29/01/2024
BWANA YESU ASIFIWE...๐.
MUNGU AKUTIE NGUVU USIPITWE NA NENO HILI ๐
๐Ni kweli Kila mtu anatamani maisha fulani,,anatamani awe kiwango fulani ambacho haelewi atafika lini..awe na maisha fulani ambayo hajui.. atayapata vipi??
..Mbaya zaidi shetani anajua matamanio ya wengi wetu..mtu atasema anajuaje anajua...maana andiko liko wazi katika Yakobo 4:1-3,..๐
Yakobo 4:1-3
[1]Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?
(...kwahiyo anajua kuwa tuna tamaa..ndio Maana kaweka vitu vya kutamanisha mbele ya macho Yetu Ili tuzidi kutamani na kujikuta tunajiingiza kwenye mambo ambayo hayampendezi Mungu...ambayo mstari wa pili unayataja..๐
[2]Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi!
[3]Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.
((ANDIKO LINASEMA TUNAOMBA VIBAYA..KWANINI??
JIBU::๐
๐Wapendwa wengi wa leo hatusomi Neno la Mungu,, hivyo hatuna hata maneno mazuri yakumwambia Mungu,,na zaidi wengi wetu...tumejikuta tumeingia kwenye wimbi la watu,wavivu wa Kila kitu,wavivu wa kusoma neno..wavivu wa maombi...wanaopenda shortcut.. Tunapenda kuambiwa POKEA FEDHA,POKEA NYUMBA,POKEA GARI na kadhalika and SHOUT AMEN..sad indeed..
my friend...Mungu hatendi kazi ivyo""
...NENO LINASEMA...๐
Mithali 8:10-11
[10]Pokea mafundisho yangu, wala si fedha,
Na maarifa kuliko dhahabu safi.
((BWANA WA MAJESHI Anasema pokea mafundisho si fedha...na Tena maarifa kuliko dhahabu safi...ivi unaelewa..na Tena mstari wa kumi na Moja anasema..๐
[11]Maana hekima ni bora kuliko marijani;
Wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo.
(Anasema..hekima ni Bora kuliko marijani na vyote vinavyotamanika havilingani nayo..."
..Ni ivi wengi wetu hatupati tunavyovitaka kwa sababu neno la Mungu halikai ndani yetu..maana Kwa Neno Mungu alifanya mbingu na nchi...Wala haisemi kwa dhahabu Wala kwa fedh Bali kwa Neno Mungu alifanya mbingu na nchi na , alifanya vyote Hadi Nuru,na Kila mmea.na Kila ndege na Kila mnyama..๐
Yohana 1:1,3
[1]Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
[3]Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
((kwahiyo Ili upate unavyovitaka kwanza lazima Neno la Mungu likae ndani yako..maana Hilo ndilo uumbaji..ili k**a ni Baraka ujitamkie mwenyewe..
โโKwahiyo NENO LA MUNGU ndio ufunguo wa baraka zako na maombi Yako...na ndilo njia ya kupata majibu ya maombi Yako,na ndio Lina Siri ya utajiri unaoutafta..Yesu Anasema..
Yohana 15:7
[7]Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
โโSWALI SASA,,MANENO YA MUNGU YANAKAAJE NDANI YETU...??
Jibu ndilo Hilo Mithali 8:10-11...tunalipokea kwa kusoma Biblia...tulipokea kwa kufundishwa na watumishi wanaofundisha Kweli ya MUNGU...ndipo saa likifanya makao ndani yetu ..tukiomba chochote tunapata na kujibiwa maombi yetu...BIBLIA HAISEMI tukitamkiwa pokea..gari au fedha...Bali tukilipokea hili neno nalikikaa ndani yetu na tukiomba lolote tutatendewa...
๐Kwahiyo unaporuhusu neno la MUNGU likae ndani Yako..wewe si maskini,, kwasababu una nguvu yakuomba lolote na likawa.. kwasababu ya utajiri unaokuwa nao kiroho..
KWA UFAFANUZI ZAIDI NGOJA TUANZIE HAPA...MUNGU AKUSAIDIE UFAHAMU WAKO UFUNGUKE...
