Vitoni emilyo Pamagila

Vitoni emilyo Pamagila all freind of me are gathered

I have reached 100 followers! Thank you for your continued support. I could not have done it without each of you. 🙏🤗🎉
14/05/2023

I have reached 100 followers! Thank you for your continued support. I could not have done it without each of you. 🙏🤗🎉

05/03/2023
14/02/2023

Happy valentine kwa nyote

Epuka
31/03/2020

Epuka

26/01/2020

Congratulation for engagement .

30/11/2016

MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI

✍🏽Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa.

👉🏾Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa

🙇🏽📚 Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi 🏡 na 🚗 🚙magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!)

👉🏾Wapo 🙇🏽📚wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana

👉🏾Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga

Hii inachangiwa na mambo mawili:-
👇🏽
I. Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli

👉🏾Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio

👉🏾Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa!

🙇🏽📚Wasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika
👇🏾
II. Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani!

👉🏾Katika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha.

✋🏾Huwezi kufika mbali kiuchumi k**a utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!

🤔Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninakwambia: K**a ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani

🛣Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti

😎Ukitaka kufanikiwa ungana na waliofanikiwa wakuelekeze

😀🙏🏽 Hii habari haitaki hasira, vumilia tu na jiongeze

19/10/2016

JPM AMPONGEZA MRISHO GAMBO KWA KUFANYA VURUGU ARUSHA.

Katika hali ya kushangaza Rais JPM amempongeza Mkuu wa mkoa wa Arusha kwa kitendo alichokifanya jana cha kuvuruga sherehe za uzinduzi na uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa hospitali ya kina mama inayofadhiliwa na Martenity Africa chini ya uratibu wa Mbunge wa Arusha mjini Mhe.Godbless Lema na taasisi ya ArDF.

Kutokana na tukio hilo watu wengi walitegemea Rais angetengua uteuzi wa Gambo lakini badala yake amempongeza na kumwambia kuwa bado ana imani kubwa ya yeye.

Akizungumza jioni ya leo kwa kujitapa, Mku huyo wa mkoa amesema kuwa alipigiwa simu nyingi sana kutoka kwa watu mbalimbali wakihofu kuwa ametenguliwa, lakini baada ya muda akapokea simu kutoka kwa Rais Magufuli akimpongeza kwa kazi nzuri aliyofanya na kumwambia kuwa bado ana "full confidence" na yeye.

*BREAKING NEWS**TCU IMETANGAZA SIFA MPYA ZA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU 2016/2017**TCU IMETANGAZA RASMI KUSHUSHA SIFA ZA KUJI...
16/09/2016

*BREAKING NEWS*

*TCU IMETANGAZA SIFA MPYA ZA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU 2016/2017*

*TCU IMETANGAZA RASMI KUSHUSHA SIFA ZA KUJIUNGA NA DIGRII 2016/2017*

*HII NI KWA WANAFUNZI WENYE DIPLOMA KWENDA DIGRII*

*MAAMUZI HAYA YAMETOLEWA LEO NA TCU,KUTOKANA VIGEZO KUWA JUU SANA*

*KUJUA SIFA MPYA ZA KUJIUNGA CHUO KIKUU 2016/17*

*SHARE KWA WENZAKO*

*MASWAYETU BLOG,TUNAKUPENDA SANA*

>>>>> www.maswayetublog.com/2016/09/breaking-newstcu-imeshusha-sifa-za.html

 

31/08/2016

KAULI 10 NZITO ZA MHE.MBOWE KUHAILISHA UKUTA.

1.“Tunajua uamuzi huu utawaumiza sana wafuasi wetu, na uamuzi huu umeniumiza sana hata mimi mwenyewe, lakini ni nani miongoni mwa viongozi wetu na wanachama wetu ambaye anaweza kuombwa kuahirisha jambo na viongozi wa madhebu na dini zote hapa nchini na akawakatalia?”

2.“Polisi na Serikali wajue kuwa, hatuahirishi maandamano na mikutano yetu kwa sababu ya mazoezi, risasi au mabomu ya polisi. Hatuahirishi kwasababu ya usafi wao, wanaofanya kesho na wala hatuahirishi kwasababu ya ndege za kijeshi zinazoruka, ila tumeamua kuwaheshimu viongozi wetu dini.”

3.“Tunawaomba wanachama wetu, wapenzi wetu na wapenda demokrasia kote nchini watusamehe na wakubali kuwapa viongozi wa dini hizi wiki tatu, watafute suluhu kwa kuonana na Rais na ikishindikana, hatutarudi nyuma. Tutaingia barabarani.”

4.“Tangu tulipotangaza operesheni Ukuta, jumla ya wanachama na viongozi wetu 230 katika maeneo mbalimbali wamek**atwa na kush*takiwa kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo uchochezi na jumla ya viongozi na wanachama wetu 28 wapo rumande mpaka sasa pasipo sababu za msingi.”

