Bunoko

Bunoko My page for my people

24/12/2015

Siri kubwa iliyofichwa katika Hatma ya maisha yetu ndiyo inayosababisha watu wengi sana tusijue kesho yetu ikoje. Laiti k**a Wadada wengi wangekuwa wanajua miaka 20 ya mtu anayemkataa leo sababu ni hohehahe kwa leo na k**a Wakaka wangejua hatma ya Wadada wanaowachukilia pouwa leo nadhani wangewatongoza kwa nguvu zao zote sababu wanajua Kesho yao ni njema.

Tatizo ni kwamba Hatma imefichwa katika maamuzi unayoyafanya leo. Mungu aliumba mti ili ndani ya Mti uweze tengeneza Rungu, Kitanda, Makochi, Meza etc. Ukitaka Mke wako ama Mume wako awe fulani unayokazi ya Kuliendeleza gogo liwe la kukufaa kwa matumizi Utakayo k**a ni Mwiko ama mtumbwi au Meza.

Nimewahi sikia Vijana Wengi Sana wanasema "Wife Material" ndo wanaolewa na Wanawake wengi wanajikuta wanahangaika kutafuta U Material wenyewe wasio ujua wakidhani wataolewa. Ukisikia Material maana yake ni "unfinished goods". Material sio Product inayoingia Sokoni. Mnunuzi wa "Material" ndiye mwenye kazi ya Kutengeneza Product aitakayo. K**a Unataka Tengeneza Soda Ya Pepsi "Material" yake hayafanani na Juice ya Azam. Ni Kazi ya Kiwanda "KUPROCESS".

Wanaume wengi sana wanataka ku kwepa kitendo cha KUPROCESS ....Material ili yawe Product unayoitaka. Kila mwanamke ni Material Kasheshe ni Kiwanda Cha Ku Process ambacho Kinaitwa Ndoa ili Mkeo awe vile unavyomtaka. Ukitaka Mkeo awe anatiririka Kiingereza basi Mpeleke pale British Council, K**a unataka Mkeo awe Sister Duu....Process Her to Be....

Wengi wanadhani Material ni Product....Kwangu hapana Material ni Malighafi Unayoweza Itumia kutengeneza Utakacho...Ukiwa Unatafuta Wife Material ama Husband Material jua ni Sawa mtu aliyenunua gogo ili kwenda Kutengeneza viti, miiko, mtumbwi etc au ni sawa aliyenunua dhahabu ghafi halafu unakazi ya kuifanya either pete, chain, kidani au chochote kila Material unaweza fanya Utakacho. Unaweza Mfanya Mkeo ama Mume vile unavyotaka awe "for good".

Ukimuacha mtu eti sababu sio type yako jua ni vile tu umekwepa jukumu la Ku Process. Usitazame Jambo leo kwa sababu ya Mtazamo wa mazingira ya sasa.

Elimu dunia

21/10/2014

via BongoSwaggz.Com

K**A UNA MOYO MWEPESI USISOME STORY HII, WENGI WAMELIA SANA !!

“Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na kumwambia, Kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake yalionyesha anaumizwa. Nilishindwa hata namna ya kuanza kufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi nimwambie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.

Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu. Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa nini?’ Sikumjibu swali lake. Kutojibu kulimfanya akasirike. Akatupa kijiko na akanikaripia, ‘wewe si mwanamume!’ Usiku ule, hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi. Nilifahamu kwamba alitaka kujua ni nini kimetokea kwenye ndoa yetu. Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa jibu wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali kitu kwangu penzi langu lilihamia kwa Mary. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote yalikuwa kwa Mary. Kwa kweli nilimdharau mke wangu!

Huku moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanya kosa, niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu. Aliangalia talaka ile na kuichana vipande vipande.

Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10 alionekana mgeni machoni mwangu. Nilimuonea huruma kwa muda, rasilimali na nguvu alizopoteza lakini sikuweza kurudi nyuma kwa sababu Mary aliuteka moyo wangu kisawasawa. Hatimaye mke wangu alilia kwa sauti mbele yangu, jambo ambalo kwa hakika nilitarajia. Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu.

Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa majuma kadhaa na sasa limeendelea kuimarika na kuwa jambo la hakika zaidi.

