New kiomboi Secondary School

New kiomboi Secondary School Ukurasa huu unawahusu wanafunzi waliosoma shule ya Sekondari New Kiomboi. lengo la ukurasa huu nikup

Vijana wenzangu wa Mkoa wa SingidaJeshi la Kujenga Taifa kupitia Ofisi ya Mshauri wa Jeshi la Akiba Mkoa wa Singida imet...
26/08/2022

Vijana wenzangu wa Mkoa wa Singida

Jeshi la Kujenga Taifa kupitia
Ofisi ya Mshauri wa Jeshi la Akiba Mkoa wa Singida imetoa nafasi za JKT kwa Vijana 315 ndani ya Mkoa wa Singida kwa Vijana wenye Elimu kuanzia Darasa la Saba hadi Shahada na Wenye Vipaji Maalumu.

Singida Manispaa 63
Manyoni 63
Iramba 63
Mkalama 63
Ikungi 63

Hivyo Vijana wenye sifa waombe kupitia Washauri wa Jeshi la Akiba katika Wilaya aliyopo.

NB.Mkoa hauna nafasi kwa ajira ya Vijana.

By Frederick Joseph Ndahani
Afisa maendeleo Vijana Mkoa wa Singida.

Kazi iendelee

06/02/2021

Uzuri wa mtu ni katika mambo matatu.

1. Kuficha ufukara wake mpaka watu wakadhania kwamba ni tajiri.
2. Kuficha hasira zake mpaka watu wakadhania kwamba hakasiriki.
3. Kuficha shida zake mpaka watu wakadhania kwamba siku zote huwa katika neema.

Siku zote kumbuka kwamba ni vyema kujizuia yafuatayo:

1. Kuzungumzia uwezo wako mbele ya dhaifu.
2. Kuzungumzia furaha yako mbele ya wenye huzuni.
3. Kuzungumzia uhuru wako mbele ya wafungwa.
4. Kuzungumzia uzazi wako mbele ya wagumba/matasa.
5. Kuzungumzia wazazi wako mbele ya mayatima.

Pia jitahidi sana:

1. Kutoandika ila jambo la heri
2. Kusema ila jambo la heri
3. Kutodhamiria ila jambo la heri.
4. Kutotamani kwa mwenzako ila jambo la heri.

“Maisha ni Mazuri sana ukiwa Mzuri”.

17/01/2021

*Matokeo ya Kidato Cha nne shule za sekondari wilaya ya Iramba
Jumla ya shule 23

*Ruruma Sec. School*
Div 1- 0
Div 2-1
Div 3-0
Div 4-19
Div 0-7
*Mtoa sec School*
Div 1-1
Div 2- 5
Div 3-9
Div 4- 28
Div 0-5
*Mtekente Sec school*
Div 1-1
Div 2-4
Div 3-4
Div 4-20
Div 0-5
*Tumaini sec school*
Div 1-24
Div 2-18
Div 3-12
Div 4-14
Div 0-0
*Lulumba sec School*
Div 1-21
Div2-21
Div3-25
Div 4-26
Div0-1
*Shelui sec school*
Div 1-5
Div 2-15
DDiv0-1Div4-71
Div 0-7
*Kisiriri sec school*
Div 1-0
Div2-2
Div 3- 3
Div 4-31
Div0-7
*New kiomboi sec*
Div 1-2
Div 2-5
Div 3-17
Div4-72
Div 0-22
*Urughu sec schoo
Div1-2
Div2-;5
Div3-5
Div4-21
Div0-15
*Kaselya sec school*
Div 1-0
Div2-5
Div3-9
Div 4-43
Div0- 2.
*Ntwike Sec School*
Div 1-0
Div 2-4
Div3-7
Div 4-47
Div 0-12
*Ushora sec school*
Div1-0
Div2-9
Div 3-13
Div4-37
Div0-7
*Mukulu sec school*
Div 1-2
Div2-4
Div3-2
Div4-39
Div0-3
*Tulya Sec school*
Div1-1
Div2-6
Div3-9
Div4-45
Div0-7.
*Mgongo sec school*
Div1-0
Div2-4
Div3-8
Div4-35
Div0-9
*Kinambeu sec school*
Div1-6
Div2-29
Div3-31
Div4-55
Div0-0
*Kidaru sec school*
Div1-3
Div2-10
Div3-16
Div4-25
Div0-2
*Kisana sec school*
Div 1-0
Div2-3
Div3-6
Div4-16
Div0-1
*Ndago sec school*
Div1-2
Div2-5
Div3-7
Div4-20
Div0-0
*Mbelekese sec School*
Div1-9
Div2-9
Div3-21
Div4-45
Div0-3
*Kyengege sec school*
Div 1-12
Div2-11
Div3-24
Div4-37
Div0-7
*Kizaga sec school*
Div1-2
Div2-11
Div3-18
Div4-78
Div0-8
*Kinampanda sec school*
Div 1-0
Div2-9
Div 3-18
Div4-76
Div0-13.