5.“Haikuwa rahisi sisi kufikia uamuzi huu, hatukuwa tayari kurudi nyuma. Lakini viongozi wa dini na taasisi zinazoheshimika hapa nchini wametusihi. Mpaka Mama Maria Nyerere ameongea na Mheshimiwa Lowassa na kutuomba tuahirishe ili watafute suluhu ya suala hili.”

6.“Hatuogopi mabomu wala risasi za polisi, tuna uwezo wa kuandamana kwasababu tunazo mbinu za kufanikisha mipango yetu. Juzi polisi walituk**ata na kuzuia kikao cha K**ati Kuu ila jana tumekifanya na wala hawajui tumefanyia wapi na saa ngapi.”

7.“Wakati tukifanya harakati hizi, tunaendelea pia kufungua kesi sehemu mbalimbali. Tundu Lissu na jopo lake tayari wameandaa mash*taka 15 ili tuweze kuyafungua katika mahak**a zetu hapa nchini. Tutadai haki mahak**ani na tutaidai barabarani.”

8.“Inasikitisha sana kuona taifa lina rais anayeomba watu wamuombee kila siku, ‘Niombeeni jamani’, lakini amekuwa akijaribu kuwakwepa viongozi wa dini kila wanapotaka kumuona ili kuzungumza naye kuhusu amri haramu ya kuzuia mikutano ya hadhara.”

9.“Viongozi wa dini walituomba wiki mbili au tatu ili wafanye mazungumzo na Rais Magufuli, sisi tumewapa mwezi mzima kabisa, ili wasake suluhu ili sisi k**a vyama vya siasa tupewe haki yetu ya kisheria na kikatiba. Ikishindikana hakika sisi hatutarudi nyuma.

10.“Salum Mwalimu bado yupo rumande kwasababu za hovyo, Polisi wamekataa kumpeleka mahak**ani leo wanadai wapo ‘busy’ eti wanazuia maandamano ya UVCCM, yalipangwa kufanyika leo. Sisi wote ni wafungwa watarajiwa lakini hatutarudi nyuma.

31/08/2016

Kuchelewa kwa ajira kunavyoumiza walimu.

NA RUSTON MSANGI.

Kada ya ualimu ndiyo yenye watumishi wengi nchini kuliko kada yoyote ile.
Licha ya kada hii kuwa na watumishi wengi,takwimu zinaonesha bado kuna upungufu wa walimu nchini hasa walimu wa sayansi . Waziri mwenye dhamana ya elimu,Profesa Joyce Ndalichako akijibu swali katika kikao cha bunge kilichopita, alibainisha upungufu wa walimu wa Sayansi 22,460.

Miaka kadhaa iliyopita,watu wengi wamepata hamasa ya kusomea fani ya ualimu ili waajiriwe na serikali.Hakika walimu wamekuwa wakiajiriwa moja kwa moja katika shule katika shule za msingi na sekondari na vyuo .

Walimu wamekuwa wakiajiriwa kwa vipindi tofauti mara wa wanapohitimu.
Kwa mfano, walimu waliohitimu mwaka 2012 walipangiwa vituo vya kazi mwezi Februari 2013. Waliohitimu mwaka 2013 walipangiwa mwezi Machi 2014 na waliomaliza mwaka 2014 walipangiwa mwezi wa tano 2015.

Lakini mamia ya walimu waliohitimu mwaka 2015 ,hawajaajiriwa,wanaendelea kusota mitaani.Kuchelewa sana kwa ajira za ualimu kumekithiri katika utawala huu wa awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.

Walimu waliohitimu mwaka 2015,wako mtaani bila ajira kwa zaidi ya mwaka sasa. Hawaijui kesho yao. Mamia ya walimu wengine waliohitimu mwaka huu 2016,wanaungana na wenzao kusota mitaani bila ajira.

Inadaiwa kuwa jumla ya wahitimu wa 2015 na 2016 ni zaidi ya walimu elfu sitini nchini .Makadirio haya yanajumuisha wahitimu ngazi ya cheti, stashahada na shahada.Hawa wote walikuwa wanasubiri ajira zilizositishwa na serikali.

Serikali ilisitisha ajira zote za serikali ikiwemo walimu, kwa lengo la kuhakiki watumishi umma ili kubaini watumishi hewa, mishahara hewa na watumishi wasio na sifa.

Lengo la serikali ni zuri, na kila mwenye mapenzi mema na Tanzania ataunga mkono hili la kupambana watumishi na Mishahara hewa.

Pamoja na nia hiyo njema, tatizo linaonekana katika njia ya kufanikisha na kufikia lengo hilo.Kadhalika ,tatizo ni namna zoezi hili linavyozidi kuchelewa , linaleta madhara katika elimu yetu ya leo na huko baadae.Inaathiri uchumi wa wahitimu wenye sifa ya kuajiriwa.

