KingPriest

KingPriest Hapa tunaifunua neema na kweli ya Mungu kwenye kila eneo la maisha ya mwamini. Growing in Grace and in the Knowledge of our Lord Jesus Christ.

Lengo ni kuujenga mwili wa Kristo kuwa wanafunzi wa Yesu waliopewa neema juu ya neema, tuweze kuishi MAISHA YA KIFALME na KIKUHANI na UTAUWA kwa ajili ya mapenzi ya Mungu. For our Life and our gospel should not be in word only, but also in power, and in the Holy Ghost, and in much assurance. (Thessalonians 1:5-6)

27/03/2026

The Apostle's Teaching

Matendo mema yaanzie ndani yako uwe mwema katika mawazo na moyo. (kiumbe kipya, - Haki na utakatifu wa kweli) haya ndio ...
09/06/2025

Matendo mema yaanzie ndani yako uwe mwema katika mawazo na moyo. (kiumbe kipya, - Haki na utakatifu wa kweli) haya ndio yatakayojitokeza nje. Yavue kwanza matendo ya mwili yote na mawazo yake mabaya.

Ephesians 4:24 mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.

BAADA YAPO NDIPO NYUMBANI KWAKO KWANZA, πŸ‘‡

1Timothy 5:8 Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.

Kwahiyo ni Unyumbu watoto na mke wako wanaishi kwa shida nyumbani ila kanisani unajikamua kupeleka sadaka, Na wazazi wako hasa wale ambao waziwazi wetu wako vijijini wanaishi maishia ya mwaka 90, halafu sisi mjini tunamtunza mchungaji/MTUMISHI balaa.

Watoto shule wanawafanyia ubahiri balaa, ila kanisani Mchungaji anakusifia kuwa wewe ni mtoaji.

Mzazi akikuomba Hela ni rahisi kusema SINA HELA, ila Mtumishi akikuomba hela hata k**a huna unasongesha unampatia.

JIRANI YAKO NI YEYOTE UNAYEKUTANA NAYE ANAYEHITAJI MSAADA UKAMSAIDIA.

Lakini sisi majirani wa namna hii hatuwaoni tunawaona watumishi na makanisani tu.

HATA PAULO ALIAMBIWA NA MITUME KUWA AWAKUMBUKE SANA MASIKINI[WAHITAJI],

Gal 2:10 ila neno moja tu walitutakia, tuwakumbuke maskini; nami neno lilo hilo nalikuwa na bidii kulifanya.

NA SIO KUWAKUMBUKA SANA WAZEE WA KANISA[AU WATUMISHI WENZAKE].

Ephesians 4:28 Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji.

[na sio apate cha kutoa kanisani au apate cha kumpa mchungaji- unless k**a mchungaji ni muhitaji]

HIVYO BASI;πŸ‘‡

1. wewe (vua matendo ya mwili, vaa haki na utakatifu wa kweli-tunda la Roho), na Fanya kazi ili usiwe na uhitaji,

1th 4: 11 Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, k**a tulivyowaagiza;
12 ili mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu cho chote.

2. nyumbani kwako(mke watoto, including wazazi k**a wanahitaji msaada)

1Timothy 5:8 Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.

3. Majirani

(hapa ni mhitaji yeyote, mfano wa yule msamaria aliyemsaidia jamaa aliyekutwa kaumizwa vibaya na wezi njiani)

Mathayo 25:34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;
35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;

Hebrews 13:16 Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka k**a hizi ndizo zimpendezazo Mungu.

4. Injili,

1Corinthians 16:6 Labda nitakaa kwenu; naam, labda wakati wote wa baridi, mpate kunisafirisha ko kote nitakakokwenda.
3John 1: 5 Mpenzi, kazi ile ni ya uaminifu uwatendeayo hao ndugu na hao wageni nao, 6 waliokushuhudia upendo wako mbele ya kanisa; utafanya vizuri ukiwasafirisha k**a ipasavyo kwa Mungu.

