22/03/2024
Matini mazuri kuliko mengine , bahasha k**a zawadi
-----------------------------------------------------
Jana tarehe 21 , Machi , mwaka huu katika majengo ya chuo kikuu cha Burundi , bewani Mutanga ilikuwa furaha tele kwa wanafunzi waliochaguliwa matini yao katika shindano lililobatizwa " zawadi ya Fasihi RUMURI , Prix littéraire RUMURI Kwa lugha ya Kifaransa au Literary Price RUMURI kwa lugha ya kimombo " .
Shindano hilo lilikuwa la tano kwenye orodha lao kuanzia mwaka elfu mbili na kumi na nne ( 2014 ). Shindano hilo lilikuwa katika lugha nne zifuatazo : lugha ya kifaransa , lugha ya kimombo , lugha ya kirundi na lugha ya kiswahili . Wanafunzi waliohudhuria katika shindano hilo la tano ni 114.
Wanafunzi 32 katika lugha ya kifaransa , wanafunzi 33 katika lugha ya kimombo , wanafunzi 28 latika lugha ya kiswahili na wanafunzi 21 katika lugha ya kirundi.Katika kila lugha , watano watano wa kwanza katika lugha hizo zote waliopewa zawadi , ukitoa lugha ya kifaransa ambacho sita ndio waliopewa zawadi
Mwanzishi wa shindano " zawadi la fasihi RUMURI " ni mwalimu -msaidizi wenye chuo kikuu cha Burundi ambaye anaitwa Aminadab HAVYARIMA. Mwalimu huyo alikuwa mwanafunzi wakati wa kuanzisha shindano hilo.
" Usipojizoeza kusoma vitabu , hutaandika kamwe mazuri " . Yaliyonenwa na mwalimu huyo Aminadab HAVYARIMANA. Kitu kingine alichosema ni kuwa waliopewa zawadi wote hawakupatwa na umasikini maishani mwao kutokana kuwa wanatafutwa na tajiri wengi au wanajiandalia kazi zao.
Kwa mchango wa mama-mlezi wa kiswahili nchini Burundi , bibi Dorothée NSHIMIRIMANA , alishukuru sana wanafunzi-wandishi waliopewa zawani na kushauri wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Burundi kuwa na hamu ya kujizoeza kuandika matini na vitabu ili nchi yetu na hawo wajulikane katika nchi za Afrika mashariki .
Wanafunzi wote wanaosoma kwenye vyuo vyote nchini burundi wanaruhusiwa kuhudhuria katika shindano hilo. Shindano hilo " Zawadi la Fasihi RUMURI linashirikiana na chuo kikuu cha Burundi , chuo kikuu cha ziwa la TANGANYIKA , Chuo kikuu cha NGOZI na chuo kikuu cha GITEGA na kupigwa jeki kifedha na ubalozi wa ufaransa nchini Burundi na chuu kikuu cha Burundi
nchini Burundi