10/03/2026
TABIA ZINAZOUA HATIMA YA KIJANA
Habari za muda huu Ndugu na jamaa zangu.Leo napenda tujifunze tabia nne tu miongoni mwa nyingi zinazoua hatima ya kijana.Fuatana nami hapa chini 👇
1.MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA🌬️
Matumizi ya dawa za kulevya ni hatari sana katika maisha ya kijana na huua hatima ya kijana kwa haraka na hàkika.
Dawa za kulevya Zina adhari kubwa za moja kwa moja kisaikolojia 🧠 na kimwili.
Dawa za kulevya huharibu uwezo wa kufikri,kumudu hisia (Emotional control) ,Hujenga mtazamo hasi katika Mambo mbalimbali na hupelekea mtu kuugua magonjwa ya Akili na mwili na hivyo kuua hatima ya mtu kabisaa.
Matumizi ya dawa za kulevya
Mfano Bangi , Co***ne, Ma*****na, Heroine na morphine, Yameua hatima ya vijana wengi sana.
Vijana wengi wamekuwa tegemezi, wagonjwa wa Afya ya Akili na mwili, wezi ,wabakaji ,wenye fujo na wauaji kwa sababu ya kutumia dawa za kulevya.
Hivyo kijana ishi maisha yenye kusudi ili kufikia hatima yako iliyo njema.
2.ULEVI🍾🥂🍻
Matumizi ya pombe Yana madhara makubwa sana katika maisha mtu katika umri wowote .
Katika kipindi Cha Ujana Afya yako inaweza kuharibika kabisaa kutokana na matumizi ya pombe, pombe inaweza kuharibu Ini,moyo ,mapafu na hatimaye baada ya muda tu kidogo hapo mbele Mtu anakuwa dhaifu sana na inakupelekea kuugua ugonjwa wa Muda mrefu au hata kufa kabla ya wakati (Premature Death).
Hata hivyo pombe hupunguza Utendaji na ufanisi wa kazi,huchajiza matumizi mabaya ya rasilimali alizonazo mtu.
Pombe hupelekea mtu kuacha au kuachishwa kazi, kuvunja ndoa🚻, Kuua mali zake mbali mbali kwa dhumuni la kupata fedha ya matumizi ya pombe au kulipa madeni yaliyotengenezwa kwa sababu ya ulevi .
Vijana wengi pia wameharibika kisaikolojia 🧠 kwa sababu ya Uraibu wa Pombe na hivyo kupoteza morali ya kutaka kufanikiwa na kubaki wanaishi tu bila malengo yeyote.Kijana amka ,sh*tuka pombe imeua hatima ya wengi sana.
3.UVIVU 🛌
Tabia ya kijana Kuishi bila kufanya kazi yoyote ya kuingiza kipato au kusaidia jamii imeua hatima ya vijana wengi sana .
Kijana anaweza kujishughulisha kwa kufanya biashara ,kazi ya kuaajiriwa ,kulima na kazi yeyote halali .
Kijana anapaswa kutengeneza hela kwa ajili ya sasa na baadaye,fedha inasaidia kutatua changamoto nyingi sana japo si zote lakini ni Muhimu sana kuwa nayo.
Matumizi mabaya ya fursa zinazokuja mbele yako hupelekea kujutia baadaye maana kuna muda Nguvu ulizonazo zitaisha,Afya ulionayo inaweza kudhoofika na fursa unazopata sasa zinaweza zisipatikane tena.
Tabia ya kijana kulala muda mrefu, kuangalia TV muda mrefu,kuchati tu muda mrefu , kufanya kazi kwa mikono milegevu imeua hatima ya vijana wengi sana Duniani.
Kijana Lazima uwe na kazi ya kufanya na ni lazima uifanye kwa bidii ili ilete matunda/faida.
4.MAHUSIANO YA KIMAPENZI 💑
Kijana anapaswa kuwa na Mahusiano yenye Afya kwa maana ya kuwa na mke au mme ,kujenga familia na kuweka malengo yatakayo itoa familia yako kutoka hatua ilipo hadi hatua zaidi iliyobora kabisaa.
Tabia ya vijana kuwa na wapenzi wengi ,kuwa na michepuko ,kujiuza kwa wadada, imeharibu hatima ya vijana wengi sana Duniani.
Kupitia kuwa na wapenzi wengi Nidhamu ya maisha hushuka na pia siyo standard ya Mungu, kunaleta matumizi holela ya rasilimali fedha.
Kuwa na wapenzi wengi hatima ya wengi imekufa kutokana na Magonjwa yanayopatikana kupitia kujamiana .
Ndoa za vijana wengi zimekufa kwa sababu ya michepuko au watu wa pembeni.
Wadada wengi wamepoteza maisha au kuishi na maradhi ya muda mrefu kwa sababu ya kujiuza.
Tunza hatima yako kwa Mahusiano yenye tija.
Usikubali utu wako utwezwe
Usinunue mafanikio kwa uchi wako
Usitafute kazi kwa uchi wako.
Usitafute amani kwa uchi wako .
Usitatue Matatizo kwa uchi wako.
Usishushe thamani yako ,usishushe Ukubwa wa kusudi ambalo Mungu ameweka ndani ya Maisha yako.
Katika kuepuka mambo hayo yote usisahau kuweka maisha yako kwa MUNGU huyo ndiye anaweza kuyaongoza maisha yako, usizitegemee akili zako mwenyewe.
Mathias samwel
10 March 2026.
Youth with Purpose.