Annas Bin Malik Islamic Class Online

Annas Bin Malik Islamic Class Online

Share

kwa ajili ya Masomo ya Qur-an

26/04/2025

س مَا الإِسْلَامُ ؟

ج هُوَ الدِّينُ الَّذِي بَعَثَ اللَّهُ بِهِ سَيِّدَنَا مُحَمَّدًا صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِهَدَايَةِ النَّاسِ وَسَعَادَتِهِمْ .

س كَمْ أَرْكَانُ الْإِسْلَامِ ؟

ج أَرْكَانُ الْإِسْلَامِ خَمْسَةٌ : الْأَوَّلُ شَهَادَةُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ ، الثَّانِي إِقَامُ الصَّلَاةِ ، الثَّالِثُ ابْنَاءُ الزَّكَاةِ ، الرَّابِعُ صَوْمُ رَمَضَانَ ، الْخَامِسُ حِجُّ الْبَيْتِ الْمُسْتَطِيعُ .

س مَا مَعْنَى أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلهَ إِلَّا اللَّهُ ؟

ج مَعْنَاهُ اعْتَقِدُ أَنَّ اللَّهَ وَاحِدٌ لَا شَرِيكَ لَهُ

Tafsiri

Swali: Uislamu ni nini?

Jibu: Ni dini ambayo Mwenyezi Mungu alimtuma kwayo bwana wetu Muhammad, Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, kuwaongoza watu na kuwaletea furaha.

Nguzo ngapi za Uislamu?

Nguzo za Uislamu ni tano: Ya kwanza ni ushahidi kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Pili ni kusimamisha maombi. Ya tatu ni kutoa zaka. Ya nne ni mfungo wa Ramadhani. Ya tano ni kuhiji Nyumba kwa wale wanaoweza kufanya hivyo.

Swali: Nini maana ya “Nashuhudia ya kwamba hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu”?

Ina maana naamini kwamba Mungu ni mmoja na hana mshirika.

16/01/2025

The phrase “Ballighu ’anniy walau ayah” (بَلِّغُوا عَنِّي وَلَوْ آيَةً) is a well-known saying attributed to Prophet Muhammad (peace be upon him).

‎“Convey from me, even if it is a single verse.”

‎Explanation:
‎1. Encouragement to Share Knowledge:
‎• The Prophet encouraged Muslims to spread knowledge of Islam, even if it’s just a small piece of information, such as a single verse of the Qur’an or a simple teaching. This highlights the importance of da’wah (inviting others to Islam) and sharing beneficial knowledge.

‎2. No Need for Extensive Knowledge:
‎• This statement reminds believers that they don’t need to be scholars or experts to share Islamic teachings. Even small, sincere efforts to spread what you know can have a significant impact.

‎3. Responsibility:
‎• It also implies that once you learn something authentic and beneficial in Islam, it becomes a responsibility to pass it on to others appropriately.

‎This saying reflects the simplicity and accessibility of sharing the message of Islam. However, it also comes with the condition that one shares authentic knowledge and avoids misrepresentation or misinformation.

07/06/2022

Assallam alleykum warahmatullah wabarakatuh

*BM 4/4/5 MLANGO WA UGAWAJI WA ZAKA YA LAZIMA*

*Hadithi za Leo, Jumatatu, tarehe 6, Dhul-Qa’da Qa’da, 1443, sawa na tarehe 6, Juni 2022*

*KUHUSU UGAWAJI WA ZAKA YA LAZIMA*

*SEHEMU YA TANO*

*640-* وَعَنْ جُبَيْرِ بْنِ مُطْعِمٍ رضي الله عنه قَالَ: { مَشَيْتُ أَنَا وَعُثْمَانُ بْنُ عَفَّانَ رضي الله عنه إِلَى اَلنَّبِيِّ ﷺ فَقُلْنَا: يَا رَسُولَ اَللَّهِ, أَعْطَيْتَ بَنِي اَلْمُطَّلِبِ مِنْ خُمُسِ خَيْبَرَ وَتَرَكْتَنَا، وَنَحْنُ وَهُمْ بِمَنْزِلَةٍ وَاحِدَةٍ. فَقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ﷺ "إِنَّمَا بَنُو اَلْمُطَّلِبِ وَبَنُو هَاشِمٍ شَيْءٌ وَاحِدٌ". } رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ .

*640.* Imepokewa kutoka kwa Jubayr bin Mutw’im رضي الله عنه akisema: “Nilitoka mimi na Uthman bin Affan tukamuendea Mtume ﷺ tukamwambia: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, umewapa Bani Al Mutwalib الخمس (fungu la tano) la ngawira za Khaybar na umetuacha sisi hujatupa chochote, ilihali sisi na wao wote ni daraja moja.” Mtume ﷺ akasema: “Hapana! Ni Bani Al-Mutwalib na Bani Hashim, tu ndiyo kitu kimoja.” [Yaani tumbo la Bani Abdi Shams (Umayya) na Bani Nawfal, ni Maqureshi, ila si kizazi cha Mtume ﷺ . Ni Bani Al-Muttwalib na Bani Hashim tu ndio kizazi cha ukoo wa Mtume ﷺ.] Ameipokea Bukhari.

*

07/06/2022

Assallam alleykum warahmatullah wabarakatuh

*BM 4/4/5 MLANGO WA UGAWAJI WA ZAKA YA LAZIMA*

*Hadithi za Leo, Jumatatu, tarehe 6, Dhul-Qa’da Qa’da, 1443, sawa na tarehe 6, Juni 2022*

*KUHUSU UGAWAJI WA ZAKA YA LAZIMA*

*SEHEMU YA TANO*

*640-* وَعَنْ جُبَيْرِ بْنِ مُطْعِمٍ رضي الله عنه قَالَ: { مَشَيْتُ أَنَا وَعُثْمَانُ بْنُ عَفَّانَ رضي الله عنه إِلَى اَلنَّبِيِّ ﷺ فَقُلْنَا: يَا رَسُولَ اَللَّهِ, أَعْطَيْتَ بَنِي اَلْمُطَّلِبِ مِنْ خُمُسِ خَيْبَرَ وَتَرَكْتَنَا، وَنَحْنُ وَهُمْ بِمَنْزِلَةٍ وَاحِدَةٍ. فَقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ﷺ "إِنَّمَا بَنُو اَلْمُطَّلِبِ وَبَنُو هَاشِمٍ شَيْءٌ وَاحِدٌ". } رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ .

*640.* Imepokewa kutoka kwa Jubayr bin Mutw’im رضي الله عنه akisema: “Nilitoka mimi na Uthman bin Affan tukamuendea Mtume ﷺ tukamwambia: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, umewapa Bani Al Mutwalib الخمس (fungu la tano) la ngawira za Khaybar na umetuacha sisi hujatupa chochote, ilihali sisi na wao wote ni daraja moja.” Mtume ﷺ akasema: “Hapana! Ni Bani Al-Mutwalib na Bani Hashim, tu ndiyo kitu kimoja.” [Yaani tumbo la Bani Abdi Shams (Umayya) na Bani Nawfal, ni Maqureshi, ila si kizazi cha Mtume ﷺ . Ni Bani Al-Muttwalib na Bani Hashim tu ndio kizazi cha ukoo wa Mtume ﷺ.] Ameipokea Bukhari.

