Majembe12

Majembe12

Share

ISAYA 62:6d
๐Ÿ‘‰Ninyi wenye kumkumbusha Bwana msiwe na kimya.

31/12/2024

๐Ÿ‘‰ Ukweli ni kwamba wengi tunatamani kuuona mwaka mpya na wengi walitamani kuuoana lakini mpaka sasa hawawezi tena maana hatupo nao tena
โœ“โœ“Tena wengi tuna mipango Mingi tunayotamani kuitimiza mwakani.

๐Ÿ‘‰ Lakini ni wazi kwamba Kuna watu mwaka 2025 unaweza ukawa mwaka wao wakumiliki na kutimiza mipango Yao na Kuna wengine unaweza ukawa mwaka wa kuanguka na Kuna wengine unaweza Kuta mwaka 2025 ukawa sawa na mwaka 2024 zaidi ikawa ni hiyo Moja iliyoongezeka na Ile Moja itakayo ongezeka kwenye miaka yao,lakini maisha Yao mengine yakabaki vile vile(Lakini k**a aishivyo Mungu aliye hai--NATAMANI KUONA KILA MTU ANAFANIKIWA KATIKA KILA HITAJI LAKE)


๐Ÿ‘‰Zaidi nataka nikukumbushe kuwa nyakati hizi usisahau ya kuwa uzima ulio nao umepewa Bure,afya uliyo nayo umepewa bure..Neema ya kuuona mwaka mpya umepewa bure maana ni hakika hakuna ulipolipia..Hivyo hatima ya mwakani pia inahitaji usimamizi wa huyo aliyekupa Bure hivyo ambayo huwezi kununua" na ni wazi bado anakusudi na wewe ndio maana wakati wengine wameshindwa kuvuka lakini wewe Unaenda kuvuka Kwa JINA LA YESU na huyo ndiye Muumba wa mbingu na nchi nayeye asema hivi..๐Ÿ‘‡

Yeremia 29:11
[11]Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.

For I know the thoughts that I think toward you, saith the LORD, thoughts of peace, and not of evil, to give you an expected end.

๐Ÿ‘‰Ni hivi mwana wa Mungu..Kila unachohitaji na kukitamani yupo Mmoja anayekijua na anayeweza kukutimizia...anasema...(atatupa sisi tumaini siku zetu za mwisho-- yaani nyakati za dhiki,nyakati za uhitaji,yeye atatupatia mwisho tunaoutamania --in English the bible says-expected end-- yaani mwisho unaotarajia.. Tena anasema anakuwazia mawazo ya amani nasi mabaya."

๐Ÿ‘‰Hivyo mwana wa Mungu chukua Nafasi hii masaa machache haya yaliyobaki kumshukuru Mungu Kwa ajili ya mwaka wote wa 2024,Tena mwombe Mungu azidi kukupa afya njema na akuvushe mwaka huu salama" Tena usisahau kumshirikisha mipango Yako ya mwakani" maana yeye anakuwazia mema....anakuwazia amani anawaza kukupatia mwisho mwema" Basi hakikisha unapovuka mwaka unavuka na haja zako zikiwa zimejulikana mbele za Mungu wako.

๐Ÿ‘‰NA HILI NI OMBI LANGU KWAKO" MUNGU ALIYE HAI MUUMBA WA MBINGU NA NCHI AKAKUPATIE KILA HITAJI LAKO KWA MWAKA MPYA 2025" ILI UKAFANYIKE BARAKA KATIKA FAMILIA YAKO,UKOO WAKO" KAZINI KWAKO" KWA NCHI YAKO NA KWA JAMII INAYOKUZUNGUKA"

BARIKIWA๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™.

27/06/2024

...โœ๏ธ

27/06/2024

....โœ๏ธ

31/03/2024

๐Ÿ‘‰Ukweli ni kwamba tunaishi kwa Neema za Mungu, na ni huruma zake ya kwamba hatuangamii..๐Ÿ‘‡

Maombolezo 3:22
[22]Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii,
Kwa kuwa rehema zake hazikomi.

