Ushauri Kuhusu Migogoro Ya Ndoa

Ushauri Kuhusu Migogoro Ya Ndoa OKOA NDOA YAKO SASA

24/11/2022

Mwanaume hakikisha unamdanganya mkeo Kwa lolote, sio kumcheet no. Wanawake wanaenjoy Sana tunavowadanganya hasa Kwa kuwaahidi vitu vzr au kuwapa maneno matamu. Hapo utamfanya akupende zaidi.

25/12/2018

Happy merry xmass and new year!! To all fans and liked this page.

25/12/2018

Merry chrismass and happy new year!! To all my fans of this page!!

MAZOEA KUPITA KIASI KWENYE MAHUSIANO NI HATARI SANA!!Kuzoeana baina ya wanandoa ni jambo zuri, kwa maana ya kila mmoja k...
03/06/2018

MAZOEA KUPITA KIASI KWENYE MAHUSIANO NI HATARI SANA!!

Kuzoeana baina ya wanandoa ni jambo zuri, kwa maana ya kila mmoja kumfahamu mwenzake, lakini kuzoeana huku kunaweza kuzalisha dharau hususani kwa upande wa mwanamke kwa kutojali usafi wake, mavazi anayovaa, chakula anchopika, nidhamu ya nyumba na mpangilio kwa ujumla.

Matatizo mengi ndani ya nyumba yanaweza kusababishwa na moja au baadhi ya tabia hizo, ambazo huenda ikawa hazitokani na dharau, bali kuzoeana, kwa mfano, siku za mwanzo wa ndoa mwanamke huwa anajali sana usafi wa mwili wake, umaridadi wa nguo anazovaa, usafi wa nyumba na nidhamu ya hali ya juu, upishi wa chakula unaozingatia vionjo na ubunifu, mapokezi yenye bashasha na wakati mwingine hata kumkumbatia mumewe arudipo kutoka kazini.

Lakini baada ya kuzoeana yote hayo hubadilika, mwanamke huhisi kuwa hana jipya la kumuonyesha mumewe, hujiona wameishakuwa watu wazima sasa, na mara nyingi utakuta mwanamke huyu anashinda na sare (uniform) moja kuanzia asubuhi hadi anapopanda kitandani usiku, mambo ya Hinna, nguo za fashion, salon, manukato, kujipamba na dhahabu huyafanya pale anapotoka kwenda harusini na sio nyumbani. Huku ndio kuzoena, na tafsiri sahihi ni kudharau.

Hivyo ili kulinda kibarua cha chako cha mahusiano ni vyema ukajifunza kila wakati kutofanya vitu ambavyo vimekuwa haviyajengi mahusiano yako.

Mahusiano yoyote yale huhitaji mtu mwenye uvumilivu, imara, mkweli na muwazi lakini hivi vyote vikishindikana basi, mahu...
03/06/2018

Mahusiano yoyote yale huhitaji mtu mwenye uvumilivu, imara, mkweli na muwazi lakini hivi vyote vikishindikana basi, mahusiano hayo huingia doa.

Watu kuwa na wapenzi wawili wawili huenda ikawa sijambo geni, lakini ni jambo geni pale mwezi wako akilifanya.

Matatizo haya yamekuwepo kwa miaka mingi, lakini sidhani k**a yatakuja kuzoeleka, maana kila mmoja hapa anahitaji upendo wa dhati na wakwake tuu, usio na kugawana na mtu mwingine.

Vitabu vya dini vinasisitiza upendo ulio mmoja katika mahusiano yaliyohalalishwa na Mwenyezi Mungu mwenyewe, 'tuliheshimu hili'.

Katika makala hii inayolenga kukuonyesha dalili za mwenzi wako kutoka nje ya mahusiano, kwa kiasi kikubwa itakusaidia wewe kuwa sehemu sahihi.

Dalili 6 zitakazokuonyesha kuwa mpenzi wako anamahusiano nje ya ndoa au urafiki wenu.

1. Mmekuwa wawazi kwa muda sasa, yani mwenzi wako amekuwa akishea na wewe mambo mbalimbali ya siku nzima, ghafla anaanza kuchelewa kurudi kutoka kazini, na akirudi hakuambii alikuwa wapi.

2. Umekuwa ukikaribishwa kumtembelea kazini kwake, lakini siku hizi anatengeneza sababu nyingi za kukuweka mbali na maeneo ya kazini kwake kabisaa.

3. Siku moja unapanda katika gari ya mkeo au mmeo alafu unataka kufungua kile kibox kilichopo pale mbele ambacho huwa kinatumika kuhifadhia vitu mbali mbali, mara unakuta kimefungwa kabisa na mwenzi wako anagoma kukifungua.