Siku iliyofuata nilikuja nyumbani kwa kuchelewa sana nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani. Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda moja kwa moja chumbani na usingizi ulinichukua mara moja kwa sababu nilikuwa nimechoka baada ya kula raha za kufa mtu na Mary

Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado akiandika. Sikujali kabisa nikajifunika vyema shuka na kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya talaka yake: hakutaka kitu chochote kutoka kwangu lakini alihitaji apate angalau mwezi mmoja wa kujiandaa kabla hajaachika. Akaomba kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja sote mimi na yeye tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa kadiri itakavyowezekana. Sababu yake ilikuwa ndogo lakini muhimu: mwanetu wa kiume alikuwa akikaribia kufanya mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu ya kuachana kwetu. Hili halikuwa tatizo kwangu, nilikubali mpango wake. Lakini alikuwa na sharti la ziada, aliniomba nikumbuke jinsi nilivyombeba siku za fungate yetu hasa siku ya harusi yetu. Akaniomba na kunisihi kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe nambeba kutoka kitandani kwetu mpaka mlango wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa kichaa. Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro nilikubaliana na masharti yake ya ajabu.

Nilimsimulia Mary kuhusu masharti ya kuachana na mke wangu. Mary alicheka sana, aliona ni ujinga. ‘Hata akitumia ujanja wa namna gani talaka ni lazima’, alisema Mary tena kwa dharau. Mimi na mke wangu hatukuwahi kugusana tangu nilipomweleza dhamira ya kumtaliki. Kwa hiyo nilipombeba kwa mara ya kwanza sote tulinuniana. Mwanetu alifurahi sana na kupiga makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama mikononi mwake’. Maneno yake yalinichoma moyoni moja kwa moja. Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni, halafu tena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi nimembeba mke wangu. Alifumba macho na kusema kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu ya talaka. Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia vibaya. Nilimuweka chini nje ya nyumba.

Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami nikaendesha gari kwenda ofisini kwangu. Siku ya pili, zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote. Aliegemea kifuani pangu. Nilisikia harufu nzuri ya uturi aliofukiza kwenye blauzi yake. Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa makini mke wangu kwa kipindi kirefu sana. Nikagundua hakuwa binti tena. Kulikuwa na mikunjo usoni na nywele zake zilianza kuwa nyeupe! Ndoa yetu imekula urembo wake. Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini namfanyia hivi.

Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati yetu zilirejea. Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi nami na tumeishi kwa miaka kumi sasa. Siku ya tano na ya sita ilikuwa wazi kwamba mapenzi yetu yalikuwa yakimea upya. Sikumwambia Mary kuhusu jambo hili. Kadiri mwezi ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke wangu na zoezi likawa rahisi zaidi. Pengine kufanya kazi hii kila siku kuliniimarisha zaidi.

Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi. Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa. Kisha akaguna, ‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa’. Nikagundua kwamba mke wangu amepungua sana, nadhani ndiyo maana niliweza kumbeba kirahisi. Ghafla jambo likanichoma... mke wangu ana uchungu na maumivu makuu moyoni mwake. Bila kujitambua nikamgusa kichwa chake. Mara mtoto wetu akatokeza na kusema ‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende kazini’. Kwake kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo la furaha sana. Mke wangu alimuonyesha ishara mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo mkuu. Niligeuza uso wangu nisije nikabadili mawazo katika dakika ya mwisho. Kisha nikambeba mikononi mwangu kutoka chumbani, sebuleni halafu mpaka mlangoni. Mkono wake laini ulikuwa umeizunguka shingo yangu kwa upendo. Nilimkumbatia mwili wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu. Lakini wepesi wake ulinitia mashaka.

Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata kupiga hatua moja. Mtoto wetu alishakwenda shuleni. Nilimshika kwa karibu na kumwambia sikubaini kwamba maisha yetu yalikosa upendo. Nikaenda zangu ofisini…. Nikashuka garini hata bila kufunga mlango. Maana nilihisi nikichelewa tu ninaweza kubadili nilichoamua.... nikapand ngazi. Mary alifungua mlango nikamwambia, ‘Samahani, Mary, sihitaji tena kumtaliki mke wangu’. Akaniangalia kwa kustaajabu, halafu akagusa kichwa changu. Akaniuliza ‘Unaumwa?’ Nikaondoa mkono wake kichwani kwangu. ‘Samahani, Mary, nimesema sitaki kumtaliki mke wangu. Nadhani ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu sikuthamini undani wa maisha yetu, mimi na mke wangu, si kwamba hatupendani. Nimetambua hilo tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha yetu, nampenda mke wangu sitamuacha mpaka kifo kitakapotutenganisha.’