๐Ÿ‘‰Pamoja na Neema iliyoachiliwa juu yetu lakini bado mwanadamu Ili uishi maisha yenye utukufu na yenye baraka za Mungu ni lazima uwe na uhusiano mzuri na Mungu"ufanye mapenzi yake Mungu, usipofanya hivyo,Mungu anajitenga nawe,ukiwa Mtu wa maovu yaani mtenda dhambi au usiyetii maagizo yaani muasi, Mungu anajitenga nawe k**a ambavyo alijitenga na Adam,baada ya kula tunda ambalo alikatazwa..๐Ÿ‘‡

Mwanzo 3:24a
[24]Basi akamfukuza huyo mtu,

๐Ÿ‘‰kwahiyo Ili utembee na Mungu lazima uishi sawa sawa na Neno lake,Ili uhusiano wako na Mungu udumishwe ni lazima utende sawa na mapenzi yake,utembee kwenye kusudi la Mungu,utii maagizo yake,Neno linasema...๐Ÿ‘‡

1 Petro 1:15-16
[15]bali k**a yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
[16]kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
(kwahiyo Mungu ni mtakatifu..we all know..wote tunajua...lakini anasema nanyi mtakuwa watakatifu k**a yeye alivyo mtakatifu zaidi anasema katika mienendo yenu yaani tabia, mawazo yaani Kwa Kila njia ya jinsi ya mwili na rohoni,kwahiyo inawezekanika kuwa mtakatifu ukiwa duniani..sio hadithi inawezekanika...maana Kuna mahali Neno pia linasema...๐Ÿ‘‡

Zaburi 16:3
[3]Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora,
Hao ndio niliopendezwa nao.
((Anasema waliopo duniani...means sio Mmoja ni wengi..
โœ“โœ“OMBI LANGU KWAKO" MUNGU AKUSAIDIE NA WEWE UKAWE MMOJA WAPO.
๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™.

SWALI? SASA UNAKUWAJE MTAKATIFU?
๐Ÿ‘‰Kwanza Ili uwe mtakatifu lazima umjue Mungu wako vyema na ujue anapenda Nini na anachukua Nini?maana ukijua hayo na kuyatenda sawa sawa ndiyo utaweza kuwa mtakatifu ila Leo nitaanza na anachukia Nini? --->>Natamani ujue Mungu anachukia vitu Gani Ili ukivijua uviache mara moja maana pia ametupa rafiki ambaye ni Roho mtakatifu atuongoze...

๐Ÿ‘‰Katika yote lazima ujue kwamba Mungu anachukia dhambi,ndivyo ilivyo Wala waovu hawatakaa nyumbani mwake..๐Ÿ‘‡

Zaburi 5:4
[4]Maana huwi Mungu apendezwaye na ubaya;
Mtu mwovu hatakaa kwako;

โœ“โœ“katika kitabu Cha Mithali Neno la Mungu limeorodhosha majambo au mambo ambayo Mungu anayachukia..kinyume chake mambo ambayo yanatutenga na Mungu na hayo ni haya...๐Ÿ‘‡

Mithali 6:16-19
[16]Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA;
Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.

[[MOJA, MBILI NA TATU...๐Ÿ‘‡]]
[17]Macho ya kiburi, ulimi wa uongo,
Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;
((kiburi mwana wa Mungu si kizuri mbele za Mungu..tunapozungumzia kiburi sio kwamba unamfanyia Mungu kiburi Moja Kwa moja..hasha!" wewe umfanyie Mungu kiburi unaweza__??kamuulize Nebukadreza kutoka kuwa mfalme Hadi kuishi k**a mnyama, au kamuulize mke wa lutu..alivyogeuka nguzo ya chumvi!!
--->>Ni hiki tunawafanyia watu wake.." wazazi,watumishi wa Mungu,marafiki zetu...yaani kile kiburi unakifanya kwa hao wanaokuzunguka ..ndicho hicho kinachohesabika mbele za Mungu na ndicho hicho anachokichukia,maana Mungu anafanya kazi ndani ya watu,kwahiyo hao unaohisi ni watu wa kawaida kumbe ndani Yao wamebeba ujumbe wa Mungu na wewe unawaletea kiburi,same kwa uongo unapokuwa Muongo mbele ya waliokuzunguka ndio huo uongo...unaohesabika mbele za Mungu..,na Tena na wauaji

