika sentensi, kisha atambue tu bila kutaja aina, anapoteza alama.
Mtahiniwa akikosa vipengele viwili, alama ni sufuri. Kwa
ISIMUJAMII
Namna ya kujibu swali la sifa za sajili katika mtihani
Kwa kila hoja, tolea sababu / maelezo na mifano ( hoja+sababu+mifano)
Tanguliza mifano kwa kifungu ‘…k**a vile…’
Tanguliza maelezo kwa kihusishi ‘…ili…’
Unaweza kukupigilia mstari hoja kuu.
TANBIHI:
kumbuka kuwa hamna alama kwa hoja pasipo mfano ;Utatuzwa sufuri!
Akronimu ya kukumbuka hoja + sababu + Mifani ni HOSANI
yaani ; Ho – Hoja, Ma -Mifano , Sa - Sababu
Sampuli ya swali
Eleza sifa mbili za sajili ya mahak**a
1. Hutumia msamiati maalum ili kurahisisha mawasiliano k**a vile ‘kukata rufaa’
2. Hutumia sentensi ndefu ndefu ili kuondoa utata katika ujumbe
MITIHANI YA AWALI YA KITAIFA (KCSE 2006-2022 )
ISIMUJAMII KCSE 2022
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
“Wateja wetu wameagiza bidhaa tena. Katoni mia mbili ziwe tayari Kufikia leo jioni. Kazi ianze mara moja.”
Bainsiha sajili ya makala haya kwa kutoa mfano kwenye makala. (alama2)
Fafanua sifa nyingine nane za sajiliu hii ambazo zingejitokeza katika makala haya. (alama8)
matumizi ya lugha ya unyeneyekevu. Kwa mfano, wafanyikazi wanapozungumza na meneja.
ISIMUJAMII KCSE 2021
Soma makala yafuatayo kisha wibu maswali.
"Karibu, karibu! Keti.
Naam, jitambulishe kwa jopo hili...
Bwana Nuru, ni jambo lipi ambalo linakufanya kuamini kwamba nafasi hii inakuafiki wewe?"
Bainisha sajili ya makala haya. (alama 1)
Eleza sifa nne za sajili hii kwa kurejelea makala haya. (alama 4)
Wewe ni kinara wa chama cha Wanamawasiliano Bora shuleni mwako.
Umepewa jukumu la kuwatangazia wenzako mashindano ya uogeleaji yakiendelea shuleni mwako. Fafanua sifa tano za lugha utakayotumia. (alama 5)
ISIMUJAMII KCSE 2020
Umewahutubia wanaeneobunge lako kuwaomba wakuchague kuwa mbunge wao. Hata hivyo, umegundua kwamba hujafanikiwa kuwavutia upande wako. Fafanua sifa kumi za lugha ambayo ungetumia. (alama 10)
ISIMUJAMII KCSE 2019
Wewe ni mhubiri katika maabadi ya Shamu. Umealikwa kuwahubiria wanafunzi wa Shule ya Upili ya Lulu. Fafanua sifa kumi za lugha utakayotumia. (alama 10)
ISIMUJAMII KCSE 2018
Soma Makala yafuatayo kisha ujibu maswali
ndugu wapenzi, waumini wenzangu, mbazi hii haionyeshi huruma ya Mwenyezi Mungu kwetu wakosefu tu, bali pia inatufunza umuhimu wa unyenyekevu na msamaha.
a) Bainisha sifa tatu za sajili ya kidini zinzojitokeza katika Makala haya (alama 3)
b) Fafanua vipengele vingine saba vya kimtindo ambavyo mhubiri huyu angetumia kufanikisha mazungumzo yake. (alama 7)
ISIMUJAMII KCSE 2017
Soma Makala yafuatayo kisha ujibu maswali
“kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa, mahak**a hii imethibitisha bila chembe ya shaka kwamba wewe mshtakiwa, Bi Mlachake Chauchau ndiye uliyepika pombe haramu ambayo ilisababisha vifo vya raia hamsini na kupofukwa kwa wengine mia moja. Unahukumiwa kwa kosa la mauaji.”
Bainisha sajili ya makala haya kwa kutolea mifano miwili kutoka kwenye makala (alama 2 )
Fafanua sifa nyingine nane za sajili hii ambazo zingejitokeza katika Makala haya (alama 8 )
ISIMUJAMII KCSE 2016
Kwa kutoa mifano maridhawa, eleza kaida zozote tano ambazo matumizi ya lugha hutegemea katika jamii (alama 10 )
ISIMUJAMII KCSE 2015
Soma Makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Mtu I: wewe njoo hapa! ( kwa sauti kubwa.) Fanya upesi!
Mtu II: (anakimbia mbio.) naja sir.
Mtu I: (anamtazama.) Unajifanya mwerevu?
Mtu II: Hapana Sir…eh… afande.
Mtu I: Jina?
Mtu II: Samwel Kiabao
Mtu I: (Huku anaandika.) Lete kitambulisho.
Mtu II: Sina hapa sir.
Mtu I: Huna kitambulisho? Utafanyiwa booking vipi?
Mtu II: Naomba…
Mtu I: Naomba! Naomba! Unaomba nini? Wazururaji k**a nyinyi tunawajua. Mnajidai hamjui kuna curfew. Mnajiponza wenyewe na kuwahasiri wenzenu. Kisha, “Serikali saidia ” Usiniharibie muda wangu. (Akiashiria ) Ingia ndani! Utakuwa mgeni wetu leo. Tutakukirimu chakula na chumba. (Anamsukuma ndani.)
a) Bainisha sajili ya Makala haya. (alama 2)
b) Eleza sifa nane za sajili hii kwa kurejelea makala haya (alama 8)
ISIMUJAMII KCSE 2014
a) Umepewa jukumu la kuwazungumzia vijana wenzako kuhusu umuhimu wa uwekezaji. Fafanua sifa tano za lugha utakayotumia. (alama 5)
b) Eleza sifa tano za sajili ya kidini (alama 5)
ISIMUJAMII KCSE 2013
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Haya ng’ara…Ng’ara leo! Nguo motomoto. Ng’ara leo kwa bei rahisi. Hamsini hamsini shati. Kuona ni bure. Bure kwa bure. shika mwenyewe ujionee. Bei nafuu. Bei ya starehe. Haya, haya. Usikose mwanangu! Fifty! Hamsa! Fifti! Hamsa na nyingine.
a) Bainisha sajili ya mazungumzo haya (alama 2)
b)Eleza sifa nane za sajili hii kwa kurejelea kifungu hiki. (al 8)
ISIMUJAMII KCSE 2012
Eleza kwa ufupi jinsi mambo yafuatayo yanavyodhibiti mitindo ya lugha.
a) Mazingira (alama 4)
b) Madhumuni (alama 2)
c) Malezi (alama 4)
ISIMUJAMII KCSE 2011
a) Bainisha changamoto tano zinazoikabili lugha ya Kiswahili k**a somo katika shule za upili nchini Kenya (alama 5)
b) Eleza namna tano za kukabiliana na changamoto ulizobainisha hapo juu (alama 5)
ISIMUJAMII KCSE 2010
"Benki yenyewe haina kitu ... CD4 count yake iko chini ... Ni emergency ... Tutampoteza ikikosekana."
Taja sajili inayorejelewa na maneno haya. (alama 2)
Fafanua sifa nne zinazohusishwa na sajili hiyo. (alama 8)
ISIMUJAMII KCSE 2009
Eleza majukumu matano matano ya Kiswahili k**a lugha ya Kitaifa na Kimataifa. (alama 10)
ISIMUJAMII KCSE 2008
Eleza huku ukitoa mifano tano za kimsingi zinazotambulisha sajili ya mazungumzo. (alama 10)
ISIMUJAMII KCSE 2007
Huku ukitoa mifano mwafaka, fafanua kaida tano katika jamii ambazo matumizi ya lugha hutegemea. (alama 10 )
ISIMUJAMII KCSE 2006
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Kwa mujibu wa sharia kifungu namba 3 sehemu ya A ya sharia za nchi, umepatikana na hatia ya kutatiza utulivu wa raia wapenda Amani kwa kuwatusi na kutisha kuwapiga. Kiongozi wa mashtaka amethibitisha haya kwa kuwaleta mashahidi ambao wametoa ushahidi usioteterek kuhusu vitendo vyako katika tukio hilo. Korti hii imeonelea una hatia na imeamuru ufungwe jela kwa muda wa miaka miwili bila faini ili liwe funzo kwako na kwa wenzako wenye tabia k**a zako. Una majuma mawili kukata rufani.
a) Lugha iliyo katika kifungu hiki hutumika katika muktadha upi? ( alama 1)
b) Toa ushahidi wa jibu lako. (alama 3)
c) Zaidi ya sifa zilizo katika kifungu hiki, eleza sifa zingine sita za matumizi ya lugha katika muktadha huu. (alama 6)
UFAHAMU
Mwanafunzi asome maswali kisha asome taarifa.
Mtindo huu humfanya mwanafunzi kusoma kwa kina na makini akichunguza sehemu zinazoelekea kujibu maswali.
Mwanafunzi atambue dhamira ya mwandishi katika taarifa. Dhamira husaidia kutapa maudhui ya kwenye taarifa.
Baadhi ya maswali huhitaji mwanfunzi kutafakari / kufikiri na kutafsiri maana badala ya kukariri.
Aghalabu taarifa huwa na msamiati mpya au mgumu. Maana ya msamiati uelezwe kulingana na muktadha wake.
Mwanafunzi apigilie mstari hoja kuu hasa kwa kuzingatia kitenzi ambcho hudokeza hoja kuu.
