CHAMA Cha Kiswahili Isiolo - chaki

CHAMA Cha Kiswahili Isiolo - chaki Kukuza.kufunza,kuimarisha lugha ya kiswahili iweze kuzungumzwa kwa ufasa k**a kigezo mwafaka cha kuunganisha watu wa matabaka yote.LUGHA MOJA,JAMII MOJA.

12/11/2023

ARTIFICIAL INTELLIGENCE -AKILI MNEMBA.

15/04/2016
18/12/2015

Maneno ambayo si ya kiswahili yanayotumiwa vibaya:
1)Gonjeka -Ugua
2)kenye - Chenye/vyenye
3)Wakisha Tv/redio -Washa
4)Tangia -Tangu
5)maziwa mala/lala- Maziwa ya mtindi/ghururi (yoghurt )
6)Kula miwa - mumucha miwa
7)Kula peremende--mumumya peremende au p**i
8)Kula miraa - tafuna miraa
9)Kunya maji -kunywa
10)Ngaro - kiu

05/12/2015

MAKOSA ---- SAHIHI
1)Bomoa nywele-fumua
2)Hamjamboni?-Hamjambo?
3)Boeka-Chushika
4)Simu inalia -inakiriza
5)Poesha chai,maji nk-poza
6)stima -umeme
7)Chunga chai/majani-chingirisha machicha
8)Panda gari -abiri
9)Osha nguo -fua
10)Oga miguu /mikono/uso -nawa

12/11/2015

Binadamu hujifungua, mnyama huzaa na ndege hutaga.
Binadamu hunenepa, mnyama hunona
Binadamu huaga, mnyama hufa.
Binadamu huwa mjamzito, mnyama huwa na mimba.
Binadamu /mnyama hukua, mimea hustawi.
Mbegu huota, meno/nywele /kucha humea.

28/10/2015

Chakula hakikarangwi ila hukaangwa. Kwa hivyo usiseme nyama Karanga. Karanga ni aina ya mmea(njugu). Njugu karanga au njugumawe hukaangwa.

23/08/2015

RUSHWA-hongo,chai,mlungula,chauchau,kiinikizo,kadhongo,chirimiri,mvunguulio,kilemba.

19/08/2015

Maneno ya Sheng' yanavyomaanisha katika KISWAHILI:
Masa-maovu,makosa
Buda-kibogoyo;ndovu mzee
Bamba-k**ata kwa nguvu na ghafla na kubaka mtu.
Kwa hivyo ni makosa kuwaita mama *masa na baba *buda.
Ukisema *amenibamba unamaana yakuwa amekubaka.

Address

Isiolo

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when CHAMA Cha Kiswahili Isiolo - chaki posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category