*UFAFANUZI*

Hadithi hii inazima kabisa utata wowote, k**a upo, kuhusu nani na nani ndio Ahlul Bayt, ukoo na kizazi cha Mtume ﷺ walioharamisha kupewa na kupokea Zaka, na badala yake wapewe hisa ya Fungu la Tano kutokana na Ghanima iliyo patikana bila ya mapigano yoyote.

Sayyidina Jubayr bin Mut’im (ambaye ni kizazi cha Nawfal na hivyo ni Quraysh) aliposikia kuwa Mtume ﷺ amewapa watoto na wajukuu wa Abdulmuttwalib mgao wa Fungu la Tano, ambalo Mwenyezi Mungu ameamrisha wapewe ndugu na jamaa wa Mtume ﷺ , kwa vile wamepigwa marufuku kupewa na kupokea Zaka, alifuatana na Sayyidina Uthman bin Affan *رضي الله عنهما* (wa ukoo wa Umayya, na hivyo ni Quraysh) kumuendea Mtume ﷺ na kutaka ufafanuzi kwanini Mtume ﷺ amewapa watoto na wajukuu wa Abdilmuttwalib, babu wa Mtume ﷺ, na kuwaacha wao ambao k**a alivyokuwa Abdulmuttwalib ni mtoto wa Abdu Manaf bin Quswayy, ni watu wa ukoo mmoja, na hivyo na wao wanastahiki kupewa mgao huo unaotokana na mali ya Khaybar ambayo imepatikana bila ya kutokea mapigano. Mtume ﷺ akawabainishia kuwa Bani Abdulmuttwalib na Bani Hashim, tu, ndio tumbo moja na ukoo mmoja. Lakini kizazi cha Nawfal na Abdishams (ambao ni watoto wengine wa Abdumanaf bin Qusywayy) si kizazi cha tumbo moja, la Abdilmuttwalib. Hivyo, kwa msingi huo watu wanaweza kuwa wanatokana na kabila moja, lakini matumbo tofauti. Na kwa maana hiyo, kizazi cha Mtume ﷺ kilichopigwa marufuku kupewa na kupokea Zaka ni watu wanaotokana na Babu mmoja,tu. wa Mtume ﷺ ; naye ni Abdulmuttwalib bin Hashim. Hao, peke yao, ndio kizazi cha Mtume ﷺ - kuanzia Al-Hassan na Al-Husayn, wajukuu wa Mtume ﷺ na mama yao, Fatma binti Muhammd *رضي الله عنها* na vizazi vyao, ikiwa pamoja na baba yao Sayyidina Aliyy in Abi Twalib. Vile vile watoto wengine wa Abdilmutwalib, k**a Sayyidina Al-‘Abbas na Sayyidina Hamza bin Abdilmuttwalib, *رضي الله عنهما* ambao walisilimu wao na watoto wao, Waislamu, ni miongoni mwa watu walioharamishwa kupewa na kupokea zaka. Ndiyo maana akawapa hisa yao ya fungu la Tano, k**a alivyo amrishwa na Mwenyezi Mungu katika Qur’ani:

*وَاعْلَمُوا أَنَّمَا غَنِمْتُمْ مِنْ شَيْءٍ فَأَنَّ لِلَّهِ خُمُسَهُ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ إِنْ كُنْتُمْ آمَنْتُمْ بِاللَّهِ وَمَا أَنْزَلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا يَوْمَ الْفُرْقَانِ يَوْمَ الْتَقَى الْجَمْعَانِ ۗ وَاللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ( الأنفال،8:41)*

_NA JUENI ya kwamba ngawira mnayo ipata, basi khums (sehemu moja katika tano) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume, *na jamaa,* na mayatima, na masikini, na wasafiri, ikiwa nyinyi mmemuamini Mwenyezi Mungu na tuliyo yateremsha kwa mja wetu siku ya kipambanuo, siku yalipo kutana majeshi mawili. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu._ (Al-Anfaal, 8:41)

Kwa ufupi, watoto wote wa Abdumanaf bin Quswayy, babu mkuu wa Maqureshi, ni Maqureshi. Lakini kizazi cha Mtume ﷺ ni watoto na wajukuu wa mtoto mmoja tu wa Abdumanafi, naye ni Abdulmutwalib bin Hashim. Watoto wengine wa Abdumanaf: Nawfal na Abdishams ni Maqureshi, lakini si kizazi cha Abdulmuttwalib bin Hashim. Hivyo, ni kizazi cha Abdulmuttwlaib na Hashim, tu, ndio tumbo moja. Wengine ni kabila moja, lakini si tumbo moja.

*NYONGEZA*: Mbali ya kuwa ni kizazi cha tumbo moja, Bani Hashim ndio watu pekee, walioshik**ana na Mtume ﷺ katika zama za Ujahiliyya, pale Maqureshi walipo chukua msimamo wa kuwapiga pande na kuwasusia, watu wote wa kizazi cha Abdulmuttwalib kutokana na msimamo wao wa kumuunga mkono na kumlinda mtoto wao Muhammad bin Abdullahi bin Abdilmuttwalib bin Hashim, wasifanye nao biashara, wala wasiowane nao, wala wasishirikiane nao katika jambo lolote. Ni kutokana na msimamo wao huo, dhidi ya Maqureshi wenziwao, ndio Mtume ﷺ akasema:

*"إنَّهم لم يفارقونا في جاهلية ولا إسلام"* رواه أحمد حديث 4068

“Hawajapata kuacha kutuunga mkono SI katika zama za Ujahiliyya wala SI katika zama za Uwislamu!” Ameipokea Ahmad, H.4069.

*YALIYOMO NA YATOKANAYO*

1. Kizazi cha Mtume ﷺ walio haramishwa kupewa na kupokea Zakka ni kizazi cha Abulmuttwalib bin Hashim tu.

2. Abdulmutwalib bin Hashim ni mmoja wa watoto wane wa Abdumanafi bin Quswayy, babu wa Maqureshi.

3. Wengine ni Hashim, ambaye kizazi chake ni Ahlul Bayt.

4. Wengine ni Nawfal na Abdi Shams bin Abdi Manaf: ambao vizazi vyao ni Maqureshi, lakini Si tumbo moja na vizazi vya Abdulmuttwlib na Hashim.

5. Ni kutokana na ukweli huo ndio maana Abu Lahab na watoto wake walikufa wakiwa Washirikina, si miongoni mwa Ahlul-Bayt.