Anaweza kuorodhesha majibu kwa takwimu za kirumu au za kiarabu
aongozwe na alama kwa kila swali kwa sababu aghalabu idadi ya alama hudokeza idadi ya hoja zitakikanazo
Jibu laweza kuwa sentensi kamilifu au kifungu isiyo kamilifu /kirai.
jibu la sentensi kamili lianze kwa herufi kubwa kisha imalizie kwa kitone
jibu la kirai lianze kwa herufi ndogo bila kitone mwishoni.
Kuna maswali funge na maswali wazi. Swali funge huhitaji idadi mahususi ya hoja, mfano- eleza sababu tatu za kuenea kwa Kiswahili. Maswali wazi haina mipaka ya majibu; alama pekee hueleza mwanafunzi kuhusu idadi ya hoja zitakikanazo.
Hoja za ziada ziepukwe.
Asijieleze kupita kiasi. Atoe jibu mola kwa moja. Likiuliza kwa nimi? jibu lianze, kwa sababu…
Asirudie ama kunukuu swali upya.
Akiulizwa maana ya msamiati, anaweza kutoa kisawe ama atoe maelezo mafupi tu.
Asiache pengo lolote. Ajaribu kujibu maswali yote. Kuacha pengo kunatangaza kutojiandaa vizuri kwa mtahiniwa husika.
Kwa hali fulani, anaweza kudondoa na kupachika majibu yake
Aepuke vifupishoj akronimu na tarakimu awezavyo.
Aandike herufi moja moja bila kasi ili hati yake isomeke vizurj.
Katika swali la mwisho azingatie muundo wa neno lililoulizwaj iwapo ameulizwa maana ya neno omba basi jibu ni sali wala si kusali. Lakini kuomba jibu ni kusali wala si sali
Aepuke makosa ya sarufi na hijai.
UFUPISHO
Maana ya ufupisho
Ufupisho ni taarifa yenye hoja kuu zilizodondolewa kutoka habari ndefu na kuandikwa kwa lugha ya nathari. Ufupisho hueleza kiini cha habari au mambo ya kimsingi katika taarifa, bila kuyatolea ufafanuzi.
Hatua za kuandika ufupisho.
Soma taarifa husika mara ya kwanza kwa haraka pasipo kutua.
Soma maswali husika ili kupata mahitaji ya mtahini
Soma taarifa kwa mara ya pili huku ukipigilia mstari hoja kuu. Unaweza ktumia takwimu kuzionyesha hoja kuu ulizopia msari.
Andika vidokezo ( nakala chafu )kwa nafsi ya MATAYARISHO ukitumia hoja ulizopigia mstari kwenye kifungu. Hoja zindikwe kwa sentensi kamili na kuorodeshwa kwa takwimu.
Andika nakala safi kwa lugha ya mtiririko / nathari na kwa aya moja pekee kwa kuunganisha hoja kuu kutoka kwa matayarisho.
Hesabu idadi ya maneno katika matayarisho na uhariri (ubadilishe ) idadi hiyo kulingana na idadi kwenye maagizo. Idadi ya maneno inaweza kuzidi kwa maneno tisa
Andika idadi ya maneno kwenye mabano mwishoni mwa ‘Nakala Safi’. Mfano, (maneno 60).
( Tanbihi: K**a utahesabu maneno ya nakala safi, usihesabu maneno yote bali ukadirie tu kwa kuhesabu idadi ya mistari kwa maneno katika kila mstari. Mfano; mistari 7 na maneno 9 kwa kila mstari itakuwa; 7 x 9 = 63. Kwa hivyo, idadi ya maneno ni takriban 63. )
Hoja kuu ni nini?
Hoja kuu ni jambo linatotokea kwa mara ya kwanza lisilokuwa maelezo, ufafanuzi, mifano au kisawe.
Mambo ya kupuuzwa unapoandika hoja kuu
Maelezo ya ziada au ufafanuzi
Mifano
visawe
visifa / vivumishi / vishazi tegemezi
tanakali
Mazingatio
Atumie maneno machache kueleza ujumbe jinsi ulivyo katika ufahamu bila kufasiri.
Asiandike ujumbe nusu: kitenzi kiwepo.
Hoja zisiwe chache - zitegemee alama mabanoni alama ni saba hoja pia ziwe saba
Arejelee aya zilizoulizwa kwa mfano aya za nne za za mwisho nne
Aratibishe hoja kulingana na aya zilivyoorodheshwa katika taarifa
Nakala ya matayarisho isikatwe
Atambue dhamira ya mwandishi
Nakala ya matayarisho aghalabu iandikwe kwa kuorodheshwa.
Kila hoja iliyoratibishwa iwe sentensi kamili
Nakala safi /jibu lake liwe katika aya moja tu
Asilipe jibu lake kichwa
Aonyeshe idadi ya maneno aliyotumia katika nakala safi tu.
Idadi ya maneno inaweza kuzidi kwa maneno tisa
Idadi ya juu ilengwe, mfano katika (70-80 ) alenge 80)
Azingatie sarufi na kuepuka makosa ya hijai
Atumie koma zaidi kuliko viunganishi.
Iwapo maneno ni mengi sana apunguze vivumishi, vielezi, na viunganishi. (hata vishazi tegemezi vivumishi na vishazi tegemezi vielezi )
Umuhimu wa kufundisha ufupisho
Hukuza uwezo wa kuelewa habari barabara.
Kupata uzoefu wa kuteua ujumbe mkuu na kuuwasilisha kwa maneno machache.
Huokoa muda. Habari zilizofupishwa husomwa kwa muda mfupi kwa sababu huelezea tu mambo muhimu.
Hurahisisha uhifadhi wa mambo akilini. Aghalabu watu huhifadhi mambo vizuri iwapo yameelezwa kwa kifupi.
Huimarisha uwezo wa kueleza mawazo ya watu wengine kwa maneno machache.
Husaidia kukuza stadi nyingine za utambuzi, k**a vile, kukumbuka (kukariri), kufahamu (kuelewa), kutekeleza (kutumia au kuhamisha uliyojifunza hadi muktadha halisi), kuchanganua, kusanisi na kutathmini.
Hukuza stadi ya kujieleza. Jaribio la ufupisho humzoesha mwanafunzi kuteua msamiati utakaofumbata ujumbe mrefu. Kwa kufanya hivi, hunoa mbinu zake za kuwasiliana.
MFANO
UFUPISHO - KCSE 2020
Ukame ni tukio hatari la kimaumbile. Athari zake hutofautiana kutokea eneo moja hadi lingine. Kwa sababu hiyo, si rahisi kuielewa dhana ya ukame; kwa hakika si rahisi kuifafanua dhana hii. Katika eneo la Bali, kwa mfano, isiponyesha kwa muda wa siku sita wenyeji huchukulia hali hiyo kuwa ukame japo kiasi hicho cha mvua ni kikubwa mno ikilinganishwa na Libya ambayo hupata kiasi kidogo cha chini ya milimita 180 ya mvua kwa mwaka.
Katika msimu mzima au zaidi. Uhaba huu wa mvua huweza kusababisha uhaba Katika hali ya kawaida (a1) ukame hutokana na kipindi kirefu cha uhaba wa mvua wa maji kwa shughuli, kundi au sekta fulani. (a2) Shughuli za binadamu huweza kufanya hali ya ukame kuwa mbaya zaidi. Shughuli hizo ni pamoja na kilimo, unyunyiziaji maji na ukataji wa miti.
Ni vigumu kubaini wakati mahususi ambao ukame huanza kwa kuwa kipindi hicho cha ukosefu wa mvua huwa cha mfululizo, na eneo huendelea kupata mvua iliyopungua kwa miezi au hata miaka. Mimea hukauka na wanyama hufa kutokana na ukosefu wa maji. Ukame basi huwa hatari kwa maisha ya binadamu na viumbe wengine wengine kwa kuwa huweza kusabibisha njaa na kuyafanya maeneo kwa majangwa.
Mbali na ukosefu wa mvua,(a3) ukame pia husababishwa wa kiangazi. Kiangazi huongeza kiwango cha joto. Joto hilo huyafanya maji yaliyohifadhiwa kuwa mvuke haraka, hivyo kiwango chake kupungua. (a4) Hali ya el ninyo pia husababishwa ukame katika baadhi ya maeneo ambayo huwa hayana mvua. Upepo huivutia mvua mahali panaponyesha na kuliacha kame eneo ambalo halina mvua ya aina hii. Hata katika maeneo yenye mvua ya el ninyo, (a5) kiangazi kikali huifuata na hivyo kusababisha ukame. Hali hii huitwa la nina. Mambo yanayotokana na (a6) mabadiliko ya hali ya anga ulimwenguni pia yanaweza kuchangia hali ya ukame. Ongezeko la joto duniani linafanya hali ya ukame kuwa mbaya zaidi.
Ukame una madhara chungu nzima kwa biunadamu. Madhara hayo huweza kuwa ya kiuchumi, kimazingira au hata kijamii. (b1) Ukame husababisha kupungua kwa mimea na mavuno. (b2) Huweza pia kutokea dhoruba za mchanga. Dhoruba hizi hutokea palipo na jangwa. (b3) Ukosefu wa maji ya kunyunyizia mimea husababisha njaa na mangonjwa k**a vile utapiamlo yanayotokana na ukosefu wa lishe bora. ( b4) Makazi ya wanyama wa nchi kavu na wale wa majini pia huathiriwa vibaya. Hali kadhalika, (b5) ukame husababisha uhamaji. Hii inamanisha kuwa jamii huweza kutoka katika makazi asilia na wakati mwingine huweza hata kuwa wakimbizi.
(b6) Ukame husababisha ukosefu mkubwa wa maji. (b7) Ukosefu huu huwa na athari hasi kwa maendeleo ya viwanda kwa kuwa vingi huhitaji kiasi kikubwa cha maji. Juu ya hayo, (b8) maji huhitajika katika kuzalisha umeme. Umeme una matumizi mengi katika viwanda, nyumbani afisini na hata hospitalini. (b9) Ukosefu wa umeme basi huwa ni tatizo kuu.
