Rap Ghetto - Concious

Rap Ghetto - Concious We gonna discuss and make decisions here and come up with a plan about what decided..

HIP HOP platform for the rap ghetto conscious members, we gonna discuss and make decisions here and come up with a plan about what decided.. the main objective of this group is to maintain the legacy of the rap ghetto conscious formed about 5 years ago��

Mpira unaenda Kasi tofauti na ww unaepata nafasi ya kuutazama kwenye video ya marudio Goli kipa anauona kwa mara moja tu...
23/05/2026

Mpira unaenda Kasi tofauti na ww unaepata nafasi ya kuutazama kwenye video ya marudio
Goli kipa anauona kwa mara moja tu Mpira ukiwa ushafika golini ukiwa na Kasi

Magoli hayo wamefungwa makipa wengi tu na huwa hawaruki wanabaki wamesimama tu
Nenda katazame marudio ya mechi ya Astonvilla vs Man U anafungwa Same Lames hakujishughulisha kabisa amefungwa Donnaruma na Bournemouth hakujishughulisha kabisa nyinyi mnataka mtu aonyeshe reaction ya kufuata Mpira wakati ushampita si kichekesho hicho

Mpira aliyepiga Okello ni K**a Kuna deflection au mzungusho nyuma ya ukuta ambao pia ulipoteza uelekeo wa Mpira na kumuadaa goli kipa

Tatizo mnauchukulia Mpira K**a mnavoutazama kwenye tv au kuhadithiana vijiweni ila K**a umecheza Mpira hata Chandimu tu utaelewa Kuna mipira ukiuzwa husumbuki unaganda K**a Sanamu

Aziz K aliwafunga mabao ya kudundisha Mpira watu wakaona K**a makipa wamepangwa alivoanza kuwafunga na wa kimataifa ndo watu wakaelewa
Mpira ni mchezo wa wazi tuache siasa
K**a wamefix mechi labda upande wa wachezaji wa ndani lakini hakuna goli la kumlaumu kipa hapo
Msiendeshwe na ushabiki wa kipumbavu mnamchafua goli kipa Ile ni kazi yake

Wachezaji wanajitoa maisha yao kutuburudisha ila sisi tunawavunja moyo tunawaumiza tunawaharibia mkate wao hususani hawa wazawa
Angefungwa DIARA au KASARI tungekaa kimya

Unajua Game ni vita alafu nyuma Kuna watu wenye akili mno.‎Mwanzo nilianza kuelewa ila hii spidi me inanipa mashaka zaid...
09/05/2026

Unajua Game ni vita alafu nyuma Kuna watu wenye akili mno.
‎Mwanzo nilianza kuelewa ila hii spidi me inanipa mashaka zaidi upo na sisi au umetoka kuja kufifisha kinachoendelea kwa Sasa

‎Nimeona watu wengi mashuhuri K**a BABU TALE n.k. wameguswa na ulichokifanya ,that's good

‎Ni kweli mullaobo ameibuka katika kipindi ambacho Mr Hip hop anarudisha regime yake, ubabe wake, na kuonyesha ukuu wake katika kulezea hisia za watu na taswira ya mitaa

‎Umekuja wakati ambao Niki Mbishi anaonekana makucha yake na vifaranga vya kuku ndo vinaaza kutoka nje

‎Ule wakati ambao mvutano wa miaka mingi umekwisha miongoni mwa makundi ya Hiphop, Tamaduni Muziki ikiwa na makomandoo K**a Niki Mbishi ,One ,Songa ,Pmawenge ,Stereo ndani ya ASHOKI moja na Nako 2 Nako na Weusi ikiwa na Joh makini,Niki wa pili ,lordeyes ,Gnako kuelekea kumtoa hip hop katika mateka ya watu wachache wanaomfungia kwa masilahi yao
‎Ngoma ya Gnako- SAWA ni utambulisho wa sura mpya katika muziki wa hip hop

‎Shaka ya shaka nyuma ya Mullaobo Kuna nani na ujio wake unamlengo gani katika kipindi ambacho mpka comedian wamehype mziki wa rap .
‎Leo game inasikilizwa na vizaz vyote watu wamesikiliza zaid mziki wa rap kuliko mziki wowote kwa time hii

‎Je? Tuko tayari kumvisha Crown ya mitaa msanii ambaye kesho atarud kwnye aina yake ya Muziki na kutuvua nguo au kutumika,
‎Ushajiuliza , athari yake ,Mtu anafanya hip hop anapokelewa anakubalika alafu kesho anarud kwenye aina nyingine ya muziki na kuwarudisha nyuma watu wote walaioanza kuamini muziki. wa Rap kupitia alichokifanya

