17/05/2026
Being a parent to an adventurer offers the chance to join the adventurers' learning circle and support the child's behavioural development.
Throughout this journey, you become a guide, counsellor, instructor, and even a senior guide.
Instead of just being an adventurer's day, World Adventurers Day becomes a family day to renew and reaffirm commitments to walk with Jesus.
Happy Adventurers Day 2026!
20/05/2022
BEST DEAL..
Ingia weekend kwa OFA kubwa ya punguzo la 50% ya bei ya kitabu (ebook) ya
UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI K**A MRADI
Badala ya Tshs. 8,000 lipa nusu bei sasa Tshs. 4,000 tu na nikuongezee kitabu cha HATUA 5 ZA LAZIMA KATIKA MRADI WA KUKU WA KIENYEJI bureeee 100%.
Tuma Tshs 4,000
Mpesa 0768678122
Tigo Pesa 0715678122
Jina Mujaya Mujaya
Kisha tuma SMS ya malipo kwenda WHATSAPP namba +255768678122 kupokea vitabu vyako.
21/04/2022
PATA KITABU 100% BUREEEE...
HATUA 5 ZA LAZIMA KATIKA MRADI WA KUKU WA KIENYEJI
"Maamuzi Muhimu Yatayoepusha Usipoteze Pesa Zako."
NDANI YA KITABU!
Matumizi ya MKEKA katika kudhibiti magonjwa korofi ya Kuku.
Gundua zaidi ya aina 30 adimu za Kuku wa Kienyeji zenye faida.
Tambua mtindo wa ufugaji kuku wa kivivu lakini wenye faida.
Siri ya kuuza bei yoyote kwa mtu yeyote.
Tuma ujumbe wenye neno KITABU kwenda WHATSAPP namba +255768678122 ukimiliki.
Kitabu hiki bei yake ni Tshs. 15,000 lakini leo utakipata bure. Hii ofa ni zawadi yako ya muda mfupi kusherekea uzinduzi wa vitabu viwili mwisho wa mwezi huu.
Baada ya leo bei ya kawaida itarudi. K**ata kitabu chako sasa hauna cha kupoteza.
Jipatie nakala yako. Tuma ujumbe sasahivi wenye neno KITABU kwenda WHATSAPP namba +255768678122.
10/04/2022
DAWA KIBOKO YA TAIFODI NA MINYOO YA KUKU
Wengi tunayafurahia mapapai k**a matunda kwa ajili ya kula pamoja na kunywa k**a sharubati (juice).
Lakini unajua k**a papai linaweza kuwa suluhisho la kudumu kwa magonjwa na changamoto mbalimbali za ufugaji wa kuku k**a vile kutibu taifodi, pullorium (ugonjwa wa kuganda choo sehemu ya haja), minyoo, ndui, kuharisha, kuhara damu (coccidiosis) pamoja na kufukuza wadudu wasumbufu k**a vile utitiri, viroboto, chawa, kupe n.k?
Basi! Papai linalojulikana kitaalamu k**a 'Carica Papaya' lina kiambata muhimu ambacho kinaitwa 'Popaine' kinachofanya miujiza hii ya uponyaji pamoja na viambata vingine.
Leo nitakwambia tu jinsi papai linavyotibu taifodi na minyoo ya kuku.
JINSI YA KUTAMBUA KUKU MWENYE MINYOO NA TAIFODI
Utajuaje kuku wana minyoo? Utaona uzito unashuka licha ya kula chakula (wanakuwa wepesi), manyoya yanavurugika n.k
Taifodi ya kuku inaonekana kwa kuangalia kinyesi chake kinakuwa na rangi ya njano iliyoiva k**a vile salfa(dawa ya kupulizia mimea) pia kuku wanaweza kuonesha dalili ya kujikunyata kwa kushusha mbawa k**a wamevaa makoti. Kuku pia huweza kupumua kwa shida na ukiwasikiliza ni k**a mlio wa filimbi.
JINSI YAKUTIBU
Kausha mbegu za papai, zitwange kupata unga.
Changanya na maji kupata uji mzito. Wanyweshe kwa kuwalazimisha kijiko kimoja cha chai kwa siku kila siku kwa muda wa siku 5.
K**a sasaivi wanaumwa na hauwezi kukausha mbegu za papai basi wamezeshe mbegu 3 hadi 5 za papai kwa siku.