6. Vizazi vyote vya Abdilmuttwalib na Hashim, tu, tena waliosilimu tu, ndio vizazi vya tumbo moja la Mtume ﷺ .

7. Watu wanaweza kutokana na Babu mmoja, lakini wakazaliwa kutokana na matumbo mbali mbali.

8. Kuna tofauti baina ya Kabila na Ukoo: Ukoo ni tumbo la uzazi, kabila ni Alama ya kijamii kutoka koo mbali mbali.

والله أعلم

وبالله التوفيق

*Jiunge na mojawapo wa kumbi za DARSA za kila siku, pamoja na Maswali na Majibu, kutoka kwa Sayyid Abdulqadir Shareef, kwa kutuma MAOMBI yako, moja kwa moja, kwenda 0786887887, KUPITIA WHATSAP! Taja majina yako halisi MATATU, na MAHALI ulipo!*

Hifadhi *DARSA HII* ndani ya simu yako ili uweze kumtumia mwenzako! ‎

*من السيد عبدالقادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم*

Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef

Kutoka Kitabu cha _Ufikiaji wa Malengo kupitia Dalili za Hadithi za Fiqhi ya Milango_, kitabu ‎ambacho ni tafsiri kamili ya Kitabu kiitwacho: ‎*بلوغ المرام من أدلة أحاديث الأحكام* ‏‎ ‎kilichotungwa na Imam *الحافظ إبن حجر العسقلانى* na kufasiriwa kwa ‎Kiswahili na ‎Sayyid ‎Abdulqadir Shareef Aalish- Shaykh Abi Bakr bin Salim.‎

16/05/2022

*BM 4/3/1 MLANGO WA SADAKA ZA KUJITOLEA*

*Hadithi za Leo, Jumatatu, tarehe 14, Shawwal, 1443, sawa na tarehe 16, Mei, 2022*

*KUHUSU SADAKA ZA KUJITOLEA*

*SEHEMU YA KWANZA*

*بَابُ صَدَقَةِ اَلتَّطَوُّعِ*



1. *Mlango Kuhusu Sadaka ya Kujitolea*

Baada ya kumaliza kutuwekea Mlango wa Zaka za Faradhi, tokea zaka ya mali, zaka ya mifugo, zaka ya mavuno hadi zaka za Fitri, Imam Ibn Hajar *رحمه الله* ametuwekea mlango huu wa Zaka ya kujitolea.

Na kujitolea, kwa upande wa Lugha, maana yake kutenda jambo pasi na kulazimishwa. Kwa upande wa Sharia, hata hivyo, kujitolea kunamaanisha kutenda jambo jema na ambalo si faradhi wala si wajibu, bali kutenda kwa hiari ili kupata Radhi na Neema za Mwenyezi Mungu. Yaani kutenda jambo kwa kujisogeza karibu zaidi na Mwenyezi Mungu, baada ya kukamilisha kutenda mambo ya wajibu na faradhi. Kwa maana hiyo, hakuna kujitolea jambo lolote lile, ambalo kwa kufanya hivyo, uwe umepuuza kutenda jambo lilio wajibu na faradhi juu yako. Ndiyo maana wanazuoni wakafafanua waziwazi kuwa mambo ya kujitolea ni mfano wa raba au vika-milisho vya mambo ya wajibu pale zinapotokea kasoro ndogo ndogo katika kutekeleza jambo la wajibu.

*التطوع تكمل به الفرائض يوم القيامة، إن لم يكن أتمها*.

“Kujitolea kunakamilisha, Siku ya Kiyama, mapungufu yaliyo tokea katika utekelezaji wa mambo ya Lazima, endapo mambo hayo hayajakamilika itkakikavyo!

Hivyo, Sadaka ya Kujitolea ni sadaka ambayo si ya wajibu juu ya mhusika, bali ni sadaka ya kujitolea kwa lengo la kutaka radhi na rehema za Mwenyezi Mungu. Yaani ni nyongeza ya kujitolea, iwe kwa kutumia nguvu za mwili, au kutoa kitu zaidi ya jukumu la mwili au zaidi ya zaka ya faradhi. Na kwa maana hiyo, sadaka ya kujitolea haina kitu maalumu, wala jambo maalumu. Wala wakati maalumu. Wala haina kiwango maalumu. Ilimradi tu, kinachotolewa au kutendwa kiwe ni nyongeza na ziada ya jambo la lazima juu ya mtu husika, na wakati huo huo liwe jambo halali na la manufaa. Yakikosekana masharti hayo basi hakuna upatikanaji wa Radhi na Rehema za Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu amesema :

*مَنْ ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَاعِفَهُ لَهُ أَضْعَافًا كَثِيرَةً ۚ وَاللَّهُ يَقْبِضُ وَيَبْسُطُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ( البقرة، 2:245)*

_Ni nani atakaye mkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema ili amzidishie mzidisho mwingi, na Mwenyezi Mungu hukunja na hukunjua. Na Kwake Yeye mtarejea._ (Al-Baqara, 2:245)

Yaani, je kuna mja yeyote anayetaka kumkopesha Mwenyezi Mungu kwa jambo la kujitolea, ili Mwenyezi Mungu amlipe kwa nyongeza nyigi sana; kwani mtoaji kwa wingi na mzuwiaji kutoa ni Mwenyezi Mungu pekaa, na kumbukeni kuwa ni Kwake Yeye pekee ndipo mtaporeja.

Mtume wetu ﷺ ametufafanulia faida ya sadaka ya kujtolea katika Hadithi nyingi, mojawapo ni Hadithi ifuatayo :

*عن أنس -رضي الله عنه- أنَّ النَّبيَّ ﷺ قالَ: "إنَّ الصدقة لتطفىء غضب الرب، وتدفع مِيْتة السوء" رواه الترمذي (664)*

Imepokewa kutoka kwa Anas *رضي الله عنه* akisema: Amesema Mtume ﷺ : “Sadaka huzima ghadhabu za Mwenyezi Mungu na huepusha kifo kibaya.” Ameipokea Tirmidhi, Hadithi 664.

Miongoni mwa mambo muhimu yanayo pendekezwa katika kutoa sadaka ya kujitolea ni mambo yafuatayo:-

Kutoa sadaka kwa siri sana ni bora zaidi kuliko kutoa kwa dhahiri, k**a ilivyo pokewa na Abu Hurayra *رضي الله عنه* kwamba Mtume ﷺ amesema kuhusu watu 7 watakao hifadhiwa chini ya kivuli cha Mwenyezi Mungu, ambapo miongoni mwa watu saba hao “…Na mtu aliyetoa sadaka akaificha kiasi kwamba mkono wake wa kushoto haujuwi kilicho tolewa na mkono wake wa kulia.” _Muttafaq alayhi._

Na sadaka inayotolewa na mtu mwenye afya yake na katika uzima wake ni bora kuliko sadaka inayo tolewa katika hali ya maradhi na shida:. Mtume ﷺ amesema:

"*تصدق وأنت صحيح شحيح*" [رواه البخاري (1353)].

“Toa sadaka yako pale una afya nzuri na una mahitaji yako mwenyewe!” Ameipokea Bukhari, H.1353.

*في رمضان أفضل منها في غيره؛ لما في البخاري (6) ومسلم (2308) عن ابن عباس قال: "إنَّ النبيَّ -صلى الله عليه وسلم- أجود الناس، وكان أجود ما يكون في رمضان*".

Na kutoa sadaka ya kujitolea ndani ya mwezi wa Ramadhani ni bora zaidi kuliko kuitoa sadaka yako ya kujitolea, ndani ya mwezi wowote mwengine, k**a ilivyo pokewa Hadithi kutoka kwa Ibn Abbas *رضي الله عنها* kwamba Mtume ﷺ alikuwa mkarimu kuliko watu wote, na alizidi ukarimu ndani ya Mwezi wa Ramadhani.” Muttafaq alayhi.

Na kuitoa pale unapo kuwa katika hali ya kuhitajia zaidi, ulicho nacho, kuliko wakati mwengine, ndiyo sadaka iliyo bora zaidi. K**a alivyo sema Mwenyezi Mungu katika Surat Al-Balad, Aya ya 14.

