12/05/2026
SI KILA MTU ANA FURAHIA MAFANIKIO YAKO KUMBUKA HILI ITAKUSAIDIA.
Kaini na Habili walikuwa ndugu wa damu lakini kufanikiwa kwa Habili kulisababisha Kaini ainuke kinyume na mdogo wake kwa kujaa wivu na matokeo yake akamuua.
Ni kweli rafiki uliye naye mnacheka na kufurahi lakini vicheko na tabasamu hilo pengine ni TABASAMU LA MAMBA ANATAFUTA NAMNA YA KUKUMEZA K**A ALIVYOMEZWA HABILI NA KAKA YAKE.
Biblia
Mwanzo 4:8 inasema:
“Kaini akamwambia Habili ndugu yake; ikawa walipokuwa shambani, Kaini akamwinukia Habili ndugu yake, akamuua.”
Mstari huu ni muhimu sana kwa sababu unaonyesha dhambi ya Kaini ilianza na tamaa ambayo badae ikawa mimba na Mimba ikazaa Dhambi kutoka moyoni mpaka kuwa chanzo cha mauaji.
Yakobo 1:15
[15]Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.
Then when lust hath conceived, it bringeth forth sin: and sin, when it is finished, bringeth forth death.
MAELEZO MENGINE
1. Kaini alikuwa tayari ameonywa na Mungu ila hakusikia.
Kabla ya mstari huu, Mungu alimwonya Kaini:
“Dhambi iko mlangoni, nayo inakutamani wewe…” — Mwanzo 4:7
Hii inaonyesha kuwa:
-Hasira ya Kaini ilikuwa tayari imeonekana.
-Mungu alimpa nafasi ya kutubu.
-Kaini hakutawala hisia zake.
-Dhambi huanza ndani ya moyo kabla haijawa kitendo ni vyema MOYO ulindwe sana.
Mithali 4:23 — “Linda moyo wako kuliko yote…”
2. Chanzo cha mauaji kilikuwa wivu na kukataliwa
Mungu aliikubali sadaka ya Habili lakini hakuiangalia ya Kaini kwa namna ileile.
Kaini:
-Alijawa na wivu,
-Akaona chuki dhidi ya ndugu yake,
-Badala ya kutubu alimshambulia Habili.
Hapa tunaona:
-Wivu usipotibiwa hugeuka kuwa chuki na Kaini ilikuwa vigumu kutubu maana alikuwa tayari mwovu amemmiliki.
1 Yohana 3:12
[12]si k**a Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.
Not as Cain, who was of that wicked one, and slew his brother. And wherefore slew he him? Because his own works were evil, and his brother's righteous.
HITIMISHO JUU YA MWANZO 4:8
-Dhambi huanza moyoni.
-Wivu na hasira vinaweza kuleta maangamizi makubwa.
-Mungu huonya kabla hukumu haijaja.
-Moyo usiotubu unaweza kumfanya mtu atende maovu makubwa.
Waefeso 4:26-27
[26]Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;
Be ye angry, and sin not: let not the sun go down upon your wrath:
[27]wala msimpe Ibilisi nafasi.
Neither give place to the devil.
MUNGU AENDELEE KUWABARIKI WATU WANGU.
MWL.AMOS KATELA(0765010034)