Aidha, (b10) ukame unajulikana kusababisha uhasama wa kijamii. Jamii huweza kuzozana na hata kupigana kutokona na uhaba wa rasilimali za asili k**a vile chakula na maji. Pia (b11) mioto mikubwa huweza kuenea haraka wakati wa ukamwe na hivyo kusababisha vifo vya binadamu na wanyama na uharabifu wa rasilimali nyingine.
Ingawa ukame husababisha madhara mengi, (c 1) binadamu wanaweza kujikinga kutokana nao kwa kupunguza makali ya ukame. Jambo la kwanza wanaloweza kufanya binadamu ni kuhifadhi maji. (c 2) Maji ya mvua yanafaa kuhifadhiwa katika mabwawa na mapipa. Haya yanaweza kutumiwa wakati wa ukame hasa katika kukuza mimea. Mkakati mwingine ni (c3 ) kutumia mbinu za kupunguza chumvi na zilizomo kwenye maji ya bahari ili yaweze kutumika katika kemikali nyingine: wa mimea. Hili litapunguza tatizo la ukosefu wa chakula. Pia ni unyunyuziaji muhimu (c4) kufanya utafiti kuhusu hali ya anga ili kupanga na kuweka mikakati ifaayo kukabiliana na hali hiyo.
Ni muhimu (c5) kuwa na mipangilio mizuri ya matumizi ya ardhi. Mathalani upanzi wa mimea itakayozuia mmonyoko wa udongo, kubadili aina ya mimea inayokuzwa sehemu fulani pamoja na upanzi wa mimea isiohitaji mvua nyingi katika maeneo kame ni hatua mwafaka. Aidha, ni vizuri (c 6 ) kupunguza matumizi ya maji hasa katika mazingira ya nyumbani kwa mfano tunapofua na kuosha. Njia nyingine ya (c 7 ) kukabiliana na tatizo hii ni kusafisha maji yaliyotumiwa ili kuyatumia tena.
Kwa maneno 50, eleza visabababishi vya ukame kwa mujibu wa taarifa. (alama 4; 1 ya mtiririko
Matayarisho
Ukame husababishwa na kuwepo na kipindi kirefu cha uhaba wa mvua hasa katika msimu mzima
Shughuli za binadamu huweza kufanya hali ya ukame kuwa mbaya zaidi husababisha ukame
Ukame pia husababishwa na kiangazi kinachoongeza kiwango cha joto ardhini
Hali ya el ninyo pia husababisha ukame katika eneo ambalo halina mvua ya aina hii.
Kiangazi kikali kinachofuata el ninyo huitwa el nina husababisha ukame.
Nakala safi
Ukame husababishwa na kuwepo na kipindi kirefu cha uhaba wa mvua. Shughuli za binadamu husababisha ukame. Ukame pia husababishwa na kiangazi kinachoongeza kiwango cha joto ardhini. Hali ya el ninyo pia husababisha ukame katika eneo ambalo halina mvua ya aina hii. Kiangazi kikali kinachofuata el ninyo huitwa el nina kusababisha ukame. Shughuli za kibinadamu husababisha mmomonyoko wa ardhi. ( Maneno 59 )
Fupisha ujumbe wa aya ya tano hadi saba kwa maneno 70. (alama 6; 1 ya mtiririko)
Matayarisho
Ukame husababisha kupungua kwa mimea na mavuno.
Kusababisha kutokea kwa dhoruba za mchanga katika maeneo yaliyo na jangwa.
Ukosefu wa maji ya kunyunyizia mimea hivyo kusababisha njaa na magonjwa.
Makazi ya wanyama wa nchi kavu na wale wa majini huathiriwa.
Hali ya afya huzorota na kunakuwa na magonjwa k**a vile utapiamlo.
Ukosefu wa maji na chakula.
Ukame husababisha uhamaji wa baadhi ya jamii kutoka makazi asilia kutokana na
Husababisha ukosefu mkubwa wa maji.
Husababisha athari kubwa kwa maendeleo ya viwanda kutokana na ukosefu wa maji.
Ukosefu wa umeme kwani maji huhitajika kuzalisha umeme.
na maji.
Ukame husababisha uhasama wa kijamii kutokana na uhaba wa rasilmali k**a chakula
makuu.
Mioto mikubwa huweza kuenea haraka katika maeneo kame na kusababisha madhara
Nakala safi
Ukame husababisha kupungua kwa mimea na mavuno. Kusababisha kutokea kwa dhoruba za mchanga katika maeneo yaliyo na jangwa. Ukosefu wa maji ya kunyunyizia mimea hivyo kusababisha njaa na magonjwa. Makazi ya wanyama wa nchi kavu na wale wa majini huathiriwa. Hali ya afya huzorota na kunakuwa na magonjwa k**a vile utapiamlo. Ukosefu wa maji na chakula. Ukame husababisha uhamaji kutokana na ukosefu wa chakula na maji. Husababisha ukosefu mkubwa wa maji.
( Maneno 76 )
Eleza masuala ambayo mwandishi ameibua katika aya mbili za mwisho kwa maneno 60. (alama 5; 1 ya mtiririko)
Matayarisho
Binadamu wanaweza kujikinga na makali ya ukame kwa kuhifadhi maji.
Maji ya mvua yanafaa kuhifadhiwa katika mabwawa na mapipa ili yatumiwe kukuza mimea wakati wa ukame.
Kutumia mbinu za kupunguza chumvi na kemikali nyingine zilizomo katika maji ya
bahari ili yaweze kutumika katika unyunyizaji mimea.
Kufanya utafiti kuhusu hali ya anga ili kupanga na kuweka mikakati ifaayo.
Kuwa na mipangilio mizuri ya matumizi ya ardhi.
Ni muhimu kupunguza matumizi ya maji hasa katika mazingira ya nyumbani.
Kusafisha maji yaliyotumiwa ili kuyatumia tena
Nakala safi
Binadamu wanaweza kujikinga na makali ya ukame kwa kuhifadhi maji.Maji ya mvua yanafaa kuhifadhiwa katika mabwawa na mapipa ili yatumiwe kukuza mimea wakati wa ukame.Kutumia mbinu za kupunguza chumvi na kemikali nyingine zilizomo katika maji ya bahari ili yaweze kutumika katika unyunyizaji mimea.Kufanya utafiti kuhusu hali ya anga ili kupanga na kuweka mikakati ifaayo. Kuwa na mipangilio mizuri ya matumizi ya ardhi.
( Maneno 65 )
HUU NI UKURASA WA MWISHO ULIOPIGWA CHAPA
03/10/2023
TikTok · ziontv23 32 likes, 2 comments. “MWALIMU BOMBA...”
14/08/2023
FASIHI SIMULIZI: SEMI
==================
06/08/2023
KAZI ZA LIKIZO YA AGOSTI -KIDATO 1 -2023
06/08/2023
AGIZA NAKALA
01/07/2023
HOJA ZA MASUALA IBUKA YA INSHA YA MAELEZO
JINSI YA KUJIKINGA NA MAGONJWA
Kula chakula chenye virutubisho vyote na madini
Kutotumia chumvi, sukari au mafuta mengi
Kufanya mazoezi
Kupimwa mara kwa mara
Kupika vyakula vizuri
Kunawa mikono na macho
Kuchemsha maji au kuyatia dawa kabla ya kuyanywa
Kutozini au kutumia kinga
Chanjo kwa watoto
Kutochangia vifaa k**a vitana na nyembe na mavazi ili kujikinga na magonjwa ya ngozi.
Kulala ndani ya neti iliyotiwa dawa
Kufyeka nyasi karibu na nyumba na kutupa mikebe iliyo na maji
Kuweka dawa kwenye vidimbwi ili kuua mbu
Kutotumia vileo k**a vile pombe na sigara
Kuzuia kunyeshewa na mvua na kuvaa mavazi mazito wakati wa baridi au usiku
Kukohoa au kupiga chafya mtu akiwa ameziba pua na midomo
kutotema kikohozi ovyo.
Kutubu dhambi, kujua Mungu na kuomba kwa afya ya kiroho.
UNYANYASAJI/UDUNISHAJI WA WANAWAKE NA UTAMADUNI/TAASUBI ZA KIUME
a). Namna/njia za unyanyasaji
Kutorithi mali
Wanawake wajane kunyang'anywa mali na kufukuzwa
Ndoa za wake wengi (uke wenza).
Kurithi wanawake (wajane) kwa lazima.
Kukeketwa.
Kutawishwa au kunyimwa uhuru wa kutoka
Kutoelimishwa eti kwa akiolewa hatafaidi familia, atapanda wanaume vichwa.
Ndoa za mapema/lazima zinazosababisha kukatiza elimu yake (mahari haiwezi kurudishwa).
Kulazimishwa kuolewa na mtu asiyempenda.
Kunyimwa haki ya kusema.
Kupigwa na kutusiwa
Kubakwa.
Kunyimwa ajira kwa vile akipata mimba atajikokota kazini na atahitaji likizo baada ya kujifungua.
Ajira ya mtoto wa k**e ambapo anafanyishwa kazi ya sulubu na kupewa mshahara duni
Kutalikiwa.
Wanaume kutokuwa waminifu kwao hata kuwanyima mahitaji na kuwapa mahawara zao
Wanaume kupuuza majukumu ya kukimu familia.
Ubadhirifu wa wanaume na hali wake zao ndio walifanya kazi za kupatia hizo pesa
Kulaumiwa mtoto akikosekana hata mke mwingine kuolewa
Mahali pa mwanamke kuwa nyumbani au haruhusiwi kufanya kazi ofisini au kuongoza
Kulazimishwa kuvaa mavazi aina fulani na kukatazwa kuvaa aina mengine
Kufanyishwa kazi za nyumbani k**a mtumwa.