MAMBO YA KUZINGATIA:
1. Mbegu zitoke kwenye papai ambalo limeivia mtini.
2. Hakikisha umethibitisha ni ugonjwa wa taifodi kweli kabla haujawapa dawa.
3. K**a kuku wanajisaidia minyoo basi unatakiwa kuongeza dawa kwa kuwanywesha utomvu wa papai pia.
JINSI YA KUVUNA UTOMVU
Wakati wa asubuhi kabla jua halijachomoza toboa papai bichi (ambalo halijakomaa) kisha kinga utomvu wake na uwapatie kuku mara moja bila kusubiri.
Dozi ni kijiko kimoja cha chakula kwa kuku wakubwa na kijiko kimoja cha chai kwa mitamba na vifaranga.
Wape dawa hii sambamba na ile ya mbegu. Ukiwapa utomvu asubuhi basi jioni wape mbegu.
Najua utakuwa umegundua sasa kwamba k**a unafuga kuku pia unatakiwa kuwa na miti ya mipapai jirani yako maana itakuweka mbali na madawa ya dukani zaidi ya asilimia 80.
Nimekuandikia kitabu chenye dawa zaidi ya 100 za asili ambazo zitakusaidia kutibu magonjwa korofi ya kuku. Usikikose kitakapotoka mwezi Juni mwaka huu.
Pia HABARI NJEMA, mwezi huu mwishoni tutapata vitabu viwili kwa mpigo ambavyo vipo kwenye hatua za mwisho kabisa za ukamilishwaji wake.
Imeandikwa na Mujaya MJ
Kwa mawasiliano +255768678122
Tuvute pamoja, akili kichwani, pesa mfukoni na Mungu moyoni.
07/04/2022
JINSI YA KUJUA MAPEMA KUKU WAKO AU KIFARANGA NI JOGOO AU TEMBE?
K**a unafuga kuku chotara au kienyeji kibiashara unatakiwa kujua k**a vifaranga wako ni majogoo au matembe mapema zaidi iwezekanavyo.
Unakuta lengo lako ni kuuza mayai lakini kwenye vifaranga wako 100, umekadiria majogoo wawe 30 na matembe 70 ila wakikua wakubwa unagundua kumbe majogoo ni 70 na matembe 30. Inakatisha tamaa.
Ungejua mapema ingekusaidia kujipanga vizuri kibiashara.
Ona k**a una lengo la kuuza mayai ingekua vema tangu siku ya kwanza unapokea vifaranga ulivyototolesha au kununua ukajua majogoo mangapi na matembe wangapi. Si ndiyo?
Kujua jinsia ya kuku kunasaidia mambo mengi sana kibiashara.
1. Programu za chakula.
Utaokoa pesa kwa kuwapa kuku chakula kulingana na malengo yako. Unaotaka kwa lengo utawapa chakula bora ili wazalishe zaidi wakati ambao hawaendani na lengo lako utawaondoa au uwape chakula kitachofanya uwauze mapema zaidi kwa faida.
2. Ukuaji unaowiana wa kuku.
Utasimamia kuku wako wasipishane sana maumbile au ukubwa wao. Kuku wasioendana na mpango wako hawatakula chakula cha kuku wenye lengo lako.
3. Kuuza kuku ambao hawazalishi kwa wakati.
Kuku ambao hawatakuzalishia utawauza haraka na kuokoa pesa za chakula na kuwahudumia.
K**a unauza vifaranga kujua jinsia kutakusaidia sana maana utaweza kuwauzia wateja kuku kulingana na malengo yao ya biashara.
Mfano: mteja akitaka kuuza nyama utamuuzia majogoo tu ya Kuroiler au Sasso lakini akitaka mayai utamchanganyia matembe mengi na majogoo machache kulingana na uwiano wa kuku wake. Hapa utauza zaidi maana mteja wako utamuondolea wasiwasi wa kungoja hadi kuku wakue ili ajue jinsia ya kuku wake.
Sasa utajuaje k**a kifaranga ni jogoo au tembe kirahisi?
Zamani imeaminika kwa makosa kwamba yai lenye tembe linakua la duara lakini la jogoo linakuwa limechongoka upande mmoja. Wengine wanaamini yai kubwa ni jogoo na dogo ni tembe au njia nyigine niya kuzamisha yai kwenye maji likielea ni tembe na likizama ni jogoo. Ahahahahah hizi njia niza uwongo HAZIFANYI kazi.