‎Mullaobo
‎Ni R***r mzuri anasound K**a NYANDU TOZZY lakini pia ni singer mzuri Sana ana sound K**a BELLE 9 ahhahaha

‎Dont be fake sisi tupo really ukiharibu tutasema that's Hip hop

‎Karibu kwenye game karibu kwenye shoo za hip hop
‎Tupo hapa tunasubiri next song hii kazi nzur na tumeshare
‎Keep moving kazi njema bro




Lazima ufate midundo na taratibu ukitoka nje ya hapo unarepresent aina nyingine ya muziki Sio hip hop Kwa mfano umerap k...
09/05/2026

Lazima ufate midundo na taratibu ukitoka nje ya hapo unarepresent aina nyingine ya muziki Sio hip hop
Kwa mfano umerap kwny beat ya amapiano hyo ni tafsiri ya kuwa umefanya mziki wa amapiano
Unakuwa umeshatoka kwny sifa za mziki mwingine
Yaani hauwezi ukafanya mziki wa reggae katika midundo wa singeli unakuwa umetoka kwny reggae umeingia kwny aina nyingine ya muziki
Ndo maana utaratibu upo kwa ajili ya kuulinda mziki husika
Juzi MONI CENTRAL ZONE amesema usimuite Tena hip hop ameona hatoke kwnye kifungo awe huru na mziki wowote anaohisi utakuwa sahihi kwa upande wake

09/05/2026
Nonstop Tz1.MIDUNDO Mcee hutumia midundo  ya hip hop amabayo ni bum bap beats ili kuenzi utamaduni wa hip hop katika upa...
08/05/2026

Nonstop Tz
1.MIDUNDO Mcee hutumia midundo ya hip hop amabayo ni bum bap beats ili kuenzi utamaduni wa hip hop katika upande wa kurap au kufoka foka Mcee hutumia midundo sahihi ya hip hop ambayo ni midundo ya Bum bap
2.VERSATILITY uwezo wake wa kubadilika badilika kutokana na midundo na hisia feeling zake pale anapowasilisha jumbe zake
3 .UANDISHI WA MISTARI hapa Mcee lazima azingatie upangaji wake wa vina katika ushairi wake katika hip-hop upangaji wake wa vina ni tofauti na mashairi ya waandishi wetu wa vitabu vya ushairi ama ngonjera vile vya kawaida (upangaji wake wa vina unatifautiana )
Sifa nyingine ni K**a
I.WORDPLAY uwezo wa kucheza na maneno Neno moja kuwa na maana zaidi ya moja na ufundi wa kutumia Neno moja kutoka katika sentensi moja kwenda nyingine zikiwa na tafsir tofauti
II.PUNCHLINES uwezo wake wa kuzungumzia jambo ushindwe kulielewa alafu anakuja kukupatia tafsiri katika mstari wake wa mwisho
III METAPHOR kutumia lugha za mafumbo pia kumfanya msikilizaji atafakari kile anachokizungumzia

Vipo vingi ila jambo kubwa zaidi kwa Mcee ni Misimamo wake kuhusiana na muziki anaoufanya kwa watu wake yeye amesimama katika misingi yake amabayo habadiliki kuendana na soko linavobadilika yeye. Anabaki akiamini falsafa zake na ni Mcee amabaye yuko huru hana kizuizi pale anapoifanya kazi yake mara nyingi hawategemei sana media ,Radio ,tv shows kuwapush mziki wao ili ujumbe waufikishe
Wao wanaamini katika jamii Yao ambayo ndio wanailisha kile wanachokitengeneza wao pasipokuwa na matakwa ya watu wengi nje ya jamii yako

Hawa Mceez wapo huru zaid na kazi zao ndo maana wanaitwa Underground wasanii wa chini ya andaki

Nonstop Tz haitwi Mc anaitwa MCEE huyu ni Lyricist who masters the craft live performance crowd engagement and lyrical s...
08/05/2026

Nonstop Tz haitwi Mc anaitwa MCEE huyu ni Lyricist who masters the craft live performance crowd engagement and lyrical skill
Huyu Sio tu master of ceremonies huyu ni host anasherehesha anatawala jukwaa na kufanya vitu vingi zaid

