25/06/2023
Habari wadau wa Genius kids school...Natumaini wote mpo salama...Tukiwa tunamalizia wikiendi ya leo, nimewiwa kushirikisha kidogo kuhusu kanuni zinazomwongoza baba , mama, au mlezi namna bora ya mwingiliano(Adult -child interavtion)na watoto zetu ili kupelekea makuzi na maendeleo mazuri ya mtoto katika nyanza zote(kiakili,kihisia,kijamii n.k)
Kanuni zinazokuongoza ni hizi zifuatazo
1.Onyesha upendo kwa mtoto..Hii ni kanuni muhimu sana kwani itamfanya mtoto akukumbuke, akupende, akuelewe na kufuata unachokitaka siku zote..Onyesha upendo kwa namna utakayoiona ni nzuri kulingana na mazingira na uchumi wako..
2.Ongea na mwanao(mtoto wako)...Tenga muda wa kukaa na mtoto wako na ongea naye...Kupitia kuongea naye utakuwa rafiki mkubwa na hakika utafirahia kesho yake....itamuesha na mengi, na itakusaidia kujua mengi....Je, ni mara ngapi unatenga muda wa kuzungumza na mtoto wako kuhusu mambo mbalimbali au mda wote tupo busy na maisha ?
3.Msifie(Praise) na kumfahamu/kumthani kwa kile anachofanya k**a ni kuzuri(Appreciably)
Hii itamtiabhamasa katika kile anachofanya na sio kila kitu ni kukosoa kosoa, hii inauwa jitahada ya mtoto kutoka ndani na kuanza kujenga zana ya kuwa yeye ni wa kushindwa kila wakati....Swali la kujiuliza je hili tunalifanya kwa kiasi gani?..
4.Msadie mtoto kuzingatia lengo (help you child to focus)
5.Panua uzoefu wa mtoto katika vitu mbalimbali....Mfano, kwa kutembelea sehemu mbaimbali/mazingira tofauti au kwa kufanya vitu tofautitofauti(exposures)
6.Msaidie mtoto wako kujifunza taratibu,maadili na ukomo wake....
7.Tusiwalazimishe watoto tunavyopenda sisi bali nini mtoto anataka kuwa..
8.Msaidie mtoto kuona yeye ni yeye na hakuna k**a yeye..
..........na,mlezi wa watoto hapa Genius kids......
Tunaendelea kupokea na kusajiri watoto katika kituo chetu , ewe mzazi mlete mwanao katika kituo chetu bora kilichopo nyasa mchema-masasi ,Mtwara.....
Watoto kuanzia wenye umri wa miaka 2.5(miwili na nusu ) mpaka mitano(5) wote mnakaribishwa.
Genius kids preschool tuna amini kesho ya mtoto inanzia hapa..0743364514/0753203352....To share is to care...😁