HuuπŸ‘† ni wajibu wa kila mkristo kushiriki kuipeleka injili kwa watu

YAANI HUWEZI KUKUTA MTU ANAUMWA ANAHITAJI MSAADA NA HELA UNAZO UKASEMA HIZI NI ZA INJILI, (priorities of Love)

5. Wachungaji wa kanisani

1Tim 5:17 Wazee [WACHUNGAJI] watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha.
18 Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake.

KUMBUKA HII KAULI PAULO KAISEMAπŸ‘† BAADA YA MAMBO YA WAJANE wa kanisani NA YA WATU WA NYUMBANI KUSHUGHURIKIWA.

Ni kwasababu wachungaji kabla kanisa halijakuwapo walikuwa na kazi zao, na makanisa yalipokuwepo WALIAMBIWA WATENDE KAZI KUWA MFANO KWA KANISA. (KIELELEZO) πŸ‘‡

mdo 2:17 Toka Mileto Paulo akatuma watu kwenda Efeso, akawaita wazee wa kanisa.[wachungaji]
33 Sikutamani fedha wala dhahabu, wala mavazi ya mtu.
34 Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na ya wale waliokuwa pamoja nami.
35 Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.πŸ‘‡

1Petro 5: 1 Nawasihi wazee walio kwenu, ...; 2 lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari k**a Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo. 3 Wala si k**a wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi.

HITIMISHO; πŸ‘‡πŸ‘‡

NAKUHAKIKISHIA UKIFUATA hivi vipaumbele;

Watumishi/wachungaji wengi watakuona wewe ni muumini Bahiri. mioyo yao haitapendezwa nawe kabisa.

wao ubahiri wanapima k**a unawapa au huwapi, bila kujua majukumu gani mengine uliyonayo, hata k**a unawapa watu mitaani misaada mingi k**a kolnelio bado atakuona wewe ni bahiri as far as hutumagi hela kwake au hutoagi kwa namna anayotegemea yeye.

HASA AKIGUNDUA KUWA UNA KIPATO KIZURI, HAPO NDIO KABISAAA...
_______
Ibrahim Nzunda
0754210627

08/06/2025

Ikiwa Una-tatizo la kiroho, Addiction, Unataka kumpokea Yesu, au tatizo lolote la kuhitaji Maombi kwa jina la Yesu. Basi utapiga 0784811512 (NB: huduma ni Bure. K**a ilivyoandikwa "Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata BURE, toeni BURE" *Mathayo 10:8).

08/06/2025

Mafundisho ya roho za mpinga Kristo ni yale yanataka wakristo waishi kana kwamba Yesu bado hajaja.

Ndugu waimbaji,Huwa nasikitika sana kuona waimbaji wanakubali kuwa "Monetized" na promoters/event managers wa mwilini,  ...
31/10/2024

Ndugu waimbaji,

Huwa nasikitika sana kuona waimbaji wanakubali kuwa "Monetized" na promoters/event managers wa mwilini, Nasikitika zaidi kuona tena watu wa Mungu kabisa ambao sio fake wananasa huu mtego kirahisi sana.πŸ‘‡

Kusema "Ukumbi ni gharama ndiyo maana tunaweka viingilio" HAINA TOFAUTI na anayeuza mafuta ya upako kwa kusema ni gharama kuyapata. Ni roho moja ya udanganyifu.

Jambo hilo linawapotezea sana vibali mioyoni mwa watu ambao mnatakiwa kuwahudumia, na mbele za Mungu mnamuudhi.

Tunajua kuwa Mungu habembelezi ibada wala hawakii tamaa utukufu.

Je, katika jambo hilo Roho Mtakatifu mmezima kabisa hawezi kuwagusa kabisa?

Zaburi 50:21: β€œNami nikanyamaza; Ukadhani ya kuwa Mimi ni k**a wewe. Walakini nitakukemea; Nitayapanga hayo mbele ya macho yako.”

Kuna haja gani ya kukodi ukumbi k**a Mungu hajawapa neema ya kufanya hivyo? Msipokodi na kukaa majumbani mnapungukiwa na nini? Kwani nyimbo zenu Mungu hajazipeleka kwa waliokusudiwa?

Warumi 12:3- 6: β€œ... Namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, ... kwa kadiri ya neema mliyopewa; ...