[[NNE NA TANO.....๐Ÿ‘‡]]
[18]Moyo uwazao mawazo mabaya;
Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu;
((Moyo ndugu yangu chunga sana moyo wako,maana mawazo mabaya yote hutoka moyoni, uzinzi..uasherati..uizi,ulevi Kila aina ya tabia mbaya inayoonekana kabla inaanzia moyoni..kwahiyo uchunge sana Moyo wako..Neno linasema...๐Ÿ‘‡
{{๐Ÿ“ŒMithali 4:23
[23]Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;
Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.}}

๐Ÿ‘‰Tena anasema miguu iliyo miepesi kukimbilia uovu"" mwana wa Mungu usiruhusu miguu Yako iwe fuata upepo wenzako wanakuambia twende disco..we no question..unajibeba...njoo tufanye hiki we kurupu...huyu hapa"" Haloo...MUNGU ANACHUKIA.

[[SITA NA SABA..๐Ÿ‘‡]]
[19]Shahidi wa uongo asemaye uongo;
Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.
((shahidi wa uongo" yaani unajua kabisa fulani hili hajafanya ni kafanya fulani...ila wewe unakomaa kumtetea mhalifu ..hili hata kwenye familia linatokea sana..lakini Leo yakupasa ujue kuwa MUNGU ANACHUKIA

๐Ÿ“Œ๐Ÿ“ŒTena Neno linasema na apandaye mbegu ya fitina kati ya ndugu" wewe unaye wagombanisha wenzako,ndugu,marafiki...yaani mchonganishi...mtu wa hila..Hutaki wenzako wake Kwa amani..Haloo...Mungu akusaidie ukabadilike Ili umpendeze.

๐Ÿ‘‰Ukweli ni kwamba haya yote ni matendo ya mwili,na tunashindwa kuyashinda kwasababu tumeamua kuisikiliza miili,lakini tukiamua kuisikiliza Roho tunaweza kuyashinda kwa kukesha na kuomba tunaweza kuyashinda yote...Neno linasema ...๐Ÿ‘‡

Wagalatia 5:16
[16]Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
((ukweli ni kwamba mtu yeyote kabla hajafanya jambo lolote baya au jema ndani yake roho inakuwa imemuambia kuwa hili si jema na hili si jema...lah! Kuna wakati tunashindwa kuisikia sauti ya Roho kwasababu...tumekaa mbali na Mungu pia..lakini lazima ujue ya kuwa Roho siku zote inapingana na mwili..๐Ÿ‘‡

Wagalatia 5:17
[17]Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.

kwahiyo tunapaswa pia katika yote Tumtafte Mungu kwa bidii ..Ili tujazwe na Roho wake na atufungue masikio ya rohoni Ili tuweze kumsikia roho wake...vinginevyo tutakuwa tunashinda majaribuni kwa kuufuta mwili na mwisho kuangukia dhambini...๐Ÿ‘‡

Mathayo 26:41
[41]Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.

NI MIMI KIJANA MWENZAKO KATIKA KRISTO YESU
NAME: ZELLA MAJEMBE

BARIKIWA ๐Ÿ™.

