Mazuri ya Uislamu

Mazuri ya Uislamu mkufunzi

21/02/2026
18/02/2026

Leo ni Ramadhani ya 1

سُئل شيخ الإسلام ابن تيمية : أيهما أنفع للعبد؟ التسبيح أم الاستغفار؟👉 Sheikhul-Islam Ibn Taymiyyah aliulizwa:Kipi kina f...
10/02/2026

سُئل شيخ الإسلام ابن تيمية : أيهما أنفع للعبد؟ التسبيح أم الاستغفار؟
👉 Sheikhul-Islam Ibn Taymiyyah aliulizwa:
Kipi kina faida zaidi kwa mja – kumtasbihi Allah (kusema Subḥānallāh) au kumuomba msamaha (istighfār)?
فأجاب:
👉 Akasema:
إذا كان الثوب نقياً فالبخور وماء الورد أنفع له.
وإذا كان دنساً فالصابون والماء الحار أنفع له.
👉 Ikiwa nguo ni safi, basi manukato na maji ya waridi ndiyo yanaifaa zaidi.
Lakini ikiwa nguo ni chafu, basi sabuni na maji ya moto ndiyo yanaifaa zaidi.
فالتسبيح بخور الأصفياء
والاستغفار صابون العصاة
👉 Kwa hiyo, tasbihi ni k**a manukato ya watu waliotakasika (wema),
na istighfār ni k**a sabuni ya wenye dhambi.
Maana kwa ufupi kwa Kiswahili
Sheikh Ibn Taymiyyah anafundisha kwa mfano:
➡️ Mtu ambaye hali yake ni njema, yuko katika utiifu na dhambi zake ni chache,
basi tasbihi (kumtukuza Allah) humfaa sana.
➡️ Lakini mtu ambaye amejichafua kwa dhambi, makosa na maasi,
basi kilicho bora kwake zaidi ni istighfār (kuomba msamaha wa Allah).
Kwa maneno mengine:
Tasbihi ni pambo la waja wema,
na istighfār ni utakaso wa waja wenye makosa.

*قال ابن رجب رحمه الله*كان السلف يدعون الله ستة أشهر أن يبلغهم رمضان، ثم يدعونه ستة أشهر أن يتقبله منهمTafsiri ya Kiswah...
08/02/2026

*قال ابن رجب رحمه الله*
كان السلف يدعون الله ستة أشهر أن يبلغهم رمضان، ثم يدعونه ستة أشهر أن يتقبله منهم
Tafsiri ya Kiswahili:
Maswahaba na wema waliotangulia walikuwa wakimuomba Allah kwa miezi sita awafikishe Ramadhani, kisha wakimuomba kwa miezi mingine sita aupokee (ibada yao ya Ramadhani).

Kauli hii inaonyesha namna wema waliotangulia walivyokuwa na hamu kubwa ya kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani na kumuomba Allah awape taufiki ya kuifaidika.

*Katika kauli za wanazuoni*قال سفيان الثوري رحمه الله:"عَلَيْكَ بِتَقْوَى اللهِ عَزَّ وَجَلَّ،وَالْزَمِ العُزْلَةَ، وَاش...
06/02/2026

*Katika kauli za wanazuoni*

قال سفيان الثوري رحمه الله:
"عَلَيْكَ بِتَقْوَى اللهِ عَزَّ وَجَلَّ،
وَالْزَمِ العُزْلَةَ، وَاشْتَغِلْ بِنَفْسِكَ،
وَاسْتَأْنِسْ بِكِتَابِ اللهِ عَزَّ وَجَلَّ."