Hapo mmekuwa na tofauti gani na Mfalme Sauli ambaye alidhani Mungu atashawishika na zile sadaka zake kuliko utii uliotakiwa?

Au hapo mmekuwa na tofauti gani na Balaam aliyedhani uwingi wa sadaka utamshawishi Mungu abadili katazo lake la kutowalaani Israeli?

Kwamba Mungu atashawishika sana kwenye hilo kusanyiko lenu hata k**a hamjajali kanuni ya kufanya mambo sawasawa na neema mliyopewa na sio sawasawa na kanuni za kimwili za namna ya kupata pesa za ukumbi?

Huu ni mtego mnaoingia kwa kuwa mnataka KUFANYA KITU AMBACHO MUNGU HAJAKUTUMA wala hajakupa neema ukifanye.
Hivyo, ITABIDI UTUMIE NJIA ZA MWILINI ZA KULIPISHA WATU K**A HIVI.

Kwani kuna hasara gani mwimbaji usipokuwa na makusanyiko ya ibada hata milele k**a tu Mungu hakupi hiyo nafasi? Kwanini ulazimishe mambo hadi ujikute unakuwa mwilini katika kupata hela za hii mikutano kwa njia za mwilini?

K**a Mungu hajawapa neema ya kuandaa kusanyiko la ibada kiasi cha watu kuingia bure, BASI MATOKEO YAKE NI KULETA MAMBO YA VIINGILIO kulipia ukumbi kwa kuwa mnalazimisha mambo na kutaka kufikia malengo ya kujitungia wenyewe wala sio ya Mungu.

Kwa hiyo, kinachofanya huo mkutano wa ibada uandaliwe sio kwa mapenzi ya Mungu. Kuna watu wamemdanganya mtumishi naye kanasa na amekuwa "monetized."

KUNIA MAKUU NDIO KUNAFANYA MTU ANASE KWENYE MTEGO WA KULIPISHA. K**A MUNGU HAJATAKA HIYO KITU KWANINI WEWE UIANDAE NA KUFANYA WATU WALIPIE?

Hii inamaanisha kuwa ni tukio la kulazimishwa, limeandaliwa kwa jinsi ya mwili.

TUNAJIINGIZA MITEGO YA KUTAKA KUMSAIDIA MUNGU.

"Walipofika kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Nakoni, Uza akanyoosha mkono na kulishika Sanduku la Mungu kwa sababu maksai walijikwaa [UZA ALITAKA KUMSAIDIA MUNGU SANDUKU LAKE LISIANGUKE]. Hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya Uza kwa sababu ya kitendo chake cha kukosa heshima, kwa hiyo Mungu akampiga, akafia papo hapo kando ya Sanduku la Mungu." (2 Samweli 6:6-7)

KITABU CHA UFUNUO  WA YESU: eschatology : Any concern uliza via comment au 0784811512 ) (NB humu sija-focus na tafsiri z...
19/10/2024

KITABU CHA UFUNUO WA YESU: eschatology : Any concern uliza via comment au 0784811512 ) (NB humu sija-focus na tafsiri za miaka au siku, Zingatia hilo kwanza).

1. Dunia ya sasa itaendelea hadi wakati wa DHIKI KUU, na dunia ya sasa itaendelea hadi mwisho wa miaka 1000 ya utawala wa Yesu.
Ili kutimiza ahadi ya Yesu ya kutawala katika kiti cha ufalme wa Daudi na kwa ajili ya ahadi ya Mungu kwa Isreal ya jinsi ya mwili).

Romans 11:26 Hivyo Israeli wote wataokoka; k**a ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

Luka 1: 32 Huyo [Yesu] atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.
33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

2. Mfalme atakayetengenezewa Sanamu yake na chapa yake, Wale wafalme wengine 10 pamoja na yule mfanya miujiza nabii wa uongo watafanya kazi katika timeline moja muda wa miezi 42,

Revelation 13:5 Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.

Ufunuo 17: 12 Na zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka k**a wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama.
13 Hawa wana shauri moja, nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao.