Ikawa k**a Mary alizinduka usingizini. Akanizaba kibao cha nguvu, akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia. Nikashuka ngazi na kuondoka zangu. Nikaingia kwenye duka la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili ya mke wangu. Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye kadi. Nikatabasamu na kuandika “Nitakubeba kila asubuhi mke wangu mpaka kifo kitakapotutenganisha”. Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu, tabasamu kubwa usoni nikakimbia mpaka chumbani, nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani.

Kumbe mke wangu alikuwa akisumbuliwa na saratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa sababu nilihamishia akili yangu kwa Mary. Alijua kwamba angekufa karibuni na alitaka asiniingize katika chuki na mwanetu k**a ningelazimisha talaka mapema.

Angalau machoni mwa mwanangu naonekana ni mume mwema.

Mungu nisaidie Nisifike huku mimi.

K**a Stori Hii Imekugusa Na Ungependa Marafiki Nao Waisome Basi Unaweza KuSHARE.

26/09/2014

Baadhi ya mambo 10 yaliyomo kwenye Rasimu ya katiba iliyowasilishwa jana Bungeni na Mwenyekiti wa K**ati ya Uandishi ya Bunge Maalumu la Katiba, Andrew Chenge ni haya!

1. Muundo wa Muungano ubaki ule ule serikali 2 na sio 3
2. Hakuna Ukomo wa Mbunge kugombea hadi atapochoka mwenyewe
3. Wananchi hawaruhusiwi kumwajibisha Mbunge aendapo kinyume
4. Mgombea binafsi Ruksa
5. Jaji mkuu na Jaji wa mahak**a kuu watateuliwa na Rais
6. Mwenyekiti, Makamu mwenyekiti wa tume ya uchaguzi watateuliwa na Rais
7. Msajili wa vyama vya siasa atateuliwa na Rais
8. Tume ya maadili ya viongozi wa umma itateuliwa na Rais
9. Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali atateuliwa na Rais
10. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Mkuu wa jeshi la polisi na usalama wa Taifa watateuliwa na Rais

Nini maoni yako juu ya hilo?

14/08/2014

MWANANGU MPENDWA, NAOMBA UNISIKILIZE KWA UZURII KABLA HUJAOA..

1. Mwanangu, mwanamke anaweza kuwa mkeo, mwingine anaweza kuwa mama wa watoto wako, lakini ukipata mwanamke ambae atakuwa k**a mama kwako, mama kwa wanao na mama kwa familia, tafadhari mwanangu usimuache huyo!

2. Mwanangu, usimfanye mwanamke wako kuwa ndio wa kupika na kufanya kazi zote za jikoni peke yake, tabia hiyo sio nzuri Kwani hata nyakati zetu, mashamba yetu yalijulikana kwa majina yetu wanaume lakini tulifanya kazi pamoja!

3. Mwanangu, nikikwambia wewe ni kichwa cha familia, simaanishi kutuna kwa pochi lako, usiangalie kabisa pochi yako, angalia k**a utaona tabasamu usoni kwa mke wako. Pesa sio kila kitu katika ndoa na haileti ukuu wa familia!

4. Mwanangu, ukitaka kuwa na maisha marefu na ukapunguza misongo ya mawazo, ongea na mkeo pangeni bajeti ya mahitaji yenu, kisha mwache mkeo awe na jukumu la kuratibu mahitaji ya kila siku ya familia kwa kumkabidhi fungu husika hata k**a limetokana na michango yenu wawili. wanawake wanajua sana kupanga bajeti na hii haitakuwa rahisi kwa yeye kutumia hela hovyo wakati akijua kuwa nyumbani kuna mahitaji ya msingi, lakini hela zikiwa mikono mwako ataendelea kuomba hata k**a utakuwa umeishiwa!