Yesu hakuwa na gari,hakuwa na nyumba..hakuwa na fedha..hakuwa na chochote ila kiuhalisia alikuwa tajiri,kwasababu vitu vyote vilikuwa chini yake,maana alisha ahidiwa na Baba yake anavyomtuma kuwa ukifanya hivi itakuwa ivo,kwahiyo alichokifanya nikushika maneno tu kuyaweka ndani yake,,
Yohana 6:57
[57]K**a vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi.
((k**a atakuwa hai kwa yeye...means atafanya yote yesu aliyo yafanya..na atetembea katika mtembeo wa Yesu..
Tena Paulo anasema juu ya utajiri wa Yesu๐
2 Wakorintho 8:9
[9]Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
..๐น Miujiza kadhaa aliyoifanya inathibitisha utajiri wake unamuona Kuna mahali aligeuza maji kuwa divai,aliwahi lisha watu zaidi ya 5000..aliwahi tuma wanafunzi wake kumletea mwanakondoo wa mtu hawamjuhi..lakini walimletea...kwanini vyote vilikuwa chini yake..na ndiyo maana yote haya yaliwezekanika...na ni kwasababu yeye aliyaweka maneno ya Baba yake ndani yake...ndio maana Kila alichokuwa anakiomba kilikuwa kinatokea...na kinakuwa.. shortly..unapoweka UHUSIANO mzuri na Mungu...wewe unakuwa juu ya vyote na unakuwa na amri na vyote...
JE SISI TUNAKUWAJE MATAJIRI KATIKA YESU..??
ukweli ni kwamba tunakuwa matajiri katika Yesu pale tu tunapopokea mafundisho yake...na maarifa yake...maana hivi viwili ukivipata ni umepata zaidi ya mwenye dhahabu na fedha..na zaidi hekima yake inapita vyote.."..unafanyika mkuu juu ya vyote..
โโNa hivi vyote tunavipata tunapokuwa wasomaji wa Neno la Mungu...ndipo tunapokea maarifa ya Mungu na hekima ya Mungu...na si kwa kuambiwa Pokea sijui Nini,, and Shout Amen๐๐ okay" sisemi ni sahihi ah sahihi hasha! Mungu ndiye anajua...ila Mimi natamani Wana wa Mungu tuwe na wingi wa Neno la Mungu ndani Yetu...tupokee maarifa yake,hekima yake..na mafundisho yake yakae ndani yetu,tusiwe wavivu katika kumtafta MUNGU ALYE HAI ILI TUJIOMBEE WENYEWE TUSISUBIRI KILA KITU TUTAMKIWE NA WACHUNGAJI WETU...""" โโMaana unaweza tamkiwa Neno la Imani...lakini k**a Neno la Mungu halimo ndani Yako...Hilo neno litapulizwa na upepo((wengi mmetamkiwa maneno ya imani..wengu mmetumia mafuta..majibga upako..ukweli wake..MUNGU ndiye anajua,lakini katika kutumia Kuna wengi wenu,Imani yenu imetumbishwa na upepo juu ya hivyo vitu..baada ya kukutana na watu wanaosema ni uchawi..,sijui uongo..unazani ni kwanini mnayumbishwa kirahisi ni kwasababu Imani yetu juu ya kristo tunaipata Kwa Neno lake KRISTO na injili ya kweli.."" k**a Kuna ukweli juu ya maji ya upako namafuta...basi Imani Yako ijengwe na Neno la Mungu na sio propaganda za Binadamu.
..Lah! Imani Yako itakuwa ni ya mashaka ambayo haitakuzalia matunda ...
โโTena natamani ujue hili ukweli injili ya Leo,Ina magugu mengi yaani watumishi wengi wamejiingiza K**a watumishi wa MUNGU..Bali wanatafuta faida zao...na tusipokuwa wasomaji wa neno la MUNGU,tutapotea pamoja nao...๐
Yeremia 23:1-2
[1]Ole wao wachungaji, wanaoharibu kondoo za malisho yangu na kuwatawanya! Asema BWANA.
[2]Kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, juu ya wachungaji wanaowalisha watu wangu, Mmetawanya kundi langu, na kuwafukuza, wala hamkwenda kuwatazama; angalieni, nitawapatiliza uovu wa matendo yenu, asema BWANA.
OMBI LANGU KWAKO, JIFUNZE KUSOMA NENO LA MUNGU ILI LIKUPE MUONGOZO NAMNA YA KUISHI NA KUFIKIA NDOTO ZAKO.
BARIKIWA๐๐๐.