Kimsingi zipo njia zaidi ya 5 zakugundua jinsia ya kifaranga hata chenye umri wa siku moja tangu kutotolewa.
1. Ukaguzi wa manyoya.
2. Ukaguzi wa sehemu ya kutolea haja.
3. Ukaguzi wa mabawa.
4. Kutazama upanga.
5. Kuangalia rangi ya manyoya ya ndani hasa k**a kuku wazazi ni mbegu (breed) tofauti.
6. Kusikiliza sauti za kuwika.
7. Kutazama tabia zao.
Kati ya njia hizi zote, njia tatu za kwanza ndiyo zina matokeo makubwa zaidi. Pia inahitaji mazoezi na uzoefu zaidi ili kufanya ukaguzi huo kwa usahihi.
Nimekuandikia kitabu chako kitakachokuvusha kiulaini kwenye changamoto hizi. Hakikisha haukikosi.
Emu niambie unataka kujua nini zaidi kuhusu utotoleshaji na malezi ya vifaranga? Nitakujibu fasta.
Imeandaliwa na Mujaya M.J
0768678122
29/03/2022
ONYO! USINUNUE WALA KUUZA KUROILER!
(Tambua SIRI KUBWA ambayo wauzaji wa kuku, mayai na vifaranga wa KUROILER hawataki uijue)
Kwenye biashara kati ya pesa na utu unachagua nini? Je, unajali mteja wako apate matokeo mazuri kulingana na malengo yake mema au unajali kupata pesa? Je, unaangalia uhalali wa biashara au unachohitaji ni kujaza mfuko wako faida?
Basi nikwambie! Baadhi ya wauzaji wa vifaranga, mayai na kuku aina ya Kuroiler wanachagua pesa kuliko utu. Wanajali mifuko yao kuliko bidhaa bora kwa wateja wao. Wanauza matarajio FEKI kwa wateja wao kwa bidhaa zilizo chini ya kiwango. Sio waaminifu, ni wezi wa biashara halali za watu.
Baadhi ya wauzaji hawa wanajua wanachokifanya lakini wameamua kuwalaghai wateja wao. Hii ni tabia mbaya sana kwenye biashara.
Nilitembelea kampuni moja kubwa tu Dar es Salaam ambayo inauza vifaranga vya Kuroiler, chakula pamoja na vifaa vya ufugaji wa kuku. Nikawauliza niliowakuta ofisini kuhusu asili na chanzo cha vifaranga wao nikagundua wanauzia watu makapi ya Kuroiler. Jinsi nilivyohoji walidhani ninatoka mamlaka za serikali wakaingiwa na hofu maana wateja wengi wakienda pale huwa wanatoa oda tu kisha wanaenda zao bila kuuliza kitu.
Siku nyingine nilipotembelea maonyesho ya wakulima na wafugaji (Nane Nane) nilipita mabanda mawili.
Moja ni mama mmoja mjasiriamali wa kuku wa Kuroiler ambaye kwenye banda lake aliandika anatotolesha na kuuza vifaranga wa Kuroiler kwa oda. Banda lake lilikua na kuku wa Kuroiler majogoo makubwa sana, ukiyaona k**a unapenda miradi ya kuku lazima uvutike.
Nilimuhoji! Kuku wazazi (parent stock) anayotumia kuzalisha vifaranga amewatoa wapi? Akasema alinunua kwenye kampuni ya ufugaji (hakutaja jina). Nikamuuliza anawaonaje kiuzalishaji wale kuku wake wa kwaza (wa kwenye kampuni) na vifaranga vyao anavyototolesha kwa ajili ya kuwauzia wengine?
Yule mama akastuka! Akauliza kwani mimi ni nani? Nikamwambia ni mtafiti tu wa maswala ya ufugaji wa kuku. Basi akaniambia, "Kiukweli, kiuzalishaji wale kuku wa kutoka kwenye kampuni ni wazuri zaidi kuliko vifaranga wao".
Nikamuuliza sasa kwanini anauza vifaranga hao wakati anajua kabisa siyo bora? Akajibu, "japo wanatofauti na wale wa kampuni, lakini matunda yao hayapishani sana."
Badae nikamuuliza swali baya sana, "Kwanini usiwauzie wateja wako hao kuku bora umechagua kuuza vifaranga dhaifu?" Akajibu kwa uchangamfu, "Nitauzaje mtaji wangu?"
Basi nikampa elimu ya ufugaji pale na kumtatulia baadhi ya changamoto zake za ufugaji wa kuku kisha nikamuacha anashangaa tu.
