VETA

VETA This is an official account for the Vocational Education and Training Authority (VETA).

20/08/2026

Enjoy the videos and music you love, upload original content, and share it all with friends, family, and the world on YouTube.

20/08/2026
20/08/2026

Home KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU ATEMBELEA BANDA LA VETA WIKI YA ELIMU UJUZI NA UBUNIFU TANGA. sematv August 20, 2026 0  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, Agosti 20, 2026 ametembelea Banda la VETA katika maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu Kitaifa ...

20/08/2026
20/08/2026
SEKIBOKO: VIJANA GEUZENI UJUZI KUWA AJIRAMwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mheshim...
20/08/2026

SEKIBOKO: VIJANA GEUZENI UJUZI KUWA AJIRA

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Husna Sekiboko, ametoa wito wa kuimarishwa kwa elimu na mafunzo ya ufundi na ujasiriamali nchini, akisema ujuzi wa vitendo unaweza kuwa silaha muhimu kwa vijana katika kukabiliana na ukosefu wa ajira kwa kujiajiri na kuunda ajira kwa wengine.

Amesema hayo jana, tarehe 19 Agosti, 2026 akiwa kwenye banda la VETA katika Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu, Jijini Tanga.

Sekiboko amesema badala ya vijana kuhitimu na kuendelea kusubiri ajira, wanapaswa kutumia ujuzi wanaoupata katika vyuo vya ufundi kuanzisha shughuli za uzalishaji, huku Serikali ikiendelea kuweka mazingira ya kuwawezesha kupata vitendea kazi, mitaji na masoko.

Amesema changamoto ya ukosefu wa ajira inahitaji suluhisho linalowafanya vijana kuwa sehemu ya uzalishaji, akisisitiza kuwa kijana mwenye ujuzi ana uwezo wa kujiajiri na baadaye kuwa mwajiri wa wengine.

“Ni bora kijana kuanza na kile kidogo alichonacho na kujenga shughuli yake mwenyewe, kwa sababu anaweza kujiajiri na baadaye kuajiri wengine. Kwa kufanya hivyo, anakuwa amefanya zaidi kwa ajili yake mwenyewe na jamii yake kuliko kusubiri ajira pekee,” amesema.

Ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea banda la VETA na kukutana na vijana na wanachuo na wahitimu wa VETA ambapo amesema ameona uwezo mkubwa walionao katika kutengeneza bidhaa na kutoa huduma zinazoweza kukidhi mahitaji ya jamii.

Kwa mujibu wa Sekiboko, vyuo vya ufundi stadi vina nafasi kubwa katika utekelezaji wa jitihada za kukabiliana na ukosefu wa ajira kwa sababu vinawapatia vijana ujuzi wa vitendo ambao unaweza kutumika moja kwa moja katika uzalishaji.

Amesema ili ujuzi huo uwe na matokeo makubwa zaidi, vijana wanahitaji mazingira mazuri ya kujifunzia, vifaa vya kufanyia kazi na fursa za kupata mitaji ili kugeuza ujuzi wao kuwa biashara na ajira.

Amehimiza vijana kutumia fursa zinazotolewa na Serikali na taasisi mbalimbali kupata ujuzi na mitaji, akisema mtaji mdogo unaweza kuwa mwanzo wa shughuli kubwa endapo utatumika vizuri.

“Lengo ni kuondokana na utamaduni wa kusubiri ajira pekee. Kijana akipata ujuzi, anaweza kuutumia kuzalisha ajira yeye mwenyewe badala ya kusubiri kuajiriwa katika taasisi,” amesema.

Amesema hatua hiyo pia inaweza kusaidia kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 kwa kuongeza idadi ya vijana wanaoshiriki katika uzalishaji na kujenga uchumi kupitia ujuzi, ubunifu na ujasiriamali.

20/08/2026
20/08/2026

nifahamishe blog

20/08/2026

nifahamishe blog

Address

VETA Head Office, 12 VETA Road, 41104 Tambukareli, P.O. Box 802, Dodoma Tanzania, Email: [email protected] Telephone: +255 26 2963661 Fax: +255 22 2863408 Url: Www.veta.go.tz
Dodoma
PLOT NO. 18

Opening Hours

Monday 07:30 - 21:30
Tuesday 08:00 - 21:30
Wednesday 07:30 - 21:30
Thursday 07:30 - 21:30
Friday 07:30 - 21:30

Telephone

+255262963661

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when VETA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share