19/08/2026
Asante kwa dhati Jumuiya ya kwa moyo wenu wa kujitolea na kufadhili safari ya elimu kwa wanafunzi wetu.
Tunajivunia kushuhudia wanafunzi wanne (4) kutoka Istiqama Tanga Islamic Secondary School, ambao walikuwa miongoni mwa wanafunzi walioomba fursa hii, wakifanikiwa kupata nafasi ya kuendelea na masomo nchini Oman. ๐ด๐ฒ
Kwa ujumla, wanafunzi wote walioomba fursa hii tunawapongeza kwa ujasiri wao wa kutafuta nafasi za kielimu na kuamini katika uwezo wao. Kila hatua waliyochukua ni sehemu ya safari yao kuelekea kutimiza ndoto zao.
Tunawashukuru sana Jumuiya ya kwa juhudi na nafasi hii adhimu, pamoja na wadau wote wanaoendelea kuwekeza katika elimu na kuwawezesha vijana wetu.
๐๐๐๐ข๐๐๐ญ๐๐ ๐ญ๐จ ๐๐ฑ๐๐๐ฅ๐ฅ๐๐ง๐๐ !