Lakini nilimpenda sana yule mama na maongezi yetu yalinifanya nijue kuwa alikuwa hajui anachokifanya kuwa ni kosa. Yeye mwenyewe alikua anashangaa kwanini uzalishaji unapishana!
USIKOSE SEHEMU YA PILI KESHO... Nitakwambia SIRI zote ambazo wauzaji wa mayai, vifaranga na kuku aina ya KUROILER hawataki ujue.
Somo hili nakupatia sababu ninakujali sana wewe na pesa zako. Sitaki upotee njia kizembe.
Imeandaliwa na Mujaya M.J
Ukihitaji namba njoo inbox.
Tuvute pamoja, akili kichwani na pesa mfukoni.
22/03/2022
Niulize swali lolote kuhusu KUKU WA KIENYEJI nami nitakujibu.
14/03/2022
MIUJIZA YA BINZARI MANJANO KATIKA KUBUSTI UZALISHAJI WA KUKU NA KUTIBU MAGONJWA
Wengi tunafahamu binzari ya manjano k**a kiungo muhimu kwenye mboga hasa nyama, pilau na biriani kinacholeta ladha tamu na mwonekano mzuri wa chakula. Binzari ya manjano pia ikiwekwa katika maharage inanoga sana na inabadilisha rangi na kuwafanya watoto wasiopenda maharage wavutiwe kula.
Lakini je, unajua binzari hii inaweza kufanya miujiza mikubwa katika matibabu ya magonjwa mengi ya kuku na kubusti uzalishaji wao wa nyama na mayai?
K**a haujui, basi upo unasoma eneo sahihi. Baada ya dakika 5 za kusoma hapa utakua mtaalamu wa kutumia binzari ya manjano kufanya miujiza ya uponyaji. Ahahahahah
Binzari ya manjano kitaalamu inajulikana k**a Curcuna Longa inatibu magonjwa mengi na kuchochea uzalishaji wa kuku. Leo nitakwambia jinsi binzari inavyotibu vidonda na magonjwa yanayopelekea kuku kupata vidonda.
Kuku wanapata vidonda kupitia kudonoana, kukatwa, kuchomwa au kukanyaga kitu chenye ncha kali, kung'atwa na wanyama au wadudu, kuvimba nyayo na miguu (Bumblefoot) na ndui ya kuku.
Matatizo haya yote kiboko yake ni binzari ya manjano. Leo kwa sababu ya muda nitakwambia tu kuhusu Bumblefoot.
Kwa tatizo la Bumblefoot unatakiwa kwanza kusahihisha makosa uliyofanya kabla haujatibu ugonjwa. Kuku wako wamevimba nyayo kutokana na uzito kupita kiasi hasa majogoo pia sakafu yako sio laini (ina changarawe, mchanga mgumu au k**a umeweka sakafu ya waya/nyavu basi hazijakaa vizuri zinawachoma kuku), bembea/vichanja vipo juu zaidi ya mita 1 kutoka sakafuni na k**a umeweka matandaza kwenye sakafu basi ujue hayana kina cha kutosha.
Baada ya kusahihisha makosa, sasa kimbia nenda ukatibu ugonjwa kiurahisi kutumia binzari ya manjano.
Chakufanya, chukua kitu chenye ncha kali k**a kisu chembamba kisha kichome kwenye moto kuua vijidudu alafu tumbua huo uvimbe kwa kuku. Kamua hadi uchafu wote utoke, safisha kwa maji ya vuguvugu yenye chumvi kwa mbaali. Ili maji yaingie kusafisha vizuri hadi ndani unaweza kutumia bomba safi la sindano kuvuta maji na kusafisha ndani ulipotoa uchafu. Pakishakuwa safi weka au nyunyizia unga wa binzari na umfunge jeraha kwa kitambaa kisafi.
Zingatia: Wakati unatumbua uwe umevaa groves, lainisha miguu kwa kuiloweka kwenye maji safi yenye sabuni ya unga kwa dk 10, ifute miguu na upake sanitizer au spirit, mfunge kuku kitambaa ili atulie kisha tumbua mguu kwa kutumia kisu kwa kukata doa au baka jeusi kwanza kisha kamua kuondoa kokwa lote.
Weka dawa hii kwenye kidonda mara moja kila siku hadi kuku atakapopona. Siku 5 nyingi utaona kuku wamepona kabisa.