4. Ghafla mkeo/mme anaanza kujifungia bafuni anapokwenda kuoga, na hakuwa anafanya hivyo, je huenda akawa anatumia muda huo kuwasiliana na mtu mwingine kwa njia ya maandishi?

5. Mke/mme wako ana mikutano au mitoko na marafiki na kumbuka kukuhusu sehemu wanayokwenda inautata, mfano disco, bar usiku alafu hakuambii n.k.

6. Mpenzi wako anageuka kuwa msiri katika mambo yake, yani anakuficha nywila/passwod ya simu au laptop yake, tofauti na mwanzoni alikuwa anakuweka wazi.

Hayo na mengine mengi yanaweza kukufanya ukaona kuwa ni sehemu kubwa ya kuwa mumeo/mkeo anamahusiano na mtu mwingine nje ya mahusiano yenu.

Angalizo: Dalili zote hizo 6 huenda mpenzi wako akawanazo baadhi tu, kwa mfano kuchelewa kazini, usiri wa kazini n.k hii aimaanishi tu ni msaliti wa mapenzi, hapana wakati mwingine ziko sababu za msingi zinazo msababisha yeye kufanya hivyo na sio kuchepuka.

INAKUHUSU SOMA NA K**A HAIKUHUSU SHARE ITAMFIKIA INAYEMUHUSU!! inashangaza sana jinsi unavyothamini cha mtu kuliko chako...
23/05/2018

INAKUHUSU SOMA NA K**A HAIKUHUSU SHARE ITAMFIKIA INAYEMUHUSU!!

inashangaza sana jinsi unavyothamini cha mtu kuliko chako, yaani Mme/Mme ni wako, umemchagua wewe hukulazimishwa lkn bado unashindwa kumthamin hata kwa kitu kidogo k**a hichi?

Ivi kweli umekoswa picha nyingine ya kusave kwenye screen phone yako mpaka uweke pcha za wazungu au masuperstaa? Inamaana sura ya mkeo au mmeo haifai kuwepo kwenye kioo mpaka uweke ya hizo takataka?

Jiulize, hivi ungekuwa ni wewe ndo mwenzi wako kaweka picha ya njemba ungejisikiaje? Afu bila aibu wengine huanza kuzisifia hizo picha badara ya kusifia ya mwenzi wake. Kwangu huo ni wehu!
Hata mpenz wako anatamani uweke sura yake hapo kwenye screen yako japo hajakwambia. Naamini kupitia huu ujumbe umejifunza kitu. Hasa wanaume japo wanawake sio sana.
Jaribu kuweka picha yake kwenye simu yako kisha tengeneza nazingira ya yeye kuishika simu yako utaona utakavo furahia. Ni jambo dogo lkn ndoa zinapata migogoro pasi na sababu za msingi.
Weka basi walau picha yako au weka picha za kwenye wallpaper ya simu yako kuliko kumdhalilisha mwenzi wako mbele ya rafiki zako.

Asante kwa kuendelea kuufuatilia ukurasa wangu, like, share na post jumbe zangu kwa marafiki zako ili ujumbe ufike kwa wahusika. Hii picha hapo chini ni mfano wa muonekano wa screen za wahusika!!

MKASA WA KUSISIMUA: HAKIKA NILIKOSEA SANA KUKUAMINI, UMEHARIBU MAISHA YANGU   sana Hii ni barua ya Fausta kwa aliyekua m...
18/12/2017

MKASA WA KUSISIMUA: HAKIKA NILIKOSEA SANA KUKUAMINI, UMEHARIBU MAISHA YANGU

sana Hii ni barua ya Fausta kwa aliyekua mumewe......

" My X Husband,

Nilikuwa binti mdogo ambae nilikuwa nikisoma chuo kikuu nikiwa na mipango mingi ya kimafanikio na malengo mengi baadae. Ndipo ulipokuja katika maisha yangu.

Nilikutana na wewe na nikakupenda, ulionekana ni mtu ambae mwenye mapenzi ya kweli, mtu unae jali na ambae hutaniacha nidondoshe chozi hata siku moja. Pamoja na hayo yote ulionekana pia u mcheshi ambae usingeacha tabasamu lipotee usoni mwangu. Hakika ulikua Mwanaume kila mwanamke angependa kuolewa nae!

Tulifungua ukurusa wetu wa uchumba, nilikupenda sana na na nadhani unalijua hilo mpaka kesho, ulinisisitizia sana suala la kufunga ndoa mapema kwani ulikua ukiniambia kuwa una wivu, kwamba wanaume wengine wanaweza wakakupiga counter attack na kunioa kisha nikuache wewe kwenye mataa.