Kudhibitiwa na wanaume zao kwa sababu ya wivu.
b). Suluhisho
Hatua kali za kisheria kwa wanaowapiga, wanaowabaka na wanaotekeleza mila ya kukeketa na ndoa za mapema
Kufanya kampeni dhidi ya mila zinazochangia udunishaji wa wanawake
Kuwashauri watoto wa k**e badala ya kuwapasha tohara waende shuleni
Kuanzisha makao ya watoto wa k**e wanaotishiwa na mila mbaya
Kumwelimisha mwanamke kuhusu haki zake
Kuhimiza wanawake kupigania haki zao
Serikali kutenga pesa za kuelimisha watoto wa k**e ili kuwapa uwezo wa kiuchumi kwani wengi hunyanyaswa kutokana na umaskini na ujinga.
Mashirika ya kutetea haki za wanawake k**a FIDA na Maendeleo ya Wanawake.
Hazina ya kutoa mikopo kwa makundi ya wanawake k.v. K.W.F.T
Kuwapa wanawake nafasi sawa za ajira
Kutekelezwa kipengele cha thuluthi ya wanawake katika uongozi.
Kupunguza alama ambazo wasichana wanazopaswa kufikisha ili kujiunga na vyuo vya elimu ya juu.
Kubuni sheria za kuwawezesha kumiliki mali
JINSI WANAUME/VIJANA WA KIUME WANAVYODHULUMIWA
Kupigwa na wazazi/waelekezi wao
Kuchomwa kwa maji moto
Kukatwa sehemu nyeti
Wanawake kutokuwa waminifu kwao.
Kutusiwa
Kutofuliwa nguo na wake zao.
Kunyimwa chakula.
Kutelekezwa.
Kunyimwa unyumba eti kulipiza/ kumwadhibu
Kazi za sulubu.
Kufanyishwa kazi fulani k.v. kufulishwa nguo na kupikishwa mke akiwepo hata mbele ya wageni
Kuzomewa/ kugombezwa wake.
Kunyimwa pesa k**a hana ajira.
b). suluhu
Hatua kali za kisheria k.m kufunwa jela kwa wanaowapiga na kuwatelekeza.
Kufanya kampeni dhidi ya mila zinazochangia udunishaji wa waume.
Kuwashauri watoto wa kiume dhidi ya kuwakabili wake bila uhasama.
Kumwelimisha mwanamme kuhusu haki zake.
Serikali kutenga pesa za kuelimisha vijana wa kiume ili kuwapa uwezo wa kiuchumi kwani wengi hunyanyaswa kutokana na umaskini na ujinga.
Mashirika ya kutetea haki za waumme yaundwe.
Kuwapa wanaume nafasi sawa za ajira.
Kusawazisha alama za wanafunzi kujiunga na vyuo vya elimu ya juu.
UFISADI
Uovu, ubaya au uharibifu.
a). Aina
shuleni
Wanafunzi kudanganya katika mtihani
Kutoza mwanafunzi wa kidato cha kwanza pesa au chakula k**a nyama ili kuwalinda.
Kujipakulia chakula kingi.
Waalimu wakuu kuitisha hongo ili kuruhusu wanafunzi wajiunge na shule zao
Kupita wengine katika foleni wanapokwenda kupata chakula au chai hata benki
Kurudishiwa bakaa/chenji nyingi dukani na kutoirejesha kwa muuza duka.
Kuokota pesa njiani na kutoulizia ni za nani
Kughushi stakabadhi za mtihani, hati za umiliki shamba.
Kunakili kanda za muziki za wengine na kuziuza.
Waajiri kuajiri watu wa familia zao au makabila yao.
Daktari kuitisha hongo ili amhudumie mgonjwa
Polisi kuitisha hongo ili aruhusu magari ya huduma kwa umma yasiyofaa kupita
Kutohoa maziwa au kuyaongezea maji ili yawe mengi
Wenye maduka kuuza bidhaa kwa bei ghali
Kuuza bidhaa k**a sukari, nyama, nafaka, gesi na mafuta ya petroli ambazo hazijatimiza uzani unaotakikana
Madereva wanaoendea mafuta ya petroli kuuza kiwango fulani cha hayo mafuta na kuongezea ya taa au diseli
Kuuzia watu dawa bandia zisizotibu magonjwa
Ulanguzi wa dawa za kulevya
Kuiba pesa kwa kutumia risiti bandia au kufuruisha bei za bidhaa ili pesa zilizo juu wahusika wagawane
Kutoa ushahidi wa uongo
Kunyang'anya wajane na yatima mali zao
Uporaji wa mali ya umma k.v. nyanja za kuchezea watoto na misitu
Hakimu kuchukua hongo aididimize kesi
Madaktari kutoza wawele ada ya juu hata kuwafanyia upassuaji wasiouhitaji ili wapate pesa.
Wafanyakazi wa halmashauri za miji kujificha wanapomwona mtu akiegesha gari ili wadai anakwepa kulipa ada ya uegeshaji ili wahongwe au walikokote gari wapate pesa zaidi.
b). Sababu Ya Watu Kuushiriki Ufisadi
Tamaa ya kutajirika
Kutofahamu madhara/matokeo yake
Kukosa njia za kukimu mahitaji
Mishahara au mapato duni yasiyomwezesha mtu kukimu mahitaji yake au ya familia
Kutotosheka kwa kile mtu alichonacho.
Hofu ya kupata hasara au kukosa ajira.
Kutomjua mungu hivyo hawana imani.
Kuzugwa au kutekwa nyara kimawazo na kuwa mtumwa na shetani.
Wengine hulichukulia k**a jambo la kawaida tu au hali ya maisha.
Imani kuwa siku hizi mtu hawezi kupata chochote bila kutoa hongo.
c). Madhara ya ufisadi
Vifo kutokana na aajali barabarani au kutotibiwa bila hongo.
Majeruhi wa ajali za ajalini wengine hulemaa wasiweze kujifanyia kazi zao.
Kufutiliwa kwa matokeo ya mtihani .
Kufukuzwa shuleni au chuoni.
Umaskini kutokana na utoaji hongo ya pesa nyingi kisha kutopata kazi na ununuzi wa bidhaa kwa bei ghali.
Kushuka kwa viwango vya elimu wasiohitimu ipasavyo wanaporuhusiwa kujiunga na shule/ vyuo fulani
Kushuka kwa viwango vya huduma kwa umma kutokana na kuajiriwa kwa watu wasiohitimu vizuri.
Afisi za serikali kuchomwa wafisadi wakijaribu kusitiri ushahidi wa ufisadi
Nchi kurudishwa nyuma kiuchumi na kimaendeleo kutokana na pesa za miradi kuporwa.
Kupoteza ajira baada ya kufutwa kazi kutokana na ufisadi
Familia kuteseka baada ya kupoteza ajira
Kufungwa jela kwa wanaopatikana na kosa la ufisadi
Uharibifu wa mazingira na madhara yanayoendana nao kutokana na ufyekaji wa misitu
Kudidimiza haki pale kesi inakatwa vibaya kutokana na hongo hata asiye na makosa aweza kufungwa
Viongozi wafisadi katika mashirika na asasi kupoteza nyadhfa
d). Suluhisho/Njia za Kuukabili/kupambana/kuzuia Ufisadi
Hatua kali za kisheria kwa wafisadi
Kulipa wafanyakazi mishahara mizuri
Kuelimisha kuhusu madhara ya usisadi
Kufuta kazi wafisadi
Kunyang'anywa pesa au mali walizopata kifisadi
Watu kutangaza mali zao k.v. kwa kujaza fomu kudhihirisha hayo
Shirika la kukagua vipimo na ubora wa bidhaa
Majina ya wafisadi kutangazwa hadharani.
Ukaguzi wa hesabu za matumizi ya pesa katika asasi za serikali
Shirika la kupambana na ufisadi lichunguze wafisadi.
Kufumania wafisadi.
Kupiga picha kwa kamera ya video wafisadi k.v. polisi wakichukua hongo
Kujifunza kutosheka kwa kile mtu alichonacho na kuishi maisha ya kiwango chake.
Kuarifu polisi au shirika la mkupambana na ufisadi kuhusu visa vya ufisadi.
Kumjua na kumcha Mungu.
DAWA ZA KULEVYA/MIHANDARATI
Dawa ambazo huathiri utendakazi wa mwili.
a).Sababu za Kutumiwa
Masurufu au kuwapa vijana pesa nyingi za matumizi
Kujipa burudani
Shinikizo la rika kwa vijana
Ukosefu wa ushauri/kutojua madhara
Matangazo ya biashara
Shida k.v. ukosefu wa ajira na mahitaji ya kimsingi
Marafiki wabaya
Kukaa katika mazingira zinamotumiwa
Malezi
Kuvunjika kwa ndoa
upweke
Kujitoa haya k.m. makahaba
Shida kazini
Kudanganywa zina manufaa k.m. kumpa mtu nguvu ya kufanya kazi au kuerevusha
Kujipa hisia za kuwa huru na ujitambuaji
b). Madhara
Magonjwa k.v. saratani na ya zinaa
Vifo kutokana na ajali, magonjwa au dawa zenyewe
Kuiba ili kupata pesa za kununulia dawa za
Ubakaji
Hufilisi watu kwa kutumia pesa nyingi hata kuuza au kuzikodisha mali zao ili kuzigharamia
Jamaa kuathirika kisaikolojia wanapoona mwenzao akiKushindwa kuendelea na masomo.
Visa vya ubakaji.
Kupotoka kimaadili k.m. kuwa mwenye matusi, kupiga wengine, kuwa mgomvi hata mzinifu.
Kuwa mchafu k**a fungo k.m. kutooga, kutofua nguo, kutochanua nywele n.k.
Kuhisi mambo yasiyokuwepo (hallucination).