14/02/2024

๐Ÿ‘‰Ukweli ni kwamba Watu Wengi tunakesha tunalia mbele za Mungu,tukiomba msamaha..na kupeleka haja zetu,Kuna mda tunapokea majibu yetu na Kuna mda hatupokei..
โœ“โœ“kuna sababu kadhaa...zinazosababisha tusipokee na tusijibiwe..Moja inawezekana tunaomba vibaya..si k**a Mungu
apendevyo..๐Ÿ‘‡

Yakobo 4:3
[3]Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.
((kwahiyo Kuna mda hatujibiwi kwasababu tunaomba vibaya...tunaomba kwa tamaa zetu...si k**a Mungu apendavyo..maana ukweli ni kwamba Mungu hutupatia kwa mapenzi yake..sio yetu..ndio maana Yesu alisema...๐Ÿ‘‡

Mathayo 6:10
[10]Mapenzi yako yatimizwe,
hapa duniani k**a huko mbinguni.
((kwahiyo Kila mtu Kuna namna Mungu kampangia..mahitaji yake na kesho yake na njia yake...Je wewe unavyoomba unaombaje?? sawa sawa na mapenzi yake au Yako?? Yesu wakati anajua kuwa atasulubiwa na akijua yote...aliomba ivi..

Mathayo 26:39
[39]Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si k**a nitakavyo mimi, bali k**a utakavyo wewe.
(ukisoma mstari wa 38..anasema..๐Ÿ‘‰Mathayo 26:38
[38]Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami.
((kwahiyo ule mwisho wake ulimtia huzuni..aliogopa alitamaani isiwe hivyo..lakini unapoenda mstari wa 39..unaona anasema lakini mapenzi Yako yatimizwe,,kwahiyo vyovyote unavyopita...kwa namna yoyote Ile lazima uyajue mapenzi ya Mungu katika Hilo...! ujue kusudi la hilo jambo,linalokupata ndipo utagundua namna Gani wapaswa kumuomba Mungu Ili mapenzi yake yatimizwe na usiliondoe tumaini lako kwake.. )

Sababu ya pili inayoweza sababisha usijibiwe maombi Yako ni KUTOKUSAMEHE.
๐Ÿ‘‰Yesu anasema katika kitabu Cha marko..๐Ÿ‘‡

Marko 11:25
[25]Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
((kwahiyo simple ni hivi Ili Upokee majibu ya maombi Yako,,jifunze kusamehe...unapoomba Toba kwa Mungu..hakikisha nawewe umewasamehe waliokukosea..la sivyo Neno liko wazi..usiposamehe hutasamehewa,,..Tena Yesu anasema...๐Ÿ‘‡

Mathayo 6:14-15
[14]Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
[15]Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.

๐Ÿ‘‰katika Yote kua,katika Hekima ya Mungu katika kulisoma Neno lake..Ili likae kwa wingi ndani Yako,Na ndipo utafahamu zaidi juu ya Mungu unayemtumikia....na Unayemuabudu.

BARIKIWA๐Ÿ™๐Ÿ™.

29/01/2024

BWANA YESU ASIFIWE...๐Ÿ™.
MUNGU AKUTIE NGUVU USIPITWE NA NENO HILI ๐Ÿ‘‡
๐Ÿ‘‰Ni kweli Kila mtu anatamani maisha fulani,,anatamani awe kiwango fulani ambacho haelewi atafika lini..awe na maisha fulani ambayo hajui.. atayapata vipi??
..Mbaya zaidi shetani anajua matamanio ya wengi wetu..mtu atasema anajuaje anajua...maana andiko liko wazi katika Yakobo 4:1-3,..๐Ÿ‘‡
Yakobo 4:1-3
[1]Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?
(...kwahiyo anajua kuwa tuna tamaa..ndio Maana kaweka vitu vya kutamanisha mbele ya macho Yetu Ili tuzidi kutamani na kujikuta tunajiingiza kwenye mambo ambayo hayampendezi Mungu...ambayo mstari wa pili unayataja..๐Ÿ‘‡

[2]Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi!
[3]Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.
((ANDIKO LINASEMA TUNAOMBA VIBAYA..KWANINI??