Revelation 19:20 ... yule nabii wa uongo... , yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake;

huu ndio wakati wa ile chapa na mateso makuu, ambayo yanafanyika mwishoni kabisa kabla Yesu hajasimamisha utawala wake wa miaka 1000

NB: Huu Muda wa miezi 42 ndio muda pia ambao kutakuwa na wale manabii wawili wa Mungu (mizeituni miwili), na mwisho wa hawa manabii wa Mungu ni kuuliwa na huyo mfalme hapo juu.

TUNAJUA NI NDANI YA MUDA HUO KWAKUWA HAWA WAWILI WALIUAWAWA NA HUYO MFALME MWENYE SANAMU NA CHAPA.

Ufunuo 11: 3 Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali wamevikwa magunia.
4 Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele za Bwana wa nchi.
5 Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa.
6 Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo.
7 Hata watakapoumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao, naye atawashinda na kuwaua.
8 Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu, uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wao aliposulibiwa.

3. Yesu mwenyewe ndiye atakomesha huo utawala wa chapa 666, NA HAO WAWILI YAANI MFAMLE NA NABII WAKE WAO UONGO WATAKUWA WA KWANZA KUTUPWA KWENYE ZIWA LA MOTO BILA KUFA KWA JINSI YA MWILI, WATATUPWA HAKIWA HAI K**A WALE WALIOJARIBU KUMPINGA MUSA WALIVYOZAMISHWA CHINI YA ARDHI WAKIWA HAI.

Ufunuo 19: 20 Yule mnyama akak**atwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa *wangali hai* katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;

mfano sawa na wale waliompinga Musa (Numbers 16:30 Lakini Bwana akiumba kitu kipya, na hiyo nchi ikifunua kinywa chake na kuwameza, pamoja na wote walio nao, *nao washukia shimoni wali hai;* ndipo mtatambua ya kwamba watu hawa wamemdharau Bwana)

21 na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.

KUMBUKA HAPO πŸ‘†YEYE SHETANI HAINGIZWI ZIWA LA MOTO BADO

4. UFUFUO WA KWANZA UNAFANYIKA NA KUANZA KWA UTAWALA WA MIAKA 1000

Ufunuo 20:6 Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.

NB: Utawala wa miaka 1000 utafanyika kwenye dunia hii hii ya sasa kabla ya uumbaji wa nchi mpya.

5. hiyo No 4 ndio inaambaatana na Kumfunga shetani shimoni kwa miaka 1000 kwanza, ili Yesu na watu wake walioshiriki ufufuo wa kwanza watawale dunia .

HIKI KIPENGELE NI CHA MUHIMU ILI KUTIMIZA UNABII ALIOPEWA DAUDI KUWA MZAO WAKE ATAKAA KWENYE KITI CHAKE CHA UFALME (UFALME WA DAUDI AMBAYE ALITAWAKA K**A MWANADAMU 100% AKIWA ANAONEKANA WAZI KWA WANDAMU NA SIO KWAMBA ALIKUWA ULIMWENGU MWINGINE. SO NAYE YESU ATAFANYA HIVYOHIVYO NA KUITAWALA DUNIA NZIMA, NA KUTIMIZA AHADI YA MUNGU KWA IBRAHIMU KUWA UZAO WAKE UTATAWALA DUNIA YOTE PHYSICALLY K**A AKINA DAUDI WALIVYOFANYA.

na kutimiza ahadi kwa Isreal juu ya kuja kwa Yesu k**a mfalme wao waliyetabiriwa. AHADII HII HADI LEO ISREAL WANAISUBIRI, kupata Mfamle atakayewaokoa na adui zao (mataifa mengine )

Luka 1: 70 K**a alivyosema tangu mwanzo Kwa kinywa cha manabii wake watakatifu;
71 Tuokolewe na adui zetu Na mikononi mwao wote wanaotuchukia;
72 Ili kuwatendea rehema baba zetu, Na kulikumbuka agano lake takatifu;
73 Uapo aliomwapia Ibrahimu, baba yetu,
74 Ya kwamba atatujalia sisi, Tuokoke mikononi mwa adui zetu, Na kumwabudu pasipo hofu,
75 Kwa utakatifu na kwa haki Mbele zake siku zetu zote.