Hivyo ajira za walimu kuzidi kuchelewa kutokana na uhakiki, kunaweza kuleta madhara yafuatayo:

Mosi, Kupoteza weledi wa walimu. K**a ilivyo kwa taaluma nyingine ulimwenguni, namna unavyokaa muda mrefu bila kufanyia kazi ndivyo ambavyo utaalamu hupotea siku hadi siku.

Kwa walimu hawa waliosomeshwa kwa pesa za watanzania masikini za mkopo na wazazi, utaalamu wao unazidi kupotea kiasi kwamba hata akija kupata hiyo ajira kuna vitu muhimu vitakosekana kwao.

Pili, Kuongeza zaidi tatizo la ajira nchini. Hii inasababishwa na hali ya mrundikano mkubwa wa vijana wasio na ajira kutokana na kwamba kundi kubwa kutoka vyuoni, lipo mtaani bila shughuli rasmi ya kufanya, k**a ajira hakuna hata uchumi utatetereka.

Tatu, Kusabanisha familia za wahusika kuishi katika mazingira magumu maradufu. Familia nyingi hutumia rasilimali zao kuwekeza kwenye elimu ya vijana wao, ikiwemo kuuza mashamba na kufanya biashara, kwa matarajio kwamba wakihitimu na kupata ajira mambo yatakuwa mazuri, lakini hali ikiwa tofauti k**a hivi familia za wahusika huishi kwa dhiki sana.

Nne, Inaweza kuwa sababu ya walimu wengi kwa kipindi hiki kuamua kuachana kabisa na ualimu kwa kwa maana ya kufundisha , Na kuamua kufanya shinguli nyingine binafsi au kwenye mashirika mbalimbali. Hii sio dalili nzuri.

Tano, Hali hii ikiendelea hivi itasababisha walimu wengi wenye weledi wa kutosha kuamua kufanya kazi na shule za binafsi, kuna walimu wengi wamesita kusaini mikataba shule binafsi, lakini hali ikiendelea hivi wengi watamwaga wino kusaini mikatana shule binafsi.Shule za serikali zitaendelea kuwa na uhaba wa walimu.

Sita, Husababisha kuwanyima haki wanafunzi ya kufundishwa kwa kuwa na walimu waliopo kwenye ajira hawatoshi kukidhi mahitaji.

Saba, Kusababisha migogoro isiyo ya lazima baina ya walimu wanaosubiri ajira dhidi ya serikali.

Kwa madhara haya yanayotokea na yanayoandaliwa kutokea zaidi, ni vizuri Serikali, wahitimu na CWT kufanyia kazi yafuatayo:

Mosi, Serikali ifanye juu chini iajiri walimu hawa katika mfumo mpya hata k**a zoezi la uhakiki halijaisha, hii inawezekana kwa kuwa uhakiki unawahusu watumishi waliopo kazini, hivyo ajira mpya inaweza kuendelea kwa utaratibu wao mpya ambao hautaleta usumbufu wala kuathiri zoezi hilo.

Pili, Serikali kupitia wizara ya elimu kwa kushirikiana na taasisi za elimu nchini ihakikishe inaanda mfumo maalumu utakaowawezesha wahitimu wote ikiwemo walimu, kuwa na ujuzi ambao hautategemea sana ajira ili kuendesha maisha, Hii itapunguza mzigo kwa serikali juu ya kutoa ajira kwa wahitimu wengi.

Tatu, Chama cha walimu Tanzania( CWT), kiunde mfumo maalumu utakaosaidia kushughulika na walimu wanaosubiri ajira. Walimu hawa wamekuwa k**a yatima na wanyonge hawana Msemaji wala mtetezi.Viongoz wa CWT wanadaiwa kuwa walaji tu wa posho zinatokana na makato kwenye mishahara ya walimu.

Nne, Walimu wanaosubiri ajira kutafuta fursa zingine. Hii itasaidia sana kuendesha maisha yetu ya kila siku bila kutegemea ajira ya serikali wala yeyote yule. Kwa kuwa likijitokeza tatizo k**a hili mambo yote yanasimama.

Yakifanyika haya na mengine ambayo wahanga wamekuwa wakipaza sauti zao kuyasema kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari ,itasaidia sana.

Sisi k**a watanzania wenye nia njema na tunaopenda taifa liwe na nidhamu ya utumishi wa umma, tunaunga mkono uhakiki kufanyika .Tunasisitiza zoezi hili kuendelea kwa kufauata kanuni, sheria na taratibu za nchi. Lakini isiwe sababu ya walimu kuteseka kutokana na kuchelewa kwa ajira.

Mwandishi ni mchambuzi wa masuala ya Elimu.
Namba yake ya simu:0684 731516
Barua pepe:[email protected]

30/08/2016

Mh naibu Katibu Mkuu
Na wanachamaaa 18 wanyimwa dhamaanaa Mkoani Simiyu leo

Haki huchelewa tu.

Address

Kiomboi
Kiomboi

Telephone

+255765318688

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Vitoni emilyo Pamagila posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Vitoni emilyo Pamagila:

Shortcuts

Share

Category