Binzari ya manjano ni tiba supa kwa magonjwa ya numonia ya fangasi (Aspergillosis), minyoo, kikohozi, mafua, kuharisha, ndui ya kuku, kuhara damu (coccidiosis) na magonjwa mengine yanayosababishwa na bakteria.
Kwa wale wanaopenda pesa za chapchap binzari ya manjano ni rafiki yao wa karibu kwani matumizi yake hongeza utagaji wa mayai, mayai hata ya kuku wa kisasa yanaweza kufanywa kuwa na kiini cha njano k**a vile ya kuku wa kienyeji wa shamba, hufanya kuku wakue haraka, wawe wazito na wachangamfu n.k
Nipo ninakuandalia kitabu chako ambacho Mungu akipenda mwezi wa 6 kitakuwa mkononi mwako ili ujue mambo haya kwa undani na uwe unasikia magonjwa kwa majirani tu. Ahahahahah
Kitabu kitakua na dawa zaidi ya 100 zenye kutibu karibu magonjwa yote yanayosumbua kuku wako. Pia nitakuwekea na busta kibao za chakula zitakazofanya upate mshiko fasta bila kusubirisubiri afu na bidhaa zako ziwe bora bila mshindani.
Kwa leo naishia hapa. Niambie unataka kujifunza nini zaidi? Nitakuandalia mada yako maalumu hapahapa.
Somo hili ni zawadi kwako baada ya jana Singida Poultry Farm kuleta mrejesho mzuri sana baada ya kufanyia kazi kwa mafanikio somo nililoweka siku ya ijumaa kuhusu JINSI YA KUWAPATIA KUKU CHAKULA BORA BILA GHARAMA.
Masomo mengi yatakuja baada ya kupokea mrejesho kutoka kwako jinsi unavyotumia masomo haya.
Tuvute pamoja. Pesa mfukoni, akili kichwani na Mungu moyoni.
10/03/2022
HATUA ZA KUCHUKUA KABLA YA UJENZI WA BANDA LA KUKU
"Njia Rahisi za Kupunguza Gharama Zisizo na Lazima"
Ujenzi wa banda la kuku unagharimu sehemu kubwa ya fedha zako iwe unaanza au unaendeleza mradi wako. Haijalishi malighafi, ufundi na usanifu lakini gharama za ujenzi wa banda huwa inachukua karibu nusu ya mtaji wako wote.
Ukikosea kwenye kukadiria ukubwa wa banda na vifaa vya ujenzi maana yake umeongeza gharama ambazo zitapunguza faida yako mwishoni mwa mradi.
Changamoto kubwa unayotakiwa kuitatua ni kukadiria ukubwa kamili wa banda unaoendana na mahitaji yako, banda lisiwe kubwa sana ukapata hasara au likawa dogo sana ukapata shida ya magonjwa, ukuaji hafifu, msongo n.k
Changamoto hizi utaziepuka ukijua mapema unatakiwa kufanya nini kabla haujamuita fundi ili uanze ujenzi.
Hatua za kuchukua
1. Amua unafuga kuku kwa malengo gani? Nyama, mayai au vyote viwili.
2. Aina gani ya kuku utafuga. Kuna aina nyingi za kuku na kila moja ina banda lake maalumu linalofaa.
3. Mtindo wa ufugaji utakaotumia.
4. Usanifu wa banda.
5. Vifaa vya ujenzi utakavyotumia na gharama za ufundi. Fanya makadirio halisi ya gharama kabla haujaanza ujenzi.
6. Manunuzi ya vifaa na malighafi za ujenzi.
7. Ujenzi.
Ukiruka hatua hizi jiandae kupata hasara. Wafugaji wengi wamekosea na kujikuta wana magofu makubwa ya mabanda bila kuku au wana mlundikano mkubwa wa kuku katika eneo dogo.
Nimekuandikia kitabu chako kitakachokuvusha katika hatua hizi zote saba kiurahisi bila stress na kuokoa fedha ambazo ungezipoteza bila sababu yoyote.
Habari njema, kitabu kitakuwa mkononi mwako mwezi wa 6 mwaka huu.
Ili uwe wa kwanza kukipata hakikisha unaweka namba yako ya simu hapa au unatuma ujumbe "kitabu" kwenda +255768678122.
27/02/2022
Ninakuandikia kitabu kuhusu matibabu ya magonjwa ya kuku. Unatamani nini kisikosekane kwenye kitabu hicho?