Mimi nilisita sana hilo suala, nilikusisitizia kuwa uniache mpaka nimalize masomo yangu ya chuo kikuu kwani ilikuwa imebaki miaka miwili tu, vilevile nilikueleza kuwa wazazi wangu wasingekubaliana kabisa na hilo wazo lako! Lakini wewe hukunisikia! Ulibaki na msimamo wako wa kutaka kufunga ndoa na mimi, kwamba ningeendelea na chuo baada ya ndoa.

Mwanamke gani ambae angekuwa tayari kukupoteza wewe? Bila kufikiri nilikubali unioe na niliwaeleza wazazi wangu hilo suala. Nakumbuka wazazi wangu walikuja juu sana, hawakutaka kunielewa kabisa!! Waliniuliza mara kumi kumi huyo mtu umemchunguza kweli? Mimi niliwahakikishia asilimia mia moja kuwa wewe u mwanaume unaepaswa kunioa!

Nilikuwekea dhamana ya uaminifu kwa wazazi wangu, na kwa vile mimi ndiye nilikuwa mtoto wao wa kwanza na wa k**e pekee walinisikiliza na kutaka niwe makini nikuchunguze vizuri. Hilo halikunipa wasiwasi! Nilishakupenda na niliona wewe ndio mtu sahihi wa kuanzisha familia pamoja. Nilikupenda na sikuona tatizo lolote.

Vikao vilifanyika pande zote bila tatizo lolote, ulinioa mume wangu tena kwa sherehe ya harusi kubwa pale mjini, ilihudhuriwa na watu wengi sana ambapo mimi sikufikiri k**a ingalikuwa vile. Tuliingia rasmi katika maisha ya ndoa!

Maisha ya ndoa yalinoga, mimi malkia ulikuwa ukiniambia kuwa unanijali sana na kweli ulinijali, kwamba maisha yako bila mimi si kitu...kweli ulinipenda, unaweza usikumbuke maneno matamu uliyokuwa ukiniambia lakin yote mimi nayakumbuka na bado yapo kifuani pangu! Niliacha marafiki zangu, familia yangu, mkoa wangu, nikabadilisha hadi jina langu na kutumia lako hii yote kwa ajili yako tu!

Taratibu ukaanza kubadilika, ukaanza kuniambia kwamba siwezi kuendelea kusoma, nililalamika sana na bila kugundua kuwa ulikuwa ukivunja ahadi yako. Ulinilazimisha niache chuo, pasina kujua kufanya vile ni kukosa kabisa mkopo wa elimu ya juu huko mbeleni, sijui ulikuwa na roho gani mbaya ilikuingia! Ukaanza kuwa na hasira na mimi! Hukuisha kunitukana na kunikebehi kila uliporudi toka kazini! Ulininyanyasa pasina kuwa na huruma kuwa nilikua nimebeba kiumbe chako tumboni mwangu.

Nilikuwa mpole, muda mwingine kosa ulikua ukifanya wewe ili kuepuka shari nikawa nikiomba samahani mimi. Mume wangu ulibadilka! Ukawa unarudi nyumbani usiku sana huku umelewa! Ulitukana matusi yote nayoyajua hapa duniani. Ukaenda mbali zaidi na kuanza kutembea na wanawake hovyo hovyo! Najiuliza mpaka leo! Ni kwamba sikukuchunguza vizuri au ni wewe tu ulichukulia ndoa k**a mchezo wa kuigiza.

Tena nakumbuka mimba ilipofikisha miezi nane uliniambia hunipendi kabisa, kwamba hukutaka kunioa mimi, kwamba nilikuwa manamke kwanza mbaya, mpumbavu na mzigo kwako hayo yalikuwa maneno yako. Na kwamba unampenda mwanamke mwingine. Nilijihisi kusalitiwa sana sio siri uliniumiza sana ila sikufikiria kukuacha! Nilijipa matumaini tu kuwa utakuja kubadilika na kurudi k**a zamani.

Lakini haikuwa hivyo mpaka pale ilipofika wakati niliposhikwa na uchungu nikiwa peke yangu nyumbani wewe ukiwa baa unakunywa pombe! Nilikupigia simu uje unichukue na gari yako kwamba ninakaribia kujifungua unipeleke hospitali lakini ulinijibu kwamba niache usumbufu upo unakunywa na warembo! Ulikuwa na roho gani mume wangu???

Majirani zangu ndio walikuja kunichukua baada ya kusikia kelele za kuomba msaada, walinipeleka hospitali na nikajifungua kwa operation mtoto wa k**e! Nilishukuru Mungu kwa zawadi ya mtoto, ila nilisikitika kwa zawadi nyingine ambayo ulinipa! Zawadi ya ugonjwa wa UKIMWI! Inaniuma mume wangu! Umeharibu malengo yangu!

Uliniachisha chuo, ambako nilikua ninaenda vizuri na masomo yangu ya udaktari, ulinitenganisha na rafiki zangu, ndugu zangu na familia yangu! Alimradi niwe na wewe tu.

