19/07/2020
VITU 9 VYA KUFANYA KATIKA MIEZI AMBAYO UNASUBIRIA KWENDA CHUO:
Written by: MOHAMEDI MTETEZI on JULY 19, 2020 in YOUR GUIDE TO UNIVERSITY LIFE.
Hongera sana kwa kumaliza form six, ni hatua kubwa sana uliyofikia. Haijalishi umepata matokeo uliyoyategemea au ambayo haukuyategemea, kumaliza form six is an accomplishment in life, hivyo hongera.
Kuna miezi k**a mitano mpaka kwenda chuo, yani una muda mrefu sana wa kusubiria chuo kabla ya kwenda chuo.
Kuna wale watakaoenda jeshi ambao pia at least wanapata kutumia miezi yao mitatu, ila Kuna wale ambao hawatochaguliwa jeshi hivyo wapo muda mrefu nyumbani bila kufanya chochote na unajiuliza naweza kuutumiaje muda wangu huu I got you covered.
Watu wanasema you only live once, na muda ni Mali. Kwa hiyo miezi yote hiyo ni Mali, inaweza kukuongezea kwemye maisha lakini pia inaweza ukaitumia vizuri kabla haujaenda chuo na kuwa busy na hivyo kushindwa kuwa na muda huo tena maishani
You never live the same moment twice, so miezi hii unaweza uka;
1. Utumia kuwa karibu na ndugu zako au familia… Ukishanza chuo utakuwa busy kuwa karibu nao k**a ulivyokuwa, na k**a ukipata chuo mbali na nyumbani basi hautopata muda wa kuwa karibu nao k**a ulivyokuwa.
2. Jifunza skills mbali mbali online… K**a unasmartphone, unaweza kujifunza chochote unachotaka kujifunza bure mtandaoni, kwa kutumia YouTube videos ama online platform nyingine zinazofundisha skills k**a graphic designing, photography nk, pia tutembelee sisi tukupe maarifa K**a haya.
3. Jifunza computer na course nyingine za muda mfupi zinazotolewa na vyuo ama sehemu mbali mbali wanazofundisha short course
4. Safiri sehemu mbali mbali ambazo haujawahi kwenda, unaweza ukasafiri kutembelea ndugu na jamaa
5. Soma vitabu na kujifunza kupitia waliokutangulia na kujifunza hekima zao
6. Pata tempo sehemu ya kujishikiza au volunteer sehemu.. Hasa ukiomba sehemu zinazoendana na course uliyoomba ili ukapate background ya kitu unachotaka kukisomea. Kufanya tempo inasaidia kujua k**a ungependa kusomea unachoenda kusomea au ubadilishe, as well as unaweza ukawa unapata hela Kwenye tempo pia. Ingawa tempo ni ngumu ukapata, but ni vizuri kutafuta pia usivunjike moyo.
7. Kufanya research ya chuo utakachosoma na course.pia sisi tunatoa ushauri wa jinsi ya kuchagua chuo bora na kozi inayokufaa.
8. Kupumzika haswa kwasababu umesoma muda mrefu na huu ni muda mchache wa kupumzika ili kwenda kusoma tena, so pumzisha akili, enjoy this resting time, "while you get ready to go back to studies".
9. Fanya shopping ya vitu utakavyovihitaji ukiwa chuo.
I hope utaweza kutumia muda wako huu vizuri, and I wish you all the best wakati unasubiria kwenda chuo.
NB:Tunatoa ushauri wa Mambo yote ya chuo bure kabisa.
Call:0676084414.
WhatsApp:0676084414
Email: [email protected]