Wengine kushindwa kuolewa na kutoweza kupata watoto k.m. watumiaji wa miraa.
Kuvunjika kwa ndoa kutokana na kupiga mke, kutumia pesa vibaya.
Kufutwa kazi k.m. kutokana na ulevi.
Wazimu
Uhalifu
Jamaa ya mtumizi kuteseka ikimwona mwenzao akiangamia kutokana na kuzitegemea dawa za kulevya
Mhusika huathirika kimwili na kisaikolojia
Huathiri ukuaji wa mwili na akili
Wazimu
Huathiri uwezo wa kufikiri kwa kuua seli za ubongo
Hufanya mtu kupotoka kimaadili k.m. upyaro, vita, uchoyo, uzinifu
Kuvunjika kwa ndoa
Kufukuzwa shuleni
Kufungwa jela
Kuzaa watoto ambao hawajatimiza uzani wa wastani
Kufa kwa neva na viungo kukatwa
c). Suluhisho
Kuelimisha watu kuhusu madhara ya dawa za kulevya
Watu kumjua Mungu
Matibabu ya kurekebisha watumwa wazo
Kujitenga na marafiki wabaya
Kutoingia katika mandhari zinamotumiwa
Maelekezo kuhusu dawa za matibabu kufuatwa ipasavyo
Kutotumia dawa za matibabu kwa matumizi mengine yasiyo ya kutibu
Ukaguzi wa wageni na mizigo katika viwanja vya ndege
Hatua za kisheria kwa walanguzi, wauzaji na watumiaji
Kuongeza nafasi za ajira
Kukomesha matangazo ya biashara ya dawa hizo
Kuandika matahadharisho katika chupa na pakiti za vileo
UHALIFU/UTOVU WA USALAMA
a). Chanzo
Umaskini kusababisha wizi na uisadi
Dawa za kulevya kusababisha wizi au kubaka
Marafiki wabaya
Malezi mabaya
Malezi mabaya k.m. mtoto akiiba na kupelekea wazazi, wazazi hawamuulizi alikotoa vitu hivyo.
Tamaa ya mali kufanya watu kuiba, kushiriki ufisadi, n.k.
Hasira au kushindwa kujidhibiti kusababisha kumpiga na kumuumiza mtu hata kumuua
Tamaa kubwa au uchu kusababisha ubakaji.
Chuki na wivu huweza kusababisha mauaji
b). madhara
hofu/woga kutanda
kufukuza wawekezaji
umasikini/kupoteza mali
husababisha vifo
kuhama kwa watu/kutoroka
uhasama baina ya waja
uchumi wa hudorora/zorota
huibua utegemezi maana watu hawajabuni kiteka uchumi kwa woga wa kuibiwa
b). Suluhisho
Hatua kali za kisheria
Kuongeza askari kwani idadi yao ni dogo ikilinganishwa na raia
Kuunda vikundi vya kujilinda
Vituo vya polisi kuongezwa
Vitu vya thamani kuwekwa mahali salama k.m. benki
Kutotembea nyakati za usiku
Kutoendea mahali kusikofaa k.v. vichochoroni
Kuweka ua na lango
Mavazi yanayofaa kuzuia ubakaji
Kutoa mafunzo ya kujikinga
Nambari za simu za dharura za kuripotia uhalifu
Kumjua Mungu
Kuongeza nafasi za ajira
a). HAKI ZA BINADAMU
Kuishi
Kuingiliana/kutangamana
Uhuru na usawa
Elimu
Kuwa na Makazi
Kuwa/kupata Afya
Kiwango cha kurithisha cha maisha
Kukula chakula
Kuabudu
Kufanya kazi
Kumiliki mali
Kutunzwa uzeeni/ hifadhi ya jamii/wasio na uwezo
Kupiga kura
Kutobaguliwa
Kutoteswa kuminya habari
Uhuru wa kuongea/usemi
Kutembea na kuishi popote
Kesi kuendeshwa kwa haki
Kujitetea anaposhutumiwa
Kuoa au kuolewa na unayemtaka
Utulivu k.m. mtoto au mke asipigwe ama kuteswa
Huduma za matibabu
Jina na utaifa wakati wa kuzaliwa
Mtoto mlemavu apewe huduma maalum
Alindwe kutokana na mateso, kazi ya sulubu na kuhusishwa vitani
Alindwe dhidi ya mila na tamaduni zisizofaa
Haki ya kupata burudani
Haki ya faragha/ kuhifadhi siri zake
JINSI YA KUWALINDA NA KUWATUNZA WATOTO
Sheria kubuniwa za kuwalinda
Hatua kali kisheria kwa wanaodhulumu watoto
Shirika la kupigania haki za watoto
Makao ya watoto wanaokimbia wa dhuluma
Hazina ya wizara na maeneo bunge ya kufadhili watoto maskini (bursary)
Watoto kuelimishwa kuhusu haki zao
Kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kulinda mtoto
Elimu ya bure ili watoto maskini wafaidi
Shule maalum kwa watoto walemavu
Wananchi kuchanga kusaidia watoto maskini
Makanisa kusaidia watoto yatima
Shule kuwapa watoto maskini ufadhili
MAZINGIRA
Hali au mambo yanayomzunguka kiumbe katika sehemu anakoishi.
a). Jinsi Yanavyoharibiwa
Kufyeka misitu ili kupata mahali pa makazi ama kulima
Kufuga mifugo kupita kiasi
Kutupa taka ovyoovyo
Moshi kutoka katika magari na viwanda huchafua hewa
Dawa na mbolea za kemikali za kilimo huchafua udongo na maji.
Migodi kuacha mashimo ardhini ambayo hujaa maji na kuwa hatari kwa binadamu na kizalio cha mbu.
Kelele za vyombo vya mziki, viwanda, honi za magari na ndege
mafuriko kuchanganya choo pamoja na maji safi
Taka kutoka nyumbani na viwandani kuelekezwa mitoni.
b). Madhara
Ongezeko la joto duniani
Mvua za gharika
Uhaba wa mvua
Ukame na njaa
Uhaba wa maji
Kufa kwa wanyama wa majini k**a samaki
Magonjwa na vifo kutokana na kuathiriwa na maji machafu
Magonjwa ya mapafu kutokana na hewa chafu
Ukosefu wa mvua /kataji wa miti
Mmomonyoko wa udongo
Uhaba wa chakula
Maradhi yanayotakanana uchafu- mathalani kipindupindu
Vifo vya watu na binadamu kutokana na athari za madhara haya mfano saratani ya ngozi
Hewa huchafuka kutokana a moshi kutoka viwandani
Mazingira huchukiza
c). Suluhisho
Kupanda miti kusiko na miti na kule misitu imefyekwa
Elimu kuhusu madhara ya kuharibu mazingira na jinsi ya kuyatunza Uhaba wa maji.
Kukagua viwabda na hatua za kisheria k**a vinavyoachilia taka katika mazingira
Kutumia samadi badala ya mbolea za kemikali na dawa za kiasili kuua wadudu katika mimea na mifugo
Kutaifisha misitu
Askari wa kulinda misitu
Kutumia kawi mbadala na ambazo hazichafui mazingira k.v. kutokana na maji na jua
Mashimo na mapipa ya kutupa taka
Kuweka mifugo kulingana na eneo la malisho
Kutolima kando ya mito
Kutia choo cha binadamu dawa kabla ya kukiachilia mitoni
Kutumia magari ya umma
Kutumia taka k**a malighafi na kutumia vile vitu vyaweza kutumika tena
USALAMA BARABARANI
a). Vyanzo vya ajali
Madereva kutohitimu vizuri
Magari mabovu
Kutotii sheria za barabarani
Njia mbovu
Kubeba abiria na mizigo kupita kiasi
Kuendesha magari kwa kasi
Waabudu shetani kusababisha magari kupoteza mwelekeo
Kupita magari mengine bila uangalifu
Ulevi na athari zake
Wenda miguu kutokuwa waangalifu wanapovuka barabara
Kutodhibiti usukani vizuri
Uchovu kusababisha usingizi
Dawa za matibabu
Abiria kutolalamika au hata kumwambia dereva aendeshe kwa kasi wafike haraka
Kuchanganyikiwa
b). Suluhisho ya ajali/mapendekezo
Hatua za kisheria kwa wakiukaji kanuni za barabarani
Kuondoa polisi wafisadi barabarani
Kukarabati barabara
Ukaguzi wa magari ili kuhakikisha yafaa kuwa barabarani
Kufunza madereva upya
Mikanda au mishipi ya kujifunga kuzuia kujeruhiwa vibaya na vifo ajali ikitokea
Kuweka vidhibiti mwendo
Vifaa vya kutambulia madereva walevi na kasi ya magari
Uangalifu wakati wa kupita magari mengine
Kuwa mwangalifu wakati wa kuvuka barabara
a). SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Uvumbuzi wa umeme unaotumiwa kuangazia na kuendesha vyombo vingi
Matibabu kuwezesha watu kuishi kwa muda mrefu k.m. dawa,chanjo, upasuaji, upachikwaji viungo, miale ya kutibu saratani, n.k.
Kurahisisha na kuharakisha usafiri k.m. magari, pikipiki, ndege, k.m.
Kurahisisha na kuharakisha mawasiliano kunakosaidia wakati wa dharura k.m. rununu, mtandao, nukulishi, n.k.
Upashaji wa habari kuwezesha kupata habari kutoka kote duniani k.m. mtandao, redio, runinga, n.k.