*و في وقت الحاجة أفضل منها في غيرها؛ لقوله تعالى: {أَوْ إِطْعَامٌ فِي يَوْمٍ ذِي مَسْغَبَةٍ (14)} [البلد]*

_Au kumlisha (Yatima Maskini) siku ya njaa. Yatima aliye jamaa._ (Al-Balad, 90:14-15)

Na hakuna sadaka kidogo. Kila sadaka hata iwe kidogo vipi, ujira wake ni mwingi. Mtume ﷺ ametuhimiza kutoa sadaka hata k**a ni nusu ya kokwa ya tende:

*عن عدي بن حاتم قال: قال رسول الله -صلى الله عليه وسلم-: "اتَّقوا النار، ولو بشق تمرة". رواه البخاري (1351)، ومسلم (1516)*

Imepokewa kutoka kwa Adiyy bin Hatim *رضي الله عنه* akisema: Amesema Mtume ﷺ : “Jiepusheni na Moto hata k**a kwa kutoa nusu ya kokwa ya tenda!” _Muttafaq alayhi_

Na ni dhambi kutoa sadaka ukafuatiliza na masimbulizi na maudhi. Mwenyezi Mungu amesema:

*يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُمْ بِالْمَنِّ وَالْأَذَى} [البقرة: 264].*

_Enyi mlio amini! Msivuruge sadaka zetu kwa masimbulizi na maudhi_. (Al-Baqara, 2:264)

Wala usichague vilivyo vibaya ndiyo ukavitoa na kuficha vilivyo vizuri:

*يا أ أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنْفِقُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّا أَخْرَجْنَا لَكُمْ مِنَ الْأَرْضِ ۖ وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنْفِقُونَ وَلَسْتُمْ بِآخِذِيهِ إِلَّا أَنْ تُغْمِضُوا فِيهِ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ( البقرة ،(2:267)*

_Enyi mlio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa._ (Al-Baqara, 2:267)

Na Mwenyezi Mungu ametukumbusha kwa kutwambia:

*{لَنْ تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّى تُنْفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ} [آل عمران: 92]*

_Hamtaipata Pepo mpaka mtowe vile mnavyo vipenda._ (Al-Imran, 3:92)

Hayo ndiyo maelezo mafupi kuhusu Sadaka ya kujitolea na fadhila zake. Sasa tusome kwa pamoja Hadithi zifuatazo kutoka kwenye midomo mitukufu ya Bwana wetu Muhammad ﷺ .

والله أعلم

وبالله التوفيق

*Jiunge na mojawapo wa kumbi za DARSA za kila siku, pamoja na Maswali na Majibu, kutoka kwa Sayyid Abdulqadir Shareef, kwa kutuma MAOMBI yako, moja kwa moja, kwenda 0786887887, KUPITIA WHATSAP! Taja majina yako halisi MATATU, na MAHALI ulipo!*

Hifadhi *DARSA HII* ndani ya simu yako ili uweze kumtumia mwenzako! ‎

*من السيد عبدالقادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم*

Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef

Kutoka Kitabu cha _Ufikiaji wa Malengo kupitia Dalili za Hadithi za Fiqhi ya Milango_, kitabu ‎ambacho ni tafsiri kamili ya Kitabu kiitwacho: ‎*بلوغ المرام من أدلة أحاديث الأحكام* ‏‎ ‎kilichotungwa na Imam *الحافظ إبن حجر العسقلانى* na kufasiriwa kwa ‎Kiswahili na ‎Sayyid ‎Abdulqadir Shareef Aalish- Shaykh Abi Bakr bin Salim.‎

NI RUHUSA KUNUKUU, k**a ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.

[email protected]

20/01/2022

Unapo ingia chooni sema:
*بسمِ الله. اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِـكَ مِـنَ الخُـبثِ وَالخَبائِث* .

Na unapo toka sema:
*غُفـرانَك. الحمد لله الذى أذهب عنى الأذى وعافانى*

_Wa billah attawfiq_

11/01/2022

*BM.28\12 MLANGO WA MASUALA YA MAITI*

*Hadithi za Leo, Jumaane, tarehe 8, Jumadal-Aakhir, 1443, sawa na tarehe 11, Disemba, 2022*

*KUHUSU MLANGO WA JENEZA*

*SEHEMU YA KUMI NA MBILI*

*540*- وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: { كُفِّنَ رَسُولُ اَللَّهِ ﷺ فِي ثَلَاثَةِ أَثْوَابٍ بِيضٍ سَحُولِيَّةٍ مِنْ كُرْسُفٍ, لَيْسَ فِيهَا قَمِيصٌ وَلَا عِمَامَةٌ. } مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ.

*540.* Imepokewa kutoka kwa ‘Aisha رضي الله عنها akisema: “Alikafiniwa Mtume ﷺ katika nguo (shuka) tatu nyeupe kutoka Yemen zilizo tengenezwa kutokana na pamba. Hakuvalishwa kanzu wala kiremba.” _Muttafaq alayhi_.

*541-* وَعَنِ ابْنِ عُمَرَ -رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا- قَالَ: { لَمَّا تُوُفِّيَ عَبْدُ اَللَّهِ بْنِ أُبَيٍّ جَاءٍ اِبْنُهُ إِلَى رَسُولِ اَللَّهِ ﷺ. فَقَالَ: أَعْطِنِي قَمِيصَكَ أُكَفِّنْهُ فِيهِ, فَأَعْطَاه ُ]إِيَّاهُ] } مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ.

*541.* Imepokewa kutoka kwa Ibn Umar رضي الله عنهم akisema: “Alipofariki Abdullahi bin Ubayy alikuja mtoto wake kwa Mtume ﷺ akamwambia: “Naomba kanzu yako nikamkafinie baba yangu.” Mtume ﷺ akampa kwenda kumkafinia baba yake.” _Muttafaq alayi._

*542*- وَعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ اَلنَّبِيَّ ﷺ قَالَ: { الْبَسُوا مِنْ ثِيَابِكُمُ الْبَيَاضَ, فَإِنَّهَا مِنْ خَيْرِ ثِيَابِكُمْ, وَكَفِّنُوا فِيهَا مَوْتَاكُمْ } رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ إِلَّا النَّسَائِيَّ, وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ .

*542.* Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas رضي الله عنهم akisema: “Amesema Mtume ﷺ: “Pendeleeni kuvaa nguo nyeupe katika mavazi yenu kwani nguo nyeupe ndiyo bora ya nguo zenu. Na wakafinini maiti wenu kwa nguo nyeupe !” Wamepokea Maimamu watano isipo kuwa Nasai na ameisahihisha Tirmidhi.

*543-* وَعَنْ جَابِرٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ﷺ { إِذَا كَفَّنَ أَحَدُكُمْ أَخَاهُ فَلْيُحْسِنْ كَفَنَهُ } رَوَاهُ مُسْلِمٌ.

*543.* Imepokewa kutoka kwa Jabir رضي الله عنه akisema: “Amesema Mtume ﷺ : “Akimkafini mmoja wenu mtu wake basi amkafini vizuri au kwa kitambaa kizuri cheupe.”

