Lake Victoria Bible College Mwanza

Lake Victoria Bible College Mwanza Bible Study For Children Ministry CHILDREN MINISTRY

19/03/2023

πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”

19/03/2023

πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”

Karibuni sana Lake Victoria Bible College Mwanza
14/06/2022

Karibuni sana Lake Victoria Bible College Mwanza

14/06/2022
15/01/2020

Fanyia wengine vile upendavyo kufanyiwa

11/01/2020

πŸ€”πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ‘πŸ€

MUNGU WAPONYE NA WASAIDIE WAIMBAJI.
26/12/2019

MUNGU WAPONYE NA WASAIDIE WAIMBAJI.

UJUMBE WANGU WA KUMALIZA MWAKA KWA WAIMBAJI WANAOANZA HUDUMA HII.

Mungu amekupa huduma nzuri sana lakini inahitaji unyenyekevu sana maana aliyepewa wa kwanza (rucifer) ilimshinda kwa sababu ya kiburi.

Ufuatao ni ushauri wangu, ili ufike mbali.
1. Ukiitwa kuimba na ukanyimwa nauli usitangaze wala kunung'unika.

2. Ukipewa kuimba wa kwanza usijione hujaheshimiwa, maana kuimba mwisho baada ya wengine kuimba haimaanishi wewe ni mwimbaji mkubwa kuliko wengine.

3. Ukiitwa kuimba wakati wa kutoa sadaka usijisikie vibaya na kudhani wamekudharau, sadaka ni sehemu ya ibada hivyo imba kwa furaha, usitishwe na movement za watu, UKIHISI HAWAKUSIKILIZI JIFUNZE KUJISIKILIZA MWENYEWE.

4. Ukiitwa kuimba watu wanapotoka usikasirike, imba kwa furaha maana ibada yako ya sifa inamuhusu Mungu ambaye wakati huo anakuwepo wala hatoki, HIVYO MUHESHIMU HUYO.

5. Ukisahauliwa kupewa nafasi ya kuimba usihangaike kukumbusha kuwa upo. KAMWE USING'ANG'ANIZE MAANA ALIYEKUPA HUDUMA ANAJUA UPO, HIVYO USIMCHUKIE MWONGOZA IBADA KWA KUKUSAHAU, RATIBA ZA KUIMBA ANAZO MUNGU HUYO UNAMUONEA TU.

6. Ukiambiwa ratiba jumapili zimebana uje kuimba ibada za katikati ya wiki, usiseme hawajakuheshimu MAANA SIKU ZOTE NI ZA MUNGU K**A ILIVYO JUMAPILI NENDA KAIMBE TENA USIKOSE.

7. Ukialikwa na kukuta watu wachache kuliko ulivyodhani USIPUNGUZE KIWANGO NA MORALI YAKO YA KUHUDUMU. JIWEKEE MALENGO YA KUKUTANA NA MTU MMOJA NA HUYO MTU UWE WEWE, ILI HATA UKIKOSA MTU UJIIMBIE WEWE NA UMUIMBIE MUNGU WAKO KWA SIRI. Ukifanya hivyo hata ukimkuta mmoja utakuwa na amani maana utaona mko wengi kuliko ulivyopanga.

8. Ukikuta vyombo vibovu usilaumu maana hujachangia gharama za vyombo, Fanya kilichokuleta, KUMBUKA WAO WAMEVIZOEA NA WANAKUSIKIA NA UBOVU WA VYOMBO VYAO HIVYO K**A UNAJISIKIA WEWE INATOSHA, TIMIZA WAJIBU WAKO.

9. Ukilazwa sehemu duni, ukapewa chakula duni, usihame wala usiombe chakula bora zaidi, labda k**a utafanya hivyo kwa gharama zako, ila pia tumia hekima ili wenyeji wako wasijisikie vibaya wakakwazika. MAANA UWEZO WAO HUENDA UMEISHIA HAPO NA WALICHOKUANDALIA NDIO CHA KIWANGO CHA JUU NA MWISHO WA UWEZO WAO, USIENDE ZAIDI YAO BALI TUMIA HEKIMA, MAANA HUTAKONDA WALA KUFA UKICHUKULIANA NAO.

10. Ukiombwa wimbo usikatae ila k**a una sababu basi tumia hekima kuwaelewesha, maana wanaweza kuomba wimbo nawe ndani yako ukasikia Roho anakuongoza kuimba wimbo mwingine, BILA SHAKA ROHO WA MUNGU ATAKUPA AMANI NA HEKIMA YA KUAMUA NA WOTE WAKABAKI NA AMANI.

11. K**a itatokea mwenzio kafanya vizuri na kashangiliwa kuliko WEWE usione wivu, na k**a roho itakuuma basi pambana nayo kwa kumuombea ili akisimama tena wamshangie zaidi ya vile roho ilivyokuuma.

12. Usiposhangiliwa usijisikie vibaya ukahisi umekosea, kushangiliwa ama kutoshangiliwa sio ishara ya kufanya vizuri ama vibaya.

13.Uwapo ugenini jiepushe kukaribisha watu hasa wa jinsia tofauti mahali unapolala hata k**a ndugu ni zako onana nao kanisani, MAANA HAKUNA ATAKAYEJUA NI NDUGU YAKO. NA IKITOKEA WAMEKUJA BASI ZINGATIA USHUHUDA NA USALAMA ILI KUMPONYA MWENYE MASHAKA.

14. Ukiimba kaa mahali ulipoandaliwa, usitoke mpaka ibada iishe, hata k**a unabanwa na haja,, k**a unauwezo wa kuvumilia kaa maana hautakufa. USIENDE NJE NA KUANZA KUPIGA STORY NI UTOTO NA UTOVU WA NIDHAMU KWA MUNGU NA KWA WENYEJI WAKO.

15. Usilazimishe vitu, usilazimishe na kushawishi nguvu ya Mungu, wakati ndani ya moyo wako unajua haipo, usinene lugha ambayo chanzo sio Roho wa Mungu, ili kuwahadaa watu uko rohoni, kwanza umeitwa kuimba fanya kazi yako. BALI KILA JAMBO LIFANYIKE KWA DALILI YA ROHO MTAKATIFU.

MWISHO UWE NA KIASI KWA KILA JAMBO.
Nawatakiwa mwaka mpya mwema naamini Mungu kakupa kazi njema sana, ila vitu hivi vinaweza kuiharibu huduma yako na kusababisha usidumu k**a ilivyokusudiwa.

Mkutano wa injili Kabangaja
16/10/2018

Mkutano wa injili Kabangaja

Address

Nyamanoro
Mwanza

Telephone

+255765360969

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Lake Victoria Bible College Mwanza posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category