Grace of God Ministry

Grace of God Ministry Zaburi 23

15/08/2026

I am sure I know but I don't know what I know can you know what I know or even you don't know what I know. OK let's ask Him He knows everything.

23/07/2026

*Mathayo 12:36-37*

[36]Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.
[37]Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.

Wapendwa tumuombe Mungu sana tuepuke kuongea maneno yasiyo na maaana au msingi. Tusishabikie tunapoona mtu anamdhalilisha mtu mwingine au mtu anamsengenya mwingine nawe ukashabikiaa. Mungu ameonya na k**a yupo anaayefanya hivyo atubu na kubadilika. Barikiwa sana kwa kulielewa neno. Amen

*Mpendwa nakutakia Ijumaa njema na MKONO wa BWANA wenye nguvu ya aajabu na uweza wa ajabu aawape haja ya mioyo yenu.*

23/07/2026

*Kutoka 23:25-30*

[25]Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.
[26]Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza.
[27]Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao. [28]Nami nitapeleka mavu mbele yako, watakaomfukuza Mhivi, na Mkanaani, na Mhiti, watoke mbele yako.
[29]Sitawafukuza mbele yako katika mwaka mmoja; nchi isiwe ukiwa, na wanyama wa bara wakaongezeka kukusumbua.
[30]Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako, hata utakapoongezeka wewe, na kuirithi hiyo nchi.

Mpendwa Mungu anatuwazia mema. Hivyo tusilalamike kuhusu kuendelea kuwaona adui zetu kuwa bado wapo. Mungu amesema katika mstari wa 27......
Adui zetu watafukuzwa kidogo kidogo hadi watakapoisha hivyo tusianze kumlalamikia Mungu mbona watesi wangu bado wapo na mimi naomba kila siku? Usikate tamaa sala zako na maombi zimefika mbele ya Jehova na utaona mambo makubwa na magumu usiyoweza kuyajua yataondoka. Make sure unasimama katika Imani yako vizuri.

*Uwe na Alhamis njema. Na Mungu mwenye nguvu akutendee mema.*

22/07/2026

*Hesabu 23:1-2,6-8,11-12*

[1]Balaamu akamwambia Balaki, Nijengee hapa madhabahu saba, ukaniandalie hapa ngโ€™ombe waume saba, na kondoo waume saba.
[2]Balaki akafanya k**a Balaamu alivyonena. Balaki na Balaamu wakatoa sadaka, ngโ€™ombe mume mmoja na kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu.
[6]Akarudi kwake, na tazama, amesimama karibu na sadaka yake ya kuteketezwa, yeye na wakuu wote wa Moabu pamoja naye.
[7]Akatunga mithali yake, akasema, Balaki amenileta kutoka Aramu,
Mfalme wa Moabu kutoka milima ya mashariki,
Njoo! Unilaanie Yakobo,
Njoo! Unishutumie Israeli.
[8]Nimlaanije, yeye ambaye Mungu hakumlaani?
Nimshutumuje, yeye ambaye BWANA hakumshutumu?
[11]Balaki akamwambia Balaamu, Umenitendea nini? Nimekuleta ili Uwalaani adui zangu, na tazama, umewabariki kabisa kabisa.
[12]Naye akajibu, akasema, Je! Hainipasi kuangalia, niseme neno lile BWANA atialo kinywani mwangu?

Mpendwa katika maisha yetu yapo mambo yanayotutesa kwa sababu wapo watu waliokwenda katika madhabahu zao za giza wakatulaania magonja, wakatulaania tusifanikiwe na wametoa sadaka kubwa na nyingine nyingi. Lakini sikia hili neno
๐Ÿ‘‡
Isaya 54:17

[17]Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.
๐Ÿ‘‡
*Isaya 7:7*
[7]Bwana MUNGU asema hivi, Neno hili halitasimama wala halitakuwa.
๐Ÿ‘‡
*Zaburi 105:15*
[15]Akisema, Msiwaguse masihi
wangu,
Wala msiwadhuru nabii zangu.

Mpendwa Mungu anatupenda na anatuwazia mema hivyo hatakubali kuona adui akitulaani katika madhabahu zao akanyamaza. Mungu ametutetea bila hata sisi kujua k**a tupo kwenye hatari.

*Nikutakie Jumatano njema Mpendwa Endelea kumwamini na kumtii. Omba bila kuchoka.*

18/07/2026

*Isaya 45:1-3*

[1]Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi
wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza viuno vya wafalme; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa.
[2]Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma;
[3]nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.

*Mpendwa nakutakia Jumamosi njema yenye Utulivu wa Amani na Furaha.*

14/07/2026

*Wakolosai 2:14-17*

[14]akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutush*taki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;
[15]akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.
[16]Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
[17]mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.

*Mpendwa nakutakia Jumatano njema iliyojaa nguvu za Yehova.*

12/07/2026

*HASIRA SIYO NZURI*

*Mithali 29:22*
๐Ÿ‘‡
[22]Mtu wa hasira huchochea ugomvi;
Na mtu mwenye ghadhabu huasi sana.
๐Ÿ‘‡
*Mathayo 5:22-26*
[22]Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.
[23]Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, [24]iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.[25]Patana na msh*taki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule msh*taki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.
[26]Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.
๐Ÿ‘‡
Wapendwa tujitahidi kupendana tusipende makasiriko kwa maana hasira inaleta magonjwa mengi k**a Presha, Kisukari, Matatizo ya Afya ya Akili n.k.
๐Ÿ‘‡
*. Yakobo 1:19-20*
[19]Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;
[20]kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu.
๐Ÿ‘‡
*Waebrania 12:14*
[14]Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;

*Mpendwa naomba ufanikiwe katika mambo yako yote. Na mkono wa Kuume wa Mungu uwe juu ya kila kitu kiitwacho kwa majina yakwako. Barikiwa Mpendwa. Uwe na Jumapili Njema*

11/07/2026

*Zaburi 3:1,3-8*

[1]BWANA, watesi wangu wamezidi kuwa wengi,
Ni wengi wanaonishambulia,
[3]Na Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu. [4]Kwa sauti yangu namwita BWANA Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu. [5]Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, Kwa kuwa BWANA ananitegemeza.
[6]Sitayaogopa makumi elfu ya watu,
Waliojipanga juu yangu pande zote.
[7]BWANA, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, Maana umewapiga taya adui zangu wote; Umewavunja meno wasio haki. [8]Wokovu una BWANA; Baraka yako na iwe juu ya watu wako.

*Mpendwa nakutakia Jumamosi njema. Baraka zake Mungu Mwenyezi ziwe juu yakwako na watu wakwako.*

Address

Dodoma
Dodoma

Telephone

+255717295344

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Grace of God Ministry posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category