*UFAFANUZI*

Hadithi zote hizi nne zinatusimulia na kutufunza hukumu kadhaa zenye kuhusiana na sanda ya maiti.

a) Hadithi ya Mama Aisha رضي الله عنها inatuelimisha kuwa ni Sunna kumvesha maiti sanda ya shuka tatu nyeupe za kitambaa cha pamba, pasi na kumvesha kanzu wala kilemba. Hivyo ndivyo alivyo vishwa Mtume ﷺ sanda yake.

b) Hadithi ya Ibn Umar رضي الله عنهما inatutajia kuwa inajuzu kwa maiti kuveshwa nguo ya mtu mwengine iliyo kwisha tumiwa; khasa ikiwa nguo hiyo ni ya mja mwema. Ila Mtume ﷺ alifanya hivyo kumridhisha mtoto wa Ibn Salulu anaye itwa Abdullah bin Abdillah bin Ubayy bin Salul, ambaye alikuwa Mwislamu na Swahaba mwema, aliyemuomba Mtume ﷺ ampe kanzu yake ili akamkafini baba yake huyo, na Mtume ﷺ akamridhia na kumpa, na baadae akamuomba Mtume ﷺ amswalie, na Mtume ﷺ akamswalia, lakini baadae akateremshiwa Wahy kuka-tazwa Mtume ﷺ kuwaswalia Wanafiki k**a Abdullah bin Ubayy bin Salul.

c) Hadithi ya Ibn ‘Abbas رضي الله عنهما inatutajia Sunna ya kupendelea kuvaa nguo za rangi nyeupe, na hata kutumia nguo za rangi nyeupe kuwakafini maiti wetu.

d) Vile Hadithi ya mwisho ya Jabir bin Abdillah inatufundisha kuwa tunapo wakafini maiti wetu basi tuwakafini vizuri na kwa shuka nzuri, nyeupe. Yaani tusifanye ubakhili wa kuwazika katika matambara au shuka za zamani.

Hivyo, Hadithi zote hizi zinazungumzia baadhi ya hukumu muhimu zenye kuhusiana na sanda ya maiti, tokea upande wa idadi ya mashuka, aina yake na hata rangi yake; na kwamba yote hayo ni Sunna. Kwa maneno mengine, vile hadithi zote zinabainisha kuwa ni wajibu wa kutoshelezana kumvisha sanda maiti, sifa za sanda yenyewe ni mambo ya sunna. Yaani si lazima sanda iwe nyeupe, wala si lazima sanda iwe inatokana na kitambaa kilicho tengenezwa kutokana na pamba. Ila, k**a tutavyo kuja kuona, ni makuruhu sana kumvisha maiti sanda ya kitambaa cha ghali, au kitambaa cha fahari.

*YALIYOMO NA YATOKANAYO*

1. Idadi bora ya mashuka ya sanda, kwa maiti mwanamume, ni mashuka matatu, meupe, na ikiwezekana yawe ya kitambaa cha pamba.

2. Mtume ﷺ alikafiniwa kwenye shuka tatu nyeupe zilizo tengenezwa kutokana na pamba.

3. Si Sunna bali ni makuruhu kumvisha kanzu au kilemba maiti k**a ndiyo sanda yake; isipo kuwa pakikosekana shuka za sanda.

4. Si Sunna ila si haramu kumvisha maiti sanda ya rangi nyengine, iwapo ndiyo iliyo patikana tu.

5. Gharama za sanda ya maiti inatolewa kutoka na mali yake aliyo acha, ila inajuzu kwa ndugu na jamaa zake kumnunulia sanda.

6. Wajibu wa mwanzo wa kumvisha sanda maiti ni juu ya ndugu na jamaa zake, khasa warithi wake.

7. Mpangilio wa shuka tatu ni kuwa zinapangwa moja juu ya nyengine na kisha maiti anawekwa juu yake na kufunika shuka ya mwanzo inayo gusa mwili wake, upande wa kulia juu ya upande wa kushoto; kisha shuka ya pili chini yake, na kumalizia kwa shuka ya tatu. Kisha zinafungwa kwa papi za shuka hizo hizo.

8. Shuka hizo zinapaswa kuwa ndefu zaidi kufunika urefu wa mwili wa maiti, k**a kuzidi futi moja kila upande.

9. Maiti ya manamke inakafiniwa katika shuka tano nyeupe na za pamba: Shuka ya kiunoni, Mtandio, Kanzu au shuka iliyo pasuliwa kati k**a shingo, na mashuka mawili zaidi.

10. Mtoto mdogo wa kiume, ambaye hajabalighi, anakafiniwa kwenye shuka moja, lakini inajuzu kumkafini kwenye shuka tatu.

11. Mtoto wa k**e, ambaye hajabalighi, anakafiniwa katika shuka mbili na shuka iliyo pasuliwa shingo, lakini bila ya mtandio.

12. Wajibu kwa maiti yeyote ni kukafiniwa angalau katika shuka moja, yenye kusitiri mwili wake wote, bila ya kujali jinsia wala umri wa maiti husika. Ila Sunna ni maelezo ya hapo juu.

13. Kujuzu kutabaruku kwa athari za Mtume ﷺ ila hatonufaika nazo mnafiki au asiye kuwa Mwislamu.

14. Unafiki ni hatia kubwa katika Uwislamu, na mnafiki ni mtu mwenye nyuso mbili; mzandiki, bazazi, fattani, mzabzabina.

15. Kujuzu bali ni Sunna kumfurahisha Mwislamu au kumkidhia haja yake; ndivyo alivyo fanya Mtume ﷺ kumridhia Abdullah bin Abdillah bin Salul.

16. Fadhila za Sayyidina Abdullah bin Abdillah bin Salul, mtoto wa Abdullah bin Salul, kiongozi wa wanafiki Madina..

17. Kila mtu anabeba mwenyewe dhambi zake; _Haibebeshwi nafsi dhambi za nafsi nyengine_*ولا تزر وازرة وزرى أخري*

18. Kuvaa nguo nyeupe, kwa walio hai, ni Sunna na ni Sunna kuwakafini maiti wetu kwa shuka nyeupe.

19. Mwenye kuvaa nguo nyeupe ili kufuata Sunna ya Mtume ﷺ anapata thawabu za kufuata nyayo za Mtume ﷺ .

20. Inapendekezwa kuchagua kitambaa cheupe kizuri, kipya na kisafi kwa kumkafini maiti.

21. Makuruhu kumkafini maiti katika kitambaa kibaya, kikuukuu, au tambara la mifuko ya unga.

والله أعلم

وبالله التوفيق

*Jiunge na mojawapo wa kumbi za DARSA za kila siku, pamoja na Maswali na Majibu, kutoka kwa Sayyid Abdulqadir Shareef, kwa kutuma MAOMBI yako, moja kwa moja, kwenda 0786887887, KUPITIA WHATSAP! Taja majina yako halisi MATATU, na MAHALI ulipo!*

Hifadhi *DARSA HII* ndani ya simu yako ili uweze kumtumia mwenzako! ‎

من السيد عبدالقادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم

Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef

Kutoka Kitabu cha _Ufikiaji wa Malengo kupitia Dalili za Hadithi za Fiqhi ya Milango_, kitabu ‎ambacho ni tafsiri kamili ya Kitabu kiitwacho: ‎بلوغ المرام من أدلة أحاديث الأحكام ‏‎ ‎kilichotungwa na Imam الحافظ إبن حجر العسقلانى na kufasiriwa kwa ‎Kiswahili na ‎Sayyid ‎Abdulqadir Shareef Aalish- Shaykh Abi Bakr bin Salim.‎

NI RUHUSA KUNUKUU, k**a ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.

