Mzazi Makini Tz

Mzazi Makini Tz πŸ‘¨β€πŸ‘©β€πŸ‘§ Elimu β€’ Malezi β€’ Nidhamu
πŸ“š Tunawasaidia wazazi/ walezi kufuatilia,Kuboresha maendeleo ya mtoto shuleni
πŸ“² Ushauri & Mafunzo kwa wazazi

Kuwa single mother haimaanishi mtoto wako atakosa mwelekeo.Upendo, mazungumzo ya kila siku, nidhamu na ufatiliaji mzuri,...
10/02/2026

Kuwa single mother haimaanishi mtoto wako atakosa mwelekeo.
Upendo, mazungumzo ya kila siku, nidhamu na ufatiliaji mzuri,
unaweza kumjenga mtoto mwenye:
πŸ“š ufaulu wa darasani
🀝 ujuzi wa kijamii
❀️ maadili ya maisha

Usijilaum sana,Unatosha,Unajitahidi na mtoto wako anaona.
🌱 Mzazi Makini tupo na wewe bega kwa bega

17/01/2022

Je umekutana na changamoto gani wakati umeenda kumuandikisha mtoto wako shuleni??

02/10/2021

Toa dukuduku lako juu ya utoro wa wanafunzi shuleni

17/09/2021

Ni changamoto gani mzazi unapitia pindi mtoto wako akiwa likizo.?

03/06/2021

Je mzazi/mlezi ni changamoto gani mtoto wako anakutana nayo shuleni ?funguka

08/04/2021

''Zaidi ya watanzania 5,000 walikuwa na sifa za kukaa hapo mlipokaa nyie leo lakini Mungu amependa nyie mkae hapo leo, Mkawatumikie watanzania bila ubaguzi, mkawe msaada sio bugudha na udharimu, msiwe kero kwa watanzania mkasimie haki, hiyo ndio kazi ninayowatuma'' - Rais Samia Suluhu.

β€œTAMISEMI mnajukumu kubwa la Elimu na Afya za Watanzania, mkasimamie miradi ya Elimu hasa shule za Sekondari za Wasichana, Kuna mahitaji ya Walimu zaidi ya 6000, Utumishi mpo hapa naomba muajiri hao walimu wakatoe huduma kwa Watanzania mkashughulike hilo mara moja”- Rais Samia Suluhu.

Toa Neno la shukrani Kwa Mh raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
06/04/2021

Toa Neno la shukrani Kwa Mh raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Tukiwathamini walimu, lengo la elimu bora litatimia?
16/10/2020

Tukiwathamini walimu, lengo la elimu bora litatimia?

JE? Mzazi / mlezi ni mara ngapi umewahi kukagua madadftari ya mtoto wako anapotoka shuleni?
15/08/2020

JE? Mzazi / mlezi ni mara ngapi umewahi kukagua madadftari ya mtoto wako anapotoka shuleni?

27/06/2020

Wizara ya Elimu imetoa maelekezo kufuatia malalamiko kuhusu ulipaji ada na malipo mengine kwa shule za msingi na sekondari zisizo za Serikali zitakapofunguliwa baada ya janga la corona na kusisitiza wanafunzi wote wapokelewe ili kuendelea na masomo June 29,2020.

Wizara imesema ada za shule kwa shule zisizo za Serikali (baada ya shule kufunguliwa) zilipwe kulingana na makubaliano yaliyoafikiwa mwanzoni mwa mwaka wa masomo na kusisitiza maelekezo ya awali kwamba kusiwepo na nyongeza yoyote katika kiwango cha ada.

Wizara hiyo imesema kwakuwa shule zilifungwa wakati muhula wa masomo ukiwa unaendelea wanafunzi wote wapokelewe ili kukamilisha muhula huo, upande wa malipo ya chakula na usafiri shule zichambue gharama inayopaswa kupungua kwa siku ambazo wanafunzi hawakuwa shuleni.
Wizara imewataka Wazazi kuzingatia kuwa kiwango cha ada mashuleni huwa kinakadiriwa kwa kuzingatia gharama za uendeshaji wa shule ambazo ziliendelea kuwepo hata shule zilipofungwa ikiwemo mishahara ya watumishi, ankara za umeme na maji nk

Address

3223
Moshi
25104

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00

Telephone

+255759776332

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mzazi Makini Tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Mzazi Makini Tz:

Shortcuts

Share

Category