10/01/2021

'Hakuna kipindi kigumu katika maisha k**a pale unapokuwa kwenye shida peke yako.Wakati ambao changamoto zinakuzonga,wakati ambao shida hutawala,wakati ambao shida huwa ndugu yako. Lakini nyakati hizi huwa muhimu kutambua wale watu muhimu unaopaswa kuwa nao katika nyakati tofauti tofauti za jua na mvua'

05/01/2021

USAJILI WA WATAHINIWA WA KUJITEGEMEA WA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) NA MAARIFA (QT) 2021 UMEANZA TAREHE 1 JANUARI NA UTAFUNGWA TAREHE 28 FEBRUARI 2021

04/01/2021

IKO WAPI ZAMANI?

✏ Zamani nyumba zetu zilikuwa na vyumba vichache na sehemu ya kukaa tu, tunakutana ndugu, jamaa na majirani.

✏ Lakini leo nyumba zetu kubwa na zina vyumba vingi, isipokuwa hazina watu ila ardhi na kuta tu.

✏ Huyu kasafiri na yule kajilipuwa nchi nyingine, huyu kakasirika haongei na mtu na mwingine yupo hoi na Dunia.

✏ Zamani chakula chetu ni wali, mihogo, ndizi, magimbi, dagaa, au ugali kwa Mchicha.

✏ Tunatandika mkeka au jamvi chini na tunakula sahani moja sote, tunacheka kwa furaha mpaka jirani wanatusikia.

✏ Lakini leo hii sufuria au hotpot imejaa nyama, kuku na minofu ya samaki na kila mmoja na sahani yake ya aina tofauti .

✏ Basi mnakaa sehemu zipo tupu, unatamani ndugu au jirani wawepo, wazibe hilo pengo.

✏ Zamani tunakaa uwani na babu, anatuhadithia hadithi, tunakunywa chai kwa upendo na kucheka kwa pamoja kwa tabasamu mpaka meno yetu yanaonekana.

✏ Na leo kukaa kwetu ni kwenye simu za mkononi, internet na kuchat tu kwenye whatsApp,Imo, instagram, facebook na mitandao mingine ya kijamii, tumekuwa tupo kwingine kabisa.

✏ Zamani tunauliziana, kujuliana hali, kutembeleana, na tunakutana kwa furaha na kukumbatiana.

✏ Leo ni sikukuu mpaka sikukuu au harusi hadi harusi au mpaka kuwe na maziko ndiyo tunatembeleana au kuonana tena kwa kujilazimisha, hata salaam ya mungu hatusalimiani, na kukaa kwetu kwa mioyo ya moto.

✏ Zamani mtu akiumwa kati yetu, tunakusanyika ndugu na majirani.

✏ Leo ndugu hakujali, hana muda na wewe na anakuambia niwahi mimi taabani hoi.

✏ Zamani ilikua ndugu anamuenzi ndugu yake na dada yake, kwa kila alichonacho hata k**a kachoka au ana stress.

✏ Leo unamkuta mtu hapati kula na ndugu yake yupo kazama katika neema, anajifanya kakasirika kwa sababu za kijinga, na kukata mawasiliano kwa miaka.

✏ Leo pesa inabadili nafsi ya mtu, hajali ndugu wala jirani, utu unapotea anasahau k**a kuna kufa au Dunia ina mwisho .

✏ Mpo wapi watu wa zamani mje muone vipi mioyo ilivyo kati ya ndugu leo hii..!!

