25/11/2024
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII ATEMBELEA KITUO CHA MAFUNZO YA MISITU NA VIWANDA VYA MISITU (FWITC)
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) leo Novemba 25, 2024 ametembelea Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Viwanda vya Misitu Mafinga (FWITC) kwa lengo la kukagua shughuli zinazofanyika hapa Kituoni.
Mhe. Chana amezungumza na wanafunzi wanaosoma fani ya Misitu na Viwanda vya Misitu ngazi ya VET level I ,II & III na kuwataka wasome kwa bidii ili kuweza kuwa wahifadhi wazalendo pamoja na kuongeza thamani kwenye mnyororo wa mazao ya misitu.
Mhe. Chana pia amepata nafasi ya kukagua shughuli zinazofanyika kwenye karakana ya kutengeneza samani na kupongeza uongozi wa Kituo kwa kuzalisha samani bora na za kisasa.