Shik**ana na kumcha Mwenyezi Mungu Aliyetukuka,

zingatia (kujilinda na yasiyokufaa),
shughulika na nafsi yako mwenyewe,

na upate utulivu kwa kushik**ana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.
📚 الجرح والتعديل (٨٧/١)

━━━━━━━━━━━━━━━

03/02/2026

*NI IPI HALI YAKO NA MANENO YA MOLA WAKO MLEZI*

🍃🥒▫️Amesema Imaam Qurtubiy (Rahimahu Allaah):

🍃🥒▫️ولـمّا كان هذا الكتاب (القرآن) بهذه المنزلة حيث نزل به أمين السماء على أمين الأرض، عزمتُ أن أفني فيه عمري وأستفرغ فيه طاقتي
Na pindi kilipokuwa hichi kitabu (Qur'aan) na kwa daraja hili (tukufu) ikawa ameteremka nayo muaminifu wa mbinguni (Jibriil alayhi ssalaam) kwa muaminifu wa ardhini Muhammad (swalla Allaahu alayhi wasallama), nimedhamiria kumalizia kwayo Umri wangu na kutoa kwa ajili yake nguvu zangu

تفسير القرطبي

🍃🥒▫️Huyu ndiye imaam Qurtubiy (Allaah amrehem) amesema na juhudi zake zimeonekana ni kwa namna gani ameitumikia QUR'AAN kiongozi wa wafasiri wa QUR'AAN

🍃🥒▫️Je kwangu na kwako kati ya masaa 24 ya siku yako ni masaa au dakika ngapi umeipa qur'aan kwa kuisoma, kujifunza na kuzingatia au hata kuiskiliza?

*🍃🥒▫️Katika nguvu zako ni kiasi gani cha nguvu umewekeza katika QUR'AAN?*

*---▪︎●◽◽●▪︎---*

```TARJAMA: SHEIKH ABUU FAT'HIYAH KHAMIS KIZA, حفظه الله تعالى ورعاه```

*🍃VUNA THAWABU KWA KUENEZA ELIMU HII🍃*

*🥒USIBADILISHE ...... CHOCHOTE🥒*
🍃🥒➿➿➿➿➿➿➿➿🥒🍃

03/02/2026

*NASAHA*

🍃🏐▪️قال عطاء بن أبي رباح رحمه الله :
Amesema A'twaa bin abiy Rabaah (Allaah amrehem):

🍃🏐▪️تفقَّدوا إخوانكم بعد ثلاثٍ ؛
wajulieni hali ndugu zenu baada ya siku tatu

🍃🏐▪️ فإن كـانوا مرضى فـعُودوهم ،
ikiwa watakuwa wagonjwa basi muwatembelee

🍃🏐▪️ أو مشاغيل فأعينوهم ،
au wakiwa wameshughulishwa (na mambo) basi muwasaidie.

🍃🏐▪️أو كانوا نسوا فذكِّروهم".
au wakiwa wamejisahau (katika ibada na mambo muhimu) basi muwakumbushe

قوت القلوب (٣٦٨/٢)

🍃🏐▪️Undugu na urafiki ni katika mafungamano muhimu sana kuchungwa na kuhifadhiwa, kuna haki nyingi za ndugu kwa ndugu yake sawa uwe undugu wa nasaba au undugu wa uislam ambao ni kiunganishi kikubwa mno na chenye nguvu kinacho waunganisha watu zaidi ya kiunganishi cha nasaba

🍃🏐▪️Ndugu kwa ndugu yake ana haki nyingi ikiwemo kumnasihi na kumsaidia na kumuelekeza, kwa kumjulia hali ndio jambo ambalo litahakikisha kutekelezwa kwa haki hizi na nyingine pia

🍃🏐▪️kwa kumjulia hali ndugu yako, unajua maendeleo yake ya kidini na kiafya na kutambua mabadiliko yake kwa wakati na kujua yanayo msibu

*🍃🏐▪️hapo kumetajwa siku 3 sisi tunaishi miezi k**a si miaka k**a hakuna matukio hakuna kujuliana hali na undugu wetu kwa sehemu kubwa umebakia katika matukio tuu, yakiisha hakuna kujuliana hali wala salaam, kuna haja kubwa ya mabadiliko*

*---▪︎●◽◽●▪︎---*

```TARJAMA: SHEIKH ABUU FAT'HIYAH KHAMIS KIZAحفظه الله تعالى ورعاه```

*🍃VUNA THAWABU KWA KUENEZA ELIMU HII🍃*

*🏐USIBADILISHE ...... CHOCHOTE🏐*
🍃🏐➿➿➿➿➿➿➿➿🏐🍃

02/02/2026

Kifo huja gafla

Address

Mbagala
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mazuri ya Uislamu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category