[email protected]

22/12/2021

***KISA CHENYE MAFUNZO**

Sayyedna Suleiman (A.S) alikuwa na Urafiki mkubwa na Malaika wa Mauti
Basi Siku moja Sayyedna Suleiman bin Daudi (A.S) akiwa ameketi wakibadilishana mawazo na Malaika wa Mauti alikuja bwana mmoja akamualika Sayyedna Suleiman kwenye harusi ya mwanaye"

Yule bwana alipoondoka Malaika wa Mauti akamwambia Sayyedna Suleiman Usiende kwenye hiyo harusi kwa sababu nimetizama kwe orodha yangu nimeona jina la bibi harusi kwa hiyo ndoa hiyo haitofanyika kwa sababu bibi harusi mtarajiwa atakuwa amefariki kabla ya ndoa!

Basi Sayyedna Suleiman hakwenda kwenye harusi ile lakini baada ya mda akapata habari kwamba Harusi ile imefanyika na wala bibi harusi hakufariki!!
Sayyedna Suleiman akawa anajiuliza imekuwaje baada ya muda kupita akaja malaika wa mauti kwa Suleiman!
Sayyedna Suleiman kwa shauku akamuliza Ewe Malaika wa Mauti imekuje na mbona ulisema harusi haitofanyika kwamba bibi harusi atafariki kabla ya ndoa mbona harusi imefanyika na wote wapo hai"

Malaika wa mauti akamwambia Ewe Nabii wa ALLAH hakika mda mchache kabla haijafika bibi harusi alijiwa na bibi kizee MchaMungu huku akiwa ni mwenye njaa Kali akamuomba bibi harusi yule chakula basi huruma akampa chakula na pesa ambazo zingetumika kwenye harusi yake
Wakati bibi yule anataka kuondoka alimuombea dua bibi harusi k**a vile alivyomsitiri kwenye dhiki yake"

Basi Mwenyezi Mungu alipokea dua ya bibi kizee yule na amemuongeza bibi harusi umri na watoto mpaka vitukuu"

In Shaaa ALLAH Watukufu ndugu Zangu tujitahidi sana kutoa sana sadaka na kuombeana dua njema "
Hakika Sadaka ni Ibada yenye Manfaa Makubwa Duniani na Akhera"

12/11/2021

AQIQA NDIO NINI, NA NINI UTARATIBU WA MBUZI WA AQIQA

Nimeulizwa masuali mawili, NANUKUUl-‎

SWALI.1.‎

‎“Asalam alaykum. Naomba ufafanuzi hivi mtoto mchanga ‎anaponyolewa nywele kwa mara ya kwanza nakisha nywele zake ‎kupimwa na kutolewa sadaka fedha ama dhahabu kwa uzito ‎unaolingana. Jambo hili limethibiti katika dini ama la?”‎

SWALI. 2.‎

‎“Je,Utaratibu wa aqiqa upoje?‎

Au kuchinja tu na kugawa nyama yatosha ? Au kisha pana duaa ‎maalumu ya kuomba? Utaratibu wale haswaa upoje?” ‎

SWALI. 3. assalaam alaykum naomba kuuliza jee mbuzi wa aqiqi ‎unaweza kuwapika kwenye shughuli ikawa km sadaka au wtt ‎yatima au madrasa kuna sherehe ukafanyia chakula?‎

JIBU.‎

BISMILLAH.‎

Naam limethibiti, kwa kauli na vitendo, k**a tutavyo ona baadae.‎

Kwanza, AQIIQA ni nini?‎

Aqiiqa, kwa upande wa lugha, ni nyewele za mtoto mchanga ‎aliyezaliwa nazo.‎

Kwa upande wa Sharia, Aqiiqa maana yake mnyama anayechinjwa ‎kwa kuzaliwa mtoto, na kunyolewa nywele zake (aqiiqa yake). ‎

Mtume ‎صلى الله عليه وسلم‎ amesema: ‎

كل مولود مرهون بعقيقته تذبح عنه يوم سابعه ويحلق ويسمى (رواو أبو داؤد (2838) أحمد (5.7) ‏النسائى(4220)‏‎ Kila mtoto aliyezaliwa yumo kwenye rehani mpaka ‎achinjiwe mbuzi wake siku ya asaba, na anyolewe nywele, na ‎kupewa jina” Abu DAud, Ahmad na Nasai.‎

Hivyo, Aqiiqa ni Sunna kukbwa sana, (isipokuwa kwa Abu Hanifa, ‎yeye anasema Si sunna wala Si faradhi, ni jambo la kujitolea tu) ‎

Kwa upande wa maulamaa wengine, hata hivyo, Aqiiqa ni Sunna ‎iliyotiliwa mkazo, ‎سنة مؤكدة‎ sawa sawa na Mbuzi wa Udh-hiya, kwa ‎upande wa masharti yake, aina ya mnayma, na umri wa mnyama ‎huyo.‎

Miongoni mwa masharti yake ni kwamba asiwe na kilema chochote, ‎na asiwe chini ya umri wa miaka mwili. Na ni kondoo au mbuzi. Ila ‎inajuzu, vile vile, kwa mwenye uwezo zaidi, ngamia au ng’ombe. ‎Yaani, ngamia bora kuliko ng’ombe, na ng’ombe bora kuliko mbuzi ‎au kuondoo. ‎

Sunna ya Aqiiqa kwa mtoto wa kiume ni mbuzi wawili na kwa mtoto ‎wa k**e mbuzi mmoja. ‎

Na mwenye jukumu al kuchinga na Mzee wa mtoto: Baba kwanza, ‎anafuatiwa na Babu, Ami, Kaka mkubwa na kadhalika.‎

Wakikosekana wanaumbe basi upande wa kuukeni: Mama mzazi, ‎Bibi, Shangazi, Khaloo (mama mdogo), Dada na kadhlika.‎

Na gharama za mnyama zitoke kwenye mali ya Mzazi, na SI kutoka ‎kwenye mali ya mtoto mwenyewe aliyezaliwa (iwapo kuna urithi ‎wake). ‎

KUCHINJA SIKU YA SABA NA KUPEWA JINA

Aqiqa inatakikana achinjwe Siku ay Saba, baada ya kuzaliwa mtoto, ‎na mtoto anyolewe nyewele, kwa mara ya kwanza, na kisha ‎zipimwe kwa madini k**a fedha, na uzito wa madini hiyo utolewe ‎sadaka.‎

Hivyo ndivyo alivyofanya Mtume ‎صلى الله عليه وسلم‎ kwa wajukuu zake ‎wawili, al-Hasan na al-Husayn. Aliwachinjia wanyama kondoo ‎wawili, wa mkono wake mtukufu. ‎

Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas ‎رضي الله عنه‎ akisema: Aliwachinjia ‎Aqiiqa Mtume ‎صلى الله عليه وسلم‎ al-Hasan na al-Husayn kondoo kila ‎mmoja” Abu Daud H.2841.‎

Na imepokewa kutoka kwa Ibn Abbs ‎رضي الله عنهما‎ akisema: Amesema ‎Mtume ‎صلى الله عليه وسلم‎ “Aqiqa ya msichana ni mbuzi mmoja na aqiiqa ‎ya mvulana ni mbuzi wawili” Abu Daud.‎

Vile vile imepokewa kutoka kwa Umm Kurz al-K’abiyya ‎رضي الله عنها‎ ‎akisema: Nimesika Mtume ‎صلى الله عليه وسلم‎ akisema: Aqiiqa ya mvulana ‎ni mbuzi wawili wanaofanana (umri na sifa) na ya msichana ni ‎mbuzi mmoja” Abu Daud, Kitaab al-Adhaahi, H. 2834.‎