Matendo 1: 6 Basi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?
7 Akawaambia, Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe.

πŸ‘† HIYO NDIO MITUME WALIDHANI INATAKIWA KUTIMIA BAADA TU YA YESU KUFUFUKUA. (WALIKUWA HAWAJUI KUWA KUNA NYAKATI ZINAITWA "NYAKATI/MAJIRA ZA MATAIFA" ambazo ziliingizwa katikati ya wiki 70 za unabii wa isreal/ Mungu alifanya temporary suspension ya hesabu ya wiki mpaka "MAJIRA YA MATAIFA" UTAKAPOTIMIA)

Nyakati za mataifa ndio hizi zilizopo sasa, ambazo zimeingizwa katikati ya majuma 70 ya Isreal, Baada nyakati za mataifa kuisha ndipo hesabu ya Majuma ya Isreal ita-resume.

Luka 21: 24 Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata *majira ya Mataifa* yatakapotimia.

Romans 11:25 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.

NA HUO MUDA WA MIAKA 1000 YA YESU DUNIANI K**A MFALME WA DUNIA NDIO WAKATI AMBAO ISAYA 65:20-25 ITATIMIA PIAπŸ‘‡

Isaya 65: 20 Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia[MAANA YAKE MAUTI ITAKUWEPO K**A KAWAIDA KWAKUWA ITAKUWA KWENYE HII DUNIA YA SASA]; bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa.[MAANA YAKE DHAMBI ITAKUWA IPO]
21 Nao watajenga nyumba, na kukaa ndani yake; watapanda mizabibu, na kula matunda yake.
22 Hawatajenga, akakaa mtu mwingine ndani yake; hawatapanda, akala mtu mwingine; maana k**a siku za mti ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu, na wateule wangu wataifurahia kazi ya mikono yao muda wa siku nyingi.
23 Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa kwa taabu; kwa sababu wao ni wazao wa hao waliobarikiwa na Bwana, na watoto wao pamoja nao.
24 Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.
25 Mbwa-mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, na simba atakula majani k**a ng'ombe; na mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote, asema Bwana.

6. baada ya huo Muda kuisha ndipo shetani atafunguliwa (ili tena wale UZAO WA ADAMU WA KWANZA waliozaliwa na kuishi nyakati za Yesu Nao wapate kujaribiwa, WANADAMU HAO WAKAJARIBU KUFANYA UASI, NA KUJARIBU KUUHARIBU ULE MJI ULIOSHUKA KUTOKA MINGUNI (MAKAO MAKUU YA UTAWALA WA YESU KWENYE DUNIA AMBAYO ITAKUWA BADO NI HII HII)

UFUNUO 20: 7 Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake;
8 naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni k**a mchanga wa bahari.
9 Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala.

7. THEN NDIPO SHETANI NAYE ANAUNGANISHWA KWENYE ZIWA LA MOTO, ANAKUWA NI KIUMBE WA TATU KIUNGIA HUMO

Ufunuo 20: 10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.

8. BAADA YA MAMBO HAYO NDIPO UFUFUO WA PILI UNATOKEA, KWA AJILI YA HUKUMU YA MILELE KWA KILA MWANADAMU NA KILA MALAIKA.

Daniel 12:2 Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.

UFUNUO 20: 11 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.
12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.
13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.

1kor 6: 3 Hamjui ya kuwa [watu wa Yesu] mtawahukumu malaika, ?

9. BAADA YA No 8 ndipo AHADI YA MBINGU MPYA NA NCHI MPYA ITATIMIZWA NA MAANDIKO HAYA KUTIMIA

EBRANIA 1: 10 ... Wewe,Bwana,hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi, Na mbingu ni kazi za mikono yako; 11 Hizo zitaharibika, bali wewe unadumu; Nazo zote zitachakaa k**a nguo, 12 Na k**a mavazi utazizinga, nazo zitabadilika;

2Peter 3:13 Lakini, k**a ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.

ufunuo 21:1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
____________
Ibrahim Nzunda
0784811512

Si halali kunena kwa lugha mbele ya halaiki bila kufasiri. Unaweza kufanya hivyo bila fasiri personaly kwenye maombi yak...
17/10/2024

Si halali kunena kwa lugha mbele ya halaiki bila kufasiri. Unaweza kufanya hivyo bila fasiri personaly kwenye maombi yako binafsi na sio ukiwa mbele ya watu unahubiri katikati ya mahubiri unanena kwa lugha bila kufasiri ili kusisitiza jambo lakini hutoi tafsiri.