Utengenezaji bidhaa viwandani kuharakishwa kutokana na mitambo inazoendesha na tarakilishi
Mimea na mifugo wanaokomaa haraka na walio na mazao mengi
Roketi inayowezesha kwenda katika mwezi na sayari nyingine
Silaha k**a bunduki za kupambana na maadui na wahalifu
Burudani bora k.m. sidi, video, mtandao, n.k.
b). Madhara hasi/ubaya/maovu ya teknolojia
Uavyaji mimba
Mauaji ya huruma
Tishio la dunia kuangamia kutokana na silaha za nuklia na viini vinavyotengezezewa maabarani
Uhalifu kuongezeka kutokana na wingi wa bunduki, simu na mtandao
Vyakula kutokana na mimea ina mifugo iliyokuzwa kisayanzi kudhuru afya
Wizi wa viungo vya mwili hata kuhasiwa bila hiari
Ajali za barabarani na za ndege zinazoua watu wengi
Upotoshaji kimaadili k**a vile filamu chafu katika mitandao na sidi
Kutumia vijusi kutengenezea viungo
Ongezeko la joto duniani kutokana na uchafuzi wa hewa
Ugaidi kutokana unaotekelezwa kwa mabomu
SIMU ZA RUNUNU
a). Faida
Kurahisha na kuharakisha mawasilano
Kupunguza gharama za usafiri
Mtandao huelimisha na hufahamisha habari
Kutuma pesa
Kuweka pesa/akiba
Burudani k.m. nyimbo, michezo
Kupiga nduru uhalifu unapotokeo
Ajira kwa wauzaji na watengenezaji
Ushuru kwa serikali
Shajara, kalenda, kamera, kikokotozi
b). Madhara
Burudani kusababisha ajizi
Uhalifu
Gharama kubwa hasa kuweka chaji na malipo kabla ya kutumia kuongea au mtandao
Mtandao kupotosha kimaadili
Hutoa miale ambayo yaweza kusababisha saratani
Kudanganya katika mitihani
Kufungwa jela kutokana na arafa za vitisho na matusi
RUNINGA/MAGAZETI
a). Faida
Ajira kwa wanahabari na watangazaji
Matangazo ya biashara
Kufunza maadili k.m. michezo ya kuigiza na vichekesho.
Kutuwezesha kufahamu sehemu nyingine za nchi na dunia
Kuelimisha k.v. vipindi vya fasihi
Kutalii Burudani
Kupasha habari
Kuangazia sehemu na watu wenye shida
Kukuza lugha
Kukuza uzaleno
b). Madhara hasi
Ajizi
Kupotosha kimaadili
Filamu ziazohimiza watu kuwa wazinifu.
Matangazo ya vileo
Kuenezea chuki na propaganda
Kuiga utamaduni wa kigeni usiofaa k.v. mavazi, talaka
Gharama ya kununulia
Kutopata muda wa kushauri watoto na kuomba
Wanafunzi kutosoma jioni
Mke na mume kutoongea kujadili mwelekeo wa familia
Wanaume kuchelewa kurudi nyumbani usiku wakitazama mpira
Migogoro kwa kutaka kutazama vipindi tofauti
Kelele na usumbufu kwa waliolala
UTALII
Hali ya kuzuru kwa kusafiri mbali ili kujivinjari au kufurahia mandhari
a). Faida
Fedha za kigeni
Ajira katika hoteli, udereva, n.k.
Uhifadhi wa mazingira
Kuboreshwa kwa miundo msingi
Mapato kwa serikali kutokana na ada ya kuingilia mbugani na kodi za mikahawa
Amani na maelewano nchini na duniani
Kuhifadhi mila na tamaduni zetu
Kupa nchi umaarufu duniani
Maeneneo kame kuweza kutumiwa ipasavyo k**a kivutio chao
Soko kwa mazao ya kilimo
Kuwapa wauzaji vinyago mapato
b). Ubaya/madhara hasi
Magonjwa k.v. ya zinaa
Matumizi ya mihandarati
Tabia zisizofaa k.v. Usenge zinazovunja ndoa na kueneza magonjwa k**a ukimwi
Upuuzaji wa miradi ya maendeleo serikali ikijengea watalii hoteli za kifahari na viwanja vya ndege ambavyo hutumika kwa nadra sana
Kusababisha watoto kuacha shule ili wawe wanawaelekeza wapate pesa
Kuhimiza mauaji wa wanyama kwa kununua pembe na ngozi
Kelele za magari yao husumbua wanyama na kukanyaga na kuharibu lishe yao
c). suluhu/Jinsi ya kuvutia watalii zaidi
Kudumisha usalama
Kuimarisha miundo msingi
Kutangaza nchi na vivutio nje
Kupunguza malipo katika hoteli za watalii
Kufahamisha wananchi kuhusu vivutio kupitia vyombo vya habari
Kuongezea wafanyakazi mishahara ili kuweka akiba waweze kuzuru maeneo yenye vivutio
Kuwapa wafanyakazi likizo ya kutosha
UMASKINI
a). visababishi vya umasikini
b). Suluhisho
Kuongeza nafasi za ajira
Kutoa mikopo rahisi kulipa
Kupunguza bei ya pembejeo
Elimu ya bure
Kupigana na ufisadi
Upangaji uzazi ili kupunguza idadi ya watu
Bei bora ya mazao ya kilimo
Kazi kwa vijana
UKEKETAJI
a). Sababu
Kupunguza tamaa
Njia ya kukomaa
Mila na tamaduni
Kuwatofautisha na wengine.
Ushujaa
b). Madhara
Kifo kwa kutokwa na damu sana
Uenezaji wa magonjwa
Shida wakati wa hedhi na kujifungua
Ndoa kuvunjika
Kibali cha kujiingiza katika myenendo isiyofaa
Utengano kati ya waliotahiriwa na ambao hawajatahiriwa -migogoro
Kuzua utabaka baina ya waliopashwa na wasiopashwa tohara
c). Suluhisho
Hatua za kisheria kv kuwafungulia mastaka
Elimu kuhusu madhara hasi yatolewe
Mawaidha kwa wasichana dhidi ya ukeketaji
Makao ya watoto kuanzishwa
Wasichana wafadhiliwe kwenye shule za mabweni
Kuunda shirika la kulinda watoto wa k**e
GHARAMA YA JUU YA MAISHA NCHINI KENYA.
Jinsi serikali inapambana nayo
Kupunguza bei ya bidhaa ya kimsingi
Kupunguza/kufutilia mbali ada za huduma za kimsingi k**a vile matibabu, elimu, n.k
Kusisitiza ulipaji wa ushuru na wote
Kupanua nafasi za kazi/ajira
Kupambana na tatizo la ufisadi
Kuhimiza wananchi na mashirika mbalimbali kubuni nafasi za kazi
Kupunguza/kuunganisha idara mbali mbali za serikali kuu na kaunti
NJAA
a). visababishi vya njaa
matumizi mabaya ya ardhi ya upanzi
kiangazi kingi kinachoathiri mimea
maradhi na wadudu wanokula mimea
matumizi mabaya ya chakula
mbinu mbaya ya kuhifadhi chakula
wizi/utapeli wa vyakula na mabwenyenye
maswala ya ujenzi wa makazi(real estate)
ukosefu wa pembejeo
idadi kubwa ya watu/walaji
miundo misingi duni km barabara inayopelekea chakula kuharibikia shambani
utegemezi wa vyakula vya msahada
mipango duni ya serikali/wananchi kuhusu maswala ya vyakula
kudhamini mimea isiyolika.
Uhamiaji mijini- vijana wengi walio na nguvu za upanzi wamehamia mijini.
Ukosefu/mipango duni kuhusu chakula.
b). Njia za kupunguza/kuzuia njaa
Kilimo cha unyunyizaji maji
Kupunguza bei za pembejeo
Njia bora za kuhifadhi mazao
Mimea na mifugo inayokomaa haraka
Utumizi wa samadi na mbolea
Kuelimisha wakulima kuhusu kilimo bora
Kutayarisha mashamba mapema
Serikali kununua mazao ya wakulima na kuyahifadhi.
Wakulima kuhimizwa wapande kwa kupewa pembejeo kwa bei nafuu.
Serikali kuhimiza njia za kisayansi za upanzi(GMO)
DINI
a). Uzuri wa dini
Kufunza maadili
Kusaidia maskini
Kuanzisha shule na hospitali
Ajira kwa padri, kasisi n.k.
Kuandaa watu kwa maisha baada ya kifo
Kufariji/kuliwaza wenye dhiki
b). Ubaya wa dini
Tamaa ya pesa
Biashara
Ubakaji wa watoto
Kuuza uponyaji
Nyingine kutosaidia wenye shida
Vita/jihadi(wislamu)
Kuruhusu waovu bora watoe pesa
Kutoenda hospitalini
Kuendeleza maovu k.v. uzinifu, ushirikina, uabudu shetani, n.k.
MAASI YA VIJANA
a). visababishi
Dawa za kulevya
Shiniko la kikundi/rika
Filamu mbaya
Kudhibitiwa kupita kiasi
Kukosa nidhamu
Malezi mabaya/udekezaji
Kubomoka kwa msingi wa jamii
Ufukara kusababisha kujiunga na makundi haramu
Kukata tamaa
Kutumiwa vibaya na wanasiasa
b). Suluhisho
Kujiondoa kundini
Kuimarisha uchumi
Kuwashauri vijana
Kujenga udhabiti wa jamii
Utiifu na unyenyekevu
Kuwa na usemi
Kuvumiliana na kusameheana
Uaminifu na kuaminiana
Kutochagulia watoto taaluma na wachumba
Wazazi kutolazimisha watoto taaluma au kozi wasizotaka
Kutumia pesa vyema bila ubadhirifu
Kutopendelea na kulinganisha watoto kiuwezo
kutotumia dawa za kulevya
Kuomba pamoja
wazazi kutopendelea watoto fulani
Baba kutimiza majukumu yake ya kukimu jamii
Kutodhibiti mke na watoto kupita kiasi
Uadilifu
Kushiriki kazi
MAMBO YANAYOATHIRI UTAIFA/UMOJA NA UTANGAMANO/AMANI
Ufisadi k.v. kuajiri watu kimapendeleo
Ukabila
Viongozi kueneza chuki
Serikali kutoakisi uwakilishaji wa taifa zima
Usalama kukosekana
Ukosefu wa ajira
Matamshi mabaya ya viongozi
Kupanda kwa gharama ya maisha
Majanga ya kiasili
Kutojenga miundo msingi kwa usawa
Kupendelea maeneo fulani katika ugawaji wa raslimali
Ukimbizi wa ndani kwa ndani
Ubomoaji wa nyumba
b). Suluhisho
Lugha ya taifa kuhimizwa
Kukabiliana na ufisadi
Usawa katika ugawaji wa raslimali
Kuelimisha kuhusu umoja wa kitaifa
Tamasha za kitamaduni
Kutalii sehemu nyingine za nchi
Ndoa za makabila tofauti
Serikali ya muungano
Viongozi wachochezi kuchukuliwa hatua kisheria
USAFIRI WA MATATU
a). Faida
Kurahisisha na kuharakisha usafiri
Njia murwa ya ajira.