JIBU::๐Ÿ‘‡
๐Ÿ‘‰Wapendwa wengi wa leo hatusomi Neno la Mungu,, hivyo hatuna hata maneno mazuri yakumwambia Mungu,,na zaidi wengi wetu...tumejikuta tumeingia kwenye wimbi la watu,wavivu wa Kila kitu,wavivu wa kusoma neno..wavivu wa maombi...wanaopenda shortcut.. Tunapenda kuambiwa POKEA FEDHA,POKEA NYUMBA,POKEA GARI na kadhalika and SHOUT AMEN..sad indeed..
my friend...Mungu hatendi kazi ivyo""
...NENO LINASEMA...๐Ÿ‘‡

Mithali 8:10-11
[10]Pokea mafundisho yangu, wala si fedha,
Na maarifa kuliko dhahabu safi.
((BWANA WA MAJESHI Anasema pokea mafundisho si fedha...na Tena maarifa kuliko dhahabu safi...ivi unaelewa..na Tena mstari wa kumi na Moja anasema..๐Ÿ‘‡
[11]Maana hekima ni bora kuliko marijani;
Wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo.
(Anasema..hekima ni Bora kuliko marijani na vyote vinavyotamanika havilingani nayo..."
..Ni ivi wengi wetu hatupati tunavyovitaka kwa sababu neno la Mungu halikai ndani yetu..maana Kwa Neno Mungu alifanya mbingu na nchi...Wala haisemi kwa dhahabu Wala kwa fedh Bali kwa Neno Mungu alifanya mbingu na nchi na , alifanya vyote Hadi Nuru,na Kila mmea.na Kila ndege na Kila mnyama..๐Ÿ‘‡

Yohana 1:1,3
[1]Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
[3]Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
((kwahiyo Ili upate unavyovitaka kwanza lazima Neno la Mungu likae ndani yako..maana Hilo ndilo uumbaji..ili k**a ni Baraka ujitamkie mwenyewe..
โœ“โœ“Kwahiyo NENO LA MUNGU ndio ufunguo wa baraka zako na maombi Yako...na ndilo njia ya kupata majibu ya maombi Yako,na ndio Lina Siri ya utajiri unaoutafta..Yesu Anasema..

Yohana 15:7
[7]Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.

โœ“โœ“SWALI SASA,,MANENO YA MUNGU YANAKAAJE NDANI YETU...??
Jibu ndilo Hilo Mithali 8:10-11...tunalipokea kwa kusoma Biblia...tulipokea kwa kufundishwa na watumishi wanaofundisha Kweli ya MUNGU...ndipo saa likifanya makao ndani yetu ..tukiomba chochote tunapata na kujibiwa maombi yetu...BIBLIA HAISEMI tukitamkiwa pokea..gari au fedha...Bali tukilipokea hili neno nalikikaa ndani yetu na tukiomba lolote tutatendewa...

๐Ÿ‘‰Kwahiyo unaporuhusu neno la MUNGU likae ndani Yako..wewe si maskini,, kwasababu una nguvu yakuomba lolote na likawa.. kwasababu ya utajiri unaokuwa nao kiroho..

KWA UFAFANUZI ZAIDI NGOJA TUANZIE HAPA...MUNGU AKUSAIDIE UFAHAMU WAKO UFUNGUKE...
Yesu hakuwa na gari,hakuwa na nyumba..hakuwa na fedha..hakuwa na chochote ila kiuhalisia alikuwa tajiri,kwasababu vitu vyote vilikuwa chini yake,maana alisha ahidiwa na Baba yake anavyomtuma kuwa ukifanya hivi itakuwa ivo,kwahiyo alichokifanya nikushika maneno tu kuyaweka ndani yake,,

Yohana 6:57
[57]K**a vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi.
((k**a atakuwa hai kwa yeye...means atafanya yote yesu aliyo yafanya..na atetembea katika mtembeo wa Yesu..

Tena Paulo anasema juu ya utajiri wa Yesu๐Ÿ‘‡

2 Wakorintho 8:9
[9]Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
..๐ŸŒน Miujiza kadhaa aliyoifanya inathibitisha utajiri wake unamuona Kuna mahali aligeuza maji kuwa divai,aliwahi lisha watu zaidi ya 5000..aliwahi tuma wanafunzi wake kumletea mwanakondoo wa mtu hawamjuhi..lakini walimletea...kwanini vyote vilikuwa chini yake..na ndiyo maana yote haya yaliwezekanika...na ni kwasababu yeye aliyaweka maneno ya Baba yake ndani yake...ndio maana Kila alichokuwa anakiomba kilikuwa kinatokea...na kinakuwa.. shortly..unapoweka UHUSIANO mzuri na Mungu...wewe unakuwa juu ya vyote na unakuwa na amri na vyote...

