28/02/2023
Mambo vipi? Mchana huu tumekuandalia machache kati ya mengi tuliyokuandalia na mtandaoni utakuwa nami Elisante Kivuyo , na hizi ni baadhi ya taarifa utakazozisikia:
šUingereza na Umoja wa Ulaya zimetangaza "ukurasa mpya" katika uhusiano baada ya miaka mingi ya mvutano wa Brexit, huku wakikubaliana kuhusu marekebisho ya sheria za biashara huko Ireland Kaskazini
š§Ukraine imesema kuwa vikosi vyake vipo chini ya shinikizo katika mji wa Bakhmut, ambao umeharibiwa vibaya katika jimbo la mashariki la Donetsk, ambalo Urusi imekuwa ikijaribu kulikamata kwa miezi kadhaa
ā Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya nchi 30 zimeahidi kutoa msaada wa kiutu wa takribani dola bilioni 1.2 kwa ajili ya mamilioni ya watu wa Yemen
ā Matokeo ya awali katika uchaguzi wa Nigeria uliofanyika mwishoni mwa wiki yanaonesha Bola Tinubu kutoka chama tawala akiwa kileleni.
:DW