tzcuom

tzcuom

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from tzcuom, College & University, Mbeya.

08/03/2025

Happy Women's day!

28/11/2024

Catholic University Of Mbeya (CUoM) in collaboration with Stetson University, College of Law (From Florida, USA), invites you to the International Environmental Moot Court Competition on 'Subsistence Use and Trophy Hunting.' This prestigious event will take place at the Catholic University of Mbeya from November 28th to 29th, 2024, at the CUOM Conference Hall from 09:00Hrs. Don’t miss out!

Photos from tzcuom's post 08/11/2024

Wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Madibira iliyopo Wilaya ya Mbarali, Mkoani Mbeya leo wametembelea Chuoni CUoM wakiongozwa na Afisa Masoko CUoM Bw. Filbert Athanas.
Wanafunzi hao wamefika Chuoni ili kupata ufafanuzi kuhusu kozi zitolewazo Chuoni kwetu, Kupata taarifa zaidi kuhusu Chuo chetu na pia kujionea mandhari ya chuo na miundombinu iliyopo Chuoni inayotumika katika ufundishaji.

Photos from tzcuom's post 02/11/2024

Katika kuhitimisha Semina Elekezi kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza, Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Romuald haule leo amazungumza na wanafunzi wa Mwaka wa kwanza wa Shahada na Stashahada ya Juu ya Elimu.
Prof. haule amewapongeza wanafunzi wote waliochaguliwa CUoM kwa mwaka wa masomo 2024/2025 na pia kuwakumbusha mambo muhimu mbalimbali ya kuzingatia kwa kipindi chote wawapo chuoni ikiwepo kuzingatia maadili ya kitanzania, kusoma kwa bidii na kuhudhuria darasani vipindi vyote, ulinzi na usalama binafsi pamoja na kufuata sheria za chuo.
Pia amewasisitiza kuwa na matumizi mazuri ya pesa za kujikimu (Boom) kwa kila mmoja kujiwekea bajeti nzuri.

Photos from tzcuom's post 30/10/2024

Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Shahada na Stashahada ya juu ya Elimu, wakiwa katika Semina Elekezi (Orientation) iliyotolewa leo katika kumbi za Mihadhara (RD I & RD II) hapa Chuoni. Mafunzo haya yana lengo la kuwawezesha wanafunzi kufahamu vyema mazingira ya chuo, Kuwapa wanafunzi uelewa na maarifa ya maisha ya chuo, Kufahamiana na Kushirikiana kijamii & Kitaaluma.

Aidha wanafunzi wapya wametakiwa wawe watiifu na kufuata sheria zote za chuo na wahakikishe usalama wao kwa kipindi chote wawapo chuoni.

Photos from tzcuom's post 30/10/2024

Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Romuald Haule akizungumza na Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Astashahada na Stashahada katika ukumbi wa Mihadhara,
Fr. Roland Dubourt (M.A). Akizungumza na wanafunzi hao Prof. Haule amewapongeza wanafunzi hao kwa kufanikiwa kujiunga na Chuo Kikuu Katoliki cha Mbeya (CUoM) na amewahakikishia kuwa wapo mahali sahihi na salama pia uwepo wa Waalimu wazuri na waliobobea katika ufundishaji.

Aidha, Prof. Haule amewaelekeza wanafunzi hao kuwatambua Wafanyakazi na kufahamu kuhusu muundo wa uongozi Serikali ya Wanafunzi (CUoMSO) na amewataka kuendelea kufuatilia ili kufahamu wapi watatakiwa kwenda pindi watakapohitaji kupata msaada wa kitaaluma au kijamii kwa kipindi chote watakachokuwa Chuoni.

Prof. Haule pia aliwasisitiza wanafunzi hao kujiepusha na mahusiano ya kimapenzi bali wazingatie lengo namba moja ambalo limewaleta CUoM, ambalo ni Taaluma/Kusoma na bila kusahau Maadili, kujituma na kumcha M/Mungu kulingana na Imani ya kila mtu ili kufanikiwa katika masomo yao.

Photos from tzcuom's post 27/10/2024

Mgeni Rasmi,Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Charles Makongoro Nyerere akizungumza na Jumuiya ya CUoM katika Warsha iliyoandaliwa na Chuo Kikuu Katoliki cha Mbeya (CUoM) kwa ajili ya kuadhimisha miaka 25 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kuangazia Falsafa ya Elimu ya Mwl. J.K Nyerere na Sera ya Elimu ya Tanzania.

Photos from tzcuom's post 27/10/2024

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Charles Makongoro Nyerere aungana na Jumuiya nzima ya Chuo Kikuu Katoliki cha Mbeya (CUoM) Kushiriki Ibada ya Misa Takatifu ilyofanyika katika Kanisa la Hija Mwanjelwa. Ibada ambayo iliongozwa na Mhashamu Baba Askofu Mkuu Gervas J. Nyaisonga ambayo ilikua kwa ajili ya kuomba Baraka za Mwenyezi Mungu kuanza mwaka mpya wa masomo 2024/2025 Salama.

Photos from tzcuom's post 23/10/2024

Baadhi ya Wanafunzi wa Astashahada na Stashahada katika programu mbalimbali wakiwa Maabara ya computer (Computer Lab) katika program maalumu yenye lengo ya kuwawezesha wanafunzi wapya kufahamu na kupata maarifa ya jinsi ya kutumia computer na kuwajengea msingi wa lugha ya kingereza.

Photos from tzcuom's post 23/10/2024

Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Astashahada na Stashahada wakiwa katika mafunzo elekezi (Orientation) yanayoendelea kutolewa hapa Chuoni. Mafunzo haya yana lengo la kuwawezesha wanafunzi kufahamu vyema mazingira ya chuo, Kuwapa wanafunzi uelewa na maarifa ya maisha ya chuo, Kufahamiana na Kushirikiana kijamii & Kitaaluma.

Photos from tzcuom's post 23/10/2024

Usajili ukiendelea kwa programu mbalimbali mwaka wa masomo 2023/2024.

23/10/2024

Don't miss out!

Want your school to be the top-listed School/college in Mbeya?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


Mbeya

Opening Hours

Monday 07:00 - 19:00
Tuesday 07:00 - 19:00
Wednesday 07:00 - 19:00
Thursday 07:00 - 19:00
Friday 07:00 - 19:00
Saturday 07:00 - 19:00