Elimu ya Fedha kwa Watoto

  • Home
  • Elimu ya Fedha kwa Watoto

Elimu ya Fedha kwa Watoto Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Elimu ya Fedha kwa Watoto, Educational consultant, Morogoro, .

Lengo ni kujenga misingi kwa watoto kwenye eneo la fedha.Inawalenga watoto wa kuanzia miaka minne kuwafundisha kwa vitendo kuhusu kipato,matumizi,madeni,akiba na uwekezaji.

Mwanao ana shilingi 10,000 na anatakiwa kununua vitu vitano(5) muhimu katika listi iliyopo chini hapo.Pia ana lengo la k...
28/01/2025

Mwanao ana shilingi 10,000 na anatakiwa kununua vitu vitano(5) muhimu katika listi iliyopo chini hapo.Pia ana lengo la kuweka akiba.Je atachagua nini na kwa nini?
☆Mkate: 2,000
☆Maziwa: 3,500
☆Juisi: 4,000
☆Chokoleti: 2,500
☆Sabuni: 1,500
☆Chipsi: 3,000
☆Mayai: 4,500

# Elimuyafedhakwawatoto

Kulikuwa na kijana mdogo aitwaye Juma, mwenye umri wa miaka 10. Juma alipenda sana kusaidia wazazi wake, lakini pia alik...
21/01/2025

Kulikuwa na kijana mdogo aitwaye Juma, mwenye umri wa miaka 10. Juma alipenda sana kusaidia wazazi wake, lakini pia alikuwa na ndoto ya kununua baiskeli. Siku moja alimuuliza baba yake, “Baba, watu hupataje fedha ili kununua vitu wanavyotaka?”

Je wanao wanajua wapi na vipi fedha zinapatikana?


15/01/2025

Chemsha Bongo kwa mwanao!

1.Unapata shilingi 500 kila siku k**a pesa za matumizi. K**a ukiweka akiba ya shilingi 200 kila siku, utakuwa na kiasi gani baada ya:

A.Wiki moja?

B.Mwezi mmoja wa Januari

2.Unataka kununua gari la kuchezea lenye thamani ya shilingi 10,000. K**a unaweka akiba ya shilingi 500 kila wiki utachukua muda gani kufikia lengo lako?

Send a message to learn more

21/11/2024

Mwalimu mzuri na bora kabisa ni *KUFANYA* . Hivi ndivyo tunavyofanya kupitia program ya Elimu ya Fedha kwa watoto ambapo watoto wanafanya kwa vitendo kabisa kwenye maeneo matano muhimu ya fedha(Kipato,matumizi,madeni,akiba na uwekezaji).Ni kila jumamosi kuanzia saa nne hadi saa sita benki ya Crdb tawi la Mandela.Ikiwa mwanao hajaanza kuweka akiba,kufanya uwekezaji basi mlete ajifunze.

Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi nusu  ya Watanzania wanaishi chini ya dola mbili(Tshs 5400) kwa siku(chini ya mstari wa u...
05/11/2024

Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi nusu ya Watanzania wanaishi chini ya dola mbili(Tshs 5400) kwa siku(chini ya mstari wa umasikini).Moja ya sababu za umasikini ni ujinga.Program ya Elimu ya Fedha kwa watoto inayoendeshwa na benki ya CRDB tawi la Mandela Morogoro kila Jumamosi imelenga kutoa Elimu kwa watoto kuhusu fedha kusaidia kupunguza umasikini kwenye jamii yetu.Anangoja nini mwanao kuungana na watoto wengine kwenye program hii?Wasiliana nami kwa nafasi yake.

*Kosa kubwa watu wengi wanalofanya kwenye fedha ni 'Wanatumia fedha ambazo hawana,kununua vitu ambavyo hawavihitaji ili ...
12/10/2024

*Kosa kubwa watu wengi wanalofanya kwenye fedha ni 'Wanatumia fedha ambazo hawana,kununua vitu ambavyo hawavihitaji ili kuwafurahisha watu ambao hawawapendi'.Msingi imara kwenye fedha ni kitu ambacho kila mtu hasa watoto wanakihitaji sana ili kuepuka makosa mengi watu wanayofanya kwenye fedha.Habari njema ni kuwa kila Jumamosi kuanzia saa nne asubuhi ni siku ya kujenga misingi hii kwa watoto wetu.Ni katika benki ya Crdb tawi la Mandela Morogoro. Usikubali mwanao akose fursa hii leo.*

*'Urithi mkubwa ambao wazazi wanaweza kuwaachia watoto wao sio fedha au mali bali namna ya kuzisimamia'. Rafiki program ...
10/10/2024