JE SISI TUNAKUWAJE MATAJIRI KATIKA YESU..??
ukweli ni kwamba tunakuwa matajiri katika Yesu pale tu tunapopokea mafundisho yake...na maarifa yake...maana hivi viwili ukivipata ni umepata zaidi ya mwenye dhahabu na fedha..na zaidi hekima yake inapita vyote.."..unafanyika mkuu juu ya vyote..
โœ“โœ“Na hivi vyote tunavipata tunapokuwa wasomaji wa Neno la Mungu...ndipo tunapokea maarifa ya Mungu na hekima ya Mungu...na si kwa kuambiwa Pokea sijui Nini,, and Shout Amen๐Ÿ™๐Ÿ™ okay" sisemi ni sahihi ah sahihi hasha! Mungu ndiye anajua...ila Mimi natamani Wana wa Mungu tuwe na wingi wa Neno la Mungu ndani Yetu...tupokee maarifa yake,hekima yake..na mafundisho yake yakae ndani yetu,tusiwe wavivu katika kumtafta MUNGU ALYE HAI ILI TUJIOMBEE WENYEWE TUSISUBIRI KILA KITU TUTAMKIWE NA WACHUNGAJI WETU...""" โœ“โœ“Maana unaweza tamkiwa Neno la Imani...lakini k**a Neno la Mungu halimo ndani Yako...Hilo neno litapulizwa na upepo((wengi mmetamkiwa maneno ya imani..wengu mmetumia mafuta..majibga upako..ukweli wake..MUNGU ndiye anajua,lakini katika kutumia Kuna wengi wenu,Imani yenu imetumbishwa na upepo juu ya hivyo vitu..baada ya kukutana na watu wanaosema ni uchawi..,sijui uongo..unazani ni kwanini mnayumbishwa kirahisi ni kwasababu Imani yetu juu ya kristo tunaipata Kwa Neno lake KRISTO na injili ya kweli.."" k**a Kuna ukweli juu ya maji ya upako namafuta...basi Imani Yako ijengwe na Neno la Mungu na sio propaganda za Binadamu.
..Lah! Imani Yako itakuwa ni ya mashaka ambayo haitakuzalia matunda ...

โœ“โœ“Tena natamani ujue hili ukweli injili ya Leo,Ina magugu mengi yaani watumishi wengi wamejiingiza K**a watumishi wa MUNGU..Bali wanatafuta faida zao...na tusipokuwa wasomaji wa neno la MUNGU,tutapotea pamoja nao...๐Ÿ‘‡

Yeremia 23:1-2
[1]Ole wao wachungaji, wanaoharibu kondoo za malisho yangu na kuwatawanya! Asema BWANA.
[2]Kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, juu ya wachungaji wanaowalisha watu wangu, Mmetawanya kundi langu, na kuwafukuza, wala hamkwenda kuwatazama; angalieni, nitawapatiliza uovu wa matendo yenu, asema BWANA.

OMBI LANGU KWAKO, JIFUNZE KUSOMA NENO LA MUNGU ILI LIKUPE MUONGOZO NAMNA YA KUISHI NA KUFIKIA NDOTO ZAKO.

BARIKIWA๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™.

31/10/2023

NENO LA SIKU

31-10-2023

SOMO:KESHO YAKO I MIKONONI MWA MUNGU

.Iko ivi Mungu anayajua MAHITAJI Yako yote,anazijua haaja zako zote na changamoto zako zote.
Na hakuna hata Moja inayomshinda kwamba hawezi kutatua..kwa maana Mungu wote ni MUWEZA WA YOTE.