5. Mwanangu, Usithubutu kumpiga mkeo, maumivu ya kipigo hukaa ndani ya moyo wake kwa muda mrefu sana na huacha kidonda ambacho hukawia sana kupona. Ni hatari sana kuishi na mwanamke mwenye majeraha moyoni!

6. Mwanangu, sasa unaamua kuoa,k**a bado utaendelea kuishi maisha k**a ya ubachela na mke wako, sio muda mrefu utakuwa bachela tena. ukioa Badilika anza kuishi maisha ya mke na mume!

7. Mwanangu, zamani,tulikuwa na wake wengi na watoto wengi kwa sababu tulikuwa na mashamba makubwa na mavuno yalikuwa makubwa, lakini kwa sasa maisha yamebadilika, kwa hiyo mkumbatie mwanamke wako peke yake kwani hakuna ardhi tena na mahitaji ya watoto ni makubwa sana. Angalia ukubwa wa familia yako!

8. Mwanangu, chini ya mwembe ambao nilikuwa nikikutana na mama yako inaweza kuwa ni hoteli kubwa kwa nyakati zenu,lakini kumbuka, kitu pekee tulichoweza kufanya chini ya mwembe ilikuwa ni kukumbatiana pekee.nakushauri ukikutana na marafiki wa k**e kikubwa unachoweza kufanya nao ni kupeana mikono na ikizidi ni kukumbatiana hadharani sio vinginevyo!

9. Mwanangu, usibadilike mara utakapoanza kupata mafanikio Zaidi, kuliko kuwahudumia hao viruka njia wa mtaani ambao hawajui mmetoka wapi na mkeo, nakushauri utumie na kufurahia mafanikio yako na mkeo ambae aliweza kusimama imara wakati wote wa mapito yenu magumu.

10. Mwanangu, kumbuka unapoanza kusema au kuona mke wako kabadilika, ujue kuwa kuna kitu ambacho ulikuwa ukikifanya umeacha kukifanya. Jitathmini na anza kufanya au kutimiza wajibu wako.

11. Mwanangu, usijaribu kumfananisha au kumlinganisha mke wako na mwanamke mwingine wa nje, kwani hata yeye anakuvumilia sana na hajakufafanisha na mwanaume mwingine yoyote huko nje na ndio maana aliamua kuwa na wewe.

12. Mwanangu, sasa hivi kuna hiki kitu kinaitwa haki za wanawake, sawa,k**a mwanamke anasema ana haki sawa na wewe katika nyumba, basi gawanya mahitaji yote ya ndani kwenu katika sehemu mbili zilizo sawa,halafu timiza nusu yako na mwambie atimize nusu iliyobaki.

13. Mwanangu, nilimuoa mama yako akiwa bado kigoli (bikra) na nilikuwa naenda sana kwao kabla sijamuoa, lakini kutomkuta mkeo bikra kusikufanye umlaumu kuwa alikuwa muhuni, kumbuka wanawake wa enzi zetu na wasasa ni tofauti, ulimchagua mwenyewe na ukigoli wake hukuujua kabisa. Usiingize mambo ya kabla ya ndoa kwenye ndoa yenu.

14. Mwanangu, sikuwapeleka dada zako shule kwa kuwa nilikuwa mjinga k**a wazee wengi wa hapa kijiji wasemavyo, tafadhari usifanye ujinga huu, kwani kiwango cha mafanikio ya wanawake sasa kimefanya wanaume waonekane ni watu wa kawaida sana na sio muhimu k**a enzi zetu. Ukijaliwa watoto wape elimu.

15. Mwanangu, zamani enzi za ujana wetu, wanawake walikuwa na urembo wa asili, ingawa siwezi kukudanganya, wengine waliongeza urembo kwa kujichora hina na hata kutoboa pua na masikio lakini usisahau hawakuonyesha maumbile yao nyeti hadharani k**a sasa. Hakikisha mkeo analijua hili!

16. Mwanangu, mama yako na mimi hatuna hisa katika kila kitu kinachoendelea kwenye maisha yenu, jaribuni kutatua changamoto zenu wenyewe bila kila mara kuja kwetu kuomba usuluhishi. Ndoa ni pamoja na ukomavu wa kutatua changamoto zenu bila kuziuza k**a gazeti kwa kila mtu.