Haikutosha umenizawadia na gonjwa la UKIMWI! nasema asante sana mume wangu, nina maumivu mno! Kwanini usingeniacha niendelee na masomo yangu kisha ndio unioe!? Kwanini ulikuja katika maisha yangu? Wewe tu ndiye uliyeharibu mipango yote ya maisha yangu. Asante sana Mume wangu.

Bado nipo katika kipindi kizito cha kutibu hii shock uliyonipa na sijui k**a nitafanikiwa kurudi katika maisha yangu ya kawaida. Bora ungenichoma kisu nife kabisa kuliko haya maumivu uliyoniachia!

Lakini napenda tu nikuulize kwanini umeharibu maisha yangu? Siku zote za furaha tulizokua pamoja hazikumaanisha chochote kwako? Je taasisi ya ndoa ni k**a utani kwako?

Najua maisha yako hayatabadilikia, bado u kijana mtamashati, handsome na mwenye pesa, lakini mimi na familia yangu ndio tunahangaika sana mimi ndio nlikua tegemeo lao kubwa sana. Sitakuja kuelewa kwanin ulinioa. Sina hasira na wewe ila nimeumia sana kwa kuharibu maisha yangu na ya familia yangu kiujumla. Nimeumia pasina kufananisha na maumivu yoyote yale.

Usijali kuhusu binti yangu mimi nitamtunza! She is my daughter!

Wasaalamu,

X-wife wako! FAUSTA"
****************
.

UJUMBE WA FAUSTA KWA MABINTI NA WANAWAKE KWA UJUMLA

1. Ombeni sana Mungu awaepushie wanaume washenzi k**a huyu
2. Kuweni makini msiwe wepesi kutekeleza maagizo ya wachumba au waume zenu pasipo kutafakari madhara yake mbeleni
3. Mume anayekusaliti na kukutesa bora kuwahi kuachana nae kabla hajakuletea magonjwa
4. Sikilizeni ushauri wa wazazi na wazee kwan mara nyingi wao huwa na uzoefu zaidi kuhusu ndoa na maisha kwa ujumla

Tafadhali usipite bila kumpa neno la POLE FAUSTA kisha SHARE

Ni matumaini yangu kwamba umejifunza kitu kupitia mkasa huu,

Nakutakia siku Njema, Mungu Akubariki na kukulinda

Jamani mmenitengaa mbona sioni comments zenu
Embu tuambiane wap kuna mapungufu maana bila nyinyi mm siwezi Fanya kitu humu
Embu like na comment bext wangu

K**a umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata k**a mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwen...
26/11/2017

K**a umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata k**a mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka.

Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida – mazoea huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.

Itafikia hatua, k**a upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na k**a ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba hamuendani humwingia.

UNAFANYAJE SASA?
Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha thamani.

Tayari tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.

ANZIA MWANZO
Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo chini.

CHUNGA KAULI ZAKO
Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli zake.

Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana k**a unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe makini zaidi mnapokuwa na watu wengine. K**a mwanamke usiwe mchangiaji hoja sana.

Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako k**a mwanamke anayejitambua.

USIRUHUSU MAPENZI
Msichana mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.

Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa asilimia kubwa.

Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo yoyote – binafsi au yanayosababishwa na uhusiano wenu, anakuwa hana uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo hilo. Utabaki wewe na matatizo yako!

HEBU TUMIA DK 5TU KUSOMA HII SMS NIMEYAPENDA SANA HAYA MANENOMwanamke ni k**a Jua unawezausione umuhimu wake, yaani kila...
18/11/2017