HILI NI KOSA AMBALO WAKORINTHO WALIREKEBISHWA LAKINI inashangaza tunaendelea na kosa lilelile.

Asema "1kor 14:27 K**a mtu akinena kwa lugha[mbele ya wote wakasikia], wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri. 28 Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na [mnena kwa lugha] anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu[Iwe binafsi ambayo wengine hawasikii/sikilizi].

TAFADHARI: Paulo hakusema lugha ni fake, hakusema sio lugha halali kwa wao kunena nje ya utaratibu, wala hakusema ni mapepo, Paulo haku-demonize kunena kwa lugha tena hakukataza. Bali alionesha kunena ambako ni kwa mpangalio atakao Mungu.
____
Concern ya Roho Mtakatifu πŸ‘‡

1Kor 14: 23 Haya! Ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wanene kwa lugha, kisha ikawa wameingia watu wajinga au wasioamini, je! Hawatasema ya kwamba mna wazimu?

Sasa hatuwezi kujifanya sisi tuna hekima kuliko Roho Mtakatifu au kujifanya hatujali wengine kuliko Roho Mtakatifu na kujifanya tunajua mambo ya Roho kuliko Roho Mtakatifu.

Hitimisho;

UKIROHO(kusema unafanya mambo kwa Roho Mtakatifu) NJE YA HEKIMA YA MUNGU SIO UKIROHO (sio kuwa katika Roho Mtakatifu) NI UIMWILINI AU UTOTO, NI MATENDO YA MWILI.

1KOR 3: 1 Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi k**a na watu wenye tabia ya rohoni [TABIA YA KIUMBE KIPYA], bali k**a na watu wenye tabia ya mwilini, k**a na watoto wachanga katika Kristo.
____
Ibrahim Nzunda
0754210627

Shetani kabla ya Yesu kufa hana Nguvu k**a Baada ya Yesu kufa msalabani. USISAHAU HILO. Kosa ni kumfikiri shetani kwa ku...
03/10/2024

Shetani kabla ya Yesu kufa hana Nguvu k**a Baada ya Yesu kufa msalabani. USISAHAU HILO.

Kosa ni kumfikiri shetani kwa kudhania anazo nguvu zilezile kana kwamba Yesu hajafa msalabani bado.

Imeandikwa "ili [Yesu] kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa." (Ebrania 2:14-15)

Hapo tunaona kumbe kabla Yesu kufa Shetani alikuwa na hali/mamlaka/nguvu ambayo ni tofauti na baada ya Mauti ya Yesu.

Matokeo πŸ‘‡

Imeandikwa "vyote ni vyenu; 22 kwamba ni Paulo, au Apolo, au Kefa; au dunia, au uzima, au mauti; au vile vilivyopo sasa, au vile vitakavyokuwapo; vyote ni vyenu; 23 nanyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.

Zingatia neno "VYOTE NI VYENU"

Hivyo Shetani hawezi kukutishia silaha ambazo hana k**a vile mauti, Shetani hiyo siraha hana kwa sasa.

Wala hana mamlaka ya kuzuia chochote katika hii dunia mtu kukipata, Hivyo matokeo aliyonayo shetani kwasasa baada ya Kristo mengi ni kwasababu ya ujinga wetu wanadamu, (Exclude majaribu anayoruhusu Mungu).

MFANO: Nikikutishia kuwa nitakupiga kwa Bomu la Nyuklia nawe ikiwa hujui k**a sina hilo bomu basi utatishika sana na hata kukimbia kabisa na kujisalimisha uwe mtumwa wangu.

Ndicho afanyacho baba wa Uongo shetani, Hana siraha ila anatishia siraha ambazo hana kana kwamba anazo.