KUPEWA JINA SIKU YA SABA

Na siku hiyo hiyo, BAADA YA KUCHINJWA AQIIQA, anapewa jina ‎mtoto, iwapo bado hajapewa. ‎

Ama ikiwa ameshapewa jina, mara tu baada ya kuzalia, au aliekewa ‎jina hata kabla ya kuzaliwa, na akapwa mara tu baada ya ‎kukzaliwa, basi siku hiyo ya Saba itakuwa ni SIKU ya kulithibitishwa ‎rasmi jina hilo, baada ya kuchinjiwa Aqiiqa yake.‎

Bora ya majina ni lile lenye kuambatanishwa na Allah, au mojawapo ‎wa Majina Yake Matakatifu, k**a Abdullah, Abdufattah, Abdulqadir, ‎Abdulwahaab, Abdulghafuur na kadhalika, kwa mtoto wa kiume. ‎

Kwa upande wa watoto wa k**e, basi bora majina ya waja wema ‎waliotangulia, Maryam, Aasiya, Fatma, Khadija, Zaynab, na ‎kadhalika.‎

Na hakuna ukaraha wala junaha kumpa majina ya ukoo, au ‎kumbukumbu ya mmojawapo wa wazazi wake, na kadhalika. ‎Ilimradi yasiwe majina mabaya, k**a Mwanashari, Magomvi, ‎Punda, Zuzu, Zumbukuku na kadhalika; Mtumeصلى الله عليه وسلم‎ ‎ameusia kuwapa watoto majina mema, na SI majina ya kuashiria ‎uovu au ubaya.‎

Na ni haramu kumwita kwa majina ya Mwenyezi Mungu; k**a al-‎Ghafuur, lakini Ghafuur inajuzu, al-Shakuur haramu, lakini Shakuur ‎inajuzu. Al-Aziz haramu, lakini Aziz inajuzu, na kadhalika.‎

MUDA WA AQIIQA. ‎

Muda wa Aqiqa ni tanagu kuzliwa mtoto hadi kubalighi. Lakini ‎akishabalighi basi fadhila za kufuata Sunna hazipo tena. Ila thawabu ‎za Sadaka zipo pale pale. ‎

Hata hivyo, yule ambaye anaamini kuwa hajachinjiwa Aqiiqa na ‎wazee wake, basi anaweza kujichinjia mweyewe utuuzimani. Kwani ‎‎– k**a tulivyosema- Aqiqa ni Sunna kubwa iliyotiliwa mkazo sana, ‎na ni k**a mbuzi wa Udh-hiya. ‎

Na isitoshe, Mtume ‎صلى الله عليه وسلم‎ alijichinjia Aqiiqa baada ya kupewa ‎Utume. Al-Bayhaqi fi al-Sunan al-kubra, Babb al-Aqiiqa Sunna: H. ‎‎9/300. Bidaayat al-Mujtahid 1/475.‎

NYAMA YA AQIIQA.‎

Nyama ya Aqiiqa inatolewa sadaka kwa masikini, na vile vile kwa ‎wanafamilia. Hivyo inajuzu watu wa nyumbani kula nyama hiyo. Ila ‎ni makuruhu kumlisha chochote aliyechinjiwa Aqiiqa hiyo.‎

Nyama ya aqiqa hugawiwa mbichi, kwa masikini na wanafamilia, ‎ndugu na jamaa, na majirani vile vile. Hiyo ndiyo sunna ya Aqiqa.‎

Inajuzu, hata hivyo, kwa sehemu ya nyama ya kuwapa masikini, ‎kuwapikia chakula na nyama hiyo, wakaja wakala. Hakuna junaha, ‎kwa vile pengine hao masikini hawana uwezo wa kupata cha kupikia ‎nyama hiyo. Kwa aili hiyo, inajuzu kuwapikia chakula masikini. ‎Lakini waliosalia wafawiwe sehem yao ikiwa mbichi.‎

KUNYOLEWA NA KUPIMWA NYWELE ZAKE KWA MADINI.‎

K**a tulivyosema, mnyama wa Aqiiqa anachinjwa siku ya Saba, ‎tokea kuzaliwa mtoto, na baadae hupewa jina, na baadae ‎hunyolewa na kupimwa nywele zake kwa madini, na uzito huo ‎kutolewa sadaka. Kwa utaratibu huo: SIKU HIYO HIYO.‎

Ikishindikana siku ya Saba, basi siku ya 14. Ikikosekana siku ya 14, ‎basi sikuu ya 21, na kuendelea hivyo hivyo. Bi. Aisha ‎رضى الله عنها‎ ‎alisema hivyo kuwajibu waliokuwa wakimuuliza swali hilo.‎

Shafiiyya na Maalikiyya, wanasema Sunna kuchinja, kumpa jina, ‎kumnyoa nywele, kuzipima kwa madini, ama dhahabu au fedha na ‎kutoa sadaka thamani ya madini hiyo.‎

Hanabila wanasema utaratibu huo huo, ila kwao wao sunna ni ‎madini ya fedha tu. ‎

Abu Hanifa – k**a tulivyosema, kwake yeye ni jambo la kujitolea ‎tu-; hivyo itategemea unataka kujitolea nini. Ni sadaka tu. Haina ‎mpango wowote ule.‎

Dalili ya Shafiiyya, Mlikilyya na Hanabila ni pamoja na Hadtihi ‎zifuatazo: ‎

ما رواه علي بن أبي طالب قال: عق رسول الله صلى الله عليه وسلم عن ‏الحسن بشاة، وقال: يا فاطمة احلقي رأسه، وتصدقي بزنة شعره فضة، ‏قال: فوزنته فكان وزنه درهماً أو بعض درهم. رواه الترمذي.. وعن أبي ‏رافع قال: لما ولدت فاطمة حسناً قالت: ألا أعق عن ابني بدم؟ قال: لا، ‏ولكن احلقي رأسه وتصدقي بوزن شعره من فضة على المساكين ‏والأوفاض، وكان الأوفاض ناساً من أصحاب رسول الله صلى الله عليه وسلم ‏محتاجين في المسجد أو في الصفة. رواه أحمد

Imepokewa na Sayyidina Aliyy bin Abi Twaalib ‎رضي الله عنه‎ akisema: ‎Aliwachinjia Aqiiqa Mtume ‎صلى الله عليه سلم‎ al-Hasan na al-Husayn mbuzi ‎mmoja kila mmoja, na akamwambia Fatma: “Wanyoe vichwao vyao, ‎na toa sadaka uzito wa fedha wa nyewele zao hizo. Anasema ‎Sayyidina Aliyy: basi nikazipima na uzani wake ukawa sawa na ‎dirham mmoja nakitu hivi” Ameipokea Tirmidhi.‎

Na imepokewa kutoka kwa Abu Raafi’ ‎رضي الله عنه‎ akisema: Alipomzaa ‎al-Hasan Bi.Fatma aliuliza kwa kusema: “Je, naweza kumchinjia ‎mtoto wangu mnyama? Mtume ‎صلى الله عليه وسلم‎ akamjibu: “Hapana! ‎Lakini mnyowe nyewele zake, na zipime kwa fedha, na toa sadaka ‎fedha hiyo ka masikini, na kwa Aqfaadh (na Awafaadh ni mafaqiri ‎wa kibaraza cha Suffa cha kando ya Msikiti wa Mtume ‎صلى الله عليه وسلم ‏‎ ‎‎). Ameipokea Imam Ahmad.‎