HEBU TUMIA DK 5TU KUSOMA HII SMS NIMEYAPENDA SANA HAYA MANENO
Mwanamke ni k**a Jua unaweza
usione umuhimu wake, yaani kila
siku unaenda mjini jua lipo tu,
unaliangalia lakini huangalii umuhimu
wake kwako. Wakati mwingine likiwa
kali unaanza kulalamika kuwa
linachoma na lina kera. Lakini
ukitafakari kidogo tu utajua kuwa bila
jua maisha yasingekuwepo. Hembu
chukulia mfano mchana kungekuwa
giza tu k**a usiku nini kingetokea?
Chakula tunachokula ni kwasababu
ya Jua, mvua ikinyesha sana
mafuriko yakitokea tunatamani jua,
kwenye baridi tunatamani pia jua,
Hatuliwazii kwasababu lipo tu na
linatimiza majukumu yake kimya
kimya bila kelele. Hiyo ni sawa na
mwanamke, ukishaoa kuna mambo
ambayo mwanamke huyafanya na
baada ya muda unaanza kuyaona ya
kawaida kawaida, chakula kinakuwa
mezani kila siku hujui kinapikwaje na
vyombo vinaoshwaje, anabeba
mimba na watoto wanazaliwa hujui
maumivu aliyoyapata lakini
unatabasmu na kucheka ukijisifia
watoto wangu na hata mkigombana
unasema niachie wanangu wewe
nenda tu tafikili unajua maumivu
aloyapata kipindi anawaleta duniani
ao watoto. Watoto wanaumwa mpaka
wanapona hujui hata wameponaje,
wanalia usiku hujui hata nani alikuwa
anawabembeleza, ukirudi unakuta
nguo safi chumba kisafi hutoi hata
shukurani kwakuwa ushasahau kua
kuna mtu anasafisha siwe safi muda
wote.Na anafanya vitu vyote hivyo
k**a Jua bila kelele lakini wewe
ukitoa elfu mbili ya sukari
utamnynayasia mpaka ndugu zake
kuwa unawalisha wewe! Hembu siku
aondoke akuachie hao watoto
unaojisifia kila siku kuwa ni wakwako
na kumuambia hajaja na kitu, uanze
kuwapikia na kuwaandaa kwenda
shule, ufue nguo zao na zako.
Unaweza kuajiri mfanyakazi lakini
hawezi kufanya hata nusu ya kile
anachokufanyia mkeo, kwani yeye
atafanya k**a kazi lakini mkeo
anafanya kwa mapenzi, hahitaji
umlipe chochote zaidi ya kutimiza
majukumu yako na kumheshimu
k**a mke katika maisha yenu. Vuta
picha umeamka mkeo hayupo, watoto
wanataka kuogeshwa kunywa chai na
kwenda shule, hapo unatakiwa
kuwahi kazini na mchana watoto
wale! Mheshimu sana mkeo kuna
mambo mengi ambayo anayafanya
ukiambiwa uyafanye ww
utachanganyikiwa na mkeo huyafanya
kwa upendo. Mwanamke anachohitaji
kwa mume ni upendo na heshima tu.
Mhudumie, mpe upendo, muheshimu
na muonyeshe kuwa kwako ana
umuhimu mkubwa, mfanye mkeo
atabasamu kila mara na familia nzima
itatabasamu
nakutakia siku njema na mafanikio mema...

SIPENDI NAMNA UNAVYOONGEA NA MIMI..."Una matatzo gani wewe? Sikukwambia mimi ufue shati langu la blue? Yaani kila siku w...
27/10/2017

SIPENDI NAMNA UNAVYOONGEA NA MIMI...

"Una matatzo gani wewe? Sikukwambia mimi ufue shati langu la blue? Yaani kila siku wewe ni kusahau tu" akamkoromea mkewe.

Mke akatazama pembeni.

"Samahani, nilisahau kabisa k**a kuna shati la kufua". Mke akaongea huku akimpa mumewe tai nyekundu.

Mume akapokea kwa kuikwapua huku akionekana dhahiri kukasirika.

"Sipendi namna unavyoongea na mimi" mke akamwambia mumewe.

"Unamaamisha nini? Zungumza ueleweke wewe mwanamke. Sina muda hapa, nachelewa ofisini kwangu". Mume akafoka.

Mke akakaa kitandani na kusema, "nenda tu kazini mume wangu".

Mume akashusha pumzi na kukaa kitandani karibu na mkewe.

"Nini kinakusumbua mke wangu?" Mume akamuuliza kwa upole kidogo.

"Hivi mim ni mke wako kweli?" Mke akauliza.

"Unawezaje kuniuliza hivyo? Umeanza lini upumbavu?" Mume akafoka tena.

Mke akamtazama tu mumewe huku akiwa kimya.

"Hiyo ndio sababu. Hebu angalia namna unavyoongea na mimi" mke akaongea zaidi.

"Kimsingi hauongei na mimi bali unaniamrisha. Unanikaripia, unanipa oda utafikiri meja wa jeshi kwa kuruta. Tokea lini wewe umekua bosi wangu? Wewe ni mume wangu na wala sio mkuu wangu...
..Nakusikia ukiyatumia maneno k**a vile 'samahani', 'tafadhali' na 'pole' kwa wafanyakazi wenzako; lakini kwangu sikumbuki ni lini uliyatamka hayo maneno. Je kuwa mke wako ndio inamaanisha mimi ni mtumwa na nastahili kuhudumiwa hovyo hovyo na mume wangu?"

Mke akatazama chini na kuendelea..