HITIMISHO

Asema " 1 Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu.
2 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. 3 Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. 4 Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu. (Wakolosai 3:1-4)
____________
Ibrahim Nzunda
0754210627

Mtu yeyote akishampokea Yesu anatakiwa mara moja kuacha mambo matatu ambayo ni lazima kuanzia siku ya kwanza bila vising...
29/09/2024

Mtu yeyote akishampokea Yesu anatakiwa mara moja kuacha mambo matatu ambayo ni lazima kuanzia siku ya kwanza bila visingizio au sababu za kutokuacha:

1. Uasherati.
2. Mambo ya ibada ya sanamu.
3. Kula damu na vitu vilivyonyongwa.

Hapa chini ZINGATIA NENO "hayo yaliyo lazima" NENO "LAZIMA" ni muhimu;

Asema "Kwa maana ilimpendeza Roho Mtakatifu na sisi, tusiwatwike mzigo ila hayo yaliyo lazima, yaani, mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongolewa, na uasherati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Wasalamu. (Matendo 15:11-29,)

Sasa kwa nini mambo haya matatu ni lazima Kuyaacha kuanzia siku ya kwanza? Kwa sababu kwa kila Mkristo, kuanzia siku ya kwanza, jambo lifuatalo Yesu nafanya ndani yake:

1. Anausulubisha mwili,
2. Mawazo yake na tamaa zake anazisulubisha
3. Anakutoa kwenye kifungo cha utumwa wa dhambi /anakupa uwezo wa wewe kutoitumikia dhambi wala tamaa za mwili

Asema 'Nao walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.' (Wagalatia 5:24)

HIYO NDIO NEEMA YA MUNGU ALIYONAYO KILA ALIYEMWAMINI YESU, KUMFANYA AWEZI KUUCHA HUO UBAYA.

MFANO: Mtu mlevi ukimwombea akaacha ulivei ghafla hiyo ni neema na sio kwakuwa amejiepusha kuacha, bali kaacha kwa neema. vivyo hivyo mkristo anayo neema juu ya kila aina ya ubaya.

Hii ya mwili wako kusulubiwa inatokea siku na sekunde ile unapompokea Yesu moyoni mwako.

Asema "mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena; (Warumi 6:6)

Hii ndio dawa ya kila "ADDICTION",

Na ikiwa Mkristo hawezi kuacha adiction yoyote ghafla iwe ni ulevi au uvutaji bangi au chochote kile ambacho ni "Addiction" ghafla au kwa maombi, basi ni lazima afundishwe 'jinsi ya kutembea kwa Roho na jinsi ya kuzima tamaa mbaya za mwili kwa Roho,' k**a ilivyoelezwa kwenye Warumi sura za 6 hadi 8.

'Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.' (Wagalatia 5:16,)

Kwa Mkristo wa kweli, uraibu ni lazima uachwe ghafla kulingana na kazi ya Kristo na Roho Mtakatifu ndani yetu. (Hekima ya Mungu ambayo pia ni Nguvu ya Mungu/neema ya Mungu).

'Kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, utakaso wenu: kwamba mjiepushe na uasherati; kwamba kila mmoja wenu ajifunze kumiliki mwili wake kwa utakaso na heshima, sio kwa tamaa mbaya k**a Mataifa wasiomjua Mungu.' (1 Wathesalonike 4:3-5, NKJV)

Hivyo, ni ushauri unaohitaji imani na uwezo wa kutembea kwa Roho.

Anasema 'k**a mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.' (Warumi 8:13)

HIVYO SASA UTAELEWA MAANA YA NENO HILI "Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema" (warumi 6:14)

Nadhani hatuna mafundisho ya kutosha juu ya 'jinsi ya kuendeka kwa Roho na jinsi ya kuzima tamaa mbaya za mwili kwa Roho wa Mungu ndani yetu.'"
___________

Ibrahim Nzunda
0754210627

28/09/2024

Watumishi tujiepushe na "Sensationalism"

21/09/2024

HUWEZI KUWA NA UZIMA WA MILELE K**A MAANDIKO KWAKO UNAONA NI HADITHI ZA KUSADIKIKA

2Timothy 3:15 na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.

Address

Morogoro
67126

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when KingPriest posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share