NB. Mtume ‎صلى الله عليه وسلم‎ si k**a alimkataza Bi. Fatma kuchinja ‎aqiqa, bali ni kwamba alitaka kuifanfya Sunna hiyo YEYE ‎Mwenyewe, ndiyo maana akamwambai Wewe wanyoye tu na pima ‎nywele zao kwa fedha na toa sadaka fedha hiyo. Maana, k**a ‎tulivyo ona hapo juu na tutavyo ona katika hadithi zifuatazo, Mtume ‎صلى الله عليه وسلم‎ aliwachinjia al-Hasan na al-Husayn kondoo wawili kwa ‎mikono yake mwenyewe. ‎
‏ ‏

HADITHI ZAIDI KUHUSU AQIQA.‎

‎1.‎ فعن سَلْمَان بْن عَامِرٍ الضَّبِّيّ قَالَ: سمعت رسول الله صلى الله عليه ‏وسلم يقول:مع الغلام عقيقة، فأهريقوا عنه دماً، وأميطوا عنه الأذى. ‏رواه البخاري. ‏‎ Imepokewa na Salmaan bin Aamir al-‎Dhwabbi ‎رضي الله عنه‎ akisema: Nimemsikia Mtume ‎صلى الله ‏عليه وسلم‎ akisema: Kila mtoto anasahiki kuchinjiwa ‎Aqiqa wake. Hivyo basi, mchinjieni mwage damu kwa ‎kuzaliwa kwake, na muondosheeni maudhi” Bukhari.‎

‎2.‎ وعن عائشةَ:أن رسول الله صلى الله عليه وسلم أمرهم عن الغلام ‏شاتان مكافئتان، وعن الجارية شاة. رواه الترمذي وقال حسن ‏صحيح، وابن ماجه، ‏‎ Imepokewa kutoka kwa Bibi Aisha ‎رضي الله عنها‎ akisema: Aliwaamrisha Mtume ‎صلى الله عليه وسلم‎ ‎wamchinjie mvulana mbuzi wawili wenye umri sawiya, ‎na msichana mbuzi mmoja”. Ameipokea Tirhimdi na ‎Ibn Majah. Amesema Tirmidhi ni Hadithi Hasanun ‎Swahih.‎

‎3.‎ Imepokewa kutoka kwa Imm Malik, kutoka kwa Jafar ‎bin Muhammd kutoka kwa Muhammad bin Aliyy Zayn ‎al-Aabidiin akisema: ‎وزنت فاطمة بنت رسول الله صلى الله عليه وسلم ‏شعر حسن وحسين وزينب وأم كلثوم فتصدقت بزنة ذلك فضة‎ “Bibi Fatma ‎alipima nywele za al-Hasan, al-husayn, na Zayna, na ‎Ummu Kulthuum, kila mmoja kwa fedha na kutoa ‎sadaka kwa uzito wake” Muwatta

‎4.‎ Imepokewa kutoka kaw Aliy bin al-Husayn bin Aliyy ‎bin Abi Twalib akisema: Alipima Fatma Binti wa ‎Mtume ‎صلى الله عليه وسلم‎ nywele za Hasan na Husayn kwa ‎fedha na akatoa sadaka uzito wake huo” Muwatta’.‎

NYONGEZA.‎

Mila ya kuchinja Mnyama wa Aqiqa ilikuwepo tokea zama za ‎Ujjahiliyya: k**a sadaka na kumuondolea mtoto kijicho na hasad. ‎Ila walikuwa na ada ya kumpaka damu ya mnyama huyo, k**a ‎ishara ya kuwa ameshafanyiwa Aqiqa. ‎

Uwislamu ulipokuja, haukupiga marfukufu Aqiiqa, k**a ilivyokuwa ‎hakupiga marufuku wanyama wa Udh-hiya. Ila ulipiga marufuku ‎kumpaka mtoto damu ya Aqiiqa, wakiamini kuwa damu hiyo ndiyo ‎unamlinda na kumhami. ‎

Badala yake ukaachia wazi waislamu kufanya lolote lile ambalo ‎halina ushirikina wala mila za kishirikina. Maswahaba walikuwa na ‎mtindo wa kumpaka mtoto zaafarani, kwenye kipaji; ili kuonesha ‎kuwa ameshafanyiwa Aqiiqa na ameshapewa jina. Hivyo, wale ‎wanaokuja kuwasalimai wazeewa mtoto, wakiona hivyo wanajua ‎kuwa ameshapewa jina. Hizi ni mila ambazo hazina mushkeli. Sisi ‎tulipakwa Hina vipajini, na tumekuwa tukifanya vivyo hivyo kwa ‎watoto wetu na wajukuu zetu.‎

Imepokewa kutoka kwa Abu Burayda al-Aslamiyy ‎رضي الله عنه ‏‎ ‎akisema: Zama za Ujahililyya, tulikuwa tukichijja mbuzi tunapopata ‎mtoto wa kiume, na tumapaka kichwa chake kwa damu ya mbuzi ‎huyo. Lakini ulipokuwa Uwislamu, tukawa tunamnyoa nyewele zake ‎na tunampaka zaafarani” Bidayat al-Mujtahidl, 1\476.‎

KUMUADHINIA MTOTO.‎

Inapendekezwa, ‎مستحب‎ na waja wema kumuadhinia mtoto sikio lake ‎la kulia na kumqimia sikio lake la kushoto; ili kutabarruk ‎تفاؤلا‎ kwa ‎matumaini mema kuwa Saudi na Qauli ya mwanzo anayo isikia ni ‎Wito wa Swala, na Majina ya Mwenyezi Mungu. Mtume ‎صلى الله عليه وسلم‎ ‎alikuwa haamini kuweko MIKOSI, kila kitu kinatoka kwa Allah, lakini ‎akiamini Fa’l = matumaini mema. Hivyo, Kumudhinia na kumkimia ‎mtoto mchanga, ikawa miito mwili hiyo ndiyo anayoisikia, mara tu ‎baada ya kuigia katika Dunia hii, ni Fa’l njema. Hakuna mushkeli. ‎

SUNNA YA KUOMBEWA NA MJA MWEMA.‎

Sunna nyengine, muhimu, ni kumapta mja mwema, kumuombea ‎dua mtoto mchanga huyo, hata k**a kabla ya kutia kinywani ‎chochote kile, na kutafuna kitu kitamu, k**a tende, na kisha ‎kuchovya kidole cha mja mwema huyo kwenye mmung’unyo wa ‎tende hiyo, na kumrambisha mtoto mchanga huyo. Hivyo ndiyo ‎alivyokuwa akifanya Mtume ‎صلى الله عليه نسلم‎ pale anapoletewa watoto ‎wachanga awaombee na kuwafungua kinywa. ‎

والله أعلم

وبالله التوفيق

السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم‎ ‎

Imejbiwa na Sayyid Abdulqadir Shareef

NI RUHUSA KUNUKUU, k**a ilivyo, pasi na kubadilisha ‎au ‎kuongeza chchote, na kuweka kwenye FB yako ‎au ‎kwenye ‎WhatsApp na kwenye Makundi ya Mitandao ya ‎Kijamii za ‎Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na kuelimisha ‎Dini. Changia ‎kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.‎

[email protected]

Want your school to be the top-listed School/college in Zanzibar?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address

Zanzibar
Zanzibar