"Unaniabisha mbele za watoto na majirani, unaninyanyasa na kunipa amri utafikiri mtoto wa sekondari. Mimi ni mwanamke wako, mke wako, nijali basi k**a msaidizi wako. Ona hua huniangalii hata machoni unapoongea na mimi. Je natia kinyaa hata sistahili kuangaliwa usoni?
..Unao muda na marafiki zako kila siku lakini kwangu huna muda, muda ulio nao kwangu ni pale unapotaka tendo la ndoa tu..na hapo ukimaliza hujali k**a mimi nimeridhika ama laa unageuka upande wa pili..hakuna maongezi, hakuna mapenzi..najichukia kwa kweli!

Mke akamtazama vizuri mumewe...Na kuendelea..

"Unapotaka kunipa kitu hunipi mkononi, unanitupia k**a mbwa. Ukiangusha kitu mimi ndio wa kukiokota huku wewe ukiwa umekaa umeweka miguu juu ya meza...
..Tukiwa tunaenda mahala hautaki kutembea karibu na mimi, natembea nyuma yako, je sina thamani ya kutembea na wewe? Umejaza rekodi na kumbukumbu ya mapungufu yangu na kila siku unayakumbushia, kwaio mimi sina zuri hata moja?
..Yuko wapi mwanaume aliekua ananijali, ananisikiliza na kunipenda? Je amefariki baada tu ya kuingia kwenye ndoa? Bado nahitaji huduma yako nzuri mume wangu, haswa wakati huu tukiwa na watoto. Onesha kunihitaji nami nitakupa mambo matamu tutakayoyafurahia sote kwa pamoja hata kwenye tendo la ndoa.
..Niite majina matamu k**a zamani, usiniite 'mwanamke' sijali sana kuhusu kukuhudumia ila nahitaji heshima. Nahitaji unifanye nijisikie ni mpenzi wako. Nikubali, kuwa mpole kwangu, ukali wako unaniogopesha kuliko hata nilivyokua namuogopa baba yangu. Mimi sio housegirl. Ni mke wako ndani ya nyumba hii.

Mke akashusha pumzi na akamtazama mumewe baada ya kuongea yote ya moyoni mwake...mume hakuongea kitu.

Mume akachukua simu yake na kupiga baadhi ya namba.

Pamoja na kumueleza yote hayo lakini bado amempotezea na kuchukua simu yake..Mke akajisikia vibaya sana.

Mke akasimama ili aondoke huku machozi yakimtoka, lakini mume akamshika mkono na kumrudisha kitandani huku akisikiliza simu aliyopiga.

Mume akaanza kuongea, "Hallo, tafadhali ahirisha kikao tufanye kesho, nimepata dharuka kidogo. Kuna jambo la kifamilia nashughurika nalo". Akakata simu.

Mume akamuona mkewe akitabasamu. Akamkumbatia mkewe na kumbusu mdomoni.

"Nisamehe mpenzi wangu, sikua nafahamu k**a nakuumiza. Je nikupe offer ya kukutoa lunch leo? Kuanzia leo na kuendelea, nitakuhudumia vizuri k**a vile unavyotamani. Mumeo nimerudi sasa !!!

Mwanamke jifunze kuongea kwa upole endapo kuna jambo haulifurahii na linakuumiza juu ya mwenzako, ni nadra sana kwa mwanaume kuwa mgumu kwa mwanamke anaenyenyekea.

03/10/2017

Hakuna binadamu asiyefahamu nini maana ya mapenzi na k**a wapo basi ni wachache sana na wanaweza kuwa hawafahamu kwa maneno lakini kivitendo wanakuwa wanafahamu aidha kwa kuona, kusikia na hata kwa wao wenyewe kushiriki kwenye mapenzi hayo.

Na hakuna binadamu yeyote asiyependa kupenda au kupendwa, wote tunapenda kupenda na pia tunapenda kupendwa in . Na siku zote ukipenda na usipopendwa pale unapopenda huwa inakuwa ni huzuni sana na wengine hufikia hatua mbaya sana za kufikiria mengine mengi tu ya hatari pale mapenzi yanapokuwa machungu kwao.

Hii ndio sababu wengi wetu huwa tunakaa pale tunapoona kweli kuna mapenzi na si kukaa pale ambapo unaona unadanganywa au kuzungushwa kila siku. Lakini kuna wakati tunaweza kujikuta hata pale tunapopenda na kupendwa pia panaharibika baada ya muda na kunakuwa na ugomvi na kukosa maelewano baina yenu na wakati mwingine usifahamu kwa nini hamuelewani au ukaelewa lakini ukakosa njia za kutatua.

Zifuatazo ni baadhi tu ya njia mbalimbali za kufanya ukae na mpenzi wako kwa muda mrefu kwenye mahusiano na mkafurahia mapenzi yenu popote pale mtakapokuwa na mtakapoishi.