17. Mwanangu, nilimnunulia mama yako kifaa cha kupikia vitumbua ili aanzishe mradi wa kuuza vitumbua, pia nilimsaidia kununua cherehani yake ya kwanza, tafadhari msaidie mke wako kutimiza ndoto zake kulingana na uwezo wako k**a ambavyo unahangaika kutimiza ndoto zako.

18. Mwanangu, usiache kutusaidia mimi na mama yako, utu uzima una changamoto nyingi sana na Mungu akikujalia utaziona muda ukifika. Pamoja na kutimiza majukumu yako k**a baba wa familia kumbuka pia bado tunaishi na wewe ni mtoto wetu.

19. Mwanangu, kila upatapo muda wa kusali, Sali na familia yako, kuna kesho ambayo huijui, ongea na MUNGU wako ambae anajua kila kitu kila siku!

20. NAKUTAKIA MAISHA MEMA YA NDOA MWANANGU. NAKUPENDA!

Ujumbe huu umeandaliwa na Boniface Ole Precious "Msakatonge" Ametoa ruhusa ya ku-share na marafiki.

04/08/2014

VNGNE NAWEKA KM REFERENCE KWANGU, MCJAL SANA

Naamini kwamba kila mmoja wetu hapa anajua ni
jinsi gani ilivyo ngumu kupata kazi. Hivi sasa
imezoeleka kabisa kuwa kupata kazi ni lazima
ubebwe, au uwe na ndugu yako mkubwa
serikalini atakayekupa ki memo ili uweze kupata
kazi bila kupitia tanuru la moto.
Hali hiyo imesababisha watu wengi hata wakiona
tangazo la ajira kukata tamaa hata kabla ya
kupeleka maombi yao ya kazi. Lakini pia sifa
zinazotakiwa ili kujaza nafasi hazitoi nafasi kwa
watafutaji wengi wa kazi na hivyo wengi
hulazimika kudanganya
Hapa chini nitataja baadhi ya uongo unaosemwa
na watu wanaoomba kazi ili angalau wapate kazi:
1. Mimi nina uzoefu wa kufanya kazi zaidi ya
moja kwa wakati mmoja - Huu ni uongo wa
dhahiri, wengi wetu tunadanganya sana kuhusu
hili, wakati hata tukipewa kazi mbili tu tunaaanza
kulalamika kwamba tunaonewa.
2. Napenda sana changamoto na huwa sikati
tamaa wakati ninapokumbana na changamotoI
kwenye kazi yangu – Mh! uongo wa mchana
kweupe. Na kwa bahati mbaya unaweza kukuta
watu wote waliofanyiwa usaili wametoa kauli
hiyo, hivi inawezekana kweli wote muwe
mnapenda changamoto wakati wengine
changamoto, ndogo tu wananawa mikono na
kusalimu amri mpaka wapate msaada
3. Mimi ni kijana ninayekaribia miaka 30 na
sijaoa (Kwa wanaume wengi) - Unaweza kuta
anakaribia miaka 40 na anaishi na hawara na
watoto kila kona aliozaa na wanawake tofauti
tofauti. siku hizi umri mkubwa ni kikwazo
makampuni mengi yanakimbilia vijana ambao
bado hajaoa na hawana majukumu, sasa ili
kupata kazi wengi hudanganya kuhusu hilo.
4. Nilikuwa natamani sana siku moja itokee
nifanye kazi na kampuni hii - Uongo mwingine
tena, unaweza kukuta wengine hata jina la hiyo
kampuni walilijua siku hiyo walipoona tangazo la
kazi.
5. Kwangu mimi mshahara siyo kipaumbele
changu, niko tayari kufanya kazi kwa mshahara
wowote mtakaonipa - Kweli? Wakati wengine
hukimbilia hapa JF kuulizia kiwango cha
mshahara wa taaluma fulani katika kampuni
anayoomba kazi......
6. Mimi naweza kufanya kazi katika timu - Wakati
wengine kazi yao majungu na kuwagawa watu
ndiyo vipaji vyao.
7. Niliacha kazi katika kampuni yangu ya awali
kwa ridhaa yangu mwenyewe ili nipate fursa ya
kutafuta kazi itakayoipa uzoefu zaidi - Nyoooo...
Labda HR wa kampuni ulipotoka asije ulizwa,
uliona lini mtu akaacha kazi kabla ya kupata
kazi, je utaishije kabla ya kupata kazi nyingine?

