DUNIA YETU

DUNIA YETU

Share

“Ukurasa huu unahusu elimu ya Jiografia ��. Tunashirikisha maarifa rahisi na ya kueleweka kuhusu Du

16/03/2026
16/03/2026

📘 SOMO LA 23

🌾 RASILIMALI ZA ASILI NA MAENDELEO

🔎 Maana ya Rasilimali za Asili

Rasilimali za asili ni vipengele vya mazingira ambavyo watu wanaweza kutumia k**a maji, misitu, madini, ardhi, na wanyama ili kuendeleza maisha yao na uchumi wa taifa.

🌍 Aina za Rasilimali za Asili

1️⃣ Rasilimali zisizo za kudumu – mfano: maji, samaki, wanyama wa porini.
2️⃣ Rasilimali za kudumu – mfano: madini, miundo ya ardhi, misitu yenye thamani.

✅ Umuhimu wa Rasilimali za Asili

Huongeza uchumi wa nchi

Hutoa ajira kwa wananchi

Hutoa chakula na malighafi

Husaidia katika maendeleo ya viwanda

Hukuza biashara na uwekezaji

⚠️ Changamoto za Rasilimali za Asili

Uharibifu wa misitu

Uharibifu wa mazingira kutokana na uchimbaji wa madini

Ukosefu wa mpango bora wa matumizi

Kutumika vibaya na kuisha haraka

📝 Maswali ya Darasani

1. Eleza maana ya rasilimali za asili.

2. Tofautisha rasilimali za kudumu na zisizo za kudumu.

3. Taja umuhimu mmoja wa rasilimali za asili kwa maendeleo.

✍️ Imeandaliwa na:
M.k.abass
🌍 Soma – Elimika – Fahamu Dunia Yako

07/03/2026

⭐ Tanzania ni moja ya wazalishaji wakubwa wa dhahabu Afrika.
⭐ Almasi hupatikana katika migodi k**a Mwadui.
⭐ Madini hutumika kutengeneza simu na kompyuta.
⭐ Baadhi ya madini huchukua mamilioni ya miaka kuundwa.
⭐ Sekta ya madini hutoa ajira kwa watu wengi.

18/02/2026

🌍 SEHEMU YA TANO: JIOGRAFIA YA BINADAMU

Jiografia ya Binadamu ni tawi la Jiografia linalochunguza watu na shughuli zao duniani.
Hujikita katika mambo k**a:

Idadi ya watu

Makazi

Uhamiaji

Shughuli za kiuchumi

Maendeleo ya jamii

Katika sehemu hii tutajifunza jinsi watu wanavyoishi, wanavyoongezeka, wanavyohama na jinsi wanavyoathiri mazingira.

📖 SOMO LA 14

👥 IDADI YA WATU (POPULATION)

🔎 Maana ya Idadi ya Watu

Idadi ya watu ni jumla ya watu wanaoishi katika eneo fulani kwa wakati maalum.

Mfano:
Idadi ya watu wa Tanzania, Afrika au Dunia nzima.

📊 Mambo Muhimu Kuhusu Idadi ya Watu

1. Msongamano wa watu – Idadi ya watu kwa kila kilomita ya mraba.

2. Ongezeko la watu – Kuongezeka kwa idadi ya watu kutokana na kuzaliwa zaidi kuliko vifo.

3. Vifo (Death rate) – Idadi ya watu wanaokufa kwa kipindi fulani.

4. Uhamiaji (Migration) – Kuhama kwa watu kutoka eneo moja kwenda jingine.

🌍 Sababu za Kuongezeka kwa Idadi ya Watu

Huduma bora za afya

Chakula cha kutosha

Amani na usalama

Kuongezeka kwa kiwango cha kuzaliwa

⚠️ Madhara ya Idadi Kubwa ya Watu

Ukosefu wa ajira

Upungufu wa ardhi

Msongamano wa makazi

Uchafuzi wa mazingira

✅ Faida za Idadi Kubwa ya Watu

Soko la bidhaa kuwa kubwa

Nguvu kazi kuongezeka

Kuongezeka kwa maendeleo ya kiuchumi

📝 Maswali ya Darasani

1. Eleza maana ya idadi ya watu.

2. Taja sababu mbili za kuongezeka kwa idadi ya watu.

3. Taja faida moja ya idadi kubwa ya watu.

✍️ Imeandaliwa na:

M.k.abass

🌍 Soma – Elimika – Fahamu Dunia Yako

15/02/2026

# Wanafunzi wangu wa Geography Study 🌍📘
Mnaweza kusherehekea Valentine’s Day ❤️ huku mkiendelea kusoma kwa bidii! Furaha na elimu vinaweza kwenda pamoja 💪✨ ゚viral Promote Assistant Master ❤

04/02/2026
04/02/2026

# M.k.abass

Want your school to be the top-listed School/college in Zanzibar?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address

Zanzibar
ZANZIBARMJINI:71101