Ushuru kwa serikali.
Ni biashara
Njia ya kutajirika
Huduma za dharura
b). Madhara
Husababisha ajali
Wizi kuzidi
Ufisadi wa polisi kuongezeka
Kuongeza nauli ghafla
Ujeuri wa madereva na mataniboi
Kuchelewesha watu njiani
MTANDAO/UTANDAWAZI
a). Umuhimu
Kupasha habari za taifa na kimataifa
Kuelimisha k.m. kuhusu afya
Kuburudisha k.m. vibonzo
Matangazo ya biashara
Ajira k.m. wahariri, wauzaji
Mapato kwa serikali
Kutangaza nafasi za ajira
Elimu k.m. uchambuzi wa vitabu vya fasihi na mashairi
Mpwito wa wakati
Kukuza umoja(kurasa za fesibuku na wazapu)
Kurahisisha utafiti
b). Hasara/ubaya/changamoto
Ulaghai/utapeli kwa kushawishiwa kupitia mtandao
Kueneza /kusambaza/kuhimiza ukabila
Ajizi
Kupotosha watu
Filamu ziazohimiza watu kuwa wazinifu.
Matangazo ya vileo/mihadarati inayoathiri kihasi
Kueneza chuki na propaganda
Kuiga utamaduni wa kigeni usiofaa k.v. mavazi, talaka
Gharama kali ya kununulia vifaa/ada ya kuingia mtandaoni
Kutopata muda wa kushauri watoto na kuomba kwa kuwa mtandaoni kila mara.
Wanafunzi kutosoma jioni/kupoteza muda
Kuvunja uchumba
Vifaa vya mtandaoni k**a simu/kompyuta huleta magonjwa ya macho na kansa
UDANGANYIFU/WIZI WA MITIHANI YA KITAIFA LA KENYA
a). Njia za udanganyifu
Matumizi ya rununu
Walimu kuwasaidia
Wanafunzi wa vidato vingine kuwafanyia
Kusaidiana kwa watahini wenyewe katika cha mtihani n.k
Kusoma kutoka vitabuni na vijikaratasi walivyovitiyarisha
Kutoa majibu mtandaoni.
Kupiga maswali na majibu picha
b).Suluhisho
Wanafunzi walenge kupata alama kulingana na uwezo wao
Wazazi wawe na matarajio kulingana na uwezo wao.
Mtazamo wa jamii ubadilishwe
Wanafunzi na shule washindane (zishindane) kulingana na kiwango
Mfumo wa elimu ubadilishwe usiegemee sana kupita mtihani pia uangazie vipawa vya wanafunzi
Wasimamizi wawe macho wakati wa kusimamia mtihani
Hatua kali kuchukuliwa kwa wale watakao juhusisha na udanganyifu (hoja zozote sita)
Kuondoa wanafunzi wengine shule wakati mtihani upo
Kupiga marufuku matumizi ya simu shuleni
Baraza la mtihani/serikali isaidie shule ziwekwe kamera zitakazonasa wezi wa mtihani
KATIBA MPYA
a). Faida
Kuzingatiwa na haki za binadamu
Ugavi wa rasilimali utafanywa kwa uwazi
Uongozi mzuri na uajibikaji
Kuwepo kwa usawa
Ugatuzi utaleta maendeleo
Kushirikisha wakenya wote katika maendeleo
Maswala ya vta baada ya ucahguzi yatotuliwa
Idara ya mahak**a kuwa kuwa
Umoja wa kitaifa
Utangamano
Utatilia maanani haki za jamii haswa zile zinazohisi kutengwa
Utaimarisha democrasia
Utaimarisha kuhusisha wananchi katika utawala
b). ubaya/hasara
Ufisadi-ubadhirifu wa pesa
Kuvuruga baadhi ya tamaduni k.m nafasi ya mwanamke
Kuendeleza ukabila - kuruhusu ugatuzi uliogawa watu kimaeneo/kikabila
Baadhi ya maeneo kubaki nyuma kimaendeleo
Migogoro kati ya viongozi k.m magavana na maseneta
Utata katika kuelewa, kutafsiri au kufasiri vifungu vya katiba mpya
Serikali kuu kutoachilia baadhi ya vitengo vya utekelezaji wa katiba mpya
Matumizi mabaya ya mamlaka na viongozi
Kuna baadhi ya vipengele vya katiba mpya ambavyo havijatiwa baadhi ya masharti
c). suluhu
vipengele tata vibadilishwe
viongozi wahakikishe katiba inafuatwa ifaavyo
hatua kali kwa viongozi wafisadi katika Nyanja za uongozi.
PESA ZA HAZINA YA VIJANA.
a). Faida.
Kuanzisha miradi ya kuwaletea pesa.
Kuinua kiwango chao cha maisha.
Utangamano wa vijana.
Kuondoa ukosefu wa kazi.
Kupunguza uhalifu na kudumisha maadili.
Kuwafanya wawajibike maishani.
Kuwashirikisha katika ukuaji wa uchumi.
Kukuza vipawa vyao.
Kuboresha miundo msingi na mazingira kwa jumla.
b). Hasara
Ubadhirifu k.m. Kushiriki anasa.
Ufisadi miongoni mwa wasimamizi
Mapendeleo kinasaba.
Kutokuwa na usawa/utaratibu wa ugawi
Chuki miongoni mwa waliopata na wale wasiopatana
Wizi/uporaji miongoni mwa vijana hasa wale masikini.
Uhuru utakuwa mwingi kwa wananchi.
Kuingiliwa na vyombo vya kisias
UMUHIMU WA KUIMARISHA MIUNDO MISINGI
a). Mifano ya miundomisingi
Barabara
Nyaya za kusambaza umeme
Bandari
Viwanja nya ndege
Reli
mabomba ya maji
umeme
shule
hospitali
b). umuhimu
Ajira –kazi za ukarabati na ujenzi huongeza nafasi za kazi
Huimarisha uchumi
Bidhaa na watu huweza kusafirisha kwa haraka
Itavutia wawekezaji wa nje
Itavutia watalii watakaotupa ushuru wa kigeni
Bidhaa zilizo na maisha mafupi k,v samaki/ matunda hufika sokoni kwa muda mzuri
Watu huweza kupata maji masafi kwa kutumia mabvomba maalum
Ajali za barbrani zaweza kuepukwa iwapo barabara zitakuwa nzuri
Mandhari hufurahisha macho
Biashara miongoni mwa nchi yetu na nchi za maeneo haya k.v Uganda , Tanzania na Sudan Kusin huweza kuimarisha – Reli kutoka Lamu hadi Sudan Kusini.
VISA VYA KISHETANI SHULENI
Mikutano ya usiku ya utoaji kafara.
Zawadi zinazotolewa za kupumbaza akili.
Kupiga chale miili/ uchoraji unaohusu utoaji damu.
Ulaji viapo.
Matumizi ya mihadarati.
Ukatili kwa wenzao wasiotaka kuungana nao.
Ugawanaji kwa vikundi.
Migomo
Uchomaji shule.
Kudharau walimu.
Matumizi ya ishara zisizoeleweka kwa kila mtu.
Ushoga/ usagaji
Vijana kuwa na pesa nyingi sana zisizoeleweka zatoka wapi.
kukaidi adhabu
kutofuata sheria za shule
mahusiano ya kimapenzi
Uavyaji mimba.
b)Mapendekezo/jinsi ya kusuluhisha
Kuimarisha ushauri – nasaha
Kukadiria masurufu ya wanafunzi na kuyawekea viwango.
Kuhamasisha wanafunzi juu ya ubaya wake.
Kuwaalika wajuzi wa kidini.
Kuwahamasisha wazazi kuhusu umuhimu wa kuwapa watoto wao mahitaji ya kimsingi.
Kuelekeza wanafunzi kuhusu mbinu chanya za kufaulu masomoni.
Kuwashirikisha katika michezo na njia mbadala za burudani.
Kuchuja sinema / filamu zinazotazamwa shuleni.
c) MIGOMO YA WANAFUNZI.
Suluhu ya migomo ya wanafunzi
Kusikiliza malilio ya wanafunzi.
Wanafunzi wenyewe wachague viranja watakao wawakilisha.
Ushauri nasaha ufanywe.
Wanafunzi wapewe muda wa kupumzika
Makaazi/darasa/mabweni kuboreshwa.
Kuondoa adhabu ya viboko shuleni.
Kuhusisha wazazi kwenye mikutano na jinsi ya kuadhibu.
Washikadau wa elimi(walimu,wazazi n.k) kuhushwa katika maslahi ya wanafunzi.
Serikali iwaadhibu walimu k**a kuwafuta kazi wanaowadhulumu wanafunzi.
Wanafunzi wanaogoma na kuharibu mali ya shule wachukuliwe hatua kali k**a kufukuzwa shuleni au kufidia mali waliyoharibu.
