27/11/2024
MAMBO MUHIMU KATIKA MAISHA UNAYOPASWA KUYAJUA.
1. Usimpigie mtu simu zaidi ya mara mbili mfululizo Ikiwa hakupokea simu yakoya kwanza na ya pili, fikiria kuwa labda ana kitu muhimu anafanya,akimaliza atakupigia.
K**a ni mtu mkuu wa watu...yaani unajua anahudumia jamii kubwa utumishi wake,anahudumia kanisa,kiongozi serikalini au taasisi fulani, usimpigie simu ila anza na ujumbe mfupi wa message kwanza ya kuomba nafasi ya kusema naye ukimwonyesha ni muhimu sana,hasa k**a namba yako hana anza na utambulisho.
2. Kamwe usiagize sahani ya gharama kubwa kwenye menyu wakati mtu anakupa chakula cha mchana / chakula cha jioni. Afadhali yeye aseme no,agiza sahani kubwa zaidi...mfano anza na kugiza chipsi kavu tu kisha yeye aseme weka chipsi mayai na mishikaki ya nundu. Fanya hivyo hasa k**a hakukutoa out ila mmekutana kwa nasibu tu.
3. Daima mpe mtu pongezi mbele za watu..bila kujali udogo wake,wala usiseme "nitampa sana umaarufu" k**a aliandikiwa kuwa maarufu atakuwa maarufu tu hata bila wewe kumtaja.
Huwezi kuwa mdogo kwa kumtendea mtu mema hadharani...
4. Ikiwa unachukua teksi na rafiki na yeye analipa sasa, jaribu kulipa wakati ujao....ukilipiwa nauli ya daladala kwenda,wewe lipa wakati wa kurudi.
5. Heshimu maoni tofauti tofauti ya watu hata k**a mengine yanakuja kitofauti kwako....Kumbuka kile ambacho ni 6 kwako kitaonekana 9 kwa mtu anayekukabili. Mbali na hilo, maoni ya pili ni mazuri kwa mbadala;
6. Usiwahi kuwakatisha watu kuzungumza. Waruhusu kumwagika Waseme wasemavyo, wasikie wote na uwachuje wote....
7. Ikiwa unamdhihaki mtu, na haonekani kufurahia, acha na usifanye tena...ukiendelea kufanya huyo mtu ataacha kukuheshimu na ataanza kukukwepa maana watu hawapendi kuchafuliwa mioyo.
8. Sema “asante” mtu anapokusaidia..na usiusahau huo msaada hata k**a kuna siku atakuudhi. Usisahau mema mengi ya mtu hata k**a kuna baya moja kakukosea Ukiacha uchawi na uuaji mengi ni ya kibinadamu tu...kumbuka wema wa mtu.
9. Sifia hadharani. Kosoa faraghani utapendwa na wengi. Ukiwa mkosoaji tu hadharani na msifiaji faraghani utaitwa mnafiki na mwenye wivu.
10. Mtu anapokuonyesha picha moja kwenye simu yake, usitelezeshe kidole kushoto au kulia. Huwezi kujua nini kinafuata...kwenye simu ya mtu ni kifaa cha kuhifadhia siri zake.
11. Mtendee mfanya usafi kwa heshima sawa na Mkurugenzi Mtendaji. Watu wakikuona hivyo watakuita asiye na dharau.
12. Ukiwa na gari yako unakatiza mitaa na vioo viko wazo,usiache kuwasalimia watembea kwa miguu hata kwa kuwapungia mkono,huwa wanafurahi sana na kujihisi kumbe na wao wanathaminiwakubwa. Hii ni kwasababu wasio na magari hudhani wenye magari wana dharau na kujiona bora kuliko waenda kwa miguu.
13. Ikiwa mtu anazungumza nawe moja kwa moja, na ukawa unatazama simu yako ni kumkosea adabu.
14. Usitoe ushauri kamwe hadi uombwe.
15. Unapokutana na mtu baada ya muda mrefu, kwenye kuzungumza naye usishangae kisa kakonda au kabongeka sana...watu hawapendi ubonge huwa unakuja wenyewe kulingana na vyakula. Na watu hawapendi pia kukonda,maradhi huja yenyewe. UWE NA HEKIMA.
16. Usiulize mtu maswali haya k**a wewe si mchunba wake,mfanya kazi wa nida au polisi:
Umri wake,mshahara wake,idadi ya watoto wake...Huo ni umbea subiri yeye atakwambia ikiwepo haja.
Zingatia biashara yako na mambo yako na kitu chochote kinachokuhusisha moja kwa moja,mengine achana nayo.
17. Ondoa miwani yako ya jua ikiwa unazungumza na mtu yeyote barabarani. Ni ishara ya heshima.
18. Usizungumze kamwe kuhusu utajiri wako katikati ya maskini. Vivyo hivyo, usizungumze juu ya watoto wako katikati ya wanawake tasa. Kwa lugha rahisi acha kujisifu mbele za watu.
19. Jizyie kujiingiza vidole puani unapokuwa na watu,maana lazima utawashika mikono.
20. Baada ya kusoma ujumbe huu mzuri na ukakubariki, na hujalipia,jaribu kusema Asante kwa ujumbe....inamtia moyo mwandishi.
Asante kwa kusoma🙏