03/08/2014

Kumekcha!!!, kesho Ndio kesho kjua n nan anakwamsha wataz katiba mpya"!"""
TANGAZO LA MDAHALO ITV LIVE KESHO JUMATATU TAREHE 04/08/2014 KATIKA UKUMBI WA BLUE PEARL HOTEL ULIOPO UBUNGO JJN DAR ES SALAAM, KUANZIA SAA 9:00 MCHANA. NADHAN HII N FRUSA YA MWSHO NA MHIMU MAANA HAWA NDO WADAU WAKUBWA WA RASIMU NA KWA KIAC KIKUBWA WAO NDO MAJIBU

WAZUNGUMZAJI NI:-

1, JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA
2.JAJI JOSEPH BUTIKU
3.DR. SALIM AHMEF SALIMU
4.MHE. SAID AWADHI
5.HUMPHREY POLEPOLE

01/08/2014

ILI UITWE BABY/DARLING /SWEETHEART HAPA MJINI LAZIMA UWE NA VITU VIFUATAVYO
1.CAR
Hii inak**ata nambari moja, sababu inaact k**a catalyst, inaspeed up other attachments to comply with ur intentions to that beautiful chick you want to hold on onto your life.

2.CASH
Hapa ndo main point hapa, mapenzi bila hela siku hizi ni sawa na gari bila matairi, hayaendi. Tusibishane katka hili, hata k**a msichana wako hapendi pesa kiasi gani but lazima uwe na money za kuhandle petty expenses hata ikiwa ni dinner Nashera au voucher, la sivyo unaumbuka mjini. Hata hilo gari hapo juu halitakua na maana k**a Cash iz a problem.

3.CLOTHES
Hapa Bro naongelea muonekano wako binafsi, ebu acha kupiga suruali zako za malinda sita zile ambazo hadi kuzivaa umegombana sana fundi Juma kwanza rangi zenyewe za suruali hudhurungi na raba k**a wakimbia marathon.

Watoto wazuri bwana wanataka gentlemen haswaa, mzee wa kutokelezea, hata k**a huna pamba kali basi ulizonazo wazipangiliaje. Hapa nadhani wadau waukweli watajua nazungumzia vitu k**a Hermes, Pierre Cardin, Luis Vuitton, Tom Clanks, na chata ka hizo.... sio unatupia singlendi ya buku sh tano ina matobo k**a neti na hupigi bafu, sahau matoto mzuri.

4.COMMUNICATION
Hapa sasa pana tatizo bwana, unajua communication nayoizungumzia hapa ni aina mbili, Verbal communication na Physical Accessories Communication watoto wazuri wa mjini wanapenda viingreza asikwambie mtu, wanamiksi yaani (tunaita code mixing)...kiswahili kidooogo then kiingereza kwa saana yabidi ujipange aisee.

Hizi like uuuuh.... mnh uknow... i kinda...uuuh... uwe vizuri mzeee la sivo utaishia kupata watoto wa Kichangani, Tandale kwa
Tumbo.... hiyo ya pili nazungumzia device sasa, Hapo jiulize unasimu ama unachombo cha mawasiliano? siku hizi wajanja tuna Apple, Samsung Galaxy, Htc, Huawei na vitu adimu ka hizo...sasa we komaa na simu zako za tochi utajuta...mtot anataka akuone mainsta nini sana.

5.CONFIDENCE
Hapa watoto wengi wakishua wanapata shida, confidence ni ability ya kuexpress ur feelings towards a girl looking at her eyes. Sasa kuna wajomba wanaona aibu mpka wanaume wenzao, sasa mtiti unakuja anapomit na mtoto mzuri hahahah. Kila kitu hapo juu anacho btu ame-lack confidence... Kalaghabao.

6.CHANCE
Chance bwana ni ile unakua na mchizi wako ana demu mzuri... halafu huyo demu ana rafiki yake mzuriii pia...aaaaaah hapo c k**a kumpa Christiano Ronaldo na Laiton baines free kick..... Si maanishi kumpindua mwenzio. Communication also mean the chances you have in your life interms of education, employment e.tc

Address

P. O Box 2145
Mwanza

Telephone

0767661782

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Bunoko posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category