*'Urithi mkubwa ambao wazazi wanaweza kuwaachia watoto wao sio fedha au mali bali namna ya kuzisimamia'. Rafiki program ya Elimu ya Fedha kwa watoto inayoendeshwa na benki ya Crdb tawi la Mandela kila Jumamosi imelenga kuwaandaa vyema watoto kwenye eneo la fedha ili waweze kumudu kusimamia fedha zao.Ni fursa nzuri kwa mwanao kuanzia miaka minne na kuendelea.Usikubali akose Jumamosi hii.*

Ubaya wa fedha ni 'labda uziwajibishe ama zikuwajibishe'.Kwa watoto kufahamu mapema namna ya kupata,kutunza na kukuza fe...
08/10/2024

Ubaya wa fedha ni 'labda uziwajibishe ama zikuwajibishe'.Kwa watoto kufahamu mapema namna ya kupata,kutunza na kukuza fedha zao itawasaidia sana kadiri wanavyokuwa.Program ya Elimu ya fedha kwa watoto inawaandaa watoto kuanzia miaka minne ili wawe na uwezo wa kuziwajibisha vyema fedha zao.Ni kila jumamosi benki ya Crdb tawi la Mandela Morogoro. Karibu umlete mwanao pia.K**a sio sasa basi lini?K**a sio yeye basi nani?

Kila siku ya maisha yetu tunaweka akiba kwenye benki ya fikra za watoto wetu.Ni akiba gani unaweka kwenye benki ya fikra...
07/10/2024

Kila siku ya maisha yetu tunaweka akiba kwenye benki ya fikra za watoto wetu.Ni akiba gani unaweka kwenye benki ya fikra zao leo?Rafiki program ya Elimu ya fedha kwa watoto inafanya kazi kujaza fikra sahihi kuhusu fedha kwa watoto wetu kuanzia miaka mnne na kuendelea.Ni kila Jumamosi benki ya Crdb tawi la Mandela Morogoro. Mlete mwanao jumamosi hii aungane na watoto wengine kwenye program hii.

Samaki hapati shida kuogelea,ndege hapati shida kupaa.Hivi ndivyo watoto wetu wanavyotakiwa kuwa kwenye eneo Zima la fed...
04/10/2024

Samaki hapati shida kuogelea,ndege hapati shida kupaa.Hivi ndivyo watoto wetu wanavyotakiwa kuwa kwenye eneo Zima la fedha.Rafiki nikukaribishe umlete mwanao aungane na watoto wengine wengi kwenye program ya Elimu ya Fedha kwa watoto ajifunze kwa kina mambo ya msingi kuhusu benki na fedha.Ni kila Jumamosi kuanzia saa nne hadi sita katika tawi la Crdb Mandela Morogoro.Kumbuka samaki mkunje...

Kwenye fedha kuna ushauri kuwa 'K**a ukifanya jinsi wengine wamekuwa wakifanya utaishia kupata matokeo ambayo wengine wa...
03/10/2024

Kwenye fedha kuna ushauri kuwa 'K**a ukifanya jinsi wengine wamekuwa wakifanya utaishia kupata matokeo ambayo wengine wamekuwa wakipata'.Ndio maana ukifwatilia sana utaona kuwa waliofanikiwa wana namna wanafanya mambo yao na walioshindwa pia wana namna yao.Program ya Elimu ya fedha kwa watoto ina lengo la kuwapitisha watoto kwenye misingi muhimu ambayo waliofanikiwa kwenye fedha wanatumia.Maeneo k**a kipato,akiba na uwekezaji ni sehemu ya machache ambayo watoto kuanzia miaka 4 wanajifunza kwa vitendo kwenye program hii.Ni kila Jumamosi kuanzia saa nne hadi sita tawi la CRDB Mandela Morogoro. Asipange kukosa Jumamosi hii.

Kuna maeneo 10 ambapo fedha imejificha.Moja ya eneo ambalo fedha imejificha ni kwenye *KAZI* .K**a kuna kitu ambacho wat...
02/10/2024

Kuna maeneo 10 ambapo fedha imejificha.Moja ya eneo ambalo fedha imejificha ni kwenye *KAZI* .K**a kuna kitu ambacho watoto wanapaswa kufahamu mapema kabisa basi ni hili 'FEDHA IMEJIFICHA KWENYE KAZI'.Kupitia program ya Elimu ya Fedha kwa watoto mwanao atapata nafasi ya kufahamu mapema kabisa ni wapi fedha imejificha ili kumjengea msingi imara kwenye fedha na maisha kiujumla.Ikiwa mwanao ana miaka 4 na kuendelea na hajabahatika kuhudhuria program hii basi anakosa kitu muhimu sana kwake.Usikubali akose jumamosi hii!

Address

Morogoro

Telephone

+255764639570

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Elimu ya Fedha kwa Watoto posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

  • Want your school to be the top-listed School/college?

Share