14/10/2015
YAA RABBI NAKUOMBA KWA MAJINA YAKO MATUKUFU NA KWA KILA AYA YA QUR AN MRUZUKU MJA WAKO HUYU AFYA NJEMA, NA NGUVU, NA TAWFIIQ, NA KILA KHERI ZA DUNIA NA YA AKHERA.
PIA YAA RABBI MWEPUSHE NA MISUKOSUKO YOTE, NA HASADI NA KILA SHARI. AMIN AMIN AMIN
YAA ILAHI Mwaka huu mpya 1437 Hijriya, ujaalie kwa Waislamu ni mwaka wa kupata amani kila kona ya DUNIA, kupata nguvu, kuhifadhiwa na shari.
Ukurasa mpya ufunguliwe na kila Muislamu, na Uislamu usonge mbele.
YAA RABBI NAKUOMBA TENA kila Muislamu awe na maisha mazuri, na awe na afya, Istiqama ktk dini, kila mwenye deni aweze kulipa, kila mwenye binti alofikia kuolewa apate Mume wa kheri. Kila mwenye maradhi apone, kila mwenye kumpenda Bwana Mtume MKARIMU azidishe mapenzi hayo, kila aliye bakhili abadilike kuwa MKARIMU, kila mwenye tabia chafu, abadili tabia kuwa njema, Yaa Rabbi ni wewe tu ndiye unaejua shida za waja wako, wengine ni fasaha kukuomba na wengine hata kueleza shida zao hawawezi, kwa huruma yako na upole wako wasamehe madhambi yao, na uwape Subra na uwape kila kheri na uwaepushe kila shari.
Walio vitani waache vita, waungane Waislamu wote wapendane wawe kitu kimoja k**a mwili mmoja. Amin