1. Kuwa na muonekano chanya kwa mpenzi wako.
Ukiwa ni mtu wa kuangalia mabaya/kasoro sana kwa mpenzi wako kuliko mazuri yake hautakuja kukaa kwenye mahusiano kwa muda mrefu hata siku moja, utaendelea kubadilisha Wmwanaume / Wanawake kila siku na mwisho wa siku utajiona huna bahati kwenye mapenzi na wakati Unayeyaharibu mapenzi yako ni wewe Mwenyewe...kakuna asiye na kasoro (Ukiwemo Wewe Mwenyewe).

Kwa hiyo muonyeshe mpenzi wako mapenzi bora na umrekebishe pale anapokosea Bila Kuwa Na Lawama Mara Kwa Mara, Kuna Makosa Mengine Ni Hakuna binadamu asiyefahamu nini maana ya mapenzi na k**a wapo basi ni wachache sana na wanaweza kuwa hawafahamu kwa maneno lakini kivitendo wanakuwa wanafahamu aidha kwa kuona, kusikia na hata kwa wao wenyewe kushiriki kwenye mapenzi hayo.

Na hakuna binadamu yeyote asiyependa kupenda au kupendwa, wote tunapenda kupenda na pia tunapenda kupendwa in return. Na siku zote ukipenda na usipopendwa pale unapopenda huwa inakuwa ni huzuni sana na wengine hufikia hatua mbaya sana za kufikiria mengine mengi tu ya hatari pale mapenzi yanapokuwa machungu kwao.

Hii ndio sababu wengi wetu huwa tunakaa pale tunapoona kweli kuna mapenzi na si kukaa pale ambapo unaona unadanganywa au kuzungushwa kila siku. Lakini kuna wakati tunaweza kujikuta hata pale tunapopenda na kupendwa pia panaharibika baada ya muda na kunakuwa na ugomvi na kukosa maelewano baina yenu na wakati mwingine usifahamu kwa nini hamuelewani au ukaelewa lakini ukakosa njia za kutatua.

Zifuatazo ni baadhi tu ya njia mbalimbali za kufanya ukae na mpenzi wako kwa muda mrefu kwenye mahusiano na mkafurahia mapenzi yenu popote pale mtakapokuwa na mtakapoishi.

1. Samehe na kusahau.
Unapomsamehe mpenzi wako kwa kosa lolote alilokosa basi hakikisha umemsamehe kiukweli na ujitahidi kusahau kosa alilotenda itasaidia uwe na amani ya moyo zaidi kuliko kumsamehe kwa usoni tu lakini moyoni ukawa na Donge bado, hii hupelekea kupunguza mapenzi kwa kiasi Fulani kwake na kujikosesha furaha ya mapenzi.Anapokosea siku nyingine usimkumbushe kosa lake la nyuma kwa sababu itamfanya ajione mwenye huzuni na ajione kuwa hakusamehewa.

2. Mpe nafasi na uhuru mpenzi wako.
Mnapokuwa kwenye mahusiano jitahidini kwa hali na mali kupeana nafasi/uhuru kwenye mambo mengi hasa yale ya kitaaluma zaidi na kimaisha.anapokwambia yupo kwenye kikao cha kikazi jaribu kumuelewa na umpe support ya kutosha kwenye kazi zake au biashara zake au hata masomo yake.
usipende sana kulalamika pale anapochelewa kurudi kazini au kutoka kwenye biashara zake bali mpokee kwa upole na baada ya kupumzika ndipo muulize kwa upole na kimahaba zaidi kwanini siku hizi anachelewa sana kurudi au kwenye biashara zake au shuleni tofauti na zamani.

Hii itajenga zaidi kuliko kubomoa kwa kulalamika na kupayuka mbele yake na huku yeye akiwa hata hajapumzika na itamfanya siku nyingine aione nyumba chungu kitu ambacho si kizuri kwenu wote wawili.

3. Mfanye mwenza wako ajivunie kuwa nawe kila wakati.
Hakikisha katika mapenzi yenu kila siku unamfanya mpenzi wako ajivunie kuwa nawe na hakikisha humfanyi ajute kwa kukuchagua wewe miongoni mwa wote aliowaona. Usijidanganye hata siku moja kuwa kwa kumpata tu na kwa yeye kukupenda basi hajaona mwingine wa kuweza kuwa naye.

Wapo wengi sana anaoweza kuwa nao lakini amekuchagua wewe katika hao wote, kwa hiyo usimfanye aanze kuwafikiria wale wengine wanaomfuatilia kila siku na kumsumbua.Ukianza kumwacha aanze kuwafikiria wengine aidha kwa wewe kuwa unamkosesha amani ya mapenzi kila mara au kwa mengine mabaya ndani ya mapenzi basi ipo siku utaishia pabaya.