๐Ÿ‘‰Lakini ili uzipate baraka zako au MAHITAJI Yako yote lazima ufuate utaratibu wa ki-Mungu, Lazima uguse moyo wake.. kwanza Mungu wetu anapenda kuheshimiwa,kuabudiwa na kusifiwa..na kuaminiwa pia anapenda kutumainiwa
..no matter the situation uko nayo..We amini Mungu nimuweza,just put your trust in Him, Don't stop praising and worshipping Him.

๐Ÿ‘‰Binadamu tuko na mawazo yetu Ivo Kuna wakati tunafanya vitu kwa mawazo yetu na mawazo yetu mara nyingi yanatupoteza.. MITHALI 5:5b anasema usizitegemee akili zako mwenyewe,
Ivo Muombe Mungu akupe ufahamu wake na hekima yake ili uweze kutenda na kufanya mambo kwa usahihi ili uifikie kesho Yako kirahisi(yaani OMBA Roho wake akuongoze)

๐Ÿ‘‰Hakikisha katika njia zako zote unamkiri yeye, katika Kila jambo ulitendalo muweke Mungu mbele, Kiri kwamba Mungu ndio ameshika kesho Yako,ndio anazijua hatua zako, ndio Kiongozi wa familia Yako,ndio afya Yako na uzima wako na mengineyo yanayokuhusu haijalishi unauaweza au huyawezi
Ndipo MITHALI 5:6b Naye atanyoosha mapito Yako
Yaani njia zako zitakuwa nyeupe na zimebarikiwa na mbaraka wa Mungu.

BARIKIWA๐Ÿ™

๐ŸŒน JESUS IS LORD โค๏ธ๐Ÿ™

30/10/2023

NENO LA SIKU

30/10/2023

SOMO:KAMA MKIKUBALI NA KUTII MTAKULA MEMA YA NCHI

Ukikubali kuisikiliza sauti ya Mungu na kutii maagizo yake,utakula mema yake..Maana Kila tunachokihitaji Kiko mkononi mwa Mungu au ndani ya UWEZO wake..
Lakini ivi vitu huvipati kwa bahati mbaya,unavipata Kwa kufuata utaratibu wake Mungu,

๐Ÿ‘‰UKUBALI VIPI NA UTII VIPI?
yaani mfano ukiitwa hatua ya kwanza unaitikia wito,
Hatua ya pili unasikiliza kilicho kwenye wito unaambiwa Nini au unaagizwa nini...
Baada ya kusikiliza wito,ukiiupokea na kuutendea kazi ndio tunaita UMEKUBALI NA UMETII

๐Ÿ‘‰Kwahiyo Mungu ametuahidi mema ya nchi,lakini hayo mema tunayapata kwa kukubali sauti ya Mungu na kutii maagizo ya Mungu,Kila mtu Kuna namna kasemeshwa na Mungu lakini shida ipo kwenye kukubali kuisikiliza sauti unayoisikia na kutii maagizo ndani ya hiyo sauti.Kuna watu wamesikia sauti ya Mungu na wameipuuza,hao watu kwao baraka,au utajiri au mema ya nchi kwao ni ndoto kwa maana anasema..

๐Ÿ‘‰BARAKA ZETU zote zipo mkononi mwa Mungu, **MITHALI 8:18 (utajiri na heshima ziko kwangu,Naam utajiri udumuo na haki pia.)**
Lakini ivi vitu vinakujia ukikubali na ukiitiii sauti ya Mungu wako.

Lakini usipoikubali sauti ya Mungu na kuitii...
Ni vigumu kula mema ya nchi
Tazama **ISAYA 1:20**
bali k**a mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha BWANA kimenena haya.
๐Ÿ‘‰Ivo ni muhimu kuisikia ukisikia sauti ya Mungu uitii Ili ule mema ya nchi,vingine Biblia inasema myaangamizwa kwa upanga..na BWANA yeye mwenyewe kwa kinywa chake amenena hayo.

๐ŸŒนGOD BLESS YOU๐ŸŒน

28/10/2023

AMEN ๐Ÿ™

Want your school to be the top-listed School/college in Mbeya?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address

Mbeya