Wanafunzi wakaguliwe kila mara ili wasimiliki silaha na petroli za kuharibu shule.
Mafundisho ya dini kuhusu maadili ihusihwe.
KUORODHESHA SHULE KUTOKANA NA MATOKEO YA MTIHANI
a). ubaya
Shule haziko katika kiwango sawa/kiraslimali.
Mbinu potovu kutumika katika ushindani ikiwemo wizi wa mitihani
Wazazi hugharamika pakubwa ili kukidhi ushindani huo,mfano ongezeko la karo.
Kuna maswala kadhaa yanayofanyika shuleni kando na Elimu ya vitabuni hivyo si haki kuordhesha shule kwa kigezo kimoja tu.
Walimu na wanafunzi hutumia muda mwingi kuboresha elimu ya vitabuni na kusahau maswala mengi muhimu k**a vile michezo.
Wanafunzi kushurutishwa kurudia madarasa.
Wanafunzi kutopata muda wa kutosha kupumzika na kutumikia jamii zao.
Kuongezeka kwa visa vya mauaji/maafa ya wanafunzi ambao hukosa nafasi ya juu au wanaolazimishwa kurudia madarasa.
Vitisha kwa walimu wakuu ambao shule zao hazipati nafasi za juu.
b).umuhimu/uzuri
Kuwepo ushindani miongoni mwa wanafunzi na walimu/shule
Huimarisha utendakazi miongoni mwa walimu/wanafunzi kufanya kazi kwa bidii
Wazazi kushiriki kikamilifu katika masomo ya watoto wao.
Ili kuimarisha kwa miundo msingi katika shule zetu/ili kuwe na matokeo bora.
MCHANGO WA VIJANA KUENDELEZA UGATUZI
Kushiriki biashara ndogo ndogo
Kushiriki katika uchaguzu wa viongozi
Wanaoajibika kushiriki katika siasa
Kushiriki katika kazi za ujenzi wa miundo msingi k**a vile barabara
Kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa amani/usalama k**a nguzo za maendeleo
Kushiriki katika makundi ya kujiinua kiuchumi
b). matatizo ya vijana
Ukosefu wa usalama
Mimba za mapema
Ukosefu wa karo ya kujiendeleza kielimu
Ukosefu wa pesa za kuanzisha miradi.
Shinikizo la rika
Utandawazi-matumizi mabaya yavyombo vya mawasiliano
Pengo kuu la kizazi
Uozowa jamii
Utumizi wa mihadarati
NDOA ZA JINSIA MOJA
a)serikali isihalalishe
ndoa k**a hizi hazikubaliwe kitamaduni
Ni kinyume cha imani za kidini
Ni imani potovu inayotokana na tamaduni za kigeni tofauti za kidini hasa ya wakisto na waislamu.
Zitzitaweza kusababisha ingawanyisha wa taifa
Zitakumja asai za ndoa
b)Zihalalishwe kenya
Nchi nyingi za kimagharibi zime halalisha, uwezekano wa kubaguliwa nimkubwa
Ni haki ya kidemokrasia ya watu.
Ni unafuu kwa walioshindwa kudunisha ndoa za kawaida
Itapunguza taasubi
MAZINGIRA
a). madhara ya uharibifu wa mazingira
Ukataji wa miti / ukosefu wa mvua
Mmomonyoko wa udongo
Uhaba wa chakula
Maradhi yanayotakanana uchafu- mathalani kipindupindu
Vifo vya watu na binadamu kutokana na athari za madhara haya mfano saratani ya ngozi
Hewa huchafuka kutokana a moshi kutoka viwandani
Mazingira huchukiza
b). Suluhu
Adhabu kali kwa wenye kuharibu miti
Upanzi wa miti
Maafisa wa kilimo kutumwa nyanjani
Wakulima kuelimishwa kuhusu njia mwafaka za kuhifadhi mazingira
Wizara ya afya kuhudumia waathiriwa wa uchafuzi huu
Wananchi wahamasishwe kuimarisha ukuzaji wachakula
Wanaohifadhi mazingira watuzwe
Sheria kwa viwanda
KUIMARISHA MASOMO
Vipindi kuongezwa.
Pawepo na walimu wa kutosha.
Vitabu vya kutosha.
Teknolojia mpya kushirikishwa kufunza Kiswahili.
Ushauri kuhusu mtazamo hasi eti Kiswahili ni kigumu.
Kubuniwa kwa Baraza la Lugha nchini ili kutoa mwelekeo kuhusu matumizi ya Kiswahili,uundaji msamiati,n.k.
Marekebisho kwa silabasi – ni pana sana kwa miaka mine.
Ushirikiano kuimarisha baina ya walimu na wanafunzi ili kukuza lugha ndani na nje ya darasa.
Kiswahili kutambulika k**a lugha ya wenyeji/wakenya na ya kujivinia(uzalendo) – si mtihani tu.
Kuandaa makongamano zaidi baina ya shule mbalimbali.
Maktaba ya shule yawe na vitabu zaidi vya Kiswahili ,vya aina kadha na majarida yajae ili kuwapa motisha.
Mashindano ya uandishi wa insha.
MAFURIKO
a). madhara
Kuharibiwa kwa barabara kwa kuwa teketeke.
Madaraja kubomoka.
Mimea kuoza – hivyo kutokua na mazao mema.
Nyumba na majengo mengine kuharibiwa.
Kukwamiza shughuli/kazi za kujitafutia riziki au za ujenzi wa taifa.
Kisingizio cha wengine kuzembea kazi.
Magonjwa kutokea.
Kiwango cha uchumi kuzorota – mavuno machache ukarabati mwingi wa miundo- msingi.
Kuzidisha umaskini.
Vifo vya watu,ndege na wanyama.
b). suluhu
kuziba vidimbwi vya maji
kuchimba mitaro ya kupitisha maji
watu kuhamia maeneo ya juu
kuunda vidude kwenye eneo ili kupunguza nguvu za maji
kupanda mimea inayotumia maji mengi
kuzuia kulima/kukingua kando ya mito
makao yasijengwe karibu na mito
MFUMO WA UGATUZI NCHINI
a).Ufanisi wa mfumo wa ugatuzi
Nafasi za kazi zimebuniwa.
Makundi na makampuni mbalimbali yanaweza kufanikiwa kupata kandarasi mbalimbali k**a vile za ujenzi wa barabara, mabwawa za taifa nk
Ugatuzi sawa wa raslimali za kitaifa kwa kaunti zote.
Huduma za serikali zimeletwa karibu na wananchi.
Wananchi wamepata fursa ya kuendeleza kaunti zao k**a inavyofaa kutegemea mahitaji yao.
Imekuwa rahisi kumulika namna ambavyo pesa zilizotengewa kaunti zinavyotumiwa.
Imeokoa wakati wa kushughulikia maswala fulani kwani hakuna kutafuta huduma mbali.
Nafasi katika taasisi za elimu ya juu zimeweza kunufaisha wenyeji kinyume na ilivyokuwa hapo awali.
Huduma nyingi za kijamii na za kimsingi zimeletwa karibu na wanaoishi katika kaunti husika.
Wananchi wanahusishwa vilivyo katika kufanya maamuzi muhimu katika maeneo yao, kwa mfano kuhusishwa katika bajeti, miradi ya shule, barabara nk.
Ushindani chanya baina ya kaunti/maeneo mbalimbali.
Ushirikiano wa kibiashara baina ya kaunti mbalimbali.
b). Changamoto za mfumo wa ugatuzi
Ufisadi miongoni mwa maafisa wa kaunti hasa wakati wa kupeana zabuni.(Ufisadi umegatuliwa)
Ukabila na mapendeleo kwa mfano kwa misingi ya ukoo au sehemu anayotoka kiongozi.
Kaunti zingine ni changa sana kiuchumi na kimaendeleo.
Mfumo huu ni swala geni zaidi nchini – kuna changamoto kwani hakuna tajriba ya awali ya kurejelea.
Huenda maeneo mengine katika kaunti yakatengwa au kupuuzwa huku mengine yakipendelewa.
Kunaweza kutokea chuki, kutoelewana na kutoaminiana miongoni mwa watu wa maeneo mbalimbali wakiwemo viongozi.
Ushindani usio na manufaa baina ya serikali za kaunti na serikali kuu.
Kunyosheana kidole cha lawama kati ya magavana na maafisa katika serikali kuu kuhusu kutokuwepo kwa miundo msingi bora.
Matumizi mabaya ya pesa kwa kutoa huduma zinazofanana kati ya serikali kuu na zile za kaunti.
Ubadhirifu na matumizi mabaya ya raslimali.
Wengi wanaoshikilia nyadhifa mbalimbali katika serikali za kaunti hawana tajriba ya kutosha.
Kuzorota kwa baadhi ya huduma k**a vile ya afya.
36. KWA NINI WATU HUNYWA POMBE
Umaskini unaosababisha upikaji wake.
Uzembe.
Ukosefu wa ajira kisha kuuza ndio mbadala
Mshahara duni.
Kutowajibika.
Shinikizo la wanarika au marafiki.
Bei yake ambayo ni rahisi/bei nafuu kuliko pombe inayotengenezwa na
kampuni k**a vile Kenya Breweries, Keroche n.k.
Kupatikana kwa urahisi.
UMUHIMU WA MICHEZO SHULENI
Huimarisha afya ya wanafunzi
Huwasaidia kutumia muda wao vyema
Huwawezesha kukuza vipawa vyao
Huwachangamsha baada ya siku nzima masomoni
Huwafunza jinsi ya kutangamana
Huwakutanisha na wanafunzi wa shule zingine
Huimarisha uhusiano kati ya wanafunzi na walimu
Huwafungulia milango ya heri baadaye maishani/ajira
Huchangia katika kujua tamaduni za wengine.