✏ Miaka na siku hazirudi nyuma, tenda wema uende zako usingoje shukrani.

✏ Unasaidia ndugu au mtu shukrani yake katika ulimi tu, lakini moyoni mwake kuna moto anasahau ihsani na kukusema kwa vibaya mno.

✏ Hamna tena undugu wa kuwakusanya pamoja k**a zamani, hamna mapenzi na upendo ndani ya mioyo, (hata heshima kwa mkubwa k**a zamani hamna).

✏ Iko wapi zamani? Mola awarehemu wa zamani waliotangulia.
Mola atujaaliye tuwe wenye kupendana na kushik**ana kwa kila hali k**a ilivyokuwa zamani.

UMOJA WETU NDIYO UNDUGU WETU...na kijana Wa mwanza

Tuwe na siku iliyonjema kwenu nyoote 🙏🏿🙏🏿

29/12/2020

SIO KILA KIZURI LAZIMA KIWE CHAKO.

"Ndugu yangu sio kila kizuri lazima ukimiliki au uwe nacho ! Vingine havikufai kutokana na mfumo wa maisha yako uliochagua au unaoishi ..Iwapo ukilazimisha kuwa navyo vitakuharibia maisha na kuwa vichungu na vibaya kwako wakati mwanzo ulivifurahia kwa uzuri na utamu wake ,wakati unajua Sio vyako. ."Naomba utambue Hata Vitu Vizuri uvionavyo vina madhara Ikiwa hukustahili kuwa navyo na Sio hitaji lako!!

_Elimika! Badilika. Nufaika!_

28/12/2020

JIBU LAKO LISIWE HAPANA

K**a unataka uwe mtu ambaye haupotezi
mwelekeo kirahisi basi kila wakati jilazimishe na
kuwaza kuhusiana na malengo yako, ndoto
zako na kwenye hatima yako mbele ambako
unaelekea.

Jambo jingine ni uwezo wako wa kusema
HAPANA.Siku moja Steve Jobs mwanzilishi
wa kampuni ya kutengeneza vifaa vya
elektroniki ya apple alipoulizwa njia ya
iliyomsaidia kufikia malengo yake ni ipi
alijibu-“Ni uwezo wangu wa kusema
hapana”.Watu wengi sana wamepotezwa
mwelekeo wa maisha yao kwa sababu ya
kushindwa kabisa kusema hapana kila
inapobidi.Hii ndio maana watu wengi sana
wamepoteza muda wao kwa mambo ambayo
hayachangii kabisa katika maisha yao na
katika malengo yao
Hata hivi leo kuna watu wengi watakuambia
vitu ambavyo kwa hakika unajua havikusaidii
chochote ila kwa uoga wa kukataa utajikuta
umekubaliana nao na mwishoni unakuja
kujilaumu. Ni lazima uwe mtu ambaye una
ujasiri wa kukataa mambo amabyo hayana
msaaada katika malengo yako makubwa.
Muda wako wa kuishi duniani ukipotea basi
ujue hauwezi kabisa kuurudisha tena, hivyo ni
lazima uamue kuutumia kufanya mambo ya
msingi tu. Kumbuka kuwa hauwezi kuhudhuria
kila kikao, hauwezi kuwa kwenye kila group la
watsapp, hauwezi kumpendezesha kila
mtu, hauwezi kwenda kwenye kila mtoko
unaoalikwa-Kila wakati jiulize, hili lina
umuhimu?K**a halina umuhimu usiogope
kusema HAPANA.
Kuanzia leo, uwe mtu mwenye ujasiri wa
kusema HAPANA kwa kila kitu ambacho
unaona kinakuondolea mweleko uliioukusudia
katika maisha yako.

13/12/2020

Karibuni kwenye ukurasa huu.

Address

Kiomboi
Kiomboi
43301

Opening Hours

Monday 00:00 - 17:00
Tuesday 00:00 - 17:00
Wednesday 00:00 - 05:00
Thursday 00:00 - 17:00
Friday 00:00 - 14:00
Saturday 10:00 - 14:15

Telephone

+255765318688

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when New kiomboi Secondary School posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to New kiomboi Secondary School:

Shortcuts

Share

Category