Hapa cjamshushia heshima Ney wamitego lakini najaribu kukueleweasha kujua tofauti kati ya Rappers na Mcee
Unapomtafsiri r***r K**a mwakilishi wa hip-hop badala ya Mcee
Unapotosha watu kwa sababu anaweza kuwa r***r mkali anawakilisha na kutetea jamii yake lakini hafati misingi
Tukisema tutumie Neno kutetea jamii K**a ni msingi wa kumweka katika level ya Umcee tunakosea
Kwa sababu pia na Kuna watu wanatetea jamii kwa mziki wa Haina tofauti je wakiingia kwny categori ya rap tutawaterm K**a ni wasanii wa hip hop hapana lazima tufuate taratibu

Hii hali ya kutokuzingatia taratibu mliwahi kumpa NEY WA MITEGO tuzo ya hip hop mbele ya FIDQ NA JOHMAKINI
Kwa nyimbo alioimba na diamond haikuwa sawa hapa hip-hop haikutendewa haki
MCEE ana rap anatumia midundo sahihi ya hip-hop na anaandika lyrics katika utaratibu unaotakiwa hizo zote ni kanuni ambazo Mcee anatumia katika shughuli zake za kurap

Lakini Ney wa Mitego ana nyimbo zake nyingi tu alikuwa anaimba hawezi kuwa Mcee ila ni r***r mzuri anawakilisha jamii

Nonstop Tz hapo kwa bilnas shida ilianzia alipoingia kwnye category ya msanii wa hip hop kwa sababu tunapomzungumzia msa...
07/05/2026

Nonstop Tz hapo kwa bilnas shida ilianzia alipoingia kwnye category ya msanii wa hip hop

kwa sababu tunapomzungumzia msanii wa hip hop hatumuangalii r***r tu k**a bilnass Ney wa mitego na wengine hapa category huwa inawatambua ma Mcee pekee maana hawa mbali na kurap ila wapo katika misingi utaratibu jinsi ya kurap katika hip hop huwa unafanyikaje

Kwa sababu hata wanamziki wa bendi nao wanatambulika K**a ni mar***r pia

Ili wasiwachanganye watu uelewa tuzo ya msanii wa hip hop category zilipaswa kuandaliwa na wanahip hop wenyew kwa mfano unakuwa na watu K**a profesa jay ,Hashimu Mdogo ,KBC,Zavara,jmoe nk itategemea na watu walioingia katika kugombea tuzo hiyo. Hawa wanaweza kukuletea .msanii wa hip hop kwa kufuata vigezo na ukaelewa

Pia K**a kutakuwa na tuzo kwa ajili ya wasanii K**a kina billnass ,ney wa mitego,na baadhi ya mar***r wanahitaji kuwa na category ya R***r Bora wa bongo fleva na Sio kutumia Neno MSANII BORA WA HIPHOP maana hapa ndo wanapowachanganya watu washindwe kuelewa

Nonstop Tz upo sahihi unaweza kuwa mwanahip hop hata bila ya kufanya Rap Lakini pia unaweza kuwa mwanahiphop kwa kurap l...
07/05/2026

Nonstop Tz upo sahihi unaweza kuwa mwanahip hop hata bila ya kufanya Rap
Lakini pia unaweza kuwa mwanahiphop kwa kurap lakini usiwe Mcee ni vile unaishi ki hip hop mavazi,uchoraji,djs,na kucheza vikawa ndani yako
Mfano huwezi kusema Chidbenz Sio hip hop kwa sababu hip-hop ni vile unavoishi na yumo ndani ya element nyingine za hiphop
Lakini tunamtoa katika sifa za Mcee
Rap Kila mtu anafanya ila kuwa mceez ni cheo kikubwa katika uchanaji ni umekithi vigezo na kufuata taratibu
kwa sababu Mcee ni nguzo katika Ile misingi ya hip hop tunayo pale
Na Mceez anarepresent hip hop kwa uwanja mkubwa kuliko nguzo zote kwa Sasa kwa sababu yeye ndo anajukwaa kubwa kuwafikia Hadhira (walengwa jamii yake)
Hata comedian wana rap je tuwatambue K**a ni hip hop hapana kurap Sio sababu ya kuwa mwanahip hop
Ukirap tutaangalia misingi umefuata
Na the way unavoishi ki hip hop (knowledge of culture and understanding)
Hata Darasa bado ni hip hop vile anavoishi na kurepresent katika njia nyingine K**a mavazi nk lakini hawezi kuwa Mcee
So tunapomchagua mwanahiphop kupitia rap hapa tutaangalia sifa za Mceez haijalishi nyimbo imeenda kiasi gani (utaratibu kwanza)

Nenda tazama video ya One inaitwa Incredible Ngoma moja ina nguzo Tano za hip-hop Kuna kitu utajifunza

Address

Dodoma

Telephone

+255653608714

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Rap Ghetto - Concious posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share