4. Msadie kwa khali na mali kila inapowezekana.
Kwenye mahusiano huwa kuna kupanda na kushuka miongoni mwa wapenzi na hasa kiuchumi na hata kisaikolojia. Hakuna kitu kizuri kwenye mapenzi k**a mtu kupata tatizo na akasaidiwa na mpenzi wake katika hali ambayo hakuitegemea, namaanisha mpenzi wako akipata tatizo lolote hakikisha wewe ndo unakuwa wa kwanza kulifahamu na kulifanyia kazi.

Sio matatizo yote yanamalizwa kwa pesa so hata ushauri na kumpa mawazo chanya inasaidia sana na kumfanya awe na furaha kuwa nawe.K**a unampenda usione tabu kumsaidia kwa kuogopa kuonekana eti unahonga, huyo ni mpenzi wako kwa hiyo jiamini na umpe kile anachostahili kusaidiwa na mpenzi wake.

Yapo mambo mengi sana ambayo k**a mkiyafanya kwenye mapenzi basi uhusiano wenu utakuwa wa kudumu na wenye furaha sana ingawa hapa nimezungumzia kwa uchache sana lakini nina imani itasaidia sana kwa wote walio kwenye mahusiano.

Mapenzi hayana ndumba au limbwata hata siku moja, unapoona wapenzi wengi wana furaha kwenye mapenzi yao ni kwa sababu wanavumiliana kwa mengi na kusameheana kwa mengi.

Sana Na Unaweza Kuyarekebisha Kwa Kukaa Chini Na Mpenzi Wako Mkayamaliza Kwa Dakika 5 Tu Lakini Wengine Huwa Issue Kubwa Kwao Na Kusababisha Mwisho Mbaya. Kanuni sita (6) za kudumu katika mahusiano ya kimapenzi.

Itunze Ndoa YakoMKE, FANYA HAYA KWA MUME WAKO.1. Muite kwa jina lake la utani2. Muache atumie mamlaka yake k**a kichwa c...
26/07/2017

Itunze Ndoa Yako

MKE, FANYA HAYA KWA MUME WAKO.

1. Muite kwa jina lake la utani

2. Muache atumie mamlaka yake k**a kichwa cha nyumba.

3. Usimcheke akiwa ameumizwa na jambo fulani.

4. Kaa kimya pale anapokuwa na hasira. Unaweza ukaenda kumuomba msamaha na kumueleza kwanini ulimkosea pale hasira zinapokua zimemuisha.

5. Kuwa na haraka ya kuomba msamaha pale unapokosea, sisitiza juu ya msamaha na mbusu pale anapokusamehe.

6. Ongelea mazuri yake na yeye kabla ndugu, jamaa na marafiki hawajafanya hivyo.

7. Waheshimu wazazi wake.

8. Msisitize kuhusu kwenda kuwasalimia wazazi wake na kuwapelekea chochote. Na afanye hvyo na kwa wazazi wako pia.

9. Msuprise kwa chakula akipendacho, hasa kipindi kile anapokuwa na msongo wa mawazo. Na kamwe usimcheleweshee chakula chake.

10. Usiruhusu dada wa kazi amhudumie chakula mume wako ukiwa nyumbani.

11. Mkaribishe kwa kumkumbatia anapotoka kwenye mihangaiko yake. Msaidie mizigo aliyokuja nayo au hata begi.

12. Tabasamu pale unapomtizama, vaa vizuri na jipendezeshe pale mnapotoka wote kwenda kwenye warsha mbalimbali.

13. Mpigie simu na umwambie kwamba unampenda na umemkumbuka

14. Muamshe asubuhi na umpe romance kiasi kwamba ifike hatua ya kuhitaji, mpe na hata jishughulisha na wanawake wengine siku hiyo.

15. Kamwe usithubutu kutamka kuwa hakuridhishi na tendo la ndoa. Tafuta njia muafaka ya kufikisha ujumbe wako.

16. Mwambie ni kiasi gani una bahati kuwa nae k**a mume wako.

17. Mkumbatie tu bila sababu yoyote ile.

18. Mshukuru Mungu kwa kukupa Adamu wako katika maisha yako.

19. Kumbuka kumuombea na kumkabidhi mikononi mwa Mungu.

20. Tengenezeni utaratibu wa familia nzima kumshukuru Mungu kwa pamoja kila asubuhi na usiku kabla ya kulala.

Mungu abariki ndoa yako. Mlio single Mkapate wapenzi wenye mapenzi ya kweli leo na daima.

Na wasio serious na mahusiano wanaokupotezea muda wako wajikatae kwako mapema ili wasikuzibie nafasi ya kutimiza kusudi la Mungu kwako.

Kwanini tusiseme "Amen"!

Share

Address

Mlowo Songwe
Mlowo
01002

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ushauri Kuhusu Migogoro Ya Ndoa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Ushauri Kuhusu Migogoro